Hatimaye nipo huru

Hatimaye nipo huru

mkuu majini hula nini??

Na wao wana adhabu siku ya kiama??
Nashukuru kwa maswali mazuri

Bahati mbaya mimi binafsi sina elimu ya majini. Niliyo yaandika ni kwa kusikia kutoka kwa Pazi na kwa kiasi katika elimu ya dini ambayo kiduchu tu nimeambulia hadi sasa lakini naendelea kujibidiisha kuiongeza.

1. Vyakula vya majini.

Kabla ya kujibu swali hili tujikumbushe kuwa majini wapo na namna mbalimbali, wapo warukao, wapo watambaao ama kutembea kama wadudu nk.

Katika makundi hayo pia wamegawanyika katika makabila (muundo) mbalimbali, hivyo utaona kwamba wapo aina nyingi sana za majini.

Kubwa katika mgawanyiko huo kuna ambao waliorejea na kufuata muongozo wa Muumba na wapo ambao ni waasi.

Vyakula vya majini waliorejea kwa Muumba hula vyakula vizuri ambapo miongoni mwake ni MABAKI YA VYAKULA VYA BINADAMU na VYAKULA VYOTE VILIWAVYO NA WANADAMU.

Vyakula vya majini waasi ni pamoja na DAMU (ikiwemo damu za ada za akina mama), MIFUPA, NYAMAFU (zikiwemo za binadamu na za wanyama pori), HAJA ZA WANADAMU (vinyesi) nk.
****

Kuna majini wanaishi majumbani mwetu, wapo tu siku zote na hawatufanyii ukorofi lakini wana 'shea' nasi vyakula kwa namna ya makombo na kwa namna ya kula tonge kwa tonge wakiamua.

Kuna majini wanaopenda kuishi ndani ya mwili wa wanadamu, na kupata mahitaji yao kupitia mwanadamu huyo ama kutimiza azma zao kupitia mwanadamu huyo.

Makazi yao mengine ni Baharini, Mapangoni, Jangwani, kwenye miti, Porini (misitu minene), Jalalani, Vyooni, majumbani nk

2. Kwakuwa majini pia wamepewa muongozo wa kufuata katika kuishi basi nao watakuwa na hukumu zao.

Ziada: Kuna majini wa dini mbalimbali, hivyo kuna majini wanaofuta miongozo ya Kikristo, Kiislam, kibudha, confucius, Hindu nk na wapo ambao hawataki kufuata muongozo wowote bali wanaishi watakavyo.
 
Nashukuru kwa maswali mazuri

Bahati mbaya mimi binafsi sina elimu ya majini. Niliyo yaandika ni kwa kusikia kutoka kwa Pazi na kwa kiasi katika elimu ya dini ambayo kiduchu tu nimeambulia hadi sasa lakini naendelea kujibidiisha kuiongeza.

1. Vyakula vya majini.

Kabla ya kujibu swali hili tujikumbushe kuwa majini wapo na namna mbalimbali, wapo warukao, wapo watambaao ama kutembea kama wadudu nk.

Katika makundi hayo pia wamegawanyika katika makabila (muundo) mbalimbali, hivyo utaona kwamba wapo aina nyingi sana za majini.

Kubwa katika mgawanyiko huo kuna ambao waliorejea na kufuata muongozo wa Muumba na wapo ambao ni waasi.

Vyakula vya majini waliorejea kwa Muumba hula vyakula vizuri ambapo miongoni mwake ni MABAKI YA VYAKULA VYA BINADAMU na VYAKULA VYOTE VILIWAVYO NA WANADAMU.

Vyakula vya majini waasi ni pamoja na DAMU (ikiwemo damu za ada za akina mama), MIFUPA, NYAMAFU (zikiwemo za binadamu na za wanyama pori), HAJA ZA WANADAMU (vinyesi) nk.
****

Kuna majini wanaishi majumbani mwetu, wapo tu siku zote na hawatufanyii ukorofi lakini wana 'shea' nasi vyakula kwa namna ya makombo na kwa namna ya kula tonge kwa tonge wakiamua.

Kuna majini wanaopenda kuishi ndani ya mwili wa wanadamu, na kupata mahitaji yao kupitia mwanadamu huyo ama kutimiza azma zao kupitia mwanadamu huyo.

Makazi yao mengine ni Baharini, Mapangoni, Jangwani, kwenye miti, Porini (misitu minene), Jalalani, Vyooni, majumbani nk

2. Kwakuwa majini pia wamepewa muongozo wa kufuata katika kuishi basi nao watakuwa na hukumu zao.

Ziada: Kuna majini wa dini mbalimbali, hivyo kunaajini wanaofuta miongozo ya Kikristo, Kiislam, kibudha, confucius, Hindu nk na wapo ambao hawataki kufuata muongozo wowote bali wanaishi watakavyo.
Aisee kumbe utofauti wetu na wao sio mkubwa sana iwapo tutaamua kufuata yale Muumba ameyataka.

Na mkuu unaweza kufafanua kidogo ile part ambayo mwamba alienda ujinini na kurudi baada ya siku 5 lakini huku ikawa kama siku 40. Huko siku zikoje na kama kuna utofauti ilipimwaje miaka yao wanayoishi ilhali muda wetu na wao ni tofauti kiasi hicho.??
 
Kuna sehemu nyingi sijasimulia, kumbuka tulikesha akiongea na mchana wake...

Kuna ambayo aliniambia nisiyaseme, ole wangu! Katika simulizi nimechengesha chengesha mengi ili kutimiza kusimulia...

Kuna makubwa!

Hivyo swali lako limeingia katika kundi hilo ingawaje kwa uchache ni kwamba tuna share kalenda moja ingawaje wao wanatumia saa ya jua, kalenda ya mwezi (moon calendar)
 
Curious???!!!

Nenda night club yenye watu wengi sana, jitahidi kuwa karibu na kila mwanamke mrembo humo kisha chunguza ngozi za mikono yao

Ukiona pattern siyo ya kashata badala yake ni draft ujuwe ni mmoja wao!

Ni mawakala wakubwa wa Ibilisi katika kuleta 'fashion' na kuieneza lengo likiwa ni lile like la kumpotosha mwanadamu

Majini wacha Mungu mara nyingi hawasumbui binadamu kwa namna yoyote ile, labda ushirikiano fulani fulani katika mambo (ambayo si ya kimaasi)

Wengi wa majini wanaowaingia wanadamu ama kuwabughuzi wanadamu ni waasi hata kama watasema wao ni wacha Mungu (waongo), watajifanya kukuamrisha kuswali nk lakini waasi wakubwa na dawa yao ni neno la Mungu tu tena uwe na imani thabiti maana ukisema maneno ya Mungu nao wanasema kwa kuwa wanayajuwa!

Usipokuwa na imani thabiti hawatoki, wanaweza kujifanya wametoka lakini ukweli wanakuwepo...

Wengine hubembelezwa kwa vyakula ili watulie....
 
Curious???!!!

Nenda night club yenye watu wengi sana, jitahidi kuwa karibu na kila mwanamke mrembo humo kisha chunguza ngozi za mikono yao

Ukiona pattern siyo ya kashata badala yake ni draft ujuwe ni mmoja wao!

Ni mawakala wakubwa wa Ibilisi katika kuleta 'fashion' na kuieneza lengo likiwa ni lile like la kumpotosha mwanadamu

Majini wacha Mungu mara nyingi hawasumbui binadamu kwa namna yoyote ile, labda ushirikiano fulani fulani katika mambo (ambayo si ya kimaasi)

Wengi wa majini wanaowaingia wanadamu ama kuwabughuzi wanadamu ni waasi hata kama watasema wao ni wacha Mungu (waongo), watajufanya kukuamrisha kuswali nk lakini waasi wakubwa na dawa yao ni neno la Mungu tu tena uwe na imani thabiti maana ukisema maneno ya Mungu nao wanasema kwa kuwa wanayajuwa!

Usipokuwa na imani thabiti hawatoki, wanaweza kujifanya wametoka lakini ukweli wanakuwepo...

Wengine hubembelezwa kwa vyakula ili watulie....
hii dhana ya kiumbe kumuingia kiumbe mwingine na kumuongoza inachanganya sana.
 
Skin pattern
Skin texture

Piga picha ngozi ya mkono wako kwa mfano, kisha zoom. Ukiweza kiweka high resolution ni vizuri zaidi.

Picha nilizoweka hapo chini ni HUMAN SKIN 100% ngozi ya binadamu.

Sasa jinni akijibadilisha kuwa kama mwanadamu ngozi yake haiwi na pattern (texture) kama ya binadamu, badala yake inakuwa draft draft ama kama pattern za ngozi za wadudu watambaao...

Macho
Nyayo
Ngozi

Sehemu hizi siyo majini wote wenye kuwez kujibadilisha na kuwa kama wanadamu

Ingawaje sikuhizi kuna lensi za macho dukani kama za majini na wanawake huziweka kama urembo...

Nyao labda watavaa viatu si rahisi kuona haraka haraka

Ngozi ndiyo rahisi.

Lakini tahadhari, majinni huwa wakali akiona unataka kumchunguza ama kumgundua.
 
Attachments

  • Screenshot_20221030-075742.jpg
    Screenshot_20221030-075742.jpg
    49.7 KB · Views: 66
  • images.jpg
    images.jpg
    45.7 KB · Views: 69
  • e1cd7349189e5c9fc2c36a7a56c4a2db.jpg
    e1cd7349189e5c9fc2c36a7a56c4a2db.jpg
    151 KB · Views: 68
  • images.jpg
    images.jpg
    45.7 KB · Views: 63
Skin pattern
Skin texture

Piga picha ngozi ya mkono wako kwa mfano, kisha zoom. Ukiweza kiweka high resolution ni vizuri zaidi.

Picha nilizoweka hapo chini ni HUMAN SKIN 100% ngozi ya binadamu.

Sasa jinni akijibadilisha kuwa kama mwanadamu ngozi yake haiwi na pattern (texture) kama ya binadamu, badala yake inakuwa draft draft ama kama pattern za ngozi za wadudu watambaao...

Macho
Nyayo
Ngozi

Sehemu hizi siyo majini wote wenye kuwez kujibadilisha na kuwa kama wanadamu

Ingawaje sikuhizi kuna lensinza macho dukani kama za majini na wanawake huziweka kama urembo...

Nyao labda watavaa viatu si rahisi kuona haraka haraka

Ngozi ndiyo rahisi.

Lakini tahadhari, majinni huwa wakali akiona unataka kumchunguza ama kumgundua.
sijaelewa. hili ya draft ndo binadamu mbona ya kwangu hakuna hata draft Moja au ni ngozi ya eleo Gani hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kawaida ya mzee wetu, simulizi zako zinakuaga na details nyingi sana za uhakika. Niko Koromije, lakini simulizi imenipeleka kote kuanzia Bagamoyo mpaka msitu wa mbirikimo.

Nangojea safari ya kurudi Pwani sasa!
jamaaa anaitisha,yaani maeneo yote hayo aliyo taja ,ya kuanzia kigoma hadi kabwe,nayafahamu sana,hasa hapo lyazumbi ndio kuna njia panda ya kwenda kabwe,kuna kuku,samaki na nyama ya mbuzi ya kufa mtu!!!na hicho kisiwa cha TUMBATU,kipo zanzibar unavuka na fibre kutoka MPEKETONI,kwa buku 2, unakutana na kisiwa kinaitwa JONGOWE!!ni hatari sana,kwa uchawi.
 
16. MAISHA MAPYA na UHURU - Ω

“Nakuusieni na kuihusia nafsi yangu juu ya kumcha Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu (aliye takasika), … hiki (Qur’an) ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na muongozo kwa wale wamchao …”

“Sisi waislamu, tuna miongozo miwili, Qur’an na Sunna. Qur’an ni maneo ya Mwenyezi Mungu na Sunna ni matendo na mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimwendee).”

“Tushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadithi za Mtume, hatuwezi kupotea.”

Hayo yalikuwa maneno ya Walii (kipenzi) wa Mwenyezi Mungu wa Utete Rufiji (kama wenyeji walivyokuwa wakimwita) wakati akinukuu aya kutoka Qur’an akiwa anatujenga kiimani.

“Katika hii Qur’an Mwenyezi Mungu ameweka elimu ya toka watu wa mwanzo mpaka watu wa mwisho, elimu zote zimo ndani ya Qur’an, historia imo, mawaidha yamo, mifano imo, visa vimo, hesabu zimo, utaratibu wa kuendesha Dunia umo ndani ya Qur’an na hiki kitabu huhifadhi waumini kwa fitina iliyomo humu duniani…” aliendelea

“Ndani ya Qur’an kuna habari za watu waliokuwepo kabla yetu, kuna habari za watu baada ya sisi kuondoka, ni hakimu baina yetu na ni upambanuzi juu ya mambo mbalimbali. Haifai kuiacha.”

“Hii Qur’an ajabu zake hazimaliziki, wana zuoni hawashibi, kila siku wanatoa faida na hata majini walipoisikia Qur’an inasomwa, wakasema hakika sisi tumesikia Qur’an ya ajabu, … inaongoza kwenye uongofu kwa hiyo tumeiamini na wala hatutofanya ushirikina…, na kwa hakika utukufu wa Mola wetu mlezi umetukuka kabisa,… hana mke wa mwana…, … na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uongo uliopindukia juu ya Mwenyezi Mungu… nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamsingizii uongo Mwenyezi Mungu…,”

Aliendelea yule mcha Mungu tutupatia mawaidha kupitia kitabu kitukufu Qur’an na kutusimulia habari za majini jinsi baadhi walivyo mrejea Mwenyezi Mungu na wengine waliendelea kukengeuka.

“Eee umesema mmetoka Bagamoyo!” aliuliza yule Walii,

“Rudini huko, kuna Sheikh Mkubwa Zawiani, utapata muongozo na elimu kadha wa kadha, kikubwa shikamaneni na hiki kitabu wala msikiache.” Alimaliza yule Walii na tukaagana na kuanza safari ya kurudi.

Nilikuwa mimi na mke wangu Behat, tulilala Rujiji Ikwiriri na siku ya pili tulifika Dar na moja kwa moja kwenda Bagamoyo.

Bagamoyo pale Zawian tukaambiwa tuende Lushoto kumtafuta Shariff Badowo ili atufanyia maombezi makubwa kabla ya kurudi Zawiani kwa ajili ya kumalizia elimu nasihi.

Tulienda Tanga, tukafika nymbani kwake lakini tukaambiwa amesafiri kwenda Mombasa, tukaambiwa tumtafute kijana mmoja pale Horohoro atatusaidia kufika kwake.

Yule kijana alikuwa ni mfanyakazi wa mabasi ya Modern (Mombasa – Tz – Zambia nk), alikuwa anaitwa Sarojo, alitusaidia sana hadi tukafika kwa Shariff Badowo na kufanya dua kubwa kubwa sijapata kuona na tulivyorudi Zawiani tulikuwa na utulivu mkubwa.
*********

Tukiwa Zawiani – Bagamoyo

“Tatizo lenu mlivyokuja mara ya kwanza hamkutaka kunisikiliza kwa kituo, wewe na kaka yako wote mlikuwa na haraka haraka kiasi cha kutopata yote ambyo nilitaka kuwaambieni.” Alikuwa anaongea Sheikh Mohamed kwa sauti yake nzito iliyojaa umwinyi mwinyi hivi kwa kutulaumu kiaina…

“Sasa ulivyorudi na kuniambia kuwa umepona, nikadhani labda umejuwa asili ya shida yako na kutatuliwa ipasavyo…” aliendelea…

“Kumbe bado kwa maoni yangu, ulikuwa kwenye safari ya kujijuwa na kujitambua… na sasa kwa vile umefikia hatua hii basi ukae kitako nikuelimishe…” alisema.

“Mwenyezi Mungu alituumba ili tumuabudu yeye, tena yeye tu na wala tusimshirikishe na miungu mingine, hayo ndiyo malengo hasa ya sisi kuumbwa, hata maumbile yetu yamewekwa kurahisisha zoezi hilo la kumuabudu yeye”

“Tukimuabudu yeye hatumuongezei chochote, na tusipomwabudu hatumpunguzii chochote, YEYE ambaye hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ile YEYE, Yu hai na ni wa kudumu, halali wala kupatwa na usingizi. NDIYE Mola wa Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina yake…”

“Anajuwa yaliyochificha mbele na nyuma, na katika sisi viumbe hatuna tujuwalo ama hatuwezi kujifunza (kupata elimu) ila kwa kuridhia kwake, na utukufu wake umeenea Mbinguni na ardhini na wala hawezi kushindwa kuvilinda viumbe vyake maana yeye ametukuka (aliye juu) na NDIYE MKUU.” Alisema Sheikh kisha akasoma aya katika mpangilio wake.

Alivyoanza kusoma nami nikakumbuka kile kikaratasi nilichopewa Kikokwe niwe nasoma mara kwa mara, maneno hayo yalikuwa sehemu ya dua ile niliyopewa huko.

Sheikh aliendelea na risala…

“Katika uumbaji wake (Mwenyezi Mungu) aliumba viumbe mbalimbali, na kila kiumbe kina mamlaka yake na mipaka yake katika kuyaendea mambo…”

Akatoa mifano mbali mbali jinsi viumbe wengi wanavyoishi humu duniani ikiwemo wadudu, hayawani na hatimaye majini na binadamu.

“Binadamu ndio tumepewa uhalifa (uongozi) katika dunia hii, yani tunatakiwa tuweze kuitawala dunia ipasavyo…”

“Majini nao wana tawala zao, wana mataifa yao, wana makabila yao, wana koo zao, wana mila zao na desturi zao, na wamepewa uwezo mbalimbali lakini pia wamewekewa mipaka…”

“Haifai kwa Majini kuingia kwenye tawala za kibinadamu na kuwasumbua watu kwa kuwapagawisha, kuwatia maradhi ama eti kujifanya wanawalinda…”

“Wao wana ‘ulimwengu’ wao na sisi binadamu tuna ‘ulimwengu’ wetu…”

“Hivyo ni makossa makubwa kwa Jinni kumuingia mwanadamu kwa namna yoyote ile kwa visingizio mbalimbali…”

“Idadi ya majini ni kubwa mara nyingi sana kuliko wanadamu, na kwa kuzingatia kuwa wao wanaishi muda mrefu kuliko wanadamu basi wingi wao huongezeka mara kwa mara kiasi cha kutapakaa duniani kote… kwa wingi wao huo hata kila mwanadamu aliye hai muda huu akikusanya majini sabini kila mmoja, basi binadamu wote watakusanya na wengi sana bado watabaki hawajakusanywa”

“Kuna elimu mbalimbali za kuweza kuwamiliki hawa majini, lakini ni moja ya elimu zilizokatazwa kwa kuwa hatimaye huleta hasara badala ya faida…”

“Lakini kwa kuwa Duniani humu kuna fitina mbalimbali ikiwemo fitna ya afya, mali, wake, waume, watoto nk basi baadhi ya watu hupatwa na husda, chuki na vijicho ambavyo huwadhuru wenzao, na kazi zote hizo hufanywa na hao majini ambao wameasi kwa kushirikiana na binadamu kwa namna mbalimbali za elimu ya kichawi”

“Elimu ya kukabiliana na matatizo hayo pia ipo, ipo kwa njia nyeusi na kwa njia nyeupe…”

“Hivyo tiba zipo, lakini kuna tiba kwa njia sahihi na zipo tiba za kwa njia ya kishirikina”

“Kufanya ushirikina na moja ya dhambi ambayo kama ikitokea umekufa bila ya kutubu basi ni dhambi isiyo sameheka labda kwa rehma zake Mola wetu maana yeye ndiye mjuzi zaidi”

“Hivyo basi ushirikina HAUFAI mbele za Mwenyezi Mungu”

“Kwakuwa tiba sahihi zipo, basi yatupasa kufuata tiba kwa njia zilizoelekezwa kwa miongozo ya dini yetu”

“Tiba isiyo sahihi utaijuwa kwa masharti yake ambayo hatimaye yanakupelekea katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa namna zote nne, kuwaza, kunena, kutenda na kutotimiza wajibu…”

“Sasa kwa kuwa ninyi mliamua kuishi kama binadamu…”

Tukawa tunaangaliana na Behat…

“…yafaa muendelee kuishi hivyo na kufuata maamrisho na makatazo yote ambayo yapo katika muongozo wa Qur’an na Sunna…”

“Pazi…!” aliniita Sheikh

“Mwenzako ana kiumbe tumboni…”

Nikawa manuangalia Behat tumboni sioni kitu zaidi ya ‘flat screen’ (hakuwa na hata kijitambi kidogo)

“Atazaliwa kiumbe ambaye sasa atakuwa mwanadamu kamili, wanenu hawatokuwa na passport ya kuingia Ujinini kama ilivyo kwenu hivi sasa ingawaje bado mpo nusu jinni.., wewe Pazi ni nusu binadamu nusu jinni na huyo mwenzako ni nusu jinni na nusu binadamu…”

Moja kwa moja nikaelewa tofauti yake kwa mmoja wetu alilala kwenye tumbo la uzazi binadamu ilhali mwingine alila kwenye tumbo la uzazi jinni.

Aliendelea kutupa risala pale weeee mwisho akasema…

“Tafuteni njia halali za kupata rizki zenu, hata kama itakuwa ni kutibu watu basi uifanye tiba iliyo sahihi kwa njia za kisunna (yaani kwa njia ya mafundisho ya Mtume Muhammad, Rehema na Amani zimwendee)

“Kitu kingine muhimu sana ni kwamba haifai kubeza dini nyingine, mfano hawa wenzetu wakristo tunaishi nao humu mjini, majumbani na kupeana heshima za kibinadamu, Kuna Kanisa kubwa kule Mantep (Sikuhizi wanaita ADEM), kuna Kanisa dogo kule miembe safa (jirani na kushukia MSALABANI) na kuna Kanisa kule Mwanakalenge. Hawa ni binadamu wenzetu na wana Imani yao thabiti katika kumwabungu Mungu wao kwa mujibu wa mafundisho yao, ukumbuke kuwa hawa pia kiongozi wao alipewa Kitabu kama ilivyo Qur’an kwa sisi. Usiwabeze wala kudharau Imani zao maana kuna wengine huenda wakawa bora mbele ya mwenyezi Mungu kuliko baadhi yetu, lakini haikatazwi kuwalingania ili waje katika uislam, tena kwa lugha iliyo nzuri na staha.”

“Kumbuka hata Nabii Mussa (Rehema na Amani zimfikie) alipoambiwa akamlinganie Firauni (Farao) aliambiwa akazungumze naye kwa upole licha ya kufuru kubwa aliyokuwa akiifanya. Kazi yetu ni kufikisha ujumbe lakini kumuongoa mja siyo kazi yetu, Allah mwingi wa Rehema sisi sote ni viumbe vyake, tusijitie ukiburi, YEYE Allah huamua atakavyo.”

Aliendelea…

“Vitabu cha elimu hiyo ya tiba zipo, vitafute ujifunze kwa walimu ukihitimu uendelee na tiba halali, kama hutoweza basi rejea kwenye kazi ya baba yako, ameshazeeka sasa afaa kusaidiwa sana…”

Alimalizia risala yake kwa kutusihi kuwa sisi bado ni nusu watu nusu majini, hivyo kiasili tuna nguvu za kijinni basi tuwe makini na maneno tuyasemayo na kujitahidi kujizuia hasira zetu maana huenda zikawa na athari kwa binadamu wa kawaida.

Tulirudi nyumbani na kumkuta mama akitusubiri kwa hamu.

“Enhe, mmeambiwaje huko?...” Mama aliuliza kwa shauku

Tukamwelezea yote na hatimaye mimi na mke wangu tukaamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwalingania watu katika dini huku nikiendeleza kazi ya Baba.

“Nadhiri yako sasa Mama inaenda kutimia…” nilisema.

Baada ya siku tatu, tuliaga kurudi Dar es Salaam kuendelea na maisha.

Leo hii tuna watoto watatu, tunaendeleza kazi ya uvuvi na uchuuzi kwa njia za kisasa, Baba na mama walishafariki, mama mkubwa pia alishafariki.

Tukapata Chakula cha mchana pamoja, kisha akanisindikiza nami nikachukuwa njia ya kurudi kwangu Upanga.

Jumamosi ile ilikuwa tulivu lakini nyumbani kwangu hapakuwa hivyo, nilikuta mke wangu amenuna, lakini nikamwambia hebu baada ya kula uje chumbani nimsimulie kisa chote nilichosimuliwa….
*******

Hakutaka nilale bali nimmalizie kisa chote maana muda tayari ulikuwa umeshaenda sana na siku Jumapili ilikuwa ndio inaingia (kwa mujibu was aa za na kalenda ya Gregori)…

Nilimkidhia haja yake baada ya kuona amevutiwa pia na kushangazwa japo kwa kuifupisha.

Mwishowe tuliendeleza ‘libeneke’ la mume na mke.

**************** MWISHO*************

Update!

Sheikh Mohamed alishafariki, Mzee Zahiri naye, Mwalimu Mwaloki, Mzee wa tiba Mlingotini, Mzee Njembi, Mcha Mungu wa Rufiji, Shariff Badowo, Shariff wa Kikokwe wote wametangulia mbele za haki.

Watu wengine ambao wametajwa katika simulizi hii sina update zao.

Imenibidi nifupishe ili niende na muda-huru niliokuwa nao maana ni mchache.

Niliamua kushea nanyi kisa hiki kama kumbukumbu ya kukumbuka uwepo wa Pazi na familia yake hapa Duniani kwa maana ya kwamba ile familia yote ilifariki kwa kuzama baharini miaka kumi na moja na siku arobaini na nane hivi ziliyopita walipokuwa wakitokea Unguja kuelekea matembezini Pemba kwenye MV. Spice Islander.

**********

Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwa hakika kwake tutarejea.

Nimeongeza maarifa mzee wangu Shukran sana shekh Jamaal
 
14. MWANZO WA MWISHO

“Mama mvalishe nguo zake huyo mgonjwa kisha mrudi keshokutwa ili kesho nikatafute dawa zake za kutumia…” nilimuaga yule mama huku akitaka kunipatia ujira lakini nilikataa maana kabisa niliona sijamaliza kazi.

Tangia nilivyoruhusiwa kuchukuwa hela kwa wateja, zile hela za miujiza sikupata tena, hata wakati wa dharura lakini nadhani kwa sababu nilikuwa na hela ndani na benki.

Kwenye rufaa niliambiwa kuwa binti ana maruhani kutoka falme nyingine za kijini ambao ni wakali na wakorofi na wanamtumia katika kufanikisha baadhi mambo yao huku duniani. Nikaambiwa niende msitu wa Mbirikimo ili kuchukuwa mizizi na majani ambayo mchanganyiko wake utawakera sana hao maruhani hadi kuondoka wenyewe.

Majini ni viumbe ambao nao wamegawanyika katika utaifa mbalimbali na makabila mbalimbali. Jinni siyo Malaika, na Malaika siyo Majini, hawa ni viumbe tofauti ingawaje waliwahi kufika hapa duniani kabla ya mwandamu kuja na kupewa utawala wa hii dunia.

Kama nilivyoandika awali kwamba Mwenyezi Mungu aliumba viumbe vya aina nyingi, tunavyovijuwa na tusivyo vijuwa, vinavyoonekana kwa macho ya kawaida na visivyoonekana kwa macho ya kawaida…

Katika simulizi za kale, tunaambiwa kuwa baada ya ulimwengu kuumbwa na viumbe wote kuumbwa kulikuwa na Amani na utulivu. Malaika walikuwepo na Majini walikuwepo. Ikatokea sababu kukawa na ugomvi kati ya majini na Malaika (hapa kabla ya binadamu kuubwa), vita ile ilipiganwa na Malaika walishinda, lakini katika vita hivyo Malaika mkuu akamuokota mtoto mdogo wa kijini na kumchukuwa na kuishi naye katika tawala za kimalaika.

Jinni yule mtoto alikuwa akiitwa Ibilisi. Na akajifunza mengi katika elimu kutoka kwa Malaika, akawa kama ni mmoja wao.

Siku ambayo Mwenyezi Mungu alipwaamrisha Malaika watii kwa salamu ule mwili wa Adam ambao ulikuwa umefinywangwa kwa udogo, Malaika walitii isipokuwa Ibilisi ambaye alijivuna na kujisivu kwamba yeye hawezi kumtiii kiumbe aliyeumbwa kwa udongo kwani yeye ni bora maana aliumbwa kwa nuru ya moto…

Ndipo Ibilisi akalaaniwa na kutupwa hewani (nje ya falme ya Malaika…). Lakini kabla ya kufukuzwa aliomba aishi muda mrefu hadi aone hao wanadamu watakavyokuwa…

Inasemekana Mungu alimkubalia lakini si kwa urefu atakao yeye bali kadri Mwenyezi Mungu atakavyoona inafaa…

Baisi Ibilisi (aka, Lucifer) akaahidi kuwapotosha wanadamu wote ili waje waadhibiwe pamoja naye, maana Ibilisi anajuwa uwepo wa paradiso na uwepo wa jehanamu…

Inasemekana Mwenyezi Mungu akamwambia kuwa hutoweza kuwapotosha watu wangu isipokuwa wale ambao ni wa motoni tu…

Kazi ya kwanza ya kupotosha Ibilisi aliianza kwa mke wa Adamu kama maandiko yanavyosema.

Kuna baadhi ya maandiko ya habari za kale huwezi kuyapata katika Biblia ama Qur’an ama vitabu vingine vya falsafa dini za kale, lakini maandiko ya namna hii yapo. ingawaje naheshimu imaani ya mapokeo ya wengine.
***********

Ipo specie ya Majini ambao huishi miaka mingi sana kiasi cha kushuhudia kizazi kirefu cha binadamu, yaani zaidi ya miaka elfu moja…

Ipo spicie ya Majini ambayo ikifikisha uzee wanarudi tena kuwa watoto na kurudia rudia kwa karne kadhaa kabla ya mwisho wa maisha yao…

Ipo spicie ya Majini ambao miaka nenda miaka rudi wao umri wato wanakuwa watoto tuu…

Ili mradi kuna spicies nyingi za majini.

Majini ikiwa ni sehemu ya Ibilisi na ndugu zake baada ya kutimuliwa Mbinguni na kuletwa duniani waliamua kuwa na makazi yao sehemu mbalimbali za ardhi ikiwemo mapangoni, chini ya maji, kwenye miti ama majabali makubwa na kazi yao kubwa ni kuwapotosha wanadamu ili wasimtii Mwenyezi Mungu kama ilivyo kwake.

Majini yamepewa uwezo mkubwa kama nilivyo eleza awali lakini hawakupewa umbo kama la binadamu na wanatamani sana wawe kama binadamu na kufanya mambo ya kibinadamu ndiyo maana huwaingia kwa namna isiyoelezeka kirasisi wanadamu na kuwatumikisha katika kufanukisha mambo yao.

Mwanadamu akiingiwa na Jini siyo lazima apige kelele, au aanguke kama tulivyo zoea, bali anaweza kutoa kauli ambazo kwa akili ya kibinadamu unajuwa huyu si binadamu kama vile kubashiri na kupatia, ama kutoa historia ya yaliyopita kwa kupatia hii yote ni kutokana na wao kuwa na umri mrefu hivyo kushuhudia mambo na kwa kuwa hawaonekani kwa macho ya kibinadamu basi pia hupeana habari juu ya yale yatakayoenda kutendeka “kwa kusikia” kutoka kwa vinywa vya binadamu ama kwa uwezo waliopewa…

Kwakuwa binadamu tulipewa utawala juu ya viumbe wote, basi kuna elimu ya kuwatawala majini ambapo wenye nayo wakiitumia vizuri inakuwa yenye manufaa na ambao watakaotumia vibaya ina kuwa na madhara makubwa.

Mfano wa wazi ni ujenzi wa mapiramidi kule Misri ni Dhahiri kuwa haikuwa kazi ya wanadamu pekee, mapango ya kule mashariki ya kati kule na hata machimbo ya mfalme Suleiman…nk.

Jini mtumwa anakuwa mtiifu kwa bwana wake na kufanya kama anvyoagizwa. Pia kuna majnini wa kutengeneza kwa kanuni, yaani ukiunganisha hiki na hiki basi hupatikana jinni, si kwa maana ya kuumba bali kwa maana ya kumuita kutoka huko aliko kwa kanuni hiyo na kuja kuwa mtumwa kwa makubaliano kadha wa kadha na bwana wake…

Katika makubaliano hayo ukiyachunguza hatimaye ni kumuasi Mwenyezi Mungu kwa kukiuka maamrisho au makatazo yake ikiwemo kula ama kunywa najisi, kuacha kufanya ibada, kuua nk.

Majini wanapenda kuishi kama wanadamu, ingawaje nao wamepewa uhuru wa maamuzi kama sisi, vivyo hivyo ikatokea Malaika fulani wawili na walitamani kuishi kama binadamu ili waone ugumu uliopo wa kuwa mwandamu na kushinda majaribu ili hatimaye kupata daraja la juu katika paradiso ya Mwenyezi Mungu kuliko Malaika kama ambavyo Mwenyezi Mungu aliwaambia Malaika kuwa ninyi sikukuumbeni kwa matamanio kama binadamu ndio maana hao watakaoshida mitihani ya duniani basi watapata ujira ulio mkubwa Paradiso pengine kuliko ninyi…

Ndipo wakajitokeza hao Malaika wawili walioomba waletwe duniani ili wapewe hayo matamanio na waishi kama wanadamu na wakaadhidi watashinda…

Inasemekana Mwenyezi Mungu akawaahidi wakishida watapata daraja la juu na wakifeli wataadhibiwa. Basi nao wakapewa hiyari kama wandamu na wakashushwa maeneo ya Iraq (kwa sasa) ambako kulikuwa na mji na watu.

Hawa malaika wawili walipewa elimu ya utabibu, wakaanza kutibia watu duniani (walikuwa na maumbile ya kibinadamu baada ya kushusha Iraq), na kwa kuwa walikuwa waadilifu na elimu nyingi basi wakapata kazi ya kusuluhisha watu pale ambapo kunatokea kuto kuelewana.

Elimu ya utabibu waliyokuja nayo ndiyo hii iliyosambaa hadi leo, ingawaje elimu nyingi iliondolewa na nyingi ikakatazwa kutumika.

Walifundisha wanadamu waliopenda kujifunza utabibu na hata baadhi ya majini walihudhuria kujifunza elimu hiyo na kuihifadhi vyema huko ujinini.

Lakini kama nilivyosema Majini wapo speices nyingi na makabila mengi, hivyo kuna makabila mengine ni wakorofi tu muda wote na specie ambayo ni comedy sana na hawana madhara sana kwa binadamu ni vibwengo (tofauti na jisi vibwengo wanavyochukuliwa hivi sana)

Jinni Ibilisi na kundi lake wakaanza kuitumia elimu ile ya utabibu kinyume nyume ili kuwadhuru watu…

Kwa mfano, ikitokea mtu amegombana na mwenzake, basi Ibilisi humfuata na kumwambia, kwa mfano, “…Wewe fulani si amekuudhi, basi mpe klorokwini 10 zote kwa mara moja, atadhurika…” ambapo elimu ya utabibu ilisema mgonjwa wa malaria yafaa apewe vidonge 10 lakini siyo kwa mara moja bali ameze labda vinne kwa siku mbili kisha siku ya tatu ameze vidonge viwili au ameze vinne leo kesho viwili na siku mbili zitakazofuata viwili viwili jumla vidonge kumi.

Hapo tiba ikageuka na kuanza kuwa na madhara, elimu ya kinyume ikaanza kusambaa dhidi ya majini na kuanza kuwafundisha wanadamu kwa ajili ya kudhuriana hatimaye lengo la Ibilisi likawa linatimia la kuwapotosha wanadamu.

Kombozi mbali mbali zikaja kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu na kurejea njia iliyo sahihi na miongozo ya vitabu ikaletwa hadi ikafika nyakati za Mtume Muhammad (rehema na Amani zimwendee)alipo pewa kitabu kiitwacho Qur’an.

Baadhi ya Majini walivyosikia, walirejea kwa Mwenyezi Mungu, wakawa wanyeyekevu lakini baadhi walibaki kwa Ibilisi na kuendeleza lengo lao la kupotosha wanadamu. Hapa ndipo kukawa na neno SHETANI.

Shetani ni kiumbe yeyote aliyemuasi Mwenyezi Mungu kwa kudhihirisha uasi wake, hivyo kuna mashetani ya kijini na mashetani ya kibinadamu na ya viumbe wengine tusio wajuwa.

Hivyo Shetani siyo lazima awe jinni, na wala si kila jinni ni shetani, wapo majini ambao ni wacha Mungu.

Wale malaika wawili waliofanywa waishi kama binadamu walifeli mtihani kwa kutofanya uadilifu kwa hukumu fulani ambapo walimpendelea mtu aliye na makossa kwa sababu ya mahaba maana walipewa matamanio, hivyo Mwenyezi Mungu amewaadhibu kama ambayo walipenda iwe, baada ya kupewa uhuru wa kuchaguwa waadhibiwe hapa Duniani hadi siku ya mwisho wa maisha yao au waachwe waendelee kuishi hadi siku ya hukumu nao wahukumiwe kama binadamu wengine.
***

Basi baba, usiku ule ikabidi nifanye safari ya kwenda Umbirikimoni kwa mara nyingine kwa ajili ya kuchukuwa miti shamba ambayo ingemtibu yule binti. Ni kwamba kuna harufu ambazo majini kwa jinsi walivyoumbwa hawazipendi, moja majani ambayo hawajapendi ni mmea uitwao “mlangajini”, hii mimea ipo upo kwa wingi maeneo ya pwani, majini pia hawapendi harufu mbaya ingawaje kuna specie ya majini wanaokula vinyesi na makazi yao ni chooni na sehemu zenye uvundo uvundo. Majini walioasi ni waongo waongo sana, anaweza kujifanya ametoka na kumwachia huru mwanadamu kumbe yupo, wengine hujifanya wapo wengi kumbe yupo peke yake ili mradi tu alete usumbufu, wengine mabubu, huwa hawataki kusema bali huandika kwa kalamu, yani unaweza kukuta mtoto mdogo wa darasa la nne kwa mfano akiwa amepandisha mashetani ataomba kalamu na karatasi na kuanza kuorodhesha vitu ama kuandika vita, tena wakati mwingine kwa lugha fasaha ambayo akiwa kawaida hawezi kuiongea wala kuaiandika, na majini wengine ni mabubu kweli. (Pazi alizidi kunifafanulia)

Nilirudi alfajiri ya Ijumaa nikiwa nimepewa ile mizizi na majani maalum kwa ajili ya kuwakera majini na maneno mengine (spells) ambayo nilifundishwa.

Jumamosi mapema walikuwa yule mama na bintiye na wateja wengine pia, basi baada ya kuwahudumia wateja wengine wa mwisho nikaanza kumuandalia dawa yule binti. Yule mama tayari nilishamwambia kuwa matibabu yake yataendelea kwa siku saba ili yakamilike.

Hapo mbezi nilishakuwa maarufu na nikawa na wasaidizi wangu watatu, mmoja ni wa kiume na wawili ni wanawake ambao ambao niliwaajiri kwa madhumuni ya usafi na kusaidia kazi ndogo ndogo hapo nyumbani. Usafiri haikuwa kipaumbele kwangu maana niliweza kwenda nitakapo bila kipingamizi.

Baada ya siku saba yule binti alipona kabisa, wakatoa shukrani zao na ujira kadri walivyojaaliawa (maana nilikuwa nimewka ndoo ya lita 18 ambapo walikuwa hela wanaweka humo bila ya hata mimi kujuwa wameweka kiasi gani ama nini) kisha wakaaga…

“Kwakuwa amepona, baada ya mwezi mmoja anaweza kuja hata peke yake ili nione maendeleo yake…” niliwaambia.

Hadi wakati huo mimi sikuwa na simu wala kuona umuhimu wake, maana nikihitaji kuongea na nimtakaye, namfuata kwa njia yangu mapema asubuhi na kuongea naye kisha narejea kwenye kazi yangu ya utabibu.

Kazi ya baba niliacha baada ya kuhamia Mbezi beach maana nilizidiwa na wateja, baba alinielewa na mama alifurahi kuwa nadhiri yake inatimia.

Kipindi chote tangia nipo kule Ilala, sikujihusisha na uhusiano kimapenzi na wanawake, badala yake nilitumia muda mwingi kufanya bada na kuwa bize na wagonjwa, wito wa yule binti safari hii (baada ya ule mwezi mmoja) haukuwa wa kimatibabu ya matatizo yake bali ilikuwa mahaba yameniingia.

Katika kuendelea kutibia kwangu nilikuwa Napata wateja wenye majini feki wengi ambao kumbe nia zao ilikuwa kuwachuna (kuwaibia kiaina) waume zao ama mabwana zao au kwa tamaa tu za kibinadamu. Hawa nilikuwa nawakataa moja kwa moja kwa kuwaambia dawa zenu hazipo kwenye fani yangu. Kuna baadhi ya wagonjwa walikuja wakilazimishwa ili wawe waganga kama ilivyokuwa kwangu, wengine kwa sababu ya bahati mbaya tu ya kuwa sehemu isostahili kwa wakati usiostahili, wengine kwa sababu ya kurogwa ma kutupiwa, wengine kwa sababu ya kimahaba baada ya kupendwa na specie ya majini wapenda ngono.

Hii specie ya majini (wanawake na majini wanaume) wakimpenda mtu basi humuandama kwa kufanya naye ngono bila ridhaa ya huyo mwanadamu kwa muda na wakati ambapo jinni huyu ataamua. Yani unaweza kuwa kwenye daladala kwa kwa mfano, ghafla jinni linamvaa binti wa watu na kuanza kufanya naye ngono, binadamu wa kawaida hawatoona lakini wataona vitendo vya huyu mgonjwa.

Wengine huingiliwa usiku wakiwa wamelala, na kuna ambao hujijuwa na kuna ambao hawajijui. Mara nyingi kwa binadamu wanawake ambao wana majini mahaba basi huzuiliwa kupata waume, na akipata hakutakuwa na amani ndani, mara mumewe asiweze kumuingilia mkewe, au akiweza basi asirudie ili mradi tu kuwe na nafasi kuwa ya jinni kufaidi ngono na huyo mtu mwanamke. Wengine huzuiliwa kupata watoto, ama akipata wanakufa ama kupotea kwa mazingira ya kutatanisha. Na kwa jinsi hii kuna watoto ambao huzaliwa na kuwa nusu jinni nusu mtu yaani mwanamke anabeba mimba ya jini. Mmoja wapo ni mimi ingawaje kesi yangu ni tofauti kidogo.

Kwa wanaume ambao hupatwa na majini mahaba nao huzuiliwa wapenzi, yaani kijana rijali anakuwa haoi, na akioa basi hafanyi sana ndani. Wengine hudiriki hata kuoa jinni kabisa na kushirikiana nao kwa mambo mbalimbali lakini watoto wanaozaliwa na majini wanawake kutoka kwa wanaume binadamu huishia kupotea kuonekana duniani ila wale wa waliokaa kwenye matumbo ya wanadamu wanawake basi huishi duniani.

Katika kuwahudumia wagonjwa, nikajifunza kumbe kuna Sehemu Rufiji kuna mcha Mungu ambaye naye anawaombea watu na mambo yao yanaenda vizuri. Nikatamani sana nifike huko lakini sijui ni kusahau ama kuzidiwa na wateja, sikupata kwenda kutembea huko hadi mwaka mmoja uliopita.

**********

Inaendelea...
NITAENDELEA BADAE NAWEKA NUKTA
 
16. MAISHA MAPYA na UHURU - Ω

“Nakuusieni na kuihusia nafsi yangu juu ya kumcha Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu (aliye takasika), … hiki (Qur’an) ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na muongozo kwa wale wamchao …”

“Sisi waislamu, tuna miongozo miwili, Qur’an na Sunna. Qur’an ni maneo ya Mwenyezi Mungu na Sunna ni matendo na mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimwendee).”

“Tushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadithi za Mtume, hatuwezi kupotea.”

Hayo yalikuwa maneno ya Walii (kipenzi) wa Mwenyezi Mungu wa Utete Rufiji (kama wenyeji walivyokuwa wakimwita) wakati akinukuu aya kutoka Qur’an akiwa anatujenga kiimani.

“Katika hii Qur’an Mwenyezi Mungu ameweka elimu ya toka watu wa mwanzo mpaka watu wa mwisho, elimu zote zimo ndani ya Qur’an, historia imo, mawaidha yamo, mifano imo, visa vimo, hesabu zimo, utaratibu wa kuendesha Dunia umo ndani ya Qur’an na hiki kitabu huhifadhi waumini kwa fitina iliyomo humu duniani…” aliendelea

“Ndani ya Qur’an kuna habari za watu waliokuwepo kabla yetu, kuna habari za watu baada ya sisi kuondoka, ni hakimu baina yetu na ni upambanuzi juu ya mambo mbalimbali. Haifai kuiacha.”

“Hii Qur’an ajabu zake hazimaliziki, wana zuoni hawashibi, kila siku wanatoa faida na hata majini walipoisikia Qur’an inasomwa, wakasema hakika sisi tumesikia Qur’an ya ajabu, … inaongoza kwenye uongofu kwa hiyo tumeiamini na wala hatutofanya ushirikina…, na kwa hakika utukufu wa Mola wetu mlezi umetukuka kabisa,… hana mke wa mwana…, … na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uongo uliopindukia juu ya Mwenyezi Mungu… nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamsingizii uongo Mwenyezi Mungu…,”

Aliendelea yule mcha Mungu tutupatia mawaidha kupitia kitabu kitukufu Qur’an na kutusimulia habari za majini jinsi baadhi walivyo mrejea Mwenyezi Mungu na wengine waliendelea kukengeuka.

“Eee umesema mmetoka Bagamoyo!” aliuliza yule Walii,

“Rudini huko, kuna Sheikh Mkubwa Zawiani, utapata muongozo na elimu kadha wa kadha, kikubwa shikamaneni na hiki kitabu wala msikiache.” Alimaliza yule Walii na tukaagana na kuanza safari ya kurudi.

Nilikuwa mimi na mke wangu Behat, tulilala Rujiji Ikwiriri na siku ya pili tulifika Dar na moja kwa moja kwenda Bagamoyo.

Bagamoyo pale Zawian tukaambiwa tuende Lushoto kumtafuta Shariff Badowo ili atufanyia maombezi makubwa kabla ya kurudi Zawiani kwa ajili ya kumalizia elimu nasihi.

Tulienda Tanga, tukafika nymbani kwake lakini tukaambiwa amesafiri kwenda Mombasa, tukaambiwa tumtafute kijana mmoja pale Horohoro atatusaidia kufika kwake.

Yule kijana alikuwa ni mfanyakazi wa mabasi ya Modern (Mombasa – Tz – Zambia nk), alikuwa anaitwa Sarojo, alitusaidia sana hadi tukafika kwa Shariff Badowo na kufanya dua kubwa kubwa sijapata kuona na tulivyorudi Zawiani tulikuwa na utulivu mkubwa.
*********

Tukiwa Zawiani – Bagamoyo

“Tatizo lenu mlivyokuja mara ya kwanza hamkutaka kunisikiliza kwa kituo, wewe na kaka yako wote mlikuwa na haraka haraka kiasi cha kutopata yote ambyo nilitaka kuwaambieni.” Alikuwa anaongea Sheikh Mohamed kwa sauti yake nzito iliyojaa umwinyi mwinyi hivi kwa kutulaumu kiaina…

“Sasa ulivyorudi na kuniambia kuwa umepona, nikadhani labda umejuwa asili ya shida yako na kutatuliwa ipasavyo…” aliendelea…

“Kumbe bado kwa maoni yangu, ulikuwa kwenye safari ya kujijuwa na kujitambua… na sasa kwa vile umefikia hatua hii basi ukae kitako nikuelimishe…” alisema.

“Mwenyezi Mungu alituumba ili tumuabudu yeye, tena yeye tu na wala tusimshirikishe na miungu mingine, hayo ndiyo malengo hasa ya sisi kuumbwa, hata maumbile yetu yamewekwa kurahisisha zoezi hilo la kumuabudu yeye”

“Tukimuabudu yeye hatumuongezei chochote, na tusipomwabudu hatumpunguzii chochote, YEYE ambaye hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ile YEYE, Yu hai na ni wa kudumu, halali wala kupatwa na usingizi. NDIYE Mola wa Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina yake…”

“Anajuwa yaliyochificha mbele na nyuma, na katika sisi viumbe hatuna tujuwalo ama hatuwezi kujifunza (kupata elimu) ila kwa kuridhia kwake, na utukufu wake umeenea Mbinguni na ardhini na wala hawezi kushindwa kuvilinda viumbe vyake maana yeye ametukuka (aliye juu) na NDIYE MKUU.” Alisema Sheikh kisha akasoma aya katika mpangilio wake.

Alivyoanza kusoma nami nikakumbuka kile kikaratasi nilichopewa Kikokwe niwe nasoma mara kwa mara, maneno hayo yalikuwa sehemu ya dua ile niliyopewa huko.

Sheikh aliendelea na risala…

“Katika uumbaji wake (Mwenyezi Mungu) aliumba viumbe mbalimbali, na kila kiumbe kina mamlaka yake na mipaka yake katika kuyaendea mambo…”

Akatoa mifano mbali mbali jinsi viumbe wengi wanavyoishi humu duniani ikiwemo wadudu, hayawani na hatimaye majini na binadamu.

“Binadamu ndio tumepewa uhalifa (uongozi) katika dunia hii, yani tunatakiwa tuweze kuitawala dunia ipasavyo…”

“Majini nao wana tawala zao, wana mataifa yao, wana makabila yao, wana koo zao, wana mila zao na desturi zao, na wamepewa uwezo mbalimbali lakini pia wamewekewa mipaka…”

“Haifai kwa Majini kuingia kwenye tawala za kibinadamu na kuwasumbua watu kwa kuwapagawisha, kuwatia maradhi ama eti kujifanya wanawalinda…”

“Wao wana ‘ulimwengu’ wao na sisi binadamu tuna ‘ulimwengu’ wetu…”

“Hivyo ni makossa makubwa kwa Jinni kumuingia mwanadamu kwa namna yoyote ile kwa visingizio mbalimbali…”

“Idadi ya majini ni kubwa mara nyingi sana kuliko wanadamu, na kwa kuzingatia kuwa wao wanaishi muda mrefu kuliko wanadamu basi wingi wao huongezeka mara kwa mara kiasi cha kutapakaa duniani kote… kwa wingi wao huo hata kila mwanadamu aliye hai muda huu akikusanya majini sabini kila mmoja, basi binadamu wote watakusanya na wengi sana bado watabaki hawajakusanywa”

“Kuna elimu mbalimbali za kuweza kuwamiliki hawa majini, lakini ni moja ya elimu zilizokatazwa kwa kuwa hatimaye huleta hasara badala ya faida…”

“Lakini kwa kuwa Duniani humu kuna fitina mbalimbali ikiwemo fitna ya afya, mali, wake, waume, watoto nk basi baadhi ya watu hupatwa na husda, chuki na vijicho ambavyo huwadhuru wenzao, na kazi zote hizo hufanywa na hao majini ambao wameasi kwa kushirikiana na binadamu kwa namna mbalimbali za elimu ya kichawi”

“Elimu ya kukabiliana na matatizo hayo pia ipo, ipo kwa njia nyeusi na kwa njia nyeupe…”

“Hivyo tiba zipo, lakini kuna tiba kwa njia sahihi na zipo tiba za kwa njia ya kishirikina”

“Kufanya ushirikina na moja ya dhambi ambayo kama ikitokea umekufa bila ya kutubu basi ni dhambi isiyo sameheka labda kwa rehma zake Mola wetu maana yeye ndiye mjuzi zaidi”

“Hivyo basi ushirikina HAUFAI mbele za Mwenyezi Mungu”

“Kwakuwa tiba sahihi zipo, basi yatupasa kufuata tiba kwa njia zilizoelekezwa kwa miongozo ya dini yetu”

“Tiba isiyo sahihi utaijuwa kwa masharti yake ambayo hatimaye yanakupelekea katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa namna zote nne, kuwaza, kunena, kutenda na kutotimiza wajibu…”

“Sasa kwa kuwa ninyi mliamua kuishi kama binadamu…”

Tukawa tunaangaliana na Behat…

“…yafaa muendelee kuishi hivyo na kufuata maamrisho na makatazo yote ambayo yapo katika muongozo wa Qur’an na Sunna…”

“Pazi…!” aliniita Sheikh

“Mwenzako ana kiumbe tumboni…”

Nikawa manuangalia Behat tumboni sioni kitu zaidi ya ‘flat screen’ (hakuwa na hata kijitambi kidogo)

“Atazaliwa kiumbe ambaye sasa atakuwa mwanadamu kamili, wanenu hawatokuwa na passport ya kuingia Ujinini kama ilivyo kwenu hivi sasa ingawaje bado mpo nusu jinni.., wewe Pazi ni nusu binadamu nusu jinni na huyo mwenzako ni nusu jinni na nusu binadamu…”

Moja kwa moja nikaelewa tofauti yake kwa mmoja wetu alilala kwenye tumbo la uzazi binadamu ilhali mwingine alila kwenye tumbo la uzazi jinni.

Aliendelea kutupa risala pale weeee mwisho akasema…

“Tafuteni njia halali za kupata rizki zenu, hata kama itakuwa ni kutibu watu basi uifanye tiba iliyo sahihi kwa njia za kisunna (yaani kwa njia ya mafundisho ya Mtume Muhammad, Rehema na Amani zimwendee)

“Kitu kingine muhimu sana ni kwamba haifai kubeza dini nyingine, mfano hawa wenzetu wakristo tunaishi nao humu mjini, majumbani na kupeana heshima za kibinadamu, Kuna Kanisa kubwa kule Mantep (Sikuhizi wanaita ADEM), kuna Kanisa dogo kule miembe safa (jirani na kushukia MSALABANI) na kuna Kanisa kule Mwanakalenge. Hawa ni binadamu wenzetu na wana Imani yao thabiti katika kumwabungu Mungu wao kwa mujibu wa mafundisho yao, ukumbuke kuwa hawa pia kiongozi wao alipewa Kitabu kama ilivyo Qur’an kwa sisi. Usiwabeze wala kudharau Imani zao maana kuna wengine huenda wakawa bora mbele ya mwenyezi Mungu kuliko baadhi yetu, lakini haikatazwi kuwalingania ili waje katika uislam, tena kwa lugha iliyo nzuri na staha.”

“Kumbuka hata Nabii Mussa (Rehema na Amani zimfikie) alipoambiwa akamlinganie Firauni (Farao) aliambiwa akazungumze naye kwa upole licha ya kufuru kubwa aliyokuwa akiifanya. Kazi yetu ni kufikisha ujumbe lakini kumuongoa mja siyo kazi yetu, Allah mwingi wa Rehema sisi sote ni viumbe vyake, tusijitie ukiburi, YEYE Allah huamua atakavyo.”

Aliendelea…

“Vitabu cha elimu hiyo ya tiba zipo, vitafute ujifunze kwa walimu ukihitimu uendelee na tiba halali, kama hutoweza basi rejea kwenye kazi ya baba yako, ameshazeeka sasa afaa kusaidiwa sana…”

Alimalizia risala yake kwa kutusihi kuwa sisi bado ni nusu watu nusu majini, hivyo kiasili tuna nguvu za kijinni basi tuwe makini na maneno tuyasemayo na kujitahidi kujizuia hasira zetu maana huenda zikawa na athari kwa binadamu wa kawaida.

Tulirudi nyumbani na kumkuta mama akitusubiri kwa hamu.

“Enhe, mmeambiwaje huko?...” Mama aliuliza kwa shauku

Tukamwelezea yote na hatimaye mimi na mke wangu tukaamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwalingania watu katika dini huku nikiendeleza kazi ya Baba.

“Nadhiri yako sasa Mama inaenda kutimia…” nilisema.

Baada ya siku tatu, tuliaga kurudi Dar es Salaam kuendelea na maisha.

Leo hii tuna watoto watatu, tunaendeleza kazi ya uvuvi na uchuuzi kwa njia za kisasa, Baba na mama walishafariki, mama mkubwa pia alishafariki.

Tukapata Chakula cha mchana pamoja, kisha akanisindikiza nami nikachukuwa njia ya kurudi kwangu Upanga.

Jumamosi ile ilikuwa tulivu lakini nyumbani kwangu hapakuwa hivyo, nilikuta mke wangu amenuna, lakini nikamwambia hebu baada ya kula uje chumbani nimsimulie kisa chote nilichosimuliwa….
*******

Hakutaka nilale bali nimmalizie kisa chote maana muda tayari ulikuwa umeshaenda sana na siku Jumapili ilikuwa ndio inaingia (kwa mujibu was aa za na kalenda ya Gregori)…

Nilimkidhia haja yake baada ya kuona amevutiwa pia na kushangazwa japo kwa kuifupisha.

Mwishowe tuliendeleza ‘libeneke’ la mume na mke.

**************** MWISHO*************

Update!

Sheikh Mohamed alishafariki, Mzee Zahiri naye, Mwalimu Mwaloki, Mzee wa tiba Mlingotini, Mzee Njembi, Mcha Mungu wa Rufiji, Shariff Badowo, Shariff wa Kikokwe wote wametangulia mbele za haki.

Watu wengine ambao wametajwa katika simulizi hii sina update zao.

Imenibidi nifupishe ili niende na muda-huru niliokuwa nao maana ni mchache.

Niliamua kushea nanyi kisa hiki kama kumbukumbu ya kukumbuka uwepo wa Pazi na familia yake hapa Duniani kwa maana ya kwamba ile familia yote ilifariki kwa kuzama baharini miaka kumi na moja na siku arobaini na nane hivi ziliyopita walipokuwa wakitokea Unguja kuelekea matembezini Pemba kwenye MV. Spice Islander.

**********

Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwa hakika kwake tutarejea.

Mkuu stori nzuri sanaa, Hongera sana kwako, btw ni kisa cha ukweli kbs au??
 
Kwa waangalia filamu kaangalieni filamu inaitwa "Three Thousands Years of Longing" ya 2022, Idris Elba ndani, mtapata kujua zaidi kuhusu Majinni.
 
Back
Top Bottom