Koyewilbard
New Member
- Oct 24, 2022
- 4
- 4
12. KUPANDA NDEGE KWA MARA YA KWANZA
"Mrudi Ujiji safari nyingine lakini siyo kwa kutafuta tiba bali kwa kunitembelea na kubadilishana mawazo." Hii ilikuwa kauli ya Mzee Njembi wakati tunaagana pale Ujiji.
Kila mara sauti hii ilikuwa inajirudia kichwani mwangu.
Jioni ile pale restaurant ya Kigoma Hotel wakati tukisubiri chakula chetu kiandaliwe, nilijaribu tena kupiga simu kwa Baba. Hakukuwa na network kwenye simu ile lakini simu iliita na mimi nikaanza kuongea na baba kiasi cha kuridhika na kisha kumpatia kaka naye akaongea halafu akampatia Shangazi naye akaongea weeee kisha akampatia Mama.
Baada ya mazungumzo na chakula tukaamua tufanye mpango wa kurudi Dar ea Salaam kwa ndege.
Kama kawaida Shangazi akaingia front na kupata taarifa za ndege.
Aliporudi alituambia kuwa kesho mchana kutakuwa na ndege ndogo itakayo waleta watu wa WFP (World Food Program), hivyo saa tano asubuhi tuwe pale uwanja wa ndege.
Tukaagana na kupumzika mimi na kaka chumba kimoja double, Shangazi na Mama chumba kimoja double.
Asubuhi baada ya breakfast ya uongo na kweli waiitayo kontineto, tuli check out na kuchukuwa teksi hadi airport ampapo hapakuwa mbali pia.
Ilipofika saa sita ile ndege ikatua na kushusha wazungu wawili na waafrika watatu, baada ya dakika chache tukafuatwa na kuambiwa tuingie kwenye Ndege maana itaondoka siyo muda mrefu.
Mimi, kaka, na Mama ndio ilikuwa mara yetu ya kwanza kupanda ndege.
Baada ya dakika chache zingine injini ikangurumishwa kwa sauti kubwa kisha ndege ikaanza kutembea kisha kutembea kwa kasi ghafla hiyoo tupo angani.
Nikakumbuka safari za usiku za kupaa na kuangalia ardhi kama mwewe...
Safari hii nilikuwa naona ardhi mchana kweupee na kufurahia mandhari ya nchi yetu na uumbaji wa Mungu.
Kutoka Kigoma tulielekea Arusha ambao rubani alituambia ana makaratasi ya kuchukuwa, kisha ndipo tukapaa tena kuelekea Dar es Salaam.
Ilikuwa safari nzuri yenye utalii wa juu kwa juu ndani yake lakini kutoka Arusha kuja Dar kuna sehemu tulipita kwenye korogesheni (turbulence) kwa sekunde kadhaa lakini tukapapita...
Tulitua DIA saa nne usiku.
Tukashuka na kumshukuru Mwenyezi Mungu na rubani, tukatoka nje ya sehemu za ukaguzi kisha tukaenda upande parking za magari kuchukuwa teksi.
Tukapata moja maridani na kutupeleka hadi Kariakoo ambapo tulikubaliana tufikie pale jirani na nyumbani, hivyo tukalala Al Uruba Hotel.
Asubuhi tukaenda pale nyumbani tulipo pangisha kuwasalimia wapangaji na kuona pakoje na mimi kutaka kujuwa kuhusu mwari Salma na mama yake.
Tukaambiwa kuwa mama Salma alifariki, kisha Salma naye akafariki.
Nikaulizia kuhusu Sinasudi nikaambiwa kuwa alikuja mara moja tu na akaondoka hajaonekana tena.
"Kuna siku alikuja akaomba funguo akaingia ndani akachukuwa nguo zake na kuongoka na begi lako... Tangia siku hiyo hatujamuona tena.. " alisema mmoja wa wapangaji.
"Baba Salma ambaye alikuwa dereva wa malori alihama baada ya misiba, hivyo vyumba vyao amepanga mtu mwingine na hela anakuja kuchukuwaga ndugu yenu. " Alisema
Mara moja tukajuwa ni ndugu yetu yupi aliyekuja kuchukuwa kodi.
Nikaomba funguo nikaingia chumbani kwangu, nikapaangalia kwa muda kisha nikafunga mlango na kumwambia yule mpangaji kiongozi kuwa, na hiki chumba pangisha, hela nitafuata mwenyewe unitunzie.
Tuliendelea kuongea pale wee hadi tukaridhika hivyo tukaamua sasa tuelekee mtaa wa Congo na Mkunguni kuangalia basi liliopo la kwenda Bagamoyo.
Bahati nzuri tukakuta basi moja la Chemsi (Champs Mulji) ambalo lilikuwa zuri sana lilitwa Msala, tukapanda na kusubiri lijae ili safari ianze.
Baada ya kuanza safari, saa mbili baadaye tulifika stendi mpya Bagamoyo palipokuwa pakiitwa "Kwa Kibwana"
Tulishuka na kijana mmoja aiywaye Kurame alitusaidia kubeba begi la Shangazi na mama kwa ujira hadi nyumbani tulipokiwa tunaenda.
Kuanzia tulivyotuwa Dar es Salaam network kwenye simu ya Shangazi ilirudi vizuri na kukawa na mawasiliano ya moja kwa moja hadi tunaingia Bagamoyo na kukuta mapokezi makubwa yameandaliwa.
Watu wa nyumbani kwa mama mkubwa eneo la Chuguuni katikati pia walikuja tukawa wote kwenye nyumba ya Kisima bluu.
Mama mkubwa hakuwa na furaha sana, niliona uso wake lakini dada zetu upande wake wao walionesha furaha kama kawaida.
Tuliongea sana pale muongeaji mkubwa akiwa Shangazi na chumvi chumvi aliongeza ili kunogesha stori.
Zawadi kidogo kutoka Dar ziligawiwa kwa wote, samaki zilizobakia kutoka Kabwe tukawaonesha wakawa wanashangaa samaki wa Ziwani kila mmoja akawa anamega kiasi na kuonja...
"Wamepooza...! Hawana chumvi" alisikika mmoja wa ndugu zetu ambaye alikuwa hodari sana kupika kama mama yake, mama mkubwa.
"Wa maji baridi hao, hawanaga chumvi" kaka alijibu.
Basi ilikuwa ni furaha sana tu kwa wote na tukala chakula saa kumi nanmoja kwa pamoja.
Uliandaliwa wali "shaba" pilau kwa mbuzi.
Baada ya mapumziko ya siku tatu niliamua kwenda Mlingotini kwa ajili ya kumsalimia mzee wa tiba.
Alifurahi sana akataka kujuwa kama nimepona, nikamuambia safari hii nimepona kabisa.
Wakati naingia pale Mlingotini niliona vitu vya ajabu ajabu (kwa macho yangu ya sasa) maana havionekani kwa macho ya kawaida, lakini niliuchuna nakujifanya sioni chochote.
Nikampa zawadi yake ya kiasi kidogo cha fedha na kuaga.
Siku iliyofuata nikaenda kwa Mwalimu Mwaloki, alifurahi na kuniombea dua kwamba, Mwenyezi Mungu azidi kunifungua niifuate iliyo kweli.
Siku hiyo hiyo nikaenda Kwa Sheik Mohamed na kumwambia kuwa alisema ukweli...
"Sheikh, hakika ulisema ukweli kuwa matibabu yangu yataanzia magharibi, lakini nadhani yameishia huko huko magharibi, mimi sasa nimepona... " Niliongea kwa kujiamini.
"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kama umepona, na kama itakuwa bado sasa njia itakuwa nyepesi, in shaa Allah tunaomba upate tahfifu" aliongea Sheikh kwa sauti yake nzito ile ya ki mwinyi mwinyi.
Nikampa hela kidogo akakataa akasema kaninunulie ubani, mtama na juzuu kwa ajili ya watoto. Basi nikakimbia dukani eneo la Gongoni na kununua vitabu na mahitaji aliyoniagoza kisha nikarudi na kumkabidhi.
Akanishika kichwa akaniombea dua...
"... (Tafsiri) Mwenyezi Mungu akuzidishie elimu na akuruzuku riziki yenye wasaa... "
Nikamshukuru pale, tukaagana kisha nikaeleka kwa mzee Zahiri.
Nikamkuta yupo katikati ya maombezi yake ya vingoma na wakina mama wakicheza na kutoa milio ya ajabu
Lakini nilivyoingia uwanjani tu pale wote wakatulia, kisha wakajipanga mstari na kuinamisha vichwa na kunisalimia " Assalaam aleikum yaa Shariff"
Tabibu Zahiri akawa anashangaa, mie nikajifanya sioni na kuendelea kuitikia salaam.
" Wa aleikum salaam yaaa ahl... " Nikasita kidogo.
Nikamgeukia Tabibu Zahiri na kumsalimia kwa unyenuekevu naye akaitikia.
Zoezi lake likawa kama limezimika hivi kwa muda, wale wamama wote walikaa kwa kutulia na kuinamisha vichwa.
Nikamshukuru kwa muongozo na kwamba alisema kweli mimi si wa upande ule bali wa kitabu, na Sheikh Mohamed amenisaidia...
Nilampa ujira wake akapokea na kuniambia kwa kuniuliza, mbona imekuwa hivi kulikoni?
Aliuliza akioneshea upande ule wa akina mama...
"Nikatoa fimbo yangu na kuwanyooshea wale akina mama na kusema
"Shatitu yaa mahulkatun..." Nikamaanisha tawanyikeni enyi viumbe wa Mwenyezi Mungu...
Mara wote pale wakalala chini kwa sekunde chache kisha wakaamka na kushangaa huku wakijikung'uta na kuuliza nini kimetokea.
Nikamwambia Tabibu Zahiri kuwa hao tayari wameshapona na hawatokuja tena hapa kwa ugonjwa huo wa kusababishwa na majini (mapepo).
Nikaaga nikaondoka huku Mzee Zahiri bado akiwa anajiuliza maswali.
Siku ukaishia hivyo.
Nikaanza kumtafuta Shariff mtoto bila mafanikio, nikaambiwa amenunua gari basi Isuzu hivyo zinamfanya awe bize nayo.
“Siku hizi yupo bize na chite ukae…” alisikia mmoja wa majirani.
Baada ya wiki mbili kuisha, nilimuaga Baba na Mama rasmi kuwa sasa naenda kuitumikia fani yangu mpya ya utabibu.
Wakanipa baraka zote na nikaenda kwa minajiri ya kuanza kufanya tiba kwa watu huku nikiendelea na kazi za baba.
Kituo cha kwanza kilikuwa pale Mkunguni na Livingstone nyumbani kwa ajili ya kuangalia kodi na kuchukuwa vitu vyangu kwa ajili ya makazi mapya nitakayo tafuta.
Nikakuta chumba kimeshapangishwa na nikapewa kodi yangu na vitu vyangu viliwekwa stoo.
Kwa hali niliyoikuta stoo sikupenda, nikamwambia yule mpangaji kiongozi kuwa pia vitu hivyo aviuze anitunzie hela yangu.
"Hivi basi nitavinunua mimi, nitajie ni kiasi gani.." alidakia haraka haraka.
Ok, hatuwezi kushindwana, nitarudi baada ya wiki moja unipatie kiasi fulani (nikamtajia pale)
Hakubisha, maana kilikuwa ni kiasi kidogo cha kawaida. Nikaondoka na kwenda lodge ya jirani.
Usiku ule niliazimia kwenda Pangani kwa yule Mganga kwenda kumshukuru kwa muongozo. Hivyo ilivyofika saa nane na nusu usiku nikafungua mlango wa lodge kisha nikaushindika (kuurudishia) na kuacha funguo mlangoni mimi nikiwa humo humo ndani ya lodge, Nikazima taa nikafanya yangu fyuuuu nikawa hewani, baada ya kutalii sehemu mbalimbali ilipokatibia saa kumi na moja nikatua jiurani na dispensary ya Kikokwe, nikawa kawaida nikaanza kutembea kwa miguu kuelekea nyumbani kwa Shariff.
Nyumba ya Shariff ilikuwa imejitenga kidogo na ilikuwa mwendo wa kama mwendo wa robo saa hivi kutoka pale zahanati.
**********
Itaendelea…
Ikiendelea nitag nimeipenda sana
