Hatimaye nipo huru

Hatimaye nipo huru

6. SAFARI IKAANZISHA SAFARI NYINGINE

Baada ya kukutana na Shariff hapo Kikokwe, tulimueleza historia nzima ya maradhi na matibabu tuliyopata. Hakufanya tiba yoyote bali alisema tupunzike hadi usiku wa manane ataamka kufanya dua.

Baada ya chakula cha jioni na mazungumzo ya kawaida ya hapa na pale tulielekezwa sehemu ya kulala, mimi na Shangazi tulipewa chumba chetu na wengine wakapewa chumba chao, wote tulilala chini kwenye magodoro ya sufi. Binafsi nililala usingizi mzito sana, na kuamka wakati jua limeshachomoza, shangazi naye vivyo hivyo na hata wale tulioambatana nao walilala fofofo.

Baada ya kujimwagia maji na kupewa kifungua kinywa ndipo yule Shariff akatuita sebuleni na kutuambia aliyaoyaona baada ya dua.

"Tumeambiwa kwamba huyu kijana anatakiwa aende upande wa magharibi ‘jua linapozamia’, huko atapata tiba yake sahihi maana maradhi yake si ya ukanda huu.

Niliposikia maneno haya nikakumbuka maneno ya Sheikh Mohamed kuwa maradhi yangu ni ya bara, nikaanza kuelewa, nikakumbuka kwamba pia mzee wa tiba Mlingotini naye alisema kuwa milango imefunga, na imeegemea magharibi. Hapa tena tunaambiwa jua linapozamia.

Tukazidi kumhoji yule Shariff akasema hajui zaidi maana taarifa hiyo ilikuja kama sauti wakati akifanya ibada zake.

Sote pale tukachoka na kuomba kurejea Tanga mjini na wala hatukutaka kuhangaika kwa matabibu wengine.

Shariff hakudai chochote na badala yake aliandika maneno machache ya kiarabu (dua) na kunipatia na kunitaka kila siku nisome kabla ya kulala.

Tukarudi Tanga mjini na kesho yake tuliamua kurudi Bagamoyo ili kupeleka ripoti ya yaliyojiri.

***********

Baada ya kikao cha Bagamoyo, ikaonekana Shangazi anunuliwe simu na Baba naye anunue simu kwa ajili ya kuwasiliana kupeana taarifa.

Wakati huo kampuni ya Mobitel walikuwa tayari wameweka minara yako baadhi ya sehemu nchini.

Zilinunuliwa simu mbili kwa bei ya milioni mbili na laki 2.

Wakati huo simu hazikuwa na simcard na hazikuwa za kuweka vocha (dollar) kama ilivyokuwa baadaye baada ya mabadiliko ya teknolojia na kuingia kwenye gsm. Ilikuwa na mwendo wa analogy.

Hadi muda huo tayari gharama kubwa ilishakuwa imetumika katika safari ya kujaribu kunitibu matatizo yangu ambapo hadi muda huo pia ufumbuzi thabiti ulikuwa haujapatikana.

Kwenda Magharibi tukafikiri ni kwenda Kigoma.

Tukapanga safari ya kwenda huko bila kujuwa tunaenda sehemu gani haswa. Lengo likawa kwanza kufika Kigoma. Tulikata tiketi daraja la pili tukiwa watu wanne, Shangazi, Mama na Kaka mkubwa.

Safari ilianza mida ya alasiri kutoka Dar es Salaam. Ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kupanda treni, pia ikawa mara yangu ya kwanza kuvuka nje ya Morogoro kuelekea bara.

Tulifika Dodoma kesho yake saa mbili hivi asubuhi. Wote tulikuwa tumejawa na mawazo hivyo mazungumzo kwenye treni hayakuwa yanaunganika .

TT alivyopita kukagua tiketi alishangaa kukuta kuna jinsia mchanganyiko kwenye chumba chetu, nadhani walikuwa hawaruhusu mchanganyiko wa wanawake na wanaume isipokuwa kama ni watoto au mke na mume. Baada ya Mama kumuelezea suala langu na kwamba ni familia moja alielewa na kwenda zake.

Tabora tulifika kesho yake tena mapema sana asubuhi na tulikaa hapo kwa muda mrefu tukisubiria mgawanyo ili mabehewa ya kwenda Mwanza yatengwe na yale ya kwenda Mpanda na Kigoma yatengwe.

Baada ya ucheleweshwaji kwa muda mrefu hatimaye tuliondoka na kufika Kigoma siku ya pili.

Siku hiyo tulilala papo hapo Stesheni maana hatukujuwa pa kuanzia

Simu ya Shangazi ikawa kopo tu maana ilikuwa haitumi ujumbe (hakukuwa na huduma hiyo) wala kupokea mawimbi ya sauti. Hakukuwa na mtandao wa simu wakati huo Kigoma.

Baada ya kutulia ndipo akili ikamjia Shangazi kuwa tutafute soko lilipo. Hapo tungepata taarifa muhimu kuhusu mueleko wa safari yetu.

Bahati nzuri soko halikuwa mbali kutoka stesheni, ni mwendo wa chini ya dakika 10 tu tena mwendo wa akina mama.

Sisi tulibaki pale stesheni na shangazi akaenda sokoni.

Alivyorudi alikuja na majibu ya kuwa inatubidi tuende Ujiji.

Tukapata mwenyeji wa kutupeleka Ujiji, tulikodi teksi maana palikuwa na kaumbali kiasi tusingeweza kwenda kwa miguu na akina mama na hali yangu ilivyokuwa.

Tukapelekwa hadi kwa Mzee Njembi, mganga maarufa sana hapo Ujiji jirani na soko waliloita la Kagera.

Baada ya maelezo marefu ya safari ya tiba yetu, yule Mganga akasema Karibuni Kigoma, jisikieni mpo nyumbani. Akasema ataanza matibabu baada ya jua kuzama.

Ilipofika saa mbili usiku jua likawa limezama, na akaja sebuleni kuniuliza majina yangu.

"Naitwa Pazi bin Mkila" nilisema.

Mganga akauliza tena, " Baba yako anaitwa nani? "

Nikamjibu anaitwa Mkila Mkila.

Kisha akaniuliza mama yangu anaitwa nani nikamtajia.

Mganga akatuambia tupumzike tuwe na amani, yeye atatupatia matibabu baada ya vikao. Sikielewa ni vikao gani lakini ilibidi kukubaliana na hali kwani tulishayavulia nguo maji, inabidi tuyaoge.

Asubuhi baada ya kifungua kinywa akatuita nje kibarazani. Tukakaa kwa pamoja na kuanza kuzungumza. Huyu mganga alikuwa mpole na sauti yenye huruma, nadhani ilikuwa ni lafudhi tu ya watu wa Kigoma ama yote mawili.

Akawa anamuangalia sana Mama yangu na kumkazia macho, kisha akamuuliza...

"Mama, huyu ni mtoto wako wa ngapi?"

Mama akamjibu "Wa saba baba, huyu ni wa saba, nina watoto wa kike watano na wawili wakiume. Wa kwanza huyo hapo" alijibu kwa kirefu huku akimuoneshea kidole kaka mkubwa.

"Inaonekana mama uliweka nadhiri kabla ya kushika uja uzito wa mtoto wako huyu, je unakumbuka? " Aliuliza mganga.

Mama aliinamisha kichwa kwa muda kisha akainua na kuanza kusema.

"Ni kweli niliweka nadhiri lakini nilisahau, ni zaidi ya miaka ishiri sasa tangia niweke hiyo nadhiri, hii ilitokea baada ya mimba mbili kutoka mfululizo kabla hazijafikisha miezi mitatu, ndipo katika kuhangaika nikawa katika ibada zangu za kutembea tembea peke yangu ufukweni mwa bahari nikajisemea kuwa nikipata ujauzito na nikifanikiwa kuzaa mtoto wa kiume basi nitamtoa wakfu."

Wakfu ni kama vile kusema kutoa mali kwa ajili ya kutumikia Dini.

"Je ulimsomesha dini." Mganga aliuliza.

"Hapana baba, alisoma ‘chuo’ tu, anajuwa kusoma kwenye juzuu ya thelathini tu, juzuu Amma" alijibu mama.

Chuo kwa mukhtadha huu ni shule ya elimu ya awali katika kuweka misingi na kufahamu kusoma na kuielewa Qur’an na mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimwendee)

Baada ya mama kufunguka pale ndipo wote tukaanza kupata mwanga wa asili ya maradhi yangu.

"Basi mama, yakupasa kutimiza nadhiri yako," alisita kidogo kisha akaendelea.

"Lakini inaonesha safari ya huyu kijana bado ndefu, hapa siyo sehemu sahihi kwake, inatakiwa avuke maji aende magharibi zaidi." Alitulia kisha akaendelea kusema.

"Sijapata muelekeo wa huko magahribi lakini najuwa wapi mtaweza kupata maelekezo ya njia ya kupita"

"Kesho asubuhi nitakujibuni panapo majaaliwa" alimaliza na kuendelea na shughuli nyingine.

Nasi tukapata wasaa wa kutembezwa Ujiji na kufika hadi mwaloni kuona ziwa Tanganyika.

Siku ikapita, tukalala. Tena tulilala vizuri bila ya rabsha yoyote.

Asubuhi baada ya staftahi tuliitwa tena na Mganga, kisha kasema…

“Nimepata njia mtakayotumia, lakini ni njia ndefu ya mzunguko” alisema Mzee Njembi, kisha akaendelea…

“Inabidi mvuke ziwa Tanganyika, lakini mkianzia hapa Kigoma itakuwa hatari kwenu, mnaweza msivuke salama. Kuna muingiliano sana wa malmaka” alisita kidogo…

Sisi tukawa tunaangaliana, moyoni nikawa nawaza, huo muingiliano wa namna gani kiasi kwamba sisi tushindwe kuvuka. Kulikuwa na usafiri wa meli na na boti za wavuvi ziendazo Zaire, sasa kwa nini tupitie njia ya mzunguko… niliwaza kichwani pamoja na mambo mengi kama ya hayo ya vikao vikao na jinsi apatavyo taarifa nk.

“Inabidi muende Mpanda, huku mtafute nja ya kufika badari ndogo ya Kabwe, hapo kuna vyombo vya kukuvusheni salama na ni pafupi kufika upande wa Zaire” Mganga alikuwa akiongea kwa kukatisha katisha lakini alionekana ana uhakika wa alisemalo.

“Msiende kwa njia ya basi Mpanda, ni fupi lakini pia siyo salama, rudini kwa treni hadi Tabora kisha mtapata treni itakayo wafikisheni Mpanda” Alisema.

Hatukuwa wa kuhoji maswali maana ilionekana bado hajaweka kituo katika kuongea kwake.

“Kutoka Mpanda sasa mtapanda basi za Sumri na kukuvusheni Mbugani hadi Lyazumbi ambapo kuna njia ya mkato kufika huko bandarini” aliongeza.

“Mkifika hapo Bandarini ‘Kabwe’ ulizieni boti ya nahodha aitwaye Ustadhi, mara nyingi boti yake hushushia mizigo bandari ya Mutindi upande huo wa Zaire, na kama mtampata mwenyewe, mwambieni mmeagizwa na Mzee Njembi, atakusaidieni zaidi.” Aliweka kituo.

Nikaiwaza hiyo safari kwa mzunguko huo, niliona shughuli ipo, lakini ndiyo maradhi tena yamenishika hakuna jinsi.

“Baba usidhani kila aendaye kwa waganga ni mshirikina, wengine ni maradhi tu yanawafanya watapetape na mwisho kujikuta wamezunguka kwa waganga wa sehemu nyingi na wakati mwingine bila kupata ufumbuzi wa uhakika.” Alisema Pazi

Mzee Njembi aliendelea kutoa maelekezo marefu huku mimi nikishangaa anajuwaje yote haya na hatimaye alimaliza na ikabidi tuage kuelekea Kigoma mjini kuangalia usafiri wa kusika Tabora.

Kwa bahati nzuri tulipata usafiri kwa gusi (goods) (treni ya mizigo) iliyokuwa inaelekea Tabora. Tuliondoka usiku na tulifika Tabora asubuhi na mchana wake tukaunganisha kwenda Mpanda.

***********

Tulivyopata kifungua kinywa palepale stesheni, Shangazi akasema tumsubiri ili aende Polisi ili atume ujumbe kwa njia ya simu ya upepo Bagamoyo.

Shangazi alikuwa mjanja mjana mwingi wa kujuwa mambo.

Mida ya mchana Shangazi alirudi na kutuambia ameshafanya booking ya tiketi kwenye Sumry na ameshatuma ujumbe Bagamoyo kwa njia ya “Police Message”

Tulitembea kwa miguu huku kaka mkubwa akiwa na kibarua kikubwa cha kubeba mabegi taratibu hadi tukafika kwenye ofisi za Sumry.

“Polisi paleeee” alisema Shangazi huku akionesha kidole ulekeo palipo hiyo polisi.

Kumbe hapakuwa mbali na ofisi za Sumry. Tulishinda hapo na kula hapo na kulala hapo hapo. Hatukuwa peke yetu bali kulikuwa na wasafiri wengi na makabila tofauti, nilijuwa hivyo kutokana na lugha zao walivyokuwa wanaongea.

Saa kumi na moja tulikuwa tayari macho, na basi letu lilikuwa tayari limeegeshwa hapo, kulikuwa na mabasi ya kwenda Sumbawanga, Tabora na kwingine.

Saa kumi na mbili na dakika chache gari ikaanza safri ya kuelekea Sumbawanga, hali ya barabara haikuwa rafiki hivyo tulitumia muda mwingi njiani hususani eneo la mbuga ya wanayama Katavi hadi tulipotokezea Lyamba-lya-mfipa ambapo ilibidi baadhi ya abiria wapungue kwenye gari ili gari kuweza kupanda mlima vizuri.

Baada ya kupanda mlipa huo, hali ya hewàa ikaanza kuwa nzuri, kaubaridi kiasi na njia haikuwa mbaya sana, hadi tunafika Lyazumbi tayari ilikuwa muda wa kula chakula cha mchana.

Sisi tukashuka na mizigo yetu, na baada ya kula tukaanza kuulizia jinsi ya kufika Kabwe. Tukapata usafiri wa gari ya kudandia ya kubeba mizigo na ikatupeleka hadi Kabwe.

Hapo kabwe tukaulizia boti ya ustadhi na kuelekezwa nyumba fulani jirani na mwalo.

“We mtoto hujambo?” aliuliza shangazi alipomuona mtoto wa miaka saba-nane hivi akipita.

“Taiutuu… asanteeeeee” alijibu yule mtoto huku akinyenyekea kama anataka kuchuchumaa .

Shangazi akaona hapa ni lugha gongana, akaamua kumsogelea mtu mzima kidogo aliyekuwa jirani na kumsalimia.

“Shikamoo mama” Shangazi alisalimia

“Malaabaaaa mwalindauliiiii” yalikuwa majibu ya yule bibi

“Ustadhi, ustadhi” Shangazi akajiongeza

Bila shaka na yule bibi akajuwa hapo hawajaelewa.

Ni kawaida sana watu wa kanda hiyo kusalimiana kwa muda mrefu na kuwa kuvuta maneno, neno ahsante pia likiwa ni sehemu ya salamu.

Yule bibi akaonesha kidole kushiria kwa ustadhi ni pale, kumbe palikuwa ni nyumba mbili tu mbele. Tukasogea hadi pale na kukaribishwa hadi ndani. Kumbe mida hiyo tuliyofika vijana wengi tayari walikuwa maeshaenda kuvua hivyo hapo kijijini walibakia watoto na watu wazima sana.

Tulikaribishwa na dada mmoja na baada ya shangazi kusema tumeelekezwa na mzee Njembi akatuchangamkia na kutukaribisha ndani.

Shangazi akajieleza weeee na mama pia alichangia, kaka mkubwa hakuwa muongeaji sana. Yule dada ambaye baadaye nilijuwa kuwa ndiye mke wa Ustadhi alitusikiliza kwa makini kisha akasema tu karibuni.

“Ustadhi anatarajia kuingia alfajiri kutokea ng’ambo.” Alisema yule dada kwa lafudhi ya Kirangi.

Tuliandaliwa chakula na sehemu ya kupumzika.

*********

Inaendelea
 
7. KUVUKA ZIWA TANGANYIKA

Alfajiri tulikisia vishindo vishindo vya mtu kurudi, lakini hatukuamka hadi palivyokucha kabisa. Tulivyopata staftahi tuliendelea na mazungumzo ya kawaida na mke wa Ustadhi wakati tukisubiri Ustadhi mwenyewe aamke maana alikesha safarini.

Majira ya saa tano na nusu hivi asubuhi Ustadhi alitoka nje na kuja kutusabahi.

“Assalaam aleikum, habari za huko mtokako, poleni kwa safari na karibuni sana Kabwe” alitusalimia salamu ndefu.

Tuliitikia kwa pamoja na kisha akaomba aletewe chai pale nje huku akianza sasa kuongeza na sisi kwa kutusikiliza.

Kama kawaida Shangazi alianza kumuelezea sababu ya safari yetu kwake, kwamba atusaidie ili tuweze kufika huko upande wa pili na wala hatupajui wapi hasa tunapotakiwa kwenda. Alimpa salamu kutoka kwa mzee Njembi…

“Alituambia tukikuona wewe basi safari yetu itakuwa salama na tutafika tuendako” alimalizia Shangazi.

“Sawa karibuni, wa aleikum salaam wa rahmatullah wa barakatu” aliitikia salam ya kutoka kwa mzee Njembi.

“Aaah ni kweli mimi nina chombo changu ambacho nakiendesha mwenyewe, na kazi yangu kubwa ni kupeleka matufa ya wateja wangu upande wa pili. Napeleka petroli, dizeli na wakati mwingine mafuta ya kula na ya kujipaka”

“Ni kazi ambayo nimeifanya kwa muda mrefu tangia kijana mdogo nilipokuja huku kutafuta maisha kutokea Irangi Kondoa”

“Kwa uzoefu nilionao ndiyo maana mzee Njembi ameniamini sana hata katika kumsaidia katika mambo yake mengine binafsi. Nilifahamiana na mzee Njembi siku chache tu baada ya kukabidhiwa chombo niwe nahodha kamili”

“kabla ya hapo nilikuwa nahodha msaidizi lakini kwa bahati nzuri tajiri mwenye chombo alinunua boti nyingine ya kisasa hivyo yule nahodha akapewa chombo kipya nami nikapewa chombo cha zamani”

“Sasa kumbe nisijuwe kuna baadhi ya watu wenyeji wa hapa hawakupenda mimi nipewe kile chombo badala yake wapewe watoto wao. Kwa sababu hiyo nilisumbuliwa sana na mauzauza ya kienyeji hapa, japokuwa nami niliaga kwetu Kondoa lakini haikufua dafu, ikabidi nianze kutafuta msaada”

“Katika kuhangaika kwangu ndipo nikakutana na Mzee Njembi kule Ujiji, hakika alinisaidia sana kiasi kwamba nilivyorudi nilifanya kazi vizuri tena kwa ufanisi na bila bughuza zozote kama za mwanzo licha ya majaribio yao kadhaa ambapo matokeo yalikuwa yanarudi kwao”

“Watu wakaanza kuniita ustadhi ustadhi, kumbe walisemezana wao kwa wao kuwa wamemchezea ustadhi sasa mambo yao hayaendi, na uaslama wao ukawa baada ya kuacha kunisumbua” Alisema kwa kirefu Ustadhi.

“Jina langu halisi ni Muharami bin Said ibn Kassim Chavai, lakini ukiulizia Muharami mji huu huwezi kunipata, we sema ustadhi tu, kila mtu hapa ananijuwa”

“Hebu fikiria, usiku mnalala asubuhi mnajikuta mpo nje barazani mmelala! Siku nyingine mnajikuta ufukweni kabisa mwa ziwa miguu ikiwa inagusa maji kidogo! Siku nyingine wote mkiamka mnakuta mmechanjwa mchirizi mmoja mgongni au kifuani, mchirizi mrefu lazima uuone au mwenzako auone! Siku nyingine unapotea tu ziwani hufika bandarini hadi unaishiwa mafuta uliyopanga kutumia! Siku nyingine unakutana na dhoruba isiyo na kichwa wala miguu yani unashangaa ghafla tu wimbi hili hapa tena mengine yanakuja dabodabo (double double)” Alituambia na kuendelea…

“Hebu niambie, wewe ungefanyeje!” aliuliza. Sisi hatukujibu kitu.

“Nilijaribu kutumia njia ninazozijuwa weee lakini haikuwezekana, nimezunguka Rukwa ya Mpanda, Rukwa ya Upimbwe, Rukwa ya Sumbawanga, Rukwa ya Unyika (siyo Unyiha), Rukwa ya Laela hadi sehemu iitwayo Mkutano jirani na Kijiji cha wachawi sikufanikiwa, maana ilikuwa inaoneka kama wote ni timu moja tu ndipo nikaanza kuhangaika kutafuta msaada nje ya mkoa huu wa Rukwa.” Alimalizizia chai yake kisha akaendelea…; wakati huo sisi tupo kimya tu tunasikiliza na kujifunza kumbe siye Pazi tu anayehangaika kutafuta kwa tabu.

“Nikaenda Kusini Mtwara jirani na Msumbiji, kule yule bibi akaniambia nimepata tabu bure kwenda huko, nigeuze niende Kigoma Ujiji pale wanapawezea Rukwa” Alisema.

Hapa sasa nikaendelea kujifunza kumbe mambo haya ya nguvu za giza zina madaraja, mipaka, mamlaka na utimu. Ama kweli unaweza ukaishi duniani na usijuwe chochote kinachoendelea katika mambo ya nguvu za giza. Vitu vinatisha sana. Nikakumbuka jinsi nilivyo pelekwa mzimuni kule Handeni na kuzungumza na viumbe visivyoonekana lakini kwa kupitia vinywa wa watoto! Sita kaa nisahau.

“Kwa mzee Njembi nilipikwa kwenye chungu cha maji moto yasiyounguza na kutengenezewa ulinzi kwa kadri mahitaji yangu yalivyokuwa na kushida majaribu ya kutisha kutoka kwa ulinzi huo, hatimaye nikawa salama na hadi leo wananiita ustadhi, siyo kwa mazuri bali kwa shughuli waipatayo pindi wakiazimia kunifanyia ubaya.” Alisema.

“Kazi zangu zilienda vizuri hadi miaka michache iliyopita nikanunua chombo changu binafsi na ndipo mzee Njembi akaanza kunitumia kumchukulia miti shamba (dawa) kutoka Zaire. Bahati mbaya ng’ambo huko kuna hatari sana ya usalama, hakuna usalama kabisa, ukienda ukirudi unamshukuru Mungu, maana unaweza kutekwa njiani na waasi wa jeshi lao huko, unaweza kutekwa na maharamia tu humuhumu na kudhulumu mali yote ili mradi usalama siyo wa uhakika huko hata njiani (ziwani)” alisema.

“Kuna siku wakati nafanya kazi zangu za usaidizi wa nahodha, niliwahi kupakia abiria kutoka ng’ambo na kuwapeleka Kigoma, walikuwa wageni kabisa, nikawafanyia ukarimu wa kuwasaidia katika mambo waliyoijia na kuhakikishia usalama wa mizigo yao njiani ziwani, baada ya kufika na wakati wa kurudi na sikuwadai ujira wowote wa ziada kwa usaidizi niliowafanyia.”

“Kumbe wale jamaa walikuwa wanajeshi waasi huko ng’ambo, mimi sikujuwa hadi siku moja chombo chetu kilipotekwa njiani na kupelekwa ng’ambo, wakachukuwa mali zote, mimi na nahodha wangu tukapelekwa kambini”

“Sasa alipokuja yule mkubwa wapo pale akaniangaliaaa, kisha akasema tupelekwe ofisini kwake, nikashangaa tunahudumiwa chakula kizuri na kupewa sehemu ya kulala pazuri. Pazuri kwa maana ya kwamba kuna hema na blangeti lililotandikwa kama kitanda. Katikati ya usiku akaja yule mkubwa wao bado akiwa amevalia magwanda yao ya jeshi na minyota nyota yake iliyo kaa vibaya, akaniita na kuniambia…”

“Mmesalimika kwa kuwa nimekutambua, wewe ni kijana mwema sana, kuna siku ulinisaidia sana. Akajitambulisha vizuri nikamkumbuka. Akaniambia atakuja kunitorosha, ameshawatuma wafuasi wake wakaniwekee pipa moja la dizeli kwenye boti na magunia, alituambia ikifika usiku wa manane atatuma askari aje atuongoze hadi kwenye boti yetu”

“Kweli usiku ule ule alikuja askari akatupa ishara ya kuwa tumfuate, tulitembea kwa kunyata hadi tulipofika ilipoegeshwa boti, akayaloweka yale magunia na kufunika injini ya boti ili isitoe mlio mkubwa ili tutoroke. Pia alituambia tupitie njia nyingine maana ile ya kawaida bado wanajeshi wanafanya doria zao za kuteka mali ili wapate kuishi huko msituni”

“Tuliwasha boti na kuondoka kwa kuelekea kaskazini kwa muda kadhaa kisha ndio tukafuata njia ya kenda uelekeo wa bandari ya Kigoma. Lakini kwa kuwa ilikuwa usiku wa giza totolo na pasipo mwezi wala nyota maana ilikuwa msimu ya mvua tukajikuta tumepotea palipo pambazuka na kuona tupo uelekeo wa hifadhi ya Jeshi letu (JW).”

“Mara tukasikia milio ya risasi na sauti kwenye spika ikituamuru tusalimu amri, tulizima injini na kusimama na kunyoosha mikono juu, kuna boti mbizi za jeshi za doria (fibre boats) zilituzingira wakiwa na silaha nzito huku mwanjeshi mmoja akiongea na simu ya upepo.”

“Sauti ya amri ikatoka kwenye boti moja” “Jitambulisheni, ninyi ni akina nani na mnatoka wapi na mnaelekea wapi?!”

“Sisi ni watanzania, sisi ni watanzania…” tulijitetea,

“Watanzania! Mbona mna boti ya waasi!” alisikika mmoja wa wale wanajeshi. Kuangalia hivi kwenye jina la boti yetu nikaona kumeandikwa BANA SUDI KIVU kwa maandishi mekundu. Kumbe tayari kule wale waasi walishajimilikisha, isingekuwa yule mkuu wao, sijui tungekuwa na hali gani”

“Sisi ni watanzania, mimi ni mfipa na mwenzangu ni mrangi” alijitetea nahodha wangu.

“Bahati nzuri kule kwenye boti ya JW kulikuwa na Msandawe, hivyo alikuwa anakijuwa kwa kubabaisha kirangi na pia alikuwepo Mpimbwe ambaye pia alikuwa anaelewa kifipa”

“Abari ja mutondo!” alisema yule mjeshi huku akituangalia, haraka haraka nikajibu “jaboa”,

“Akasema tena ikiana!”

Nikajibu fasta “anga!” hii ilikuwa kisandawe.

Urangi na Usandawe ni jirani hivyo kwa kiasi fulani unaweza kujuwa baadhi ya maneno ya lugha nyingine. Mara akadakia mjeshi mwingine “Mwalalauli” yule mwenzangu akajibu “Eenditaa!”, japo alichapia lakini ilieleweka kuwa kweli kwa hatua ya kwanza inawezekana kuwa sisi ni watanzania.”

“Tukaelekezwa kuongoza hadi nchi kavu ambako kila tulivyokuwa tunakaribia tukawa tunawaona wanajeshi wakiwa wamekaa tayari kwa mashambulizi kutushambulia”

“Tukafika nchi kavu, tukapelekwa msobe msobe hadi sehemu kavu na kuamriwa kukaa chini”

“Baada ya mahojiano pale kweli wakathibitisha kuwa sisi ni watanzania na tulitekwa, tukapewa usindikizwaji hadi tulivyotoka nje ya eneo leo, lakini walifuta yale maadishi kwa rangi nyeusi”

“Tulifika Kabwe tukiwa hatuamini macho yetu”

“Sasa katika safari zetu zilizofuata za kawaida, kuna siku tukakuta na yule mkuu wa waasi akiwa kiraia pale bandarini ng’ambo kwao, akaifuata boti yetu na kuja kutusalimia kirafiki. Akaniambia, siku nyingine nikienda niseme maneno (ambayo alinitajia) kwa mtu yoyote anayeonekana kama askari nitakuwa salama na nitafikishwa kwake”

“Kwa kupitia huyo mkuu wa waasi, nikapata uchochoro sasa wa kufanya biashara kwa uhuru maeneo hayo na kuanza kupata mafanikio hadi bosi wetu akanunua boti nyingine mpya nami nikaachiwa ya zamani hadi nikanunua boti yangu ambayo ninayo hadi leo”

“Ni boti yangu tu inaweza kutembea mwambao wote wa ng’ambo bila matatizo, ndiyo maana Mzee Njembi alikuambieni mnitafute mimi. Na hata huko msituni kwa mbirikimo nitakupelekeni maana huko ndiyo safari ya huyu kijana ilipo” akaniangalia kisha akawaangalia wenzangu.

“Lakini nasikitika, ninyi safari yetu itaishia hapa, hamuwezi kwenda kule, mtakaa hapa hadi nirudi nije nikupeni habari za ndugu yenu” alimaliza na kutulia.

Tukabaki tunatizamana pale kwa mshangao!

“Sasa ikakuwaje huyo kwenda peke yake wakati hali yake inabadilika badilika, nani atamsaidia?” mama alihoji.

“Mama wala usiwe na wasiwasi, kule mambo ni mengi, mkienda wote kutakuwa na uzito sana wa safari, niaminini mimi, muaminini mzee Njembi” alimaliza na kuingia ndani akatuacha kujidaliana.

Tulijadiliana weee na tukakubaliana akija tumwambie kaka anisindikize, Shangazi na Mama wanisubiri. Basi baada ya muda kupita alirudi na kutuuliza tumefikia muafaka gani.

Ustadhi alikuwa ni mtu wa makamo, ni mmoja wa wale warangi wenye ngozi nyeusi, mwembamba mrefu na mchapa kazi. Baadaye nilikuja kujuwa kuwa alianza shughuli za uvuvi katika bonde la Rukwa kwenye Ziwa Rukwa na hali ya mavuno ilipokuwa ngumu ndipo akaenda Ziwa Tanganyika na kuanza kazi za ubaharia, unahodha usaidizi hadi sasa amekuwa nahodha mahiri.

“Tumeamua kaka yake amsindikize” alijibu shangazi.

“Hapana, haitowezekana, najuwa kwanza hapo ninyi hayupo mwenye makarasi ya kuvukia (passport) wala kadi ya homa ya manjano, sasa huyu atasumbuliwa sana na askari wa kule na wanapenda rushwa balaa, wenyewe wanaita ‘makuta’, chukueni ushauri wangu, huyu kijana niachieni mimi, atarudi salama in shaa Allah” alisema.

Wote pale tukaangaliana, na kisha kaka akasema, “duu tulisahau kuwa tunataka kwenda nchi nyingine, maana pia kuna ishu ya visa na kulipia kwa dola (dollar), vyote hivyo hatuna”

“Kuhusu viza (visa) kama ungekuwa na passport hata ile ya karatasi tungeweza kugonga wakati wa kuingia, lakini ni vyema ninyi mkabaki hapa nami nitarudi na mwanenu salama.” Alijibu Ustadhi.

Siku ikaishia hivyo na tukapanga kesho yake usiku safari ianze. Boti ilipakiwa mapipa ya dizeli na petrol kutoka kwa wateja tayari kwa safari. Kwa kuwa sikuwa mgeni wa safari za kwenye maji sikuwa na hofu.

Baada ya chakula cha jioni, nikachukuwa rasket (kibegi kidogo kilaini cha kufaa mgongoni au begani) yangu, na suruali yangu moja tu ya savco jeans, na nilivaa mtumba wa jeans ya levi’s straus na tshirt ya mtumba ya rangirangi, kwenye rasket kulikuwa na tshirts mbili za ziada, hivyo sikuwa na mzigo mzito, tukaenda kwenye boti na nikapanda, nikakaa jirani na anapokaa nahodha.

Tulikuwa watu watano tu kwenye boti ambapo wawili walikuwa ni wateja wenye mafuta na mmoja ni msaidizi wa Ustadhi. Safari ikaanza kwa msaidizi wa nahodha kuongoza chombo.

“Tuna safari ya kilomita mia moja na ishirini hivi hadi tufike tutakapoanzia safari ya nchi kavu mimi na wewe” alisema Ustadhi.

Safari iliendelea kwa kupiga stori za hapa na pale hadi hali ya ziwa ilipobadilika na kuwa na upepo mkali na mawimbi makubwa, Ustadhi akachukuwa unahodha. Safari iliendelea, kukiwa kimya na nahodha aliyakata mawimbi kwa kuyafuata, hali iliyofanya tutumia muda mwingi kutembea umbali mfupi. Hali ilitulia baada ya kama saa moja hivi ya dhoruba. Nilishangaa sana kuona kumbe hata ziwani kuna mawimbi makubwa sana. Stori zikaanza tena na nahodha msaidizi akachukuwa unahodha kuongoza chombo.

“Unajuwa Pazi, tunapoenda sasa kushusha mzigo ni kama kilomita hamisini tu kutoka kule Kabwe, lakini, siyo hapo tutakapoanzia safari, itabidi mimi na wewe tuelekee kwingine, lakini tutatembea kando kando ya mwambao hadi tutakapofika hapo tutakapo anzia safari…” aliniambia, mie nikawa naitikia tu maana naona napelekwa kama taahira, sijui hata hatma yangu itakuwa nini maana kila sehemu naambiwa uende huku, mara uende huku ili mradi sipati suluhu ya maradhi yangu. Hata hivyo nilijipa moyo kwa historia ya Ustadhi aliyotuhadithia.

“Tutashusha mizigo sehemu panapoitwa Zongwe, kisha tutaelekea bandari ya Moba…” alisema.

Safari ya kufika bandari ya kushusha mizigo ilituchukuwa kama saa sita hivi na mizigo yote ikashushwa hapo na saa kumi na moja tukaanza safari ya kwenda huko Kaskazini kwenye hiyo bandari ya Moba ambapo napo ilituchukuwa masaa manne hivi maana chombo kilikuwa chepesi licha ya ka umbali kidogo.

“Sasa dogo!” alisema Ustadhi huku akimuelekea yule msaidizi wake

“Leo ndio mtihani wako wako wa mwisho kufudhu unahodha, itabidi urudi kule Zongwe, upakie mapipa tupu na abiria utakao wapata urudi Kabwe, na uchukuwe mizigo ya Kabwe ulete huku” aliendelea.

“Uendelee kufanya hivyo hadi siku utakaponiona bandari ya Zongwe, haya, kila la heri” alimaliza na kumuamuru aondoshe chombo kuwahi Zongwe.

**********

Itaendelea
 
Safari niliacha kuratibu baada ya kupokea taarifa kuwa ingekuwa siyo salama kwangu

Lakini watu waliandaa safari na kila wiki watu hufanya safari japo za siku chache lakini watu wana enjoy

Nami nilijumuika kwenye ruti moja ingawaje sikuingia kwa majina yangu ya humu
Naomba maelekezo namma ya kujiunga na hao wanautalii was ndani hapo nami nikainjoi kwa kadiri nitakavyojaaliwa


Simulizi mujarrab na nakwenda nayo ngadu kwa ngadu
 
8. UMBIRIKIMONI

Pale bandarini tukapata gari ya mizigo inayoenda Manono, Ustadhi kote huko alikuwa akijulikana na alikuwa akimaliza mambo yote ya kiserikali kwa rushwa (makuta). Safari ilikuwa ndefu na ya kuchosha maana gari ilikuwa imejaza mizigo sana na njia haikuwa rafiki, tulitumia siku mbili kufika Manono ambao palionekana kuchangamka sana na hata ndege (aeroplane) zilikuwa zinatua na kuruka maeneo ya jirani.

“Sasa bwana, mimi safari yangu itaishia hapa…” alianza kunipa risala baada ya kuvuka mto mkubwa na tukawa tuko eneo la Kanisa.

Tayari ilikuwa asubuhi ya siku ya tatu, baada ya kupata ugali na samaki wa asubuhi asubuhi ndipo tukavuka hadi jirani na Kanisa la mtakatifu Barbe.

“Chukuwa hela hizi, najuwa hutozitumia sana, lakini ni vyema ukawa nazo…” alinipatia noti nyingi sana za faranga za Kizaire na dola moja moja na tano tano kadhaa za Kimarekani

“Utakaa kwenye mti huu na utalala hapahapa, lakini usiku utafuatwa na kuanza safari nyingine ambayo mimi sitakiwi kwenda, nitakusubiri ng’ambo ya mto hadi utakavyorudi, uje pale pale tulipo lala utaniulizia.

“Kwenye mti huu ni stendi ya wote wale waendao huko kwenye msitu wa Mbirikimo, matibatu yako utapata huko. Haya kila la heri, mimi narudi ng’ambo” alimaliza na tukaagana huku nikibaki na wasiwasi mwingi.

Niliambiwa kuwa hapo ni stendi lakini sioni dalili yoyote ya njia ya magari jirani wala mikokoteni ya mifugo. Kulikuwa na mti mkubwa sana hapo kando kabisa ya kanisa na chini palikuwa pasafi kama pamefagiliwa. Kulikuwa na watu wengine kama wahudumu hivi wa Kanisa ambao walikuwa wanaoneka kwa mbali na watoto wadogo ambao walikuwa wakicheza kwenye viwanja vya kanisa yani kwa ufupi ni sehemu iliyokuwa hai.

Nilisimama kwa muda, nikachoka, nikakaa, mwisho nikaamua kulala na kufanya rasketi yangu kuwa mto. Usingizi mzito ulinichukuwa, hadi niliposhtuka njaa ilikuwa imeanza kuniuma na sikuona dalili ya mkokoteni wala gari. Ni sauti tu za ndege zikitua na kuruka zilikuwa zikisikika mara kwa mara. Jua likazama na giza likaanza kutamalaki.

Kitu cha ajabu niliona katika afya yangu ni kwamba baada ya ile dhoruba kule ziwani kwisha nilijisikia niko kawaida, yani siumwi tena, mwili mwepesi na nina nguvu. Chini ya mti hapo sikuondoka, nilihisi nikitoka tu labda usafiri ungefika nikiwa sipo na kukosa kwenda huko Umbirikimoni, njaa ikanizidi ndipo nikatambua kwanini aliamua tule ugali samaki asubuhi ile. Nikaanza kukumbuka safari nzima tangia tunatoka Bagamoyo hadi huku Zaire.

Bandarini kote ng’ambo ya huku nilishangaa kuona watu wakiongea Kiswahili cha ajabu, yani kuelewa inabidi usikilize kwa makini, ni Kiswahili kilicho changanyika na lugha zao na lugha za kigeni.

Usingizi ukanichukuwa tena nikiwa nimejifunika ngumi, maana sikuwa na shuka na hali ya hewa ya huku ilikuwa ni ya baridi kulinganisha na ya Kabwe…..

Nilishtushwa na sauti ikiniita jina langu, nikaamka na kufikicha macho sikumwona mtu, nikakaa kitako, nikasikia tena naitwa, “Pazi!”

Nikaitika, “Naam”,

Sauti ile ilikuwa ikitokea upande wa giza kwenye kivuli cha miti ule maana kwa upande mmoja kulikuwa kunamulikwa na miale ya taa (mienge) kutoka kanisani.

“Ukuje huku!” alisema.

Ndipo nikagundua alipo na kumfuata. Nikamuona mtoto amesimama akiwa amevaa nguo kama za ngozi. Nilipomsogelea na macho yalivyozoea giza, nikagundua hakuwa mtoto bali ni mtu mzima lakini ni mfupi sana. Nikajisemea, hawa ndio Mbirikimo alioniambia Ustadhi.

“Mbona umechelewa kuja!” alihoji. Moyoni nikajisema, mbona nipo hapa tangia mchana, nimechelewa kivipi! Nikataka kujibu lakini akanikatisha…

“Lete mukono” aliamuru, akanishika mkono wangu barabara…

“Fumba macho” akaamrisha tena.

“Usifumbule hadi nikuspikee, sawa?” aliendelea, nikaitikia sawa.

Ghafla nikaona ubaridi usio wa kawaida unaniingia mwilini na ghafla nikajihisi sina uzito kabisa! Hali ile iliendelea kwa dakika kadhaa kisha nikaona ubaridi umetoweka na akaniambia nifumbue macho.

La hawlaa, baada ya kufumbua macho nikajikuta nipo katikati ya kundi wa Mbirikimo ambao wote walishika mienge ya moto na mmoja tu ambaye alikaa kwenye kitu kama kigoda hivi alikuwa hajashika chochote, ni yeye pekee alikuwa amevaa kitu kama manyoya hivi kichwani.

“Karibu sana Pazi, kijana wetu, umechelewa sana kuja lakini karibu” alisema yule Mbirikimo mkuu kwa Kiswahili fasaha tofauti na watu wa kule. Nilibaki tu nimetoa macho.

Nikaambiwa nikae chini, na zikaletwa nyama za aina tatu kwenye majani mapana ya miti. Yaani kila jani lilikuwa na nyama kadhaa za aina yake.

“Umeikala na nzala muda murefu… karibu ukule…” sauti ya mbirikimo mwingine mmoja wa walioleta zile nyama ilisikika, alikuwa ni mwanamke.

Kusema ukweli nilikuwa na njaa sana, lakini kwa kuwa sikujuwa ni nyama gani zile nilisita kuzila…

“Kula, usiwe na wasiwasi…” mbirikimo mkuu alisema baada ya kuona nasita sita.

Nikajipangusa mkono kwenye nguo yangu na kuanza kushika funyango moja ya kutoka kwenye jani la kwanza na nikainusa.

Ilikuwa nyama kavu iliyokaushwa na moshi, ilikuwa ngumu maana niliibonyeza pia, nikairudisha.

Nikachukuwa finyango katika jani la pili hii haikuwa ngumu sana, lakini nayo ilikuwa iliyokaushwa kwa moshi nikainusa, sikuielewa hata, nikaiacha.

Nikachukuwa finyango moja kutoka jani la tatu nikainusa, hii ilikuwa ya kuchemshwa lakini haikuwa na mchuzi, haikunukia, ng’ombe, mbuzi wala nyama nilizozizoea. Nikaijaribu kuiweka mdomoni, nikatafuna nikaona inatafunika na nikaendelea kuitafuna huku nikiwaangalia wale walionizunguka muonekano wao wakiwa wameshikilia mienge ya moto, wote walionekana wakitabasamu, nikameza, nitafakamia zilizobaki katika jani hili la tatu nikala hadi nikashiba, niliziacha kadhaa pia kwenye jani hilo.

“Umekatala kula vyionde di sanji na fakushe, umependa ba muton…” alisema yule Mbirikimo mwanamke aliyenikaribisha.

Nilikuja kujuwa baadaye kuwa zile nyama ni za heshima sana katika jamii yao, kumbe fakushe ni nyama ya nguruwe pori, sanji ni ya nyani na muton ni ya kondoo.

“Tulikusubiri kwa muda mrefu lakini hukuja” alianza risala yule Mbirikimo mkuu.

“Tumetoa ishara nyingi sana ili wewe uje huku lakini ulikuwa kiburi hutaka kuja ndio maana tukawa tunakupa misukosuko ili akili yako ikumbuke kuja huku”

“Huku ni ufalme wa Mbirikimo, na huku ndipo kwenye matibabu yako ingawaje siyo hapa utakapo tibiwa…” aliendelea.

“Mpelekeni akapumzike, asubuhi akiamka mleteni nyumbani kwangu kwa ajili ya safari” alisesma.

Safari tena, niliwaza, mbona hii ni safari ya safari zisizoisha?! Nilijiuliza moyoni.

Nikachukuliwa, nikaambiwa nifumbe macho, nikashikwa mkono na sekunde chache tu nikaambiwa nifumbue. Nikajikuta nipo kwenye kiota kizuri cha miti na udongo. Nikaoneshwa sehemu ya kulala, palikuwa pametandikwa ngozi, rasketi ikaendelea kuwa ni mto wangu, nikapewa ngozi kuubwa laini ikawa ndio shuka langu na usingizi ukanichukuwa hadi nilipoamka mapema asubuhi baada ya kusikia sauti za ndege wa porini zikiimba. Kuangalia saa ni saa moja na nusu asubuhi lakini nje bado giza hapajakucha vyema. Nikajisemea, huku sasa ndio magharibi. Nikatoka nje ya kiota (nyumba) na kuanza kuizunguka na kuangalia mandhari.

Palikuwa ni msituni kabisa, ni miti tu inayoonekana, na nyumba zipo mbali mbali za mtindo huo wa kama kiota. Zimejegwa kwa miti, na matope na juu kuezekwa na nyasi na udongo. Ni nyumba ndogo ndogo tu, fupi kwenda juu.

Shughuli za kawadia zikaanza kuendelea pale kijijini msituni, nikaja kujuwa kuwa hapo ni moja ya kijiji (mji) wa Mbirikimo matabibu. Yaani watu wa eneo hilo karibia wote walikuwa wakiwasaidia Mbirikimo wenzao kutoka maeneo mengine katika kutibu maradhi mbalimbali yanayo wakabili.

Hapakuwa na barabara, kulikuwa na njia tu za waenda kwa miguu na wala sikujuwa nipo eneo gani hadi leo lakini hapakuwa jirani kabisa na ziwa Tanganyika.

Palivyokucha zaidi nikafuatwa na wamama wawili na kupelekwa nyumbani kwa Mbirikimo mkuu pale kijijini.

Mazingira yalikuwa tofauti na yale ya jana usiku maana hapa palikuwa pamezungukwa na nyumba ndogo tatu.

“Leo usiku tutaanza safari ya kwenda kwenye matibabu yako” aliniambia yule Mbirikimo mkuu baada ya kusalimiana, huyu alikuwa akiongea Kiswahili fasaha kuliko wenzake.

Nililetewa matunda pori mengi kama kifungua kinywa, baadaye nikatembezwa kijijini kuona mandhari. Mchana ilipofika nililetewa mamung’unye na maboga pamoja na nyama ambayo sasa nilishaijuwa kuwa ni ya kondoo nikala. Kisha nikaambiwa nikapumzike nilipolala jana kujiandaa na safari ya usiku. Safari hii sikujiuliza sana, nikajuwa tu yale yale!

Jioni walikuja Mbirikimo wengine wawili wanawake, wakiniletea ugali wa kitu kama mtama hivi na nyama za kondoo. Walisubiri hadi nimalize kula ndipo wakaondoka. Walikuwa wakiniangalia sana tena kwa shauku kama vile walikuwa wanataka kuniambia kitu, lakini hawakusema chochote.

Walivyoondoka nikaanza kuwaza tena kuhusu Mama yangu na Shangazi jinsi wanavyosubiri nirudi wakati mimi bado nipo safarini, niliwaza jinsi Ustadhi alivyojua yote haya na safari yake katika kujinusuru na fujo za Kabwe. Niliwaza mengi sana hadi usingizi ukanichukuwa hadi usiku wa manane nilipo shtushwa na mwanga wa miale ya moto usoni nikiguswa bega….

“Lamuka”, sauti ya Mbirikimo wa kiume aliyekuja kuniamsha ilisikika.

Nikatoka nje ya nyumba, nikaambiwa nitoe nguo zote nilizokuwa nazo, nikavalishwa kitu kama kingozi hivi kilichoziba utupu wa mbele kiasi na nyuma kiasi.

“Fumba macho” akaniambia.

Sekunde chache tu tukafika kwenye ule uwaja wa jana usiku, na watu walikuwa wamezunguka vilevile. Nikaambiwa nikae kwenye jiwe fulani hapo, wakaanza kunimwagia maji. Hayakuwa maji ya kawaida, yalikuwa kama yana dawa hivi sikuelewa mara moja ni dawa gani. Wakaniacha hadi nikauke kisha wakaniambie nisogee kwa mkubwa wa Mbirikimo.

Akanishika mkono tukawa tunaelekea gizani na kuwaacha wale mbirikimo wengine huku wakicheza ngoma zao za kurukaruka.

Gizani mbele kidogo nikaona tunaingia kama kwenye handaki hivi, nikainamisha kichwa changu maana nilikuwa mrefu kuzidi yeye, na kisha akaniambia nikae kwenye majani ambayo yaliwekwa kama mkeka.

Mara akazima ule muale wa moto aliouchukuwa kutoka kwa wenzake na giza likatamalaki. Punde si punde chumba kikajaa mwanga mkali mweupe kama wa taa na mtu akaonekana nyuma ya ule mwanga kwa namna ya siliwete (silhouette)

“Pazi, umechelewa lakini umefika, karibu sana!” sauti ilisikika nyuma ya ule mwanga. Ghafla nikajikuta nimevaa kaniki na mgolole mweupe.

Tukatoka mle handakini, akitangulia Mbirikimo mkuu nikifuatia na nyuma yangu ule mwanga mkali ukawa unatufuata. Tulivyofika nje, nikasikia tu nywele zimesisimka na ghafla fyuuuu nikawa naelea angani juu ya msitu kama mwewe nikiongozana na ule mwanga bila kuona vizuri sura ama umbo.

Haikupita sekunde nyingi tukatua mwaloni kwenye mikoko (ambayo niliitambua mara moja) na tukaanza kutembea kawaida lakini ule mwanga mkali haukuwepo tena na umbo la niliyekuwa naye likaonekana ni la binadamu. Tulitembea kawaida mchangani kisha tuakingia kwenye maji maji kwenye mikoko huku akianza kunisimulia.

“Nimekuleta huku ni kwenu, huku ni makazi ya Masharifu. Hivi sasa hapo ulipo hakuna binadamu anayeweza kukuona, wala kukugusa maana upo kama hewa. Karibu katika mji wa masharifu”

Hii si ni bahari hii? nilipata ujasiri wa kuuliza. Kabla sijajibu ghafla nikaona nimezama hapo mikokoni na kutokea mji wa ajabu.

**********

Itaendelea
 
9. UJININI ‘NUSU BINADAMU NUSU' JINI’

Mji ulikuwa wa ajabu, uliopambwa wa nakshi za kila aina, barabara nzuri lakini hakuna magari, watu wake walionekana wakitembea kawaida lakini walikuwa warefu kuliko binadamu, taa nzuri nzuri kila sehemu yani ulikuwa mji wa kuvutia usioelezeka uzuri wake.

Mazingira yalikuwa si usiku wala si mchana maana nilikuwa naweza kuona mbali bila shida lakini na taa za rangi mbalimbali zilikuwa zinawaka.Tukaenda hadi tukafika kwenye geti kubwa zuri na kuwakuta walizi wawili na kufunguliwa nikakuta ‘watu’ wamejipanga kama kutulaki hivi na moja kwa moja tukaelekea hadi kwa uwanja mkubwa ambapo mbele kulionekana mtu kama mfalme hivi ameketi kwenye kiti cha ufalme.

“Hatimaye umefika Pazi kijana wetu” sauti ya bashaha ilisikika kutoka kwa yule mfalme.

“Huku ni wapi? Na je ndiyo mwisho wa safari zangu za matibabu?” niliuliza kwa kujikaza na kutetemeka.

Alicheka sana na kisha akaniambia…

“Pazi, hauumwi, yani huna maradhi yoyote. Tumekuwa tukikulinda muda wote tangia ulivyokuwa tumboni mwa mama yako…”

“Mama yako ndiye aliyekuwa na maradhi tumboni. Maradhi yake yalitokana na husda. Husda ya uke wenza baada ya kuona mama yako amejifungua mtoto wa kiume wakati mama yako mkubwa alikuwa na watoto watano wote wanawake, hivyo ikamuingia husda na wivu na kwenda kumfanyia mama yako uchawi”

“Ni uchawi mbaya sana aliofanyiwa, uchawi uliotoka visiwani Tumbatu” akasita kidogo…

Tumbatu ni visiwa vilivyopo Zanzibar (Unguja) jirani na Nungwi

“Mama yako alitiwa viuvimbe vidogo vidogo tumboni mwake ili mimba za watoto wa kiume zisikae, pia kaka yako alipewa sumu ya kuuwawa lakini tuliwahi kumuokoa, na majaribio ya kumuua yaliendelea na tulikuwa tunazuia isitokee hivyo…” alieleza bila kufafanua.

“Baada ya mimba mbili kuporomoka kutoka kwa mama yako, kuna siku alikuwa ana huzuni sana, akawa anatembea kandokando ya bahari huko duniani huku akitoa maneno kadha wa kadha ikiwemo kuwa akipata mtoto wa kiume tena na akimzaa basi atamtoa wakfu”

“Sasa wakati anasema maneno hayo sisi kwa bahati nzuri mimi nilikuwa napita na safari zangu za kawaida… tuliamua kuchukuwa jumumu la kuilinda mimba itakayoingia…” akasita kidogo kisha akaniambia nisogee kwake kisha akasema.

“Hakuna mimba ya mtoto wa kiume ambayo ingeweza kukaa kwenye tumbo la mama yako baada ya uchawi ule, hususani kwa mbegu za kibinadamu… Pazi wewe ni mtoto wetu…” akanishika mkono na kuanza kukagua ngozi yangu.

Kwa mara ya kwanza ndipo nikagundua nami kuwa ngozi yangu haipo kawaida.

Kwa kawaida, ngozi ya binadamu wa kawaida huwa ina pattern ya kitu kama kashata kashata hivi, lakini ngozi ya kijini akijigeuza kuwa mwandamu inakuwa na pattern ya draft draft ndogo ndogo sana.

Eee majini ni viumbe kama viumbe wengine lakini wana sifa taofauti kidogo. Katika mafundisho, tunaambiwa kuwa binadamu aliumbwa kwa kutumia malighafi ya udongo mweusi, na majini waliumbwa kwa kutumia malighafi ya moto. Malaika waiumbwa kwa kutumia malighafi ya nuru ya mwanga etc.

Binadamu alipewa umbo, matamanio, uamuzi wa kuchaguwa atakalo, nk lakini alizibwa macho kuto kuona zaidi ya alivyokadiriwa nk pamoja na utawala na uongozi katika ardhi hii kwa viumbe wengine wote, Majini walipewa pia matamanio, hiyari ya kuamua watakao, uwezo wa kuona wasio yaona binadamu na uwezo wa kujibadili maumbo yao kuwa watakayo ingawaje wana umbo la asili pia, uwezo wa kusafiri mbali kwa muda mfupi nk lakini wakanyimwa utawala dhidi ya binadamu. Ndiyo kusema kwamba binadamu anaweza kuwatawala majini na kuwatumia atakavyo kama vile awezavyo kutawala wanyama na kuwatumia atakavyo ilimradi tu awe na elimu ya kutawala hao majini na hivyo viumbe wengine. Malaika wao hawakupewa hiyari ya maamuzi, wala matamanio, wamepewa uwezo mkubwa wa kusafiri mbali kwa muda mfupi, wanaweza kujibadili maumbo yao nk. Hii nayo ni topic ndefu na elimu yake ni kubwa inayohitaji uzi wake.

****

“Mama yako alishika mimba kutoka kwangu, na wewe Pazi ni mtoto wangu, na kwa kutaka kutimiza nadhiri ya mama yako ndio tukawa tunakuita uje huku lakini umechelewa kuja, ila hatimaye umefika”


He, kumbe mimi ni mtoto wa kijini! Nilijisemea na kujishangaa, nikaanza kukumbuka yote tokea utotoni, makuzi yangu na jinsi nilivyokuwa mbashiri mzuri wa mambo na mjuzi wa hesabu baada ya kuelekezwa mara moja tu na mwalimu. Sasa mbona sikuchaguliwa kwenda sekondari! Nilijiuliza. Nikakumbuka jinsi ulivyokuwa unanipenda kwa sababu ya kufanya vizuri kwenye hesabu na maswali ya udadisi kiasi cha wewe kujenga ukaribu nami wakati wote nikiwa kule Sanzale ama tukija Upanga kukutembelea.

“Nadhiri ya mama yako ni kuwa uje kumtumikia Mungu, na sisi tumeona ni vyema umtumikie Mungu kwa kuwatibu wanadamu…”

“Wanadamu hawatumii vizuri vipawa vyao, wana matatizo mengi sana ambayo wangeweza kuyatatua bila ya msaada wetu lakini ni viburi tuu vimewajaa…”

Aliendelea kutoa risala pale weee kisha akaniambia nenda kapumzike.

Nikapelekwa kwenye chumba kilichoandaliwa kwa ajili yangu, kilikuwa kizuri mno kiasi cha kushindwa kuelezea...

Nilipoamka, nikaanza kusomeshwa elimu ya utabibu, nilifundishwa tiba za miti majani na mizizi, tiba za maji, tiba za kitabu, elimu ya nyota na unajimu na kadhalika, yote haya nilijifunza kwa muda mfupi maana sikuona usiku wala mchana wala sikuwa nakula chochote hatimaye nikatunukiwa hati ya kufuzu utabibu kwa wanadamu.

Nikapewa fimbo nyeusi, usinga na nyoya mkubwa ajabu sijapata kuona…

“Unyoya huu, ukihitaji msaada wowote wa dharura, chukuwa sehemu ndogo ya unyoya uchome moto, nasi tutafika kutoa msaada…”

“Iwe dharura ya kweli na siyo kutusumbua kwani tutaacha majukumu mengine yote ili tuje kukusikiliza na kukusaidia” alisema yule mfalme.

Baba hahahha, kumbe mie ni prince! Tukacheka sana pale.

Tangia saa kumi na moja jioni alianza kunisimulia hadi saa nne usiku ambapo ilibidi nimpigie simu mke wangu Hamida kumjulisha kuwa kuna dharura nitachelewa sana kurudi hivyo asinisubiri bali ale alale.

Baada ya kupewa hati za kufuzu kwangu (fimbo, usinga na unyoya) nikapelekwa tena mbele ya baraza la kifalme na kuagwa rasmi, kisha yule mtu niliyekuja naye ambaye sasa nilitambua kuwa ni mkuu wa watumishi falme ya pale alinichukuwa na kuanza kutembea barabarani ghafla nikajikuta tumetokea pale kwenye mikoko. Cha ajabu nikawa naona bahari kama imegeuka hivi, nikiangalia jua naona inatokea upande mwingine na kuelekea kwingine.

Kumbe bwana tuko upande wa magharibi mwa Africa, niligundua hivyo baada ya kuambiwa na yule msindikizaji wangu tujongee kwenye mgahawa tukapate supu ya samaki, eee mwalo ulikuwa umejaa watu ambao walikuwa wakiongea lugha ya iliyochanganyika na kifaransa na kireno. Ajabu ghafla nami nikaanza kuongea Kireno fasaha.

“Traganos sopa jipe suprifavo…” nilijikuta nasema maneno hayo kwa maana ya kwamba atuletee supu ya samaki.

Tulikula pale kisha tukasogea kwenye hoteli ndogo tukakaa kwa ajili ya mazungumzo tukisubiri safari ya kurudi Umbirikimoni. Kutoka Ujinini nilikuwa nimefaa kanzu nzuri ya kumeremeta na kofia ya tarabushi, ndani nikiwa na suruali ambayo imeficha fimbo yangu kiunoni, usinga na unyoya.

Tulivyochoka kukaa sehemu moja, tulizurura maeneo ya bandarini tukajichanganya na wenyeji, mara mtoto mmoja akawa anakohoa sana huku akijipiga kifua, huku mama yake akiwa amemuinamia kama kumsaidia…

“Edemwa sivople mafi setof…” alisema yule mama na mara moja nikatambua anaomba msaada…

Nikamshika mgongoni kwa mkono wangu na mara akaitema kilichokuwa kinamkaba kooni, ulikuwa ni mwiba wa samaki.

“Mesii bikop” alisema yule mama kwa kifaransa.

Tukapitisha siku kwa mtindo huo hadi giza lilipoingia tukaelekea tena kule kwenye mikoko na kuanza safari ya kurudi. Safari hii niliruka mwenyewe, kasi ilikuwa ya ajabu kiasi cha kuweza kushindana na msindikizaji.

Alinitembeza huko angani sehemu mbalimbalia huku akiniambia kule tulipotoka ni Guinea ya Ikweta, tukaenda Guinea kwenyewe, Guinea Bisau, Nigeria, Sahara magharibi, Misri, Somali land na kisha muda ukawa umeenda tukarudi Umbirikimoni ambapo sasa nilipatambua kuwa ni Jamhuri ya Africa ya kati.

Nikashukia pale nje ya handaki, tukaagana na yule msindikizaji, akatoweka na ghafla akaja yule Mbirikimo mkuu na kutoa heshima kwangu kwa kuinama. Akaniongoza hadi kwa wale wengine pale walipokuwa wakicheza ngoma zao huku wakirukaruka na kunipokea kwa furaha. Nipo nikajuwa kuwa hawa siyo Mbirikimo wa kawaida bali ni aina fulani ya majini ambao pia kazi yao ni kutibu binadamu na mambo yao mengine ya kijini.

Ilipokaribia saa kumi na moja asubuhi kwa saa za kule, wote tukaanza safari ya kurudi kule kwenye kiota ambako sasa nikapatambua kuwa ni Zaire kwenye mbuga ya Salonga kaskazini. Nililala kidogo kwenye kiota changu na baadaye nikaletewa uji wa mtama na mamung’unye kama kifungua kinywa. Nguo niliamua kubadili na kuvaa zile za kwangu, kanzu na suruali yake na fulana yake na tarabushi nikaviweka kwenye rasket, usinga na unyoya pia lakini fimbo nikawa nimeishika mkononi.

Usiku ulipowadia, alikuja yule Mbirikimo aliyenitoa kule kanisani Manono. Tukafika usiku huo huo wa manane, tukaagana na mbirikimo msindikizaji, kisha nikajipumzisha kwa mtindo ule ule wa kujifunika ngumi na rasket ikiwa mto hadi palivyo pambazuka.

Nikaamua nivuke mto ili nikamtafute Ustadhi. Nikafika pale kwenye mghahawa tulipokula ugali samaki asubuhi nikamuulizia Ustaadhi.

“Ostadhi naenda fasi ya Kitololo tangu siku ya Mungu makumi matatu…” alijibu mmoja wa wahudumu pale akimaanisha aliondoka Jumapili ya mwezi mmoja uliopita!

Nikashangaa sana, yani mwezi mmoja nilikuwa Umbirikimoni!, mie niliona ni siku nne tu au tano ndizo nilikuwa huko. Nikatoka pale kwa usafiri wa mkomkoteni wa kuvutwa na ngombe hadi Kitololo na kushuka sehemu ambayo ngombe walienda kunywa maji kwenye bwawa. Nikawapa ujira wao wale vijana na kuelekea kwenye nyumba nyingi.

Nilitembea kama mwendo wa nusu saa hivi nikafika sehemu ambayo kwa muonekano palikuwa ni stendi ya magari. Nikauliza wale wapiga debe pale kuhusu Ustadhi, hakuna aliyenyoosha maelezo sahihi bali walionesha kumfahamu. Nikaulizia sehemu ya kulala… wakaniambia kuna guest house inaitwa Deluxe ndio pasafi…

Nikaomba mmoja wa wapiga debe anipeleke, wale wenzake nikawapa faranga kumi za Zaire, na huyu aliponifikisha Lodge nikampa Faranga kumi pia.

Nikajiandikisha pale mapokezi, akaomba passport, nikampta dola 10… “ooh paspo ya bien..” akasema na kwenda kunionesha chumba changu.

Sikuwa na njaa, bali hamu yangu ilikuwa kutaka kujuwa kimejiri nini baada ya kuachana na Ustadhi. Hivyo nikaoga vizuri na kuvaa zile nguo nilizotoka nazo Ujinini. Nikatoka mapokezi na kuomba kibiriti…

“Uko na kanzu ya shee na banavuta sigara!...” alishangaa na kuuliza yule mhudumu, lakini akainama na kunipatia kibiriti kilichokuwa kina njiti chache.

“Ahsante..” nilimjibu huku naondoka kuelekea chumbani.

Nikajifungia mlango, kisha nikaketi kitako na kuanza kuchoma sehemu ndogo ya ule unyoya ambapo nilikuwa nimeukunja kunja ili uenee vizuri kwenye rasket.

Ghafla nikaona upepo ukivuma, na ghalfa nikasikia sauti nyuma yangu… nikasimama na kugeuka…

“Tukusaidie nini Pazi ibn Shariff Burhan…” Kumbe yule Baba mfalme ni Shariff Burhan! Nilijiuliza

“Nataka kujuwa Ustadhi yuko wapi na ana hali gani, nataka kujuwa kaka yangu Shangazi yangu na Mama yangu wapo wapi na wana hali gani…” nilijibu

“Weka usinga chini, shika fimbo yako kwa mikono miwili kisha fumba macho” Alisema yule kiumbe aliyekuja kwa njia ya ajabu sura ya kibinadamu.

Nami nikatii, nikaketi na kufanya kama alivyosema…

Mara nikaona kitu kama ‘live video’ hivi, nikaona Ustadhi anapakia mizigo kwenye boti yake akiwa Kabwe akishirikiana na wateja wake… nikaona pale kwa Ustadhi Mama wa Shangazi hawapo bali kaka alikuwa amelala kibarazani nje ya nyumba… mara nikaona Shangazi na mama wapo Stendi kuu ya Sumbawanga wakirandaranda… Mara nikaona nyumbani Bagamoyo kumegubikwa na huzuni kubwa watu hawana furaha pamoja ya kuwa walikuwa wanakula chakula cha mchana, … mara nikaona kaburi ambalo limendikwa kwenye jiwe, Salma, na mara nikaona kaburi jingine limeandika Sinasudi ingawaje sikujuwa mara moja ni maeneo gani….

Nikafumbua macho.

Nikaangaza huku na kule sikuona mtu bali nipo peke yangu. Usingizi ukanipitia…..

Usingizini nikaota naelekezwa mambo mengine mbalimbali ya utabibu na mbinu nyingine za kijini ili kufanikisha mambo.

Nilipoamka nikawa na njaa sana, nikaenda restaurant kuagiza chakula, nikala ‘flit’ (chips) na samaki na kinywaji kama soda lakini hakikuwa na gesi kali, ilikuwa kama juisi ya kienyeji ya lozera kwenye chupa ya kisasa ya soda.

Baada ya kula, nilienda kwa mhudumu na kumuambia kuwa nitaondoka mapema asubuhi, tukaagana kwa malipo ya chumba na kuelekea kulala.

Ilipofika saa nane za usiku nikavaa kanzu yangu, nikaweka rasket yangu mgongoni nikachukuwa kila kilichochangu kisha nikasema maneno niliyofundisha usingizini na ghafla nikajikuta niko hewani naiangalia ardhi kwa jicho kama la mwewe.

Nikasikia sauti inaniambia, ruka juu zaidi, nikainua kichwa kidodo na kifua nikaona nazidi kuiacha ardhi ya kwenda juu zaidi.

Hewani huko niliona misafara ya wachawi wengi tofauti tofauti, wengine wakitumia pembe kama chombo ya usafiri, wengine wakitumia mifagio, wengine vyupa wengine wanyama ambao sikuwafahamu mara moja, wengine wakiwa wamjichomeka kitu kama gunzi hivi matakano ili mradi kulikuwa na pilika pilika misafara kadhaa lakini hawakuonekana kuniona.

Kwa kuwa Ustadhi alikuwa anakuja ng’ambo ya huku, basi nami nikaamua moja kwa moja nielekee Zongwe ambapo ndipo mizigo ya wateja wake hushushia hapo. Sikupaa kwa kasi sana maana nilikuwa nainjoi hali ile ya kuelea na kuona mengi ambayo sikuwahi kuyaona.

Palipoanza kupambazuka nikaelekea maeneo ya bandari ya Zongwe na kushukia mwaloni kabisa na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea wanaposhushia mizigo.

*******

Itaendelea
 
10. SAFARI YA KURUDI TANZANIA


Kwa mbali nikaanza kuona watu wakishusha mapipa ya mafuta kwa kuyatupa majini kisha kuya vingirisha hadi nchi kavu…

Nikasogea jirani zaidi, mmoja wa wale waliokuwa wanashusha mizigo akaniona na kushtuka na kuanza kupiga kelele…

“Sentoo Sentoo!” akimaanisha shetani shetani

Wote pale wakashtuka na kuangalia, nami nikamuita Ustadhi…

“Ustadhi, ni mimi bwana nimerudi…”

“Aaaaaah Pazi! Umenitesa sana, mbona ulichelewa kurudi” alijibu na kuja kunikumbatia.

Na wale wateja wakawa na Amani wakaja kunisalimia…

Nikakaa pembeni ili wamalizie zoezi lao la kushusha mizigo.

Baada ya ile kazi kuisha, tukaenda sehemu ya mgahawa, hatua kidogo na tuliposhushia mizigo, na kuagiza supu ya samaki huku tukiongea.

“Enhe, hebu niambie nimekaa siku ngapi… maana mimi naona ni kama siku 5 au sita tu…” nilimuuliza, naye akajibu…

“wewe si una saa hiyo ya disco bwikubwiku, angalia leo ni mwezi wa ngapi..”

Duuu ile kuangalia nikaona kabisa ni zaidi ya siku 40 tangia nitoke Kabwe.

“Enhe, lete habri za huko, umeshatibiwa? Sisi tulidhani umeshakufa, maanda kule si mchezo mchezo, mie sijawahi kufika zaidi ya kuishia pale Kanisani ambapo nilimpeleka mama mmoja hivi lakini alikaa siku mbili tu akarudi…” aliuliza na kulalama.

“Nitakuelezea, lakini niambie kwanza ilikuwaje baada ya kuniacha pale na kurudi kule ng’ambo…” nilimuuliza ili aanze yeye kusimulia.

Akaniambia kuwa baada ya kuvuka mto, alinisubiri pale kwa siku tatu, akidhani ningeweza kuwahi kurudi kama ilivyokuwa kwa mteja wake wa kwanza, lakini alipoona sirudi, Jumapili yake akaondoka kwenda Manono mjini na kunisubiria huko huku akiwa ameacha maagizo pale mgahawani kama nikirudi basi nimfuate huko manono mjini. Lakini baada ya wiki nyingine kupita bila ya taarifa zangu ndipo akaamua arudi Moba na kuacha maagizo kisha akapata boti ya kwenda hapo Zongwe tulipokutana.

“Nilikuta kijana wangu (nahodha msaidizi) amefanya kazi nzuri sana kwa siku kumi na mbili hivi nilizokuwa sipo, na wateja walimsifia kuwa sasa amekomaa kiasi cha kuitwa nahodha kamili” alisema.

“Enhe!? Nipe habari za huko!?” alidadisi.

Nikamuelezea kuwa nifuatwa na Mbirikimo pale kanisani na nikapelekwa huko Umbirikimoni na kutibiwa maradhi yangu yote, hivyo unavyoniona hapa mimi ni mzima wa afya. Akafurahi sana kisha akaniuliza…

“Vipi pesa ulitumia?”

“Hapana, sikutumia katika matibabu hadi nilivyorudi ndio nikatumia kwa ajili ya chakula na kulala lodge na usafiri… nimebakiwa na hizi hapa..” nikaingiza mkono kwenye rasket na kujaribu kuzitoia zile faranga na dola zilizobaki, lo salale! Nikaona nashika kibunda cha hela ambazo sikuwahi kuzishika…

“He, nini hiki?...” aliuliza huku akizipokea

Kilikuwa kibunda cha pesa kilicho vingirishwa na barabendi (rubberband) ambacho sikuweza kujuwa ni kiasi gani mara moja. Akaanza kuzihesabu. Kulikuwa na noti za dola kumi kumi sabini hivi na dola tano kiasi na faranga za Zaire zilizochanganyika na zile alizonipatia wakati ananiaga.

“Nadhani Mbirikimo wameamua kukuzawadia kwa kunileta huku…” tukacheka pale tukafurahi na kumalizia supu yetu.

Tuliendelea kupiga stori akinisimulia jinsi watu wanavyoenda kutibiwa kupitia njia ile ya kanisani mtini pale, akaniambia yeye hajawahi kwenda zaidi ya pale lakini anasikia watu wengine wengi huenda pale wakitokea sehemu mbali mbali.

“Kwa kweli matibabu yapo, na kwa kuwa walinipenda wakanizawadia na zawadi ya kanzu, kofia pamoja na fimbo, sikusema kuhusu usinga na unyoya wala habari zaidi ya Umbirikimoni.

“Fimbo kama za machifu hizi…” alisema huku akiishika kama anaipima uzito hivi.

Nikamkatisha kwa kumuuliza kuhusu Shangazi na Mama yangu pamoja na kaka.

Akaniambia kuwa yeye alivyorudi Kabwe baada ya kutoka huku aliwakuta salama ingawaje kaka kidogo alikuwa anaumwa kitu kama malaria, walizunguka Kabwe nzima kutafuta dawa zake maana yeye hatumii klorokwini huwa zina…

“ee najuwa, ana aleji nazo, enhe” nilimkatisha na kuruhusu aendelee

“Walivyokosa wakaamua kwenda Sumbawanga kutafuta metakelfin ambazo humtibu vizuri. Tangia walivyoenda hawajrudi na hali ya kaka yako siyo mbaya sana maana ilibidi tutumie dawa za miti shamba kujaribu kumtibu.” Aliendelea

Basi ikawa ni mwendo wa stori za furaha za hapa na pale hadi muda wa kupakia mapipa ulipofika tukaenda kushuhudia yakipangwa vyema na jioni yake tukaanza safari kurudi ng’ambo upande wa Tanzania.

Safari hii bahari ilikuwa imetulia hadi tulipofika Kabwe usiku wa manane na moja kwa moja tukaelekea nyumbani kwa Ustadhi.

Nikaenda chumba alicholala kaka kwa ajili ya kujilaza, lakini kabla sijalala nikajikuta namgusa na ile fimbo kichwani na akapiga chafya bila kufungua macho akalala tena bila kujuwa kama kuna mtu ameingia chumbani.

Nami nikapitiwa na usingizi hadi majogoo walipoanza kuwika nikafumbua macho, nikamuona kaka amekaa chini ananiangalia kwa kunishangaa…

“Shikamoo kaka, nimerudi salama, nimepona…” yalikuwa maneno yangu ya awali kwake.

Aliitikia salamu kisha mie nikaendelea kulala maana nilihisi uchovu.

Usingizini nikaota kuwa Shangazi alienda Polisi kutoa ripoti ya kupotelewa na mtoto ziwani, nikaota kuwa amewajulisha na Bagamoyo kwa njia ya ujumbe wa polisi kuwa nimepotea ziwani na nahofiwa kuwa nimefariki.

“Pazi, Pazi..!” ilikuwa ni sauti ya kaka akiniamsha ili nijiandae kupata staftahi

“Kumekucha, amka upige mswaki…” alisema.

Wakati tunakunywa chai ndipo Ustadhi akaanza kusimulia yaliyojiri…

“Alhamdulillah mdogo wako nimemrudisha salama, nilipompeleka amepata matibabu na amesema yeye mwenyewe kuwa amepona kabisa” alisema Ustadhi.

Kaka alishukuru pale kwa ukarimu na muongozo lakini naye akamuambia Ustadhi kuwa tangia ameniona anajihisi malaria kupona kabisa. Basi wote tukafurahi na tukawa sasa tunajadiliana namna ya kufanya maana akina shangazi bado wapo huko walipoenda kununua dawa na hawajarudi, tunaanzia wapi? Tulijiuliza.

“Tusubiri hadi kesho jioni, wasipoonekana basi tuanze hatua za kuwafuatilia.” Alisema Ustadhi na tukakubaliana na wazo lake.

Usiku ule boti haikupata mzigo wa kutosha hivyo haikusafiri, tulibaki na kuzurura mwambaoni mwa Ziwa Tanganyika mwalo wa Kabwe.

Siku ya pili lilipokuja gari ya mizigo, tukawaona Shangazi, mama na watu wengine wawili wakija upande wa nyumba ya ustaadhi, mara mama akaniona, akanikimbilia kwa furaha na kunikumbatia…

“Mwanangu, mwanangu, mwanangu…” ilikuwa ni kauli yake aliyoirudia rudia mara kadhaa huku akibubujikwa na machozi.

Shangazi naye akaja na kunikumbatia huku machozi yakimlengalenga.

Wale watu wengine wawili walibaki wamesimama huku wakituangalia. Nilijuwa baadaye kuwa walikuwa askari Polisi waliokuja kufanya upelelezi wa tukio lile.

Baada ya utambulisho, ilifuata kipengele cha kutoa maelezo kwa askari.

Ustadhi alielezea kuwa alinipeleka Zaire kwa ajili ya matibabu, lakini matibabu yakachukuwa muda mrefu, yeye akaamua kuniacha kule ili kazi zake zisisimame, matibabu yalivyokamilia akanifuata na kunirudisha Kabwe juzi yake usiku.

Mmoja wa wale askari akaandika maelezo. Kisha Ustadhi akaingia ndani na kutoka na kiasi cha hela kama elfu ishirini hivi na kuwapatia wale askari, wakakenua meno na kupeana mikono pale shughuli ikawa imeisha.

“Mama, inabidi urudi Sumbawanga uje ufunge jalada la shauri lako…” alisema yule askari mwingine amabaye hakuwa anaandika na kutuaga na kuondoka zao kuelekea stendi.

Tulibaki pale barazani kwa mazungumzo mbalimbali na nikamsikia Ustadhi akimuambia msaidizi wake kuwa leo ataenda peke yake nga’ambo.

Stori ziliendelea kunoga…

Shangazi: “Kwa hiyo umepona kabisa mwanagu?”

Mimi: “Ndiyo Shangazi, nawe utapona matatizo yako ya kifua kinacho kubanaga”

Shangazi akacheka, kisha akasema, “mimi huko siendi, nawaogopa hao Mbirikimo.”

Sikuwaambia habari zaidi ya Mbirikimo.

Mimi: “Hapana Shangazi, huna haja ya kwenda, nitakutibu mimi maana wamenifundisha dawa”

Mama akaniangalia kisha akasema, “Kama una dawa basi mtibu na kaka yako ambaye kila mwezi anasumbuliwa na malaria”

Mimi: “Tayari mama nimeshamtibu” kisha nikacheka

Kaka akaniangaliaaa kisha akasema, au kweli? Maana tangia nimekuona naona afya yangu ipo vizuri kuliko kawaida.

Mimi: “Ni kweli kaka, nimekutibu mara tu nilipofika”

Wote wakaangaliana na kusema “makubwa!”

Hali iliendelelea hivyo hadi jioni ikafika na tukaazimia kesho yake tuanze safari ya kwenda Lyazumbi kisha Sumbawanga kwanza.

Mke wa Ustadhi alituandalia samaki wa kukaanga wengi kama zawadi ya kula njiani huko tuendako, Ustadhi alitupatia mizizi fulani ambayo niliitambua kuwa ni ya mendreke (mandrake roots) ya kumpelekea mzee Njembi kule Kigoma na pesa kiasi kama zawadi. Lakini nikakataa kupokea pesa za Ustadhi, nikamuuliza anataka kumpa kiasi gani Mzee Njembi? Akanijbu anatamka kumpa elfu hamsini. Basi nikasema hilo nitalimaliza mimi. Nikaona Shangazi, mama na Kaka wanaangaliana.

Basi tuliagana kwa matarajio ya kuonana siku nyingine.

Alfajiri tukaondoka kwa gari ya mizigo ya kwanza, safari ilikuwa salama hadi tulipofika Lyazumbi, sisi tukashuka kwa ajili ya kupata chai.

Shangazi alikuwa mpenzi sana wa kuku, basi alifakamia kuku wa pale Lyazumbi hadi akashiba ndi. Mama, kaka na mimi ni wapenzi sana wa samaki, na tulifurahia samaki wa ziwani, maisha yetu awali tulikuwa tunajuwa ziwani Tanganyika kuna Migebuka, Sato na Sangara tu, lakini kumbe si hivyo, kuna samaki wa aina nyingi tena watamu sana ukiachilia mbali dagaa.

Baada ya mapumziko mafupi tulipata usafiri mwingine wa kwenda sumbawanga kwa gari ya serikali, lendikruza mkonga ya halmashauri. Tuliliacha lile gari ya mizigo pale wakifanya marekebisho madogo kwenye gari yao sisi ‘tukaishia…’

Haikuchukuwa muda mrefu tukaingia Namanyele mjini, tukawa na mapumziko mafupi, maana dereva alikuwa ana shuhuli fupi pale kisha tuaanza tena safari ya kwenda Sumbawanga. Njia haikuwa rafiki lakini kwa gari tuliyopanda haikutuchukuwa muda mwingi maana jioni ile kabla ya jua kuzama tuliingia Sumbawanga na dereva alitushusha ya raound about ya mkoani ambapo alituambia hapo mtaa wa pili kuna lodge nzuri tu za bei nafuu.

Tulitembea kwa miguu taratibu hadi mtaa wa pili ambapo tulipata lodge nzuri na bei ilikuwa nafuu. Baada ya wote kuoga, tulitoka kwa ajili ya kutafuta sehemu ya chakula safi. Tukauliza kwa mhudumu akatuambia…

“Shukeni na barabari hii jirani na sisiemu kuna hoteli ya Wasomali hapo wanapika vyakula vizuri”

Tukafuata maelekezo hadi hapo hotelini, hapakuwa mbali kiasi cha dakika tatu nne hivi kwa kutembea na wamama, tukapata chai ya maziwa safi, chapati mchuzi safi na matunda. Yule baba mhudumu wa Kisomali alikuwa mchangamfu, nadhani aligunduwa kuwa sisi ni wageni kwa lafudhi yetu hivyo akatupigisha stori za ukaribisho na hakika chakula kilikuwa kizuri. Baadaye nikajuwa kuwa ile ni hoteli ya kwake.

Siku ilipita, asubuhi na mapema saa mbili tukawa pale Polisi.

Njiani wakati tunaulizia jinsi ya kufika Polisi tulivyofika barabara kubwa tu ya Tunduma Sumbawanga, Shangazi netiweki ikarudi na kuanza kutuelekeza…

“Wifi, sisi tulilala upande wa kuleee…” alimuambia mama huku akionesha ng’ambo ya barabara

Basi tukajongea kwa miguu, tukapita Posta hadi kufika Polisi.

Wale askari waliokuja Kabwe wakatuona, shangazi akaitwa na faili likafungwa, kisha Shangazi akawapatia hela sikujuwa kiasi gani lakini kwa mbali niliona tu meno ya askari wakifurahi na kupeana mikono.

Akili sasa ikawa imetulia na mawazo ya kurudi Kigoma yakatamalaki.

Tukaenda ofisi za Sumry kwa ajili ya booking ya kesho asubihi.

**********

Itaendelea...
 
11. UJIJI MARA YA PILI

Akili zilitulia kiasi sasa cha kuanza kufikiri vyema na kupanga safari ya kurudi Ujiji Kigoma.

Usiku ule tuliutumia kujadili mengi yatokanayo na matibabu yangu.

Sikuthubutu kuelezea safari yangu ya Ujinini.

"Haya, na hiyo kanzu ya ajabu na fimbo umepewa huko huko? " Alidadisi Mama

"Ndiyo Mama, na huko niliambiwa kuhusu sababu iliyopelekea kupoteza ujauzito mara mbili." Nikamjibu na kuongezea, nikamueleza yote kuhusu hila za ukewenza pamoja na uchawi kutoka Tumbatu.

Mama alishangaa sana na akawa ameshika tama anawaza (nadhani alianza kuunganisha matukio yake ya ajabu yaliyomtokea huko nyuma...)

"Hata kaka alijaribiwa kuuwawa kwa sumu mara kadhaa lakini kwakuwa ana ‘malalika wakali’ imeshindikana na wakaamua kumpa ugonjwa unaofanana na malaria, ni ungonjwa wa kichawi, lakini bahati nzuri kama nilivyosema nao nimeumaliza, hatoumwa tena ugonjwa huo.

Tuliongea mengi sana na Mama akashukuru eti ametimiza nadhiri yake sasa atakuwa na amani.

Sikutaka kumuambia mama kuhusu siku ile alivyokuwa ufukweni baharini na usiku wake wakati akiwa na baba na jinsi ujauzito ulivyoingia... Niliona siyo muda muafaka.

Tulivyochoka kuongea mimi na kaka tukaingia chumba chetu kulala na Shangazi ma mama wakaingia chumba chao.

Mapema asubuhi tukaenda stendi ya mabasi kwenye ofisi za Sumry, basi lilichelewa kufika hivyo tulikaa hadi saa mbili asubuhi.

Baada ya muda basi likafika...

"Samahani abiria wetu, tulikuwa na marekebisho muhimu ndio maana basi limechelewa..." Alisema mmoja wa wahudumu wa Sumry.

Tukaruhusiwa kuingia ndani ya basi na wafanyakazi wakawa wanaweka mizigo ta abiria kwenye buti.

Nikasikia sauti ikiniambia, "ongea na baba yako kwenye simu..."

Nikamwita shangazi... "Shangazi simu yako iko wapi..?"

Akaniambia "Kopo hilo, nimeliweka kwenye mkoba wangu mdogo..."

"Naiomba" nika mwambia, akapekenyua kisha akanipatia.

"Unadhani utapana mtandao hapa!?" Aliuliza

Nikajibu "Ngoja nijaribu..."

Nikaiwasha, kisha nikasikia kale kamlio tululiii, ikawa imewaka, kuangalia signal za mnara hakuna. Nikasema ngoja nijaribu hivi hivi..

Tututu, tututututu, tu! He kama masihara simu ikaanza kuita

Ngriiin griin, griiin griin

Mara ikapokelewa...

"Haloo" upande wa pili ukajibu


"Shangazi ongea na baba" nikampatia shangazi simu.

Huku akishangaa, akasema, "Haloo"

Wakasalimiana pale, baba akauliza mko wapi, akamjibu kuwa tupo Sumbawanga tunaelekea Mpanda...

Wakaongea weee pale tena kwa sauti kubwa watu wakawa wanatuangalia sisi na muujiza wetu wa kuongea na simu ya mkononi...

Shangazi akampa mama na akamuhamikishia baba kuwa sote tupo salama apuuze zile jumbe za kipolisi kuhusu kupotea kwa Pazi.

Ghafla simu ikakatika na punde si punde safari ya kuelekea Mpanda ikaanza.

Njia haikuwa rafiki lakini kwa umahiri wa dereva safari ilikuwa nyepesi.

Tukafika Nyamanele kisha Lyazumbi kwenye kuku watamu na njia panda ya kwenda Kabwe.

Kama kawaida shangazi alikula kuku na sisi wengine tuliendelea kufaidi samaki wa ziwani zawadi kutoka kwa mke wa Ustadhi.

Safari ikaendea hadi kibaoni ambao kulikuwa na mizigo ya kupakia.

Kutoka hapo tukapita njia tofauti na ile ya kwanza wakati tunatoka Mpanda kwenda Lyazumbi.

Baada ya kilomita sabini hivi tukafika stalike.

Njiani tulivamiwa na mbong'o lakini niliwafukuza kwa muujiza wa fimbo kimya kimya.

Safari iliendelea hadi tukaingia Mpanda mjini. Ilishakuwa jioni.

"Twendeni Stesheni tukabahatishe usafii..." Aliendekeza kaka

"Hapana, tafafute lodge ya kulala tupumzike... " Nilijibu.

"Hela zimebaki chache, utaishiwa tutakwama... " Alidakia Shangazi...

"Mimi nitalipia..." Wote wakageuka kuniangalia...

"Ninazo hela kidoo nilipewa Umbirikimoni." Nikajibu huku nikiingiza mkono kwenye rasket na kutoa kibunda cha hela dola kumi kumi.

"Hizi hapa... " Niliwaonesha na wote wakapigwa na butwaa

" Dola!? " Kaka alishangaa kwa sauti.

Ndiyo, tutatafuta chenji tukifika Tabora au Kigoma.

"Hebu zilete kwanza" Shangazi akazichukuwa zile hela, akazinusa kisha akasema ni dola halali ni dola za ukweli. Kisha akaziweka kwenye mkoba wake.

Tukatafuta lodge ya jirani tukalala.

Asubuhi tukaenda Stesheni kuulizia usafiri wa treni kwenda Tabora.

"Abiria itakuwepo Alhamisi asubuhi, keshokutwa" alijibu mhudumu wa pale stesheni

"Labda nikufanyieni mpango wa gusi, litaondoka jioni hii hii ya leo, mnazo nauli hapo? " Alihoji

Shangazi akatoa pesa akampatia.

"Vizuri sana, saa kumi muwe mmeshafika hapa kwa maelekezo zaidi" akasema kisha akatuaga.

Jioni ile tulifika na kupanda lile gusi na kuanza safari na Alfajiri tukawa tumefika Tabora, tukashuka na kusubiri kukuche twende mjini benki tukabadilishe zile dola kuwa shilingi

Kwakuwa shangazi alikuwa mjanja mjanja alienda na dola kumi pale benki ya Taifa ya biashara, akapewa zaidi ya elfu kumi na tatu.

Shangazi akaamua kuongeza dola, akatoa kumi kumi nne, wakamuomba passport na urasimu mwingi, Shangazi akaondoka.

"Wamenikatalia kuchenji wanataka vibali sijui nini kujaza fomu nikaamua kutoka" Alisema Shangazi alipokuja kule nje.

Tukashauriana twende hadi Kigoma kwa kuwa kule ni mpakani lazima tutapata chenji.

Tukawa tunatembea kuelekea Stesheni.

Wakati tunakaribia, tulishuhudia vichaa wengi sana njiani na hata pale stesheni. Yani wendawazimu wengi sana nadhani palikuwa panaongoza nchi nzima.

Nikasema ngoja nijaribu hii fimbo...

Nikamgusa nayo mama mmoja kichaa aliyekuwa yupo nusu uchi kabisa akiwa na mzigo wa matambala na makopo

Mara akaanguka chini,

"We Pazi, umemfanya nini" Kaka aliuliza

Sikujibu kitu, ghafla yule kichaa akaamka, akakaa, akasimama lakini mara akachutama (akachuchumaa) huku akijiziba sehemu zake za siri...

Mama akamrushia kitenge, akakidaka akajisitiri na kuondoka eneo lile huku akiacha mzigo wake wa makopo na matambala palepale...

"Ameshapona ..." Nilisema

"Alhamdulillah" sauti ya mama ilisikika akimshukuru Mwenyezi Mungu.

Nilivyoona vile, sikuishia kwa huyo tu, nikawagusa na wengine hususani wanawake na baadhi wanaume, wote baada ya kuzinduka wakawa wanakimbia eneo walilopo na kwenda kujificha...

Watu wakaanza kujaa na kutuzingira, kila mmoja akawa anaomba afanyiwe maombi.

Vurugu ikawa kubwa pale huku kaka akiwa na kibarua kigumu cha kuwazuia watu na kuwapanga vizuri, Mama na Shangazi wakiwa wameduwaa tu wasijie la kufanya.

Nikawambia ule umati

"Akina mama, leteni vitenge kwa ajili ya kuwasitiri akina mama wenzenu ambao ni vichaa

Ghafla vikapatikana kama vitenge kumi na tatu hivi...

Nikamwambia kaka anifuate na akina shangazi wasubiri pale pale...

Nikawafuata vichaa waliokuwepo maeneo yale na kiwagusa na fimbo kisha kumuweke vitenge viwili na kuondoka

Kuna baadhi ya vichaa wakawa wananikimbia lakini nilifanikisha kumaliza vile vitenge vyote...

Mimi na kaka tukarudi pale kwa akina shangazi na kuanza kuwaambia...

"... Mwenye hirizi aivue na kuitupa hapo chini... " Nilitoa amri

Watu karibia asilimia 60 ya waliokusanyika alitupia pale hirizi, nilishangaa sana kuona wingi wa hirizi kiasi kile, na zilikuwa za mtindo mbalimbali

"Leteni mafuta ya taa" niliamrisha tena

Baada ya muda kupita nikapewa kiguduria cha lita tano...

"Leo tutachoma moto hirizi hizi, na wewe ambaye una hirizi lakini hujaileta hapa, ondoka eneo hili maana utadhurika..." Baadhi ya watu wakaondoka...

Nikazimwagia mafuta ya taa na kuzichoma moto.

Nikasogea pembeni kidogo na kuanza kuwagusa kwa fimbo wale waliokuwa jirani yangu, kila aliyeguswa alipepesuka na kukaa sawa na kuondoka, nadhani walijisikia vyema.

Zoezi liliendelea hadi lilipoingiliwa na askari mgambo wa stesheni kwa kutuambia kuwa abiria kutoka Pwani inakaribia hivyo watu wajiandae kwa kuingia...

Nikasitisha lile zoezi na watu walitaka kujuwa naelekea wapi...

"Sharifu, unaelekea Dodoma Mwanza? Unaenda Kigoma au Mpanda..."

Nilijibu kuwa tunaelekea Kigoma. Baadhi ya abiria walifurahi na wengine walihuzunika. Lakini nikawaambia, nitafanya ziara maalumu mikoa yote Tanzania, hivyo wasiwe na wasiwasi.

Hakika nilijishangaa mwenyewe kwa yale yote yaliyotokea pale. Nikawa kimya huku Kaka akiwa jirani nami na Shangazi akiwa anatabasamu huku mama machozi yakiwa yanamlengalenga.

_
Niliendelea kumsikiliza kwa makini kijana Pazi na muda ulikuwa umeenda sana maana tayari ilikuwa ni saa saba za usiku lakini sikuchoka kumsikiliza
_

Mara tukasikia honi ya treni ya kuashiria inawasili kisha ikaingia na kupaki njia namba mbili.

Baadhi ya abiria wakashuka na zoezi la kubadilisha mabehewa lilifanyika...

Baada ya saa kama tatu hivi, tukasikia sauti kutoka kwenye spika ikielekeza jinsi treni zitakavyo ondoka.

Nasi tukaingia kwenye behewa la Kigoma tayari kwa safari.

Saa mbili baadaye treni yetu iliyokuwa njia namba moja ikaanza kuondoka.

Tulisafiri usiku kucha tukisimama simama, na hatimaye alfajiri tukaingia Kigoma.

Tukachukuwa teksi ili itupeleke Ujiji kwa Mzee Njembi.

Dakika chache baadaye tukawasili na kupokelewa.
***

Mzee Njembi alifurahi sana kutuona , tukasalimiana

Na nikamkabidhi zawadi zake kutoka kwa Ustadhi, nilimpatia ile mizizi iliyokuwa imehifadhiwa vizuri na kiasi cha fedha kama elfu hamsini ambazo nilimuomba shangazi anipatie.

Tukaongea kwa kirefu na kunisifu kwa ujasiri kwa yaliyonikuta Umbirikimoni.

Hapa napo sikueleza habari za Ujinini.

Kaka akapewa mwenyeji ila aende bandarini kufanya 'chenjee' ya dola kama alivyoita yule mwenyeji.

Waliporudi kaka alisema...

"Wauza vitenge wamenichenjia tena kwa reti nzuri"

Tukafurahi kwa pamoja na kisha kumpatia Mzee Njembi shukrani ya elfu 30, akakataa, akasema "nipeni elfu kumi tu nitanunua kitu cha ukumbusho."

Baada ya chakula cha mchana tukaaga na kurudi Kigoma mjini.

Safari hii tulikuwa na hela za kutosha, tuka check in Kigoma Hotel ambayo ipo jirani tu na Stesheni papo hapo.
*********

Itaendelea...
 
12. KUPANDA NDEGE KWA MARA YA KWANZA

"Mrudi Ujiji safari nyingine lakini siyo kwa kutafuta tiba bali kwa kunitembelea na kubadilishana mawazo." Hii ilikuwa kauli ya Mzee Njembi wakati tunaagana pale Ujiji.

Kila mara sauti hii ilikuwa inajirudia kichwani mwangu.

Jioni ile pale restaurant ya Kigoma Hotel wakati tukisubiri chakula chetu kiandaliwe, nilijaribu tena kupiga simu kwa Baba. Hakukuwa na network kwenye simu ile lakini simu iliita na mimi nikaanza kuongea na baba kiasi cha kuridhika na kisha kumpatia kaka naye akaongea halafu akampatia Shangazi naye akaongea weeee kisha akampatia Mama.

Baada ya mazungumzo na chakula tukaamua tufanye mpango wa kurudi Dar ea Salaam kwa ndege.

Kama kawaida Shangazi akaingia front na kupata taarifa za ndege.

Aliporudi alituambia kuwa kesho mchana kutakuwa na ndege ndogo itakayo waleta watu wa WFP (World Food Program), hivyo saa tano asubuhi tuwe pale uwanja wa ndege.

Tukaagana na kupumzika mimi na kaka chumba kimoja double, Shangazi na Mama chumba kimoja double.

Asubuhi baada ya breakfast ya uongo na kweli waiitayo kontineto, tuli check out na kuchukuwa teksi hadi airport ampapo hapakuwa mbali pia.

Ilipofika saa sita ile ndege ikatua na kushusha wazungu wawili na waafrika watatu, baada ya dakika chache tukafuatwa na kuambiwa tuingie kwenye Ndege maana itaondoka siyo muda mrefu.

Mimi, kaka, na Mama ndio ilikuwa mara yetu ya kwanza kupanda ndege.

Baada ya dakika chache zingine injini ikangurumishwa kwa sauti kubwa kisha ndege ikaanza kutembea kisha kutembea kwa kasi ghafla hiyoo tupo angani.

Nikakumbuka safari za usiku za kupaa na kuangalia ardhi kama mwewe...

Safari hii nilikuwa naona ardhi mchana kweupee na kufurahia mandhari ya nchi yetu na uumbaji wa Mungu.

Kutoka Kigoma tulielekea Arusha ambao rubani alituambia ana makaratasi ya kuchukuwa, kisha ndipo tukapaa tena kuelekea Dar es Salaam.

Ilikuwa safari nzuri yenye utalii wa juu kwa juu ndani yake lakini kutoka Arusha kuja Dar kuna sehemu tulipita kwenye korogesheni (turbulence) kwa sekunde kadhaa lakini tukapapita...

Tulitua DIA saa nne usiku.

Tukashuka na kumshukuru Mwenyezi Mungu na rubani, tukatoka nje ya sehemu za ukaguzi kisha tukaenda upande parking za magari kuchukuwa teksi.

Tukapata moja maridani na kutupeleka hadi Kariakoo ambapo tulikubaliana tufikie pale jirani na nyumbani, hivyo tukalala Al Uruba Hotel.

Asubuhi tukaenda pale nyumbani tulipo pangisha kuwasalimia wapangaji na kuona pakoje na mimi kutaka kujuwa kuhusu mwari Salma na mama yake.

Tukaambiwa kuwa mama Salma alifariki, kisha Salma naye akafariki.

Nikaulizia kuhusu Sinasudi nikaambiwa kuwa alikuja mara moja tu na akaondoka hajaonekana tena.

"Kuna siku alikuja akaomba funguo akaingia ndani akachukuwa nguo zake na kuondoka na begi lako... Tangia siku hiyo hatujamuona tena.. " alisema mmoja wa wapangaji.

"Baba Salma ambaye alikuwa dereva wa malori alihama baada ya misiba, hivyo vyumba vyao amepanga mtu mwingine na hela anakuja kuchukuwaga ndugu yenu. " Alisema

Mara moja tukajuwa ni ndugu yetu yupi aliyekuja kuchukuwa kodi.

Nikaomba funguo nikaingia chumbani kwangu, nikapaangalia kwa muda kisha nikafunga mlango na kumwambia yule mpangaji kiongozi kuwa, na hiki chumba pangisha, hela nitafuata mwenyewe unitunzie.

Tuliendelea kuongea pale wee hadi tukaridhika hivyo tukaamua sasa tuelekee mtaa wa Congo na Mkunguni kuangalia basi liliopo la kwenda Bagamoyo.

Bahati nzuri tukakuta basi moja la Chemsi (Champs Mulji) ambalo lilikuwa zuri sana lilitwa Msala, tukapanda na kusubiri lijae ili safari ianze.

Baada ya kuanza safari, saa mbili baadaye tulifika stendi mpya Bagamoyo palipokuwa pakiitwa "Kwa Kibwana"

Tulishuka na kijana mmoja aitwaye Kurame alitusaidia kubeba begi la Shangazi na mama kwa ujira hadi nyumbani tulipokiwa tunaenda.

Kuanzia tulivyotuwa Dar es Salaam network kwenye simu ya Shangazi ilirudi vizuri na kukawa na mawasiliano ya moja kwa moja hadi tunaingia Bagamoyo na kukuta mapokezi makubwa yameandaliwa.

Watu wa nyumbani kwa mama mkubwa eneo la Chuguuni katikati pia walikuja tukawa wote kwenye nyumba ya Kisima bluu.

Mama mkubwa hakuwa na furaha sana, niliona uso wake lakini dada zetu upande wake wao walionesha furaha kama kawaida.

Tuliongea sana pale muongeaji mkubwa akiwa Shangazi na chumvi chumvi aliongeza ili kunogesha stori.

Zawadi kidogo kutoka Dar ziligawiwa kwa wote, samaki zilizobakia kutoka Kabwe tukawaonesha wakawa wanashangaa samaki wa Ziwani kila mmoja akawa anamega kiasi na kuonja...

"Wamepooza...! Hawana chumvi" alisikika mmoja wa ndugu zetu ambaye alikuwa hodari sana kupika kama mama yake, mama mkubwa.

"Wa maji baridi hao, hawanaga chumvi" kaka alijibu.

Basi ilikuwa ni furaha sana tu kwa wote na tukala chakula saa kumi na moja kwa pamoja.

Uliandaliwa wali "shaba" pilau kwa mbuzi.

Baada ya mapumziko ya siku tatu niliamua kwenda Mlingotini kwa ajili ya kumsalimia mzee wa tiba.

Alifurahi sana akataka kujuwa kama nimepona, nikamuambia safari hii nimepona kabisa.

Wakati naingia pale Mlingotini niliona vitu vya ajabu ajabu (kwa macho yangu ya sasa) maana havionekani kwa macho ya kawaida, lakini niliuchuna na kujifanya sioni chochote.

Nikampa zawadi yake ya kiasi kidogo cha fedha na kuaga.

Siku iliyofuata nikaenda kwa Mwalimu Mwaloki, alifurahi na kuniombea dua kwamba, Mwenyezi Mungu azidi kunifungua niifuate iliyo kweli.

Siku hiyo hiyo nikaenda Kwa Sheikh Mohamed na kumwambia kuwa alisema ukweli...

"Sheikh, hakika ulisema ukweli kuwa matibabu yangu yataanzia magharibi, lakini nadhani yameishia huko huko magharibi, mimi sasa nimepona... " Niliongea kwa kujiamini.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kama umepona, na kama itakuwa bado sasa njia itakuwa nyepesi, in shaa Allah tunaomba upate tahfifu" aliongea Sheikh kwa sauti yake nzito ile ya ki mwinyi mwinyi.

Nikampa hela kidogo akakataa akasema kaninunulie ubani, mtama na juzuu kwa ajili ya watoto. Basi nikakimbia dukani eneo la Gongoni na kununua vitabu na mahitaji aliyoniagoza kisha nikarudi na kumkabidhi.

Akanishika kichwa akaniombea dua...

"... (Tafsiri) Mwenyezi Mungu akuzidishie elimu na akuruzuku riziki yenye wasaa... "

Nikamshukuru pale, tukaagana kisha nikaelekea kwa mzee Zahiri.

Nikamkuta yupo katikati ya maombezi yake ya vingoma na wakina mama wakicheza na kutoa milio ya ajabu

Lakini nilivyoingia uwanjani tu pale wote wakatulia, kisha wakajipanga mstari na kuinamisha vichwa na kunisalimia " Assalaam aleikum yaa Shariff"

Tabibu Zahiri akawa anashangaa, mie nikajifanya sioni na kuendelea kuitikia salaam.

" Wa aleikum salaam yaaa ahl... " Nikasita kidogo.

Nikamgeukia Tabibu Zahiri na kumsalimia kwa unyenuekevu naye akaitikia.

Zoezi lake likawa kama limezimika hivi kwa muda, wale wamama wote walikaa kwa kutulia na kuinamisha vichwa.

Nikamshukuru kwa muongozo na kwamba alisema kweli mimi si wa upande ule bali wa kitabu, na Sheikh Mohamed amenisaidia...

Nilampa ujira wake akapokea na kuniambia kwa kuniuliza, mbona imekuwa hivi kulikoni?

Aliuliza akioneshea upande ule wa akina mama...

"Nikatoa fimbo yangu na kuwanyooshea wale akina mama na kusema

"Shatitu yaa mahulkatun..." Nikamaanisha tawanyikeni enyi viumbe wa Mwenyezi Mungu...

Mara wote pale wakalala chini kwa sekunde chache kisha wakaamka na kushangaa huku wakijikung'uta na kuuliza nini kimetokea.

Nikamwambia Tabibu Zahiri kuwa hao tayari wameshapona na hawatokuja tena hapa kwa ugonjwa huo wa kusababishwa na majini (mapepo).

Nikaaga nikaondoka huku Mzee Zahiri bado akiwa anajiuliza maswali.

Siku ukaishia hivyo.

Nikaanza kumtafuta Shariff mtoto bila mafanikio, nikaambiwa amenunua gari basi Isuzu hivyo zinamfanya awe bize nayo.

“Siku hizi yupo bize na chite ukae…” alisikia mmoja wa majirani.

Baada ya wiki mbili kuisha, nilimuaga Baba na Mama rasmi kuwa sasa naenda kuitumikia fani yangu mpya ya utabibu.

Wakanipa baraka zote na nikaenda kwa minajiri ya kuanza kufanya tiba kwa watu huku nikiendelea na kazi za baba.

Kituo cha kwanza kilikuwa pale Mkunguni na Livingstone nyumbani kwa ajili ya kuangalia kodi na kuchukuwa vitu vyangu kwa ajili ya makazi mapya nitakayo tafuta.

Nikakuta chumba kimeshapangishwa na nikapewa kodi yangu na vitu vyangu viliwekwa stoo.

Kwa hali niliyoikuta stoo sikupenda, nikamwambia yule mpangaji kiongozi kuwa pia vitu hivyo aviuze anitunzie hela yangu.

"Hivi basi nitavinunua mimi, nitajie ni kiasi gani.." alidakia haraka haraka.

Ok, hatuwezi kushindwana, nitarudi baada ya wiki moja unipatie kiasi fulani (nikamtajia pale)

Hakubisha, maana kilikuwa ni kiasi kidogo cha kawaida. Nikaondoka na kwenda lodge ya jirani.

Usiku ule niliazimia kwenda Pangani kwa yule Mganga kwenda kumshukuru kwa muongozo. Hivyo ilivyofika saa nane na nusu usiku nikafungua mlango wa lodge kisha nikaushindika (kuurudishia) na kuacha funguo mlangoni mimi nikiwa humo humo ndani ya lodge, Nikazima taa nikafanya yangu fyuuuu nikawa hewani, baada ya kutalii sehemu mbalimbali ilipokatibia saa kumi na moja nikatua jirani na dispensary ya Kikokwe, nikawa kawaida nikaanza kutembea kwa miguu kuelekea nyumbani kwa Shariff.

Nyumba ya Shariff ilikuwa imejitenga kidogo na ilikuwa mwendo wa kama wa robo saa hivi kutoka pale zahanati.
**********

Itaendelea…
 
Back
Top Bottom