Just a person
JF-Expert Member
- May 16, 2022
- 993
- 1,245
Nmechoka ata walai
Yes ni true story kwa madai yakeMkuu hii ni simulizi ya kweli?
Sehemu nyingine kuna chumvi na sehemu nyingine kuna majiYes ni true story kwa madai yake
Kama alisema basi vizuriMwenyewe alisema nikae nayo miaka 10 baada ya yeye kufariki dunia.
Lakini mengine hakuniruhusu kuyasema na sijayaandika wala sinto yaandika.
Nimezidisha mwaka 1 katika kutunza yale aliyoniruhusu kuyasimulia.
Bila shaka alijuwa ukomo wa umri wake, na huenda ikawa hawakufa majini maana maiti hazikupatikana...
Niishie hapo.
Yeye amesema huenda hajasema kwa hakika kwamba hawakufiA majini so ni probability na hata wewe unaposema miiili imekutwa Kenya ni probability kuwa na yao ilikutwa huko wewe pia huna uhakika namimi naongeza labda walirudi kwenye asili yao nayo pia ni probable sina uhakika so katika hili hakuna mwenye uhakika si wewe si yeye si mimiKama alisema basi vizuri
Kutopatikana miili yao sio kwamba hawajafia majini
Katika ile Ajali ya spice islander kuna miili iliokotwa kenya uko ambayo haina macho na sehemu kubwa ya miili yao samaki wameshaila
Kwaio labda wameliwa na samaki
Asante sana ka simulizi nzuri sana!16. MAISHA MAPYA na UHURU - Ω
“Nakuusieni na kuihusia nafsi yangu juu ya kumcha Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu (aliye takasika), … hiki (Qur’an) ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na muongozo kwa wale wamchao …”
“Sisi waislamu, tuna miongozo miwili, Qur’an na Sunna. Qur’an ni maneo ya Mwenyezi Mungu na Sunna ni matendo na mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimwendee).”
“Tushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadithi za Mtume, hatuwezi kupotea.”
Hayo yalikuwa maneno ya Walii (kipenzi) wa Mwenyezi Mungu wa Utete Rufiji (kama wenyeji walivyokuwa wakimwita) wakati akinukuu aya kutoka Qur’an akiwa anatujenga kiimani.
“Katika hii Qur’an Mwenyezi Mungu ameweka elimu ya toka watu wa mwanzo mpaka watu wa mwisho, elimu zote zimo ndani ya Qur’an, historia imo, mawaidha yamo, mifano imo, visa vimo, hesabu zimo, utaratibu wa kuendesha Dunia umo ndani ya Qur’an na hiki kitabu huhifadhi waumini kwa fitina iliyomo humu duniani…” aliendelea
“Ndani ya Qur’an kuna habari za watu waliokuwepo kabla yetu, kuna habari za watu baada ya sisi kuondoka, ni hakimu baina yetu na ni upambanuzi juu ya mambo mbalimbali. Haifai kuiacha.”
“Hii Qur’an ajabu zake hazimaliziki, wana zuoni hawashibi, kila siku wanatoa faida na hata majini walipoisikia Qur’an inasomwa, wakasema hakika sisi tumesikia Qur’an ya ajabu, … inaongoza kwenye uongofu kwa hiyo tumeiamini na wala hatutofanya ushirikina…, na kwa hakika utukufu wa Mola wetu mlezi umetukuka kabisa,… hana mke wa mwana…, … na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uongo uliopindukia juu ya Mwenyezi Mungu… nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamsingizii uongo Mwenyezi Mungu…,”
Aliendelea yule mcha Mungu tutupatia mawaidha kupitia kitabu kitukufu Qur’an na kutusimulia habari za majini jinsi baadhi walivyo mrejea Mwenyezi Mungu na wengine waliendelea kukengeuka.
“Eee umesema mmetoka Bagamoyo!” aliuliza yule Walii,
“Rudini huko, kuna Sheikh Mkubwa Zawiani, utapata muongozo na elimu kadha wa kadha, kikubwa shikamaneni na hiki kitabu wala msikiache.” Alimaliza yule Walii na tukaagana na kuanza safari ya kurudi.
Nilikuwa mimi na mke wangu Behat, tulilala Rujiji Ikwiriri na siku ya pili tulifika Dar na moja kwa moja kwenda Bagamoyo.
Bagamoyo pale Zawian tukaambiwa tuende Lushoto kumtafuta Shariff Badowo ili atufanyia maombezi makubwa kabla ya kurudi Zawiani kwa ajili ya kumalizia elimu nasihi.
Tulienda Tanga, tukafika nymbani kwake lakini tukaambiwa amesafiri kwenda Mombasa, tukaambiwa tumtafute kijana mmoja pale Horohoro atatusaidia kufika kwake.
Yule kijana alikuwa ni mfanyakazi wa mabasi ya Modern (Mombasa – Tz – Zambia nk), alikuwa anaitwa Sarojo, alitusaidia sana hadi tukafika kwa Shariff Badowo na kufanya dua kubwa kubwa sijapata kuona na tulivyorudi Zawiani tulikuwa na utulivu mkubwa.
*********
Tukiwa Zawiani – Bagamoyo
“Tatizo lenu mlivyokuja mara ya kwanza hamkutaka kunisikiliza kwa kituo, wewe na kaka yako wote mlikuwa na haraka haraka kiasi cha kutopata yote ambyo nilitaka kuwaambieni.” Alikuwa anaongea Sheikh Mohamed kwa sauti yake nzito iliyojaa umwinyi mwinyi hivi kwa kutulaumu kiaina…
“Sasa ulivyorudi na kuniambia kuwa umepona, nikadhani labda umejuwa asili ya shida yako na kutatuliwa ipasavyo…” aliendelea…
“Kumbe bado kwa maoni yangu, ulikuwa kwenye safari ya kujijuwa na kujitambua… na sasa kwa vile umefikia hatua hii basi ukae kitako nikuelimishe…” alisema.
“Mwenyezi Mungu alituumba ili tumuabudu yeye, tena yeye tu na wala tusimshirikishe na miungu mingine, hayo ndiyo malengo hasa ya sisi kuumbwa, hata maumbile yetu yamewekwa kurahisisha zoezi hilo la kumuabudu yeye”
“Tukimuabudu yeye hatumuongezei chochote, na tusipomwabudu hatumpunguzii chochote, YEYE ambaye hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ile YEYE, Yu hai na ni wa kudumu, halali wala kupatwa na usingizi. NDIYE Mola wa Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina yake…”
“Anajuwa yaliyochificha mbele na nyuma, na katika sisi viumbe hatuna tujuwalo ama hatuwezi kujifunza (kupata elimu) ila kwa kuridhia kwake, na utukufu wake umeenea Mbinguni na ardhini na wala hawezi kushindwa kuvilinda viumbe vyake maana yeye ametukuka (aliye juu) na NDIYE MKUU.” Alisema Sheikh kisha akasoma aya katika mpangilio wake.
Alivyoanza kusoma nami nikakumbuka kile kikaratasi nilichopewa Kikokwe niwe nasoma mara kwa mara, maneno hayo yalikuwa sehemu ya dua ile niliyopewa huko.
Sheikh aliendelea na risala…
“Katika uumbaji wake (Mwenyezi Mungu) aliumba viumbe mbalimbali, na kila kiumbe kina mamlaka yake na mipaka yake katika kuyaendea mambo…”
Akatoa mifano mbali mbali jinsi viumbe wengi wanavyoishi humu duniani ikiwemo wadudu, hayawani na hatimaye majini na binadamu.
“Binadamu ndio tumepewa uhalifa (uongozi) katika dunia hii, yani tunatakiwa tuweze kuitawala dunia ipasavyo…”
“Majini nao wana tawala zao, wana mataifa yao, wana makabila yao, wana koo zao, wana mila zao na desturi zao, na wamepewa uwezo mbalimbali lakini pia wamewekewa mipaka…”
“Haifai kwa Majini kuingia kwenye tawala za kibinadamu na kuwasumbua watu kwa kuwapagawisha, kuwatia maradhi ama eti kujifanya wanawalinda…”
“Wao wana ‘ulimwengu’ wao na sisi binadamu tuna ‘ulimwengu’ wetu…”
“Hivyo ni makossa makubwa kwa Jinni kumuingia mwanadamu kwa namna yoyote ile kwa visingizio mbalimbali…”
“Idadi ya majini ni kubwa mara nyingi sana kuliko wanadamu, na kwa kuzingatia kuwa wao wanaishi muda mrefu kuliko wanadamu basi wingi wao huongezeka mara kwa mara kiasi cha kutapakaa duniani kote… kwa wingi wao huo hata kila mwanadamu aliye hai muda huu akikusanya majini sabini kila mmoja, basi binadamu wote watakusanya na wengi sana bado watabaki hawajakusanywa”
“Kuna elimu mbalimbali za kuweza kuwamiliki hawa majini, lakini ni moja ya elimu zilizokatazwa kwa kuwa hatimaye huleta hasara badala ya faida…”
“Lakini kwa kuwa Duniani humu kuna fitina mbalimbali ikiwemo fitna ya afya, mali, wake, waume, watoto nk basi baadhi ya watu hupatwa na husda, chuki na vijicho ambavyo huwadhuru wenzao, na kazi zote hizo hufanywa na hao majini ambao wameasi kwa kushirikiana na binadamu kwa namna mbalimbali za elimu ya kichawi”
“Elimu ya kukabiliana na matatizo hayo pia ipo, ipo kwa njia nyeusi na kwa njia nyeupe…”
“Hivyo tiba zipo, lakini kuna tiba kwa njia sahihi na zipo tiba za kwa njia ya kishirikina”
“Kufanya ushirikina na moja ya dhambi ambayo kama ikitokea umekufa bila ya kutubu basi ni dhambi isiyo sameheka labda kwa rehma zake Mola wetu maana yeye ndiye mjuzi zaidi”
“Hivyo basi ushirikina HAUFAI mbele za Mwenyezi Mungu”
“Kwakuwa tiba sahihi zipo, basi yatupasa kufuata tiba kwa njia zilizoelekezwa kwa miongozo ya dini yetu”
“Tiba isiyo sahihi utaijuwa kwa masharti yake ambayo hatimaye yanakupelekea katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa namna zote nne, kuwaza, kunena, kutenda na kutotimiza wajibu…”
“Sasa kwa kuwa ninyi mliamua kuishi kama binadamu…”
Tukawa tunaangaliana na Behat…
“…yafaa muendelee kuishi hivyo na kufuata maamrisho na makatazo yote ambayo yapo katika muongozo wa Qur’an na Sunna…”
“Pazi…!” aliniita Sheikh
“Mwenzako ana kiumbe tumboni…”
Nikawa manuangalia Behat tumboni sioni kitu zaidi ya ‘flat screen’ (hakuwa na hata kijitambi kidogo)
“Atazaliwa kiumbe ambaye sasa atakuwa mwanadamu kamili, wanenu hawatokuwa na passport ya kuingia Ujinini kama ilivyo kwenu hivi sasa ingawaje bado mpo nusu jinni.., wewe Pazi ni nusu binadamu nusu jinni na huyo mwenzako ni nusu jinni na nusu binadamu…”
Moja kwa moja nikaelewa tofauti yake kwa mmoja wetu alilala kwenye tumbo la uzazi binadamu ilhali mwingine alila kwenye tumbo la uzazi jinni.
Aliendelea kutupa risala pale weeee mwisho akasema…
“Tafuteni njia halali za kupata rizki zenu, hata kama itakuwa ni kutibu watu basi uifanye tiba iliyo sahihi kwa njia za kisunna (yaani kwa njia ya mafundisho ya Mtume Muhammad, Rehema na Amani zimwendee)
“Kitu kingine muhimu sana ni kwamba haifai kubeza dini nyingine, mfano hawa wenzetu wakristo tunaishi nao humu mjini, majumbani na kupeana heshima za kibinadamu, Kuna Kanisa kubwa kule Mantep (Sikuhizi wanaita ADEM), kuna Kanisa dogo kule miembe safa (jirani na kushukia MSALABANI) na kuna Kanisa kule Mwanakalenge. Hawa ni binadamu wenzetu na wana Imani yao thabiti katika kumwabungu Mungu wao kwa mujibu wa mafundisho yao, ukumbuke kuwa hawa pia kiongozi wao alipewa Kitabu kama ilivyo Qur’an kwa sisi. Usiwabeze wala kudharau Imani zao maana kuna wengine huenda wakawa bora mbele ya mwenyezi Mungu kuliko baadhi yetu, lakini haikatazwi kuwalingania ili waje katika uislam, tena kwa lugha iliyo nzuri na staha.”
“Kumbuka hata Nabii Mussa (Rehema na Amani zimfikie) alipoambiwa akamlinganie Firauni (Farao) aliambiwa akazungumze naye kwa upole licha ya kufuru kubwa aliyokuwa akiifanya. Kazi yetu ni kufikisha ujumbe lakini kumuongoa mja siyo kazi yetu, Allah mwingi wa Rehema sisi sote ni viumbe vyake, tusijitie ukiburi, YEYE Allah huamua atakavyo.”
Aliendelea…
“Vitabu cha elimu hiyo ya tiba zipo, vitafute ujifunze kwa walimu ukihitimu uendelee na tiba halali, kama hutoweza basi rejea kwenye kazi ya baba yako, ameshazeeka sasa afaa kusaidiwa sana…”
Alimalizia risala yake kwa kutusihi kuwa sisi bado ni nusu watu nusu majini, hivyo kiasili tuna nguvu za kijinni basi tuwe makini na maneno tuyasemayo na kujitahidi kujizuia hasira zetu maana huenda zikawa na athari kwa binadamu wa kawaida.
Tulirudi nyumbani na kumkuta mama akitusubiri kwa hamu.
“Enhe, mmeambiwaje huko?...” Mama aliuliza kwa shauku
Tukamwelezea yote na hatimaye mimi na mke wangu tukaamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwalingania watu katika dini huku nikiendeleza kazi ya Baba.
“Nadhiri yako sasa Mama inaenda kutimia…” nilisema.
Baada ya siku tatu, tuliaga kurudi Dar es Salaam kuendelea na maisha.
Leo hii tuna watoto watatu, tunaendeleza kazi ya uvuvi na uchuuzi kwa njia za kisasa, Baba na mama walishafariki, mama mkubwa pia alishafariki.
Tukapata Chakula cha mchana pamoja, kisha akanisindikiza nami nikachukuwa njia ya kurudi kwangu Upanga.
Jumamosi ile ilikuwa tulivu lakini nyumbani kwangu hapakuwa hivyo, nilikuta mke wangu amenuna, lakini nikamwambia hebu baada ya kula uje chumbani nimsimulie kisa chote nilichosimuliwa….
*******
Hakutaka nilale bali nimmalizie kisa chote maana muda tayari ulikuwa umeshaenda sana na siku Jumapili ilikuwa ndio inaingia (kwa mujibu was aa za na kalenda ya Gregori)…
Nilimkidhia haja yake baada ya kuona amevutiwa pia na kushangazwa japo kwa kuifupisha.
Mwishowe tuliendeleza ‘libeneke’ la mume na mke.
**************** MWISHO*************
Update!
Sheikh Mohamed alishafariki, Mzee Zahiri naye, Mwalimu Mwaloki, Mzee wa tiba Mlingotini, Mzee Njembi, Mcha Mungu wa Rufiji, Shariff Badowo, Shariff wa Kikokwe wote wametangulia mbele za haki.
Watu wengine ambao wametajwa katika simulizi hii sina update zao.
Imenibidi nifupishe ili niende na muda-huru niliokuwa nao maana ni mchache.
Niliamua kushea nanyi kisa hiki kama kumbukumbu ya kukumbuka uwepo wa Pazi na familia yake hapa Duniani kwa maana ya kwamba ile familia yote ilifariki kwa kuzama baharini miaka kumi na moja na siku arobaini na nane hivi ziliyopita walipokuwa wakitokea Unguja kuelekea matembezini Pemba kwenye MV. Spice Islander.
**********
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwa hakika kwake tutarejea.
Ω
nimeumia mateso aliyopata huyo kondoo4. KAFARA
Nilitumia dawa zile kwa wiki moja na hali yangu ilionekana kama kutulia, kaka mkubwa naye aliagizwa aende mazizini (Bagamoyo jirani na kwa Kafumbo ambaye alikuwa anamiliki mgodi wa kutengeneza chumvi), kule kulikuwa na mazizi mengi ya mifugo ambayo yalikuwa yanamilikiwa na wafugaji mbali mbali.
Siku hizi eneo hilo kumejaa mahoteli ya kitalii sijui kama bado kuna mazizi ya mifugo.
Baada ya siku kumi hivi tangia nitumie zile dawa kutoka Mlingotini, safari ya kwenda huko tena ikawadia ambapo safari hii Baba, Mama, kaka mkubwa, dada yangu tulienda wote. Baba alienda kwa mzee Kafumbo kuomba usafiri wa kutupeleka Mlingotini.
Mzee Kafumbo alikuwa na gari zuri Landrover 109 pickup TZ-61.
Tukapakia Kondoo wetu mwenye rangi mchanganyiko wa nyeupe na nyeusi kwa maelekezo ya mzee wa tiba, alikuwa na pembe zilizopinda na sikujuwa hata alinunuliwa kwa kiasi gani, baba na mama wakapanda mbele, mimi , kaka na dada tukapanda nyuma, dereva alikuwa mtoto wa mzee Kafumbo.
Haikuchukuwa muda mrefu tukafika, tukapokelewa kisha kijana wa Kafumbo akaondoka na land rover kurudi mjini kuendelea na majukumu mengine.
Ilikuwa majira ya saa tatu hivi asubuhi tulipo wasili eneo hilo kwa mzee wa tiba, tulikaribishwa vizuri kisha yule kondoo akachukuliwa na kijana wa mzee wa tiba na kufunga kwenye kigogo pembeni kidogo ya eneo la machinjio ya kuku.
“Tiba ya leo ni kiboko!” alisikika yule mzee akisema kwa sauti ya kawaida.
“Tiba hii kwa hapa Tanzania nimeifanya kwa watu wawili tu kwa umri wangu huu” aliendelea yule mzee wa tiba kuongea huku akiendelea kufanya kazi zake ndogondogo.
“Mtu wa kwanza kumfanyia tiba hii ni kiongozi mkubwa wa kisiasa na wa pili ni mama mmoja hivi miaka ya nyuma…” aliendelea huku akifungua kasha maalumu liliokuwa na vitu mfano wa visu.
“Kafara nyingi za wanyama wenye miguu mine huwa nafanya kwa kuchinja, lakini kwa aina ya maradhi ya huyu kijana imenibidi nifanye kafara hii ambayo najuwa haiwezi kudunda…” alisema kwa kujigamba.
Mara akamwita yule kijana msaidizi wake na kumkabidhi visu vikali vitatu na kumwambia akamchune / kugwangua yule kondoo manyoya yake abakie na ngozi tu tena akiwa hai.
Nilishtuka sana kuona kondoo anaenda kuchunwa ngozi akiwa hai, nikamuangalia kaka mkubwa naye akanitazama lakini hatukusema neno. Mganga akatuamuru sisi tubaki nje na yeye akaingia ndani na wazazi watu. Huko sikujuwa kilichoendelea.
Huku nje, yule kijana akawa anamnyoa manyoya yule kondoo, kidogo moyo wangu ukatulia maana nilidhani anachunwa ngozi akiwa hai. Kwa ustadi mkubwa aliendelea kumnyoa zoezi lililochukuwa saa kadhaa kabla ya kumaliza na wakati huo tayari juwa lilikuwa juu ya utosi, ambapo ndio muda aliosema mzee wa tiba kuwa unafaa kwa kuanza kufanya kafara.
Kondoo akiwa hai, tayari akiwa amekwanguliwa manyoya yake karibu yote, akachukuliwa na mzee wa tiba na kuanza kumchorachora mavitu ambayo sikuyaelewa kwenye mwili wake kwa kutumia kijiti maalum na wino mwekundu (zafarani?)
Wakati yeye akiendelea kumchora yule kondoo, alimuambia yule kijana aandae ‘ziara’. Sikuelewa mara moja ziara ipi tena lakini nikaona yule kijana ameenda kuchukuwa jembe na sepetu / beleshi (spade) na kwenda pambeni kidogo ya msitu wa miembe iliyopo hapo jirani na kuanza kuchimba. Baadaye nilikuja kujuwa kumbe alikuwa anachimba kaburi. Moja kwa moja nikajuwa hapa ndipo atakapozikiwa huyu kondoo.
Muda wa kula ukafika, safari hii tulikuwa kwa jumuiya lakini wanaume peke yetu na wanawake peke yao na wala hapakuwa na vibakuli vya kupimiwa finyango za nyama ya kuku. Tulikuwa vyema tukashiba kisha mzee wa tiba akaendelea na zoezi lake la kuandika kwenye mwili wa kondoo na yule kijana akimalizia kuchima kaburi maana ardhi ya eneo lile haikuwa ngumu.
Mzee wa tiba akamaliza zoezi la kuandika kwenye mwili wote wa kondoo kisha akachukuwa shuka nyepesi nyeupe nayo akaanza kuichorachora mistari mistari na mikato mikato isiyoeleweka na maandishi kama ya kiarabu lakini yenye usanifu tofauti kabisa sijapata kuona, shuka lile lote likaenea wino wa michoro na maandishi. Alikuwa ananakili kutoka katika kitabu fulani hivi kuukuu. Sanjali na kondoo pia kulikuwa na ‘nazi kavu’ saba (inasemekana zilizo anguka zenyewe kutoka juu ya minazi), mayai viza saba, chungu cha kupikia na vifaa ambavyo sikuona vyote mara moja kwenye ambayo vilikuwa kwenye ungo, lakini niliona chumvi, mtama, kitu kama buni (kahawa) na vingine vingi sivikkumbuki.
Tukaiwa wotekwenye kilinge cha nje ya nyumba, tukakaa kama nusu duara hivi, kukaletwa jiko la mkaa na chungu kikabandikwa, kondoo akasogezwa jirani, mayai na nazi nazo ziliwekwa chini kwenye jamvi. Mzee wa tiba akaanza kwa kusoma pale haraka haraka sana kisha akawa anaweka mavitu yale yaliyokuwemo kwenye ungo ndani ya chungu huku yule msaidizi wa kike akikoroga…
Zoezi iliendelea kwa muda, yule kijana akaamriwa amfungue kondoo Kamba zote, muda wote kondoo alikuwa akilia kwa namna ya kuomba msaada
(wafugaji watanielewa)
Baada ya kufunguliwa Kamba, kondoo badala ya kukimbia, aliendelea kutulia huku makamasi yake yakimchuruzika. Mzee alizidi kusoma mazitu yake, chungu kilizidi kukarangizwa mavitu yasiyoeleweka na kutatarika na kondoo alizidi kutulia, akaacha kulia na hatimaye akalala kwa namna ya kupumzika huku akihema kwa kasi.
Chungu kilikamilika kukarangizwa kikaipuliwa na kubandikwa chungu kingine chenye majani ya aina tofauti tofauti na kufunikwa. Kondoo aliendelea kulala chini na safari hii alilaza kichwa chake chini kama vile amezirai au amekufa. Yule mgaga akachukuwa lile shuka lenye maandishi mengi mekundu na kumfunika na akaendelea kusoma.
Baada ya muda mzee wa tiba alimuamuru yule kijana msaidizi wake ambebe yule kondoo akiwa na shuka lake waelekee kwenye kaburi. Pia sisi alitupa ishara ya kwamba tumfuate, tulienda sote isipokuwa yule dada msaidizi na mama. Kufika kule yule kijana akaambiwa amuweke kondoo kwenye kaburi, ambapo alivyomshusha tu, kondoo hakulala tena bali alisimama lakini bila kupiga kelele, alikuwa kama amezubaa hivi, huku akiwa na shuka lake mgongoni.
Mzee wa tiba aliendelea kusoma mavitu yake hadi kondoo akalala tena chini, kijana akaambiwa amfunike vizuri shuka kisha akaendelea kusoma huku anaweka udongo kwenye kaburi. Zoezi liliendelea hadi kondoo alipozikwa (akiwa hai?)
Juu ya kaburi halikuinuliwa kama makaburi mengine bali paliwekwa ‘levo’ ya usawa wa ardhi, kisha akatuambia turudi kule kilingeni zoezi bado linaendelea.
Kufika kule kilingeni nikapewa kidoga na kuamriwa nikae hapo, kisha kile chungu ambapo kilikuwa tayari kimechemka haswa kikaletwa mbele yangu na kisha nikaona nafunikwa shuka kubwa na kuambiwa niachame mdomo halafu chungu kikafunuliwa.
Lo salale! Hewa ikaanza kuwa nzinto ndani ya shuka nikawa kama nakosa hewa (nakosa pumzi), mwili wote ukajaa jasho kiasi cha nguo nilizovaa kulowa chapachapa. Baadaye nikazoea hali hile ya hewa chache na baada ya dakika chache tu nikafunuliwa wakaniangalia kisha wakanifunika tena. Zilikuwa ni zoezi la kama dakika kumi hivi lakini niliona kama ni saa nzima.
Baada ya zoezi hilo niliambiwa nikae kwenye mkeka nivue shati ambalo kwa wakati huo lilikuwa halitamaniki kwa jasho. Nikamuona yule dada msaidizi wa mganga ameshika kiwembe kipya aina ya topaz…
“Tulia nikuchanje eee mdogo wangu, utapona tu” alisema yule dada.
Kusema ukweli baada ya kutoka ndani ya lile shuka nilijisikia vizuri sana, nilipumua vizuri na kujihisi nina afya ‘tele’. Katika maisha yangu hadi wakati huo nilikuwa sijawahi kuchanjwa hata mara moja, hivyo lile zoezi lilikuwa la kuogofya sana kwangu. Nahisi yule dada aliniona na kuelewa hisia zangu ndiyo maana akanituliza kwa maneno yake na sauti nyororo ya kuliwaza.
Nilichanjwa kichwani chale mbili mbili utosini, kwenye paji la uso mwanzo wa nywele na kisogoni. Pia aliendelea kunichanja kifuani, mikononi na miguuni halafu akazunguka mgongoni ambapo alinichanja nyuma ya shingo na kiunoni. Mwote humo alikuwa akichanja chale mbilimbili ndogo ndogo kwa haraka sana na kila sehemu alipochanja damu ilikuwa inatoka.
Yule dada akaletewa kibuyu ambacho ndani kulikuwa na dawa ya kimiminika kama mafuta hivi meusi na kuanza kupipaka kwa mtiririko kama alivyo nichanja. Alipomaliza akapewa kikopo kingine cha dawa ya unga unga mweusi na kupaka sehemu zote zilizochanjwa bila kufuata mpangilio. Alipomaliza alinielekeza nitulie pembeni kwenye mkeka. Hapo nilikuwa nasikilizia maumivu ya chale pamoja na hii dawa ya pili ya unga unga maana ilikuwa inauma sana.
**********
Zoezi lilisha kwa wazazi wangu kupewa maelekezo mengine kisha wakapewa zile nazi zote na mayai yote tulkaanza safari ya kurudi barabarani ili kufika njia kuu ya Kaolee. Wakati tupo njiani kabla ya kufika barabara kuu ya Kaole kuna njia panda fulani hivi za watembea kwa miguu, nikaona baba anavuja zile nazi moja baada ya nyingine huku mdomo kama anasema vitu ambavyo sikuvisikia. Nazi zote saba zikaisha, tukawa tunaendelea na safari ya kwenda barabara kuu.
Kabla hatujatokeza barabara kuu, nikapewa yale mayai moja baada ya jingine na kuamriwa kurusha kinyume nyume bila kuangalia nyuma hadi yakaisha yote. Muda huo wote tupo kimya na tukawa tumekaribia kabisa barabara kuu ambayo ilikuwa ni ya vumbi.
Ilikuwa inaelekea majira ya saa kumi na moja hivi jioni, hivyo tulichelewa lile basi la Mbegani, ikabidi tukeni chini kusubiria usafiri mwingine lakini ni wa kubahatisha maana mabasi ya kutokea Dar es Salaam yalikuwa yakipita njia ya Zinga-Kiromo-Ukuni hadi mjini Bagamoyo wakati sisi njia tuliyopo ni ya Zinga -Pande -Kaole -Mjini Bagamoyo.
Kwa bahati nzuri baada kama ya dakika arobaini hivi za kusubiri likaja basi moja kutoka Dar es Salaam linalomikikiwa na Shariff wa Bondeni, basi hilo kwa jina maarufu likikuwa linaitwa UWEMBE na kwa siku hiyo alikuwa analiendesha dereva mmoja aitwaye Mantibo.
Basi lilikuwa limejaza sana maana lilikuwa ‘linaokota’ abiria wote kwa kuwa njia hiyo haikuwa na mabasi mengi hivyo ilikuwa ni namna pia ya kusaidia abiria licha ya jambo la biashara.
Tulifika nyumbani jua likiwa limeshazama, Mama aliniambia nisioge siku hiyo hadi kesho, nikapewa dawa na mama za kunywa usiku huo na asubuhi pia na kuendelea kufanya hivyo kwa siku saba.
**********
Inaendelea
Hata miminimeumia mateso aliyopata huyo kondoo
Hichi kipande kimenitoa machozi11. UJIJI MARA YA PILI
Akili zilitulia kiasi sasa cha kuanza kufikiri vyema na kupanga safari ya kurudi Ujiji Kigoma.
Usiku ule tuliutumia kujadili mengi yatokanayo na matibabu yangu.
Sikuthubutu kuelezea safari yangu ya Ujinini.
"Haya, na hiyo kanzu ya ajabu na fimbo umepewa huko huko? " Alidadisi Mama
"Ndiyo Mama, na huko niliambiwa kuhusu sababu iliyopelekea kupoteza ujauzito mara mbili." Nikamjibu na kuongezea, nikamueleza yoye kuhusu hila za ukewenza pamoja na uchawi kutoka Tumbatu.
Mama alishangaa sana na akawa ameshika tama anawaza (nadhani alianza kuunganisha matukio yake ya ajabu yaliyomtokea huko nyuma...)
"Hata kaka alijaribiwa kuuwawa kwa sumu mara kadhaa lakini kwakuwa ana ‘malalika wakali’ imeshindikana na wakaamua kumpa ugonjwa unaofanana na malaria, ni ungonjwa wa kichawi, lakini bahati nzuri kama nilivyosema nao nimeumaliza, hatoumwa tena ugonjwa huo.
Tuliongea mengi sana na Mama akashukuru eti ametimiza nadhiri yake sasa atakuwa na amani.
Sikutaka kumuambia mama kuhusu siku ile alivyokuwa ufukweni baharini na usiku wake wakati akiwa na baba na jinsi ujauzito ulivyoingia... Niliona siyo muda muafaka.
Tulivyochoka kuongea mimi na kaka tukaingia chumba chetu kulala na Shangazi ma mama wakaingia chumba chao.
Mapema asubuhi tukaenda stendi ya mabasi kwenye ofisi za Sumry, basi lilichelewa kufika hivyo tulikaa hadi saa mbili asubuhi.
Baada ya muda basi likafika...
"Samahani abiria wetu, tulikuwa na marekebisho muhimu ndio maana basi limechelewa..." Alisema mmoja wa wahudimu wa Sumry.
Tukaruhusiwa kuingia ndani ya basi na wafanyakazi wakawa wanaweka mizigo ta abiria kwenye buti.
Nikasikia sauti ikiniambia, "ongea na baba yako kwenye simu..."
Nikamwinta shangazi... "Shangazi simu yako iko wapi..?"
Akaniambia "Kopo hilo, nimeliweka kwenye mkoba wangu mdogo..."
"Naiomba" nika mwambia, akapekenyua kisha akanipatia.
"Unadhani utapana mtandao hapa!?" Aliuliza
Nikajibu "Ngoja nijaribu..."
Nikaiwasha, kisha nikasikia kale kamlio tululiii, ikawa imewaka, kuangalia signal za mnara hakuna. Nikasema ngoja nijaribu hivi hivi..
Tututu, tututututu, tu! He kama masihara simu ikaanza kuita
Ngriiin griin, griiin griin
Mara ikapokelewa...
"Haloo" upande wa pili ukajibu
"Shangazi ongea na baba" nikampatia shangazi simu.
Huku akishangaa, akasema, "Haloo"
Wakasalimiana pale, baba akauliza mko wapi, akamjibu kuwa tupo Sumbawanga tunaelekea Mpanda...
Wakaongea weee pale tena kwa sauti kubwa watu wakawa wanatuangalia sisi na muujiza wetu wa kuongea na simu ya mkononi...
Shangazi akampa mama na akamuhamikishia baba kuwa sote tupo salama apuuze zile jumbe za kipolisi kuhusu kupotea kwa Pazi.
Ghafla simu ikakatika na punde si punde safari ya kuelekea Mpanda ikaanza.
Njia haikuwa rafiki lakini kwa umahiri wa dereva safari ilikuwa nyepesi.
Tukafika Nyamanele kisha Lyazumbi kwenye kuku watamu na njia panda ya kwenda Kabwe.
Kama kawaida shangazi alikula kuku na sisi wengine tuliendelea kufaidi samaki wa ziwani zawadi kutoka kwa mke wa Ustadhi.
Safari ikaendea hadi kibaoni ambao kulikuwa na mizigo ya kupakia.
Kutoka hapo tukapita njia tofauti na ile ya kwanza wakati tunatoka Mpanda kwenda Lyazumbi.
Baada ya kilomita sabini hivi tukafika stalike.
Njiani tulivamiwa na mbong'o lakini niliwafukuza kwa muujiza wa fimbo kimya kimya.
Safari iliendelea hadi tukaingia Mpanda mjini. Ilishakuwa jioni.
"Twendeni Stesheni tukabahatishe usafii..." Aliendekeza kaka
"Hapana, tafafute lodge ya kulala tupumzike... " Nilijibu.
"Hela zimebaki chache, utaishiwa tutakama... " Alidakia Shangazi...
"Mimi nitalipia..." Wote wakageuka kuniangalia...
"Ninazo hela kidoo nilipewa Umbirikimoni." Nikajibu huku nikiingiza mkono kwenye rasket na kutoa kibunda cha hela dola kumi kumi.
"Hizi hapa... " Niliwaonesha na wote wakapigwa na butwaa
" Dola!? " Kaka alishangaa kwa sauti.
Ndiyo, tutatafuta chenji tukifika Tabora au Kigoma.
"Hebu zilete kwanza" Shangazi akazichukuwa zile hela, akazinusa kisha akasema ni dola halali ni dola za ukweli. Kisha akaziweka kwenye mkoba wake.
Tukatafuta lodge ya jirani tukalala.
Asubuhi tukaenda Stesheni kuulizia usafiri wa treni kwenda Tabora.
"Abiria itakuwepo Alhamisi asubuhi, keshokutwa" alijibu mhudumu wa pale stesheni
"Labda nikufanyieni mpango wa gusi, litaondoka jioni hii hii ya leo, mnazo nauli hapo? " Alihoji
Shangazi akatoa pesa akampatia.
"Vizuri sana, saa kumi muwe mmeshafika hapa kwa maelekezo zaidi" akasema kisha akatuaga.
Jioni ile tulifika na kupanda lile gusi na kuanza safari na Alfajiri tukawa tumefika Tabora, tukashuka na kusubiri kukuche twende mjini benki tukabadilishe zile dola kuwa shilingi
Kwakuwa shangazi alikuwa mjanja mjanja alienda na dola kumi pale benki ya Taifa ya biashara, akapewa zaidi ya elfu kumi na tatu.
Shangazi akaamua kuongeza dola, akatoa kumi kumi nne, wakamuomba passport na urasimu mwingi, Shangazi akaondoka.
"Wamenikatalia kuchenji wanataka vibali sijui nini kujaza fomu nikaamua kutoka" Alisema Shangazi alipokuja kule nje.
Tukashauriana twende hadi Kigoma kwa kuwa kule ni mpakani lazima tutapata chenji.
Tukawa tunatembea kuelekea Stesheni.
Wakati tunakaribia, tulishuhudia vichaa wengi sana njiani na hata pale stesheni. Yani wendawazimu wengi sana nadhani palikuwa panaongoza nchi nzima.
Nikasema ngoja nijaribu hii fimbo...
Nikamgusa nayo mama mmoja kichaa aliyekuwa yupo nusu uchi kabisa akiwa na mzigo wa matambala na makopo
Mara akaanguka chini,
"We Pazi, umeafanya nini" Kaka aliuliza
Sikujibu kitu, ghafla yule kichaa akaamka, akakaa, akasimama lakini mara akachutama (akachuchumaa) huku akijiziba sehemu zake za siri...
Mama akamrushia kitenge, akakidaka akajisitiri na kuondoka eneo lile huku akiacha mzigo wake wa makopo na matambala palepale...
"Ameshapona ..." Nilisema
"Alhamdulillah" sauti ya mama ilisikika akimshukuru Mwenyezi Mungu.
Nilivyoona vile, sikuishia kwa huyo tu, nikawagusa na wengine hususani wanawake na baadhi wanaume, wote baada ya kuzinduka wakawa wanakimbia eneo walilopo na kwenda kujificha...
Watu wakaanza kujaa na kutuzingira, kila mmoja akawa anaomba afanyiwe maombi.
Vurugu ikawa kubwa pale huku kaka akiwa na kibarua kigumu cha kuwazuia watu na kuwapanga vizuri, Mama na Shangazi wakiwa wameduwaa tu wasijie la kufanya.
Nikawambia ule umati
"Akina mama, leteni vitenge kwa ajili ya kuwasitiri akina mama wenzenu ambao ukichaa
Ghafla vikapatikana kama vitenge kumi na tatu hivi...
Nikamwambia kaka anifuate na akina shangazi wasubiri pale pale...
Nikawafuata vichaa waliokuwepo maeneo yale na kiwagusa na fimbo kisha kumuweke vitenge viwili na kuondoka
Kuna baadhi ya vichaa wakawa wananikimbia lakini nilifanikisha kumaliza vile vitenge vyote...
Mimi na kaka tukarudi pale kwa akina shangazi na kuanza kuwaambia...
"... Mwenye hirizi aivue na kuitupa hapo chini... " Nilitoa amri
Watu karibia asilimia 60 ya waliokusanyika alitupia pale hirizi, nilishangaa sana kuona wingi wa hirizi kiasi kile, na zilikuwa za mtindo mbalimbali
"Leteni mafuta ya taa" niliamrisha tena
Baada ya muda kupita nikapewa kiguduria cha lita tano...
"Leo tutachoma moto hirizi hizi, na wewe ambaye una hirizi lakini hujaileta hapa, ondoka eneo hili maana utadhurika..." Baadhi ya watu wakaondoka...
Nikazimwagia mafuta ya taa na kuzichoma moto.
Nikasogea pembeni kidogo na kuanza kuwagusa kwa fimbo wale waliokiwa jirani yangu, kila aliyeguswa alipepesuka na kukaa sawa na kuondoka, nadhani walijisikia vyema.
Zoezi liliendelea hadi lilipoingiliwa na askari mgambo wa stesheni kwa kutuambia kuwa abiria kutoka Pwani inakaribia hivyo watu wajiandae kwa kuingia...
Nikasitisha lile zoezi na watu walitaka kujuwa naelekea wapi...
"Sharifu, unaelekea Dodoma Mwanza? Unaenda Kigoma au Mpanda..."
Nilijibu kuwa tunaelekea Kigoma. Baadhi ya abiria walifurahi na wengine walihuzunika. Lakini nikawaambia, nitafanya ziara maalumu mikoa yote Tanzania, hivyo wasiwe na wasiwasi.
Hakika nilijishangaa mwenyewe kwa yale yote yaliyotokea pale. Nikawa kimya huku Kaka akiwa jirani nami na Shangazi akiwa anatabasamu huku mama machozi yakiwa yanamlengalenga.
Niliendelea kumsikiliza kwa makini kijana Pazi na muda ulikuwa umeenda sana maana tayari ilikuwa ni saa saba za usiku lakini sikuchoka kumsikiliza
Mara tukasikia honi ya treni ya kuashiria inawasili kisha ikaingia na kupaki njia namba mbili.
Baadhi ya abiria wakashuka na zoezi la kubadilisha mabehewa lilifanyika...
Baada ya saa kama tatu hivi, tukasikia sauti kutoka kwenye spika ikielekeza jinsi treni zitakavyo ondoka.
Nasi tukaingia kwenye behewa la Kigoma tayari kwa safari.
Saa mbili baadaye treni yetu iliyokuwa njia namba moja ikaanza kuondoka.
Tulisafiri usiku kucha tukisimama simama, na hatimaye alfajiri tukaingia Kigoma.
Tukachukuwa teksi ili itupeleke Ujiji kwa Mzee Njembi.
Dakika chache baadaye tukawasili na kupokelewa.
***
Mzee Njembi alifurahi sana kutuona , tukasalimiana
Na nikamkabidhi zawadi zake kutoka kwa Ustadhi, nilimpatia ile mizizi iliyokuwa imehifadhiwa vizuri na kiasi cha fedha kama elfu hamsini ambazo nilimuomba shangazi anipatie.
Tukaongea kwa kirefu na kunisifu kwa ujasiri kwa yaliyonikita Umbirikimoni.
Hapa napo sikueleza habari za Ujinini.
Kaka akapewa mwenyeji ila aende bandarini kufanya 'chenjee' ya dola kama alivyoita yule mwenyeji.
Waliporidi kaka alisema...
"Wauza vitenge wamenichenjia tena kwa reti nzuri"
Tukafurahi kwa pamoja na kisha kumpatia Mzee Njembi shukrani ya elfu 30, akakataa, akasema "nipeni elfu kumi tu nitanunua kitu cha ukumbisho."
Baada ya chakula cha mchana tukaaga na kurudi Kigoma mjini.
Safari hii tulikuwa na hela za kutosha, tuka check in Kigoma Hotel ambayo ipo jirani tu na Stesheni papo hapo.
*********
Itaendelea...
SubHii ni simulizi ya yaliyomtokea mtoto wa marehemu rafiki yangu Mwinyi Mkila wa Bagamoyo.
***********
1. ALFA
Nilifahamiana na Mwinyi Mkila katika harakati za kutafuta shamba Bagamoyo na hatimaye kwa msaada wake nilipata shamba kubwa eneo la Sanzale miaka hiyo ya 1980's.
Mwinyi Mkila alikuwa na watoto kadhaa na mmoja wa watoto hao anaitwa Pazi. Kijana Pazi ndiye mzuwanda kwa Mwinyi Mkila kwa bi mdogo maana Mwinyi Mkila alikuwa na wake wawili.
Mwinyi Mkila mpaka mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na shughuli za uvuvi na uchuuzi
wa mazao ya baharini. Alikuwa na Jahazi, Mashua, Dau, Ngalawa na Mitumbwi ambayo alikuwa akiwapa
wavuvi kwa mikataba maalumu ya kufanya nao kazi na kumuuzia kitakacho patikana.
Mazao hayo ya baharini hususani samaki yalikuwa yakipelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa. Sasa huyu kijana Pazi ndiye aliyekuwa akisimamia zoezi zima la uuzwaji samaki hao na mazao mengine ya baharini katika soko la Feri (Dsm)
Miaka ya 1990's nilipokutana naye Feri wakati nimeenda kununua kitoweo, Pazi alikuwa hayupo kama kawaida, alikuwa amekonda na macho yamekuwa angavu zaidi na kama anatumia nguvu nyingi hivi
ili kuangalia.
Nilipo mjulia hali zaidi ndipo akaniambia kuwa amepata na maradhi yasiyo julikana na akasema kuwa hali yake kila siku inazidi kudhoofu.
Familia ya Mwinyi Mkila haikuwa na shida ndogo ndogo za kiuchumi kwani baba yao alikuwa mkwasi
na maarufu sana Bagamoyo na ukanda wa Pwani kwa ujumla na watoto wake karibuni wote wa kiume
walirithi kazi ya baba yao.
Bada ya mazungumzo ya muda mrefu na Pazi tukaagana na kila mmoja akaendelea na shughuli zake.
***********
Miaka kumi na moja hivi baadaye nilikutana tena na Pazi lakini katka hali tofauti sana na akiwa na afya njema na akaniomba nikapajuwe nyumbani kwake alipojenga sasa hivi.
Tulikutana na Pazi Long-room TRA mkabala na kituo cha mabasi Stesheni - Dar es Salaam siku ya Ijumaa. Akaomba niongozane naye hadi kwake 'Mbezi beach'. Kwa kuwa nilikuwa tayari nimeshamaliza shughuli zangu nilizojipangia kwa siku hiyo, nilikubali kuongozana naye na tukafika kwake eneo la Mbezi Juu kama unataka kwenda Salasala.
Baada ya mazungumzo ya awali ndipo akaanza kunihadithia.
"Baba, hujafa hujaumbika!" alisema Pazi.
"Enhe!?", niliitikia kwa shauku ya kutaka kujuwa zaidi na zaidi.
Pazi alianza kunisimulia:-
***********
Tangia nasoma shule ya Msingi Kizuiani Bagamoyo, nimekuwa nikimsaidia Baba kazi zake za uvuvi. Japo wakati huo nilikuwa siendi baharini kuvua, lakini vyombo (mashua nk) vinaporudi huwa nakuwa pwani ufukweni nikisimamia yale niliyopangiwa na wakubwa wangu.
Jahazi letu kazi yake kubwa ilikuwa ni kusafirisha mizigo kutoka huku Bagamoyo kwenda Unguja na mizigo ya Unguja kuileta Bagamoyo. Mashua ilikuwa kwa ajili ya kazi za uvuvi maalum ambapo chombo hukabidhiwa nahodha, yeye ndiye anakuwa na jukumu la kuwatafuta wavuvi atakao shirikiana nao katika zoezi zima la uvuvi. Dau mara zote tumekuwa tukiwakodisha 'Wakojani' kwa ajili ya shughuli zao za uvuvi wa 'juya' kisha wao huwa huru kuuza mavuno popote lakini hukilipia chombo kwa fedha taslimu kila siku warudipo kuvua kwa kadri tulivyo kubalina. Ngalawa na mitumbwi pia huwa wanalipa kwa fedha taslimu na wapo huru kuuza sehemu yoyote ingawaje mara nyingi huja kutuuzia sisi wenyewe.
Jahazi, Dau, Ngalawa wanatumia 'tanga', lakini mtumbwi wanatumia 'makasia' peke yake na kwenye Mashua wanatumia tanga pamoja na injini.
Baada ya kumaliza darasa la saba wavuvi wa mashua walipanga kwenda 'dago' maeneo ya Sadani na Mkwaja kwa ajili ya zoezi la kuvua 'kamba' na 'kaji' (prawns), na Kamba koche (robuster), niliamua kuongozana nao kwa kuwa sasa nilikuwa huru zaidi kiliko wakati nikisoma.
Tulijiandaa vyema kwa ajili ya safari hiyo ya kwenda kupiga kambi (dago) kwa kubeba unga wa ugali, mafuta kidogo ya kupikia na vifaa vya uvuvi kama vile nyavu maalumu kwa ajili ya kuvulia kamba na kaji, Petroli ya kutosha, tofali za barafu za kutosha na vifaa vingine.
Siku ya safari tulisubiri maji yajae kusogea ufukweni ili chombo kiweze kuelea kwa sababu 'yalikupwa'. Muda wa kuanza safari ulipowadia nahodha aliamrisha baharia mmoja ashike 'upondo' na kuanza kukitembeza chombo huku baharia mwingine akivuta kamba ya nanga kurahisisha uelekeo wa kuielekea nanga ili ipandishwe na safari ianze.
Nahodha aliwasha mashine Yamaha Enduro supa 40 (horse power 40), nanga ikang’olewa (ikaingizwa kwenye mashua) na safari ikaanza mdogo mdogo. 'Hatukutweka tanga' kwa kuwa hali ya bahari ilikuwa shwari hivyo hakukuwa na upepo wa kutosha kuiendesha mashua kwa kasi.
Ilikuwa mida ya alasiri ndipo tuling'oa nanga kuelekea dagoni, na tulifika Mkwaja usiku mwingi na nahodha aliamuru nanga ishushwe 'nje kidogo' kwenye maji mengi kabla ya kufika ufukweni ili tupate kulala kabla hapajakucha tukiwa ndani ya mashua.
Palivyokucha tulisogeza chombo ufukweni, tukashusha mizigo yetu na kuanza kuandaa kambi. Siku nzima siku hiyo ilikuwa ni kujenga vibanda. tulijenga vibanda vitatu ambapo banda kuu lilikuwa la nadhodha na wasaidizi wake wawili, na mizigo yote ilikuwa hapo, mabanda mawili yaliyobaki yalikuwa ya wavuvi ambapo wanne walikaa kwenye kila banda. Mabanda haya ni yale ya kusimikwa kwa miti na kuezekwa kwa makuti juu ambapo msuko wa aina ya 'kumba' na 'pande' ilitumika na pembeni kulizibwa vivyo hivyo kwa makuti ili kukabiliana na upepo kutoka baharini hususani nyakati za usiku.
Kwa kuwa nilikuwa kijana mdogo tena mfupi, sikuruhusiwa kuingia baharini kwa ajili ya kuvua, bali niliachwa kambini pamoja na msaidizi wa nahodha kama walinzi mashahidi wa kambi. siku ya kwanza hadi ya tatu zoezi liliendelea vizuri, na tulifanikiwa kupata kaji wengi sana pamoja na kamba wachache.
Wavuvi wenyewe hujuwa ni wakati gani na sehemu gani waende kuvua. kamba na kaji huvuliwa kwa nyavu moja kushikwa na wavuvi wawili mmoja huku na mwingine kule kisha wakianzia maji mengi na kutembea taratibu kuja maji machache na hatimaye kuwanasa kamba na kaji na mazao mengine ya baharini yaliyonasa kwenye nyavu kisha huja kando kando ya bahari na kuanza kuchambua, kamba na kaji huhifadhiwa kwenye tenga, samaki wengine waliwao huwekwa kwa ajili ya kitoweo na baadhi
ya viumbe wengine wa bahari hurudishwa baharini ama kuachwa tu wakizagaa.
Siku ya nne nilibaki peke yangu kambini na ndiyo nadhani ikawa ni sababu ya maradhi yangu yaliyonisumbua kwa muda mrefu sana.
Kambini kwetu asubuhi wavuvi hunywa supu ya samaki tu na kujiandaa na kazi kwa kuangalia mwenendo wa maji. baada la zoezi la uvuvi asubuhi, wakirudi hupikiwa ugali kwa samaki kisha kusubiri zoezi lingine kulingana na mwendendo wa maji, hivyo kwa siku
huwa kuna mazoezi mawili makuu ya kuvua kamba na kaji.
Sasa siku hiyo mida yao kurudi ili wapate chakula cha mchana ilikuwa majira ya saa sita hivi, hivyo nami katika harakati za kumsaidia mpishi wa zamu (msaidizi wa nahodha) kuwasha moto, nikapatwa na gumbizi (kuzunguzungu) na kuanguka chini. Sikuelewa kilichondelea hadi baadaye nilipopata fahamu nikawaona wavuvi wote wamenizunguka huku nahodha akiniuliza ninajisiaje sasa.
"Najisikia vizuri ila nahisi uchovu tu, kwani kimetokea nini?" nilijibu na kuuliza.
Nahodha akaniambia kuwa nilianguka na kusogezwa kibandani na msaidizi wake na nikawa kama nimezimia na kupoteza fahamu, wao waliitwa kuja kunisaidia haraka kwa kunipepea na kunimwagia maji ndipo nikazinduka.
Nikapewa supu ya Samaki aina ya 'Songolo' nikanywa nikapata nguvu kidogo na ugali ukasongwa
wengine wote walikula lakini mimi nilitosheka na supu ya samaki sikujisikia kula tena. Zoezi la jioni walibaki watu watatu pale kambini pamoja nami, yaani nahodha na wasaidizi wake wawili, wavuvi wengine waliendelea kuvua.
Kwakuwa ilikuwa msimu wa 'bamvua' lenye samaki wengi, haikutuchukua zaidi ya siku kumi kujaza
vyombo vyetu vyote samaki aina ya kamba na kaji. Lilifanyika zoezi la ziada kwa ajili ya uvuvi wa maji mengi ili kupata samaki wakubwa kwa njia ya 'mishipi', basi wiki hiyo iliyofuata tulitumia usiku wa kiza kwenda kuvua Jodari, Sehewa, Papa, Chewa na Nguru. Kambini tulikuwa tunawaacha wavuvi wanne wakilinda samaki na kambi kwa ujumla, mimi hawakutaka kuniacha kwa kuhofia nisije nikaanguka tena wao wakiwa mbali.
Zoezi hili la usiku nilikuwa nikilifurahia kwa kuwa hatuingii ndani ya maji, bali tunawasha tu 'karabai' na kuweka chambo kwenye ndoano na kuanza kuvua huku 'mishoto' ikiwa jirani kwa ajili ya 'kuwatuliza' samaki wasumbufu kabla ya kumtoa kwenye ndoano.
Tulipata Jodari wachache, sehewa wengi, nguru wachache, papa mmoja na chewa mkubwa mmoja kwa zoezi zima la wiki hiyo. Chakula Unga kutoka mjini Bagamoyo tulichukuwa wa kutosha wiki nne, lakini Nahodha aliamuru turudi mjini baada ya wiki tatu na nusu kwa kuwa tulishapata mavuno ya kutosha.
***********
Safari ya kurudi ilianza, lakini kwa upande wangu niliona vituko njiani kadha wa kadha, tulianza safari
jioni sana ili tutembee usiku kucha na asubuhi tuwe tumefika. Ilikuwa ni kawaida ya vyombo vyetu kuja 'kutua' maeneo ya pwani ya msikiti wa Ijumaa Bagamoyo "nchi pana", (siku hizi wanapaita kwa Zakaria / Alfazul).
Kituko cha kwanza ni kuona moto mwekundu ukiwaka baharini pasipo na chombo chochote,
awali nilidhani ni wavuvi wenzetu wakivua lakini nilipo muuliza nahoda alinijibu kuwa hapana,
siyo wavuvi, wale ni "vibwengo"
'Wakati nasoma kizuiani, nimesikia simulizi nyingi za vibwengo, leo hatimaye naaza kushuhudia
mubashara', nilijisemea.
Vimbwengo kwa simulizi ni aina fulani ya viumbe ambavyo aghalabu hupatikana maeneo yenye maji mengi mfano wa mabwawa makubwa, mito, maziwa, bahari. Viumbe hivi husemekana vina uwezo wa kujibadilisha muonekano wao, na wakiwa katika umbo la mfano wa mwanadamu basi huwa wafupi. wana uwezo wa kuonekana na kupotea kwa ghafla. hupenda kuwatisha binadamu lakini inasemekana hawana madhara makubwa kwa binadamu.
Inasemekana pia ni aina fulani ya kabila moja ya jamii (specie) ya majini. Sasa ile mioto ilikuwa inaonekana na tunapoikaribia inapotea na kuonekana umbali mwingine.
************
Inaendelea...
mkuu mie sina mengi yakusema ila niseme tu hii dunia ina mateso mengi sana yakila namna,nimejifunza mengi kwakushuhudiaHata mimi
Wakati nahadithiwa nilidhani anachunwa ngozi hadi aliponifafanulia
Alinyolewa manyoya!
Ila kufa kwa kukosa hewa iwe kwenye maji, au moto chochote kitakachoziba usipate hewa hakielezeki!
Aisee kama kawaida yako, simulizi nzuri sana hii. Maeneo yote ni halisi b'se katika "uzururaji" wangu nimefika mpaka Moba... kwahiyo wakati nasoma I was visualizing haAmin
Wenyeji wa maeneo niliyotaja kama wapo humu watakuja kushuhudia.



