Hatimaye nipo huru

Hatimaye nipo huru

2. MALARIA NA TIBA

Tulivyo anza kuona nchi kavu kwa mbali, nahodha aliamuru kibendera kipandishwe ili iwe kama ishara ya maandalizi makubwa yanahitajika, wakati huo hatukuwa na simu, 'rediokol' wala vifaa vya kutuongoza zaidi ya ujuzi wa nahodha na mabaharia wengine kwa kutumia elimu ya nyota angani na uzoefu maeneo na miamba bahari.

Tulifika majira ya saa moja hivi asubuhi, maana muda mwingi tulitumia upepo kama nishati ya kutusafirisha kwa sehemu kubwa ya bahari tukiweka akiba petroli kwa dharura.

Mwinyi Mkila akiwa na wafanyakazi wake wengine walikuja kutupokea, wakiwemo 'bwana samaki' (afisa wa Serikali anayehusika na mali bahari), watu wengine wengi wakiwemo watoto wa rika tofauti maana ilikuwa ni siku ya Jumamosi.

Kwa mazingira ya pwani, ni kawaida ya watu kujaa wakati chombo kikiingia kutoka uvuvini, wengine kutafuta kitoweo, wengine kuchuuza na wengine kuburudisha macho tu.

Kwakuwa uvuvi ule ulikuwa ni maalumu, watu wa nje wigo wa Mwinyi Mkila walibaki kushuhudia tu kilichoendelea.

Kamba na kaji walipimwa kwenye mizani ili kupata idadi ya kilo zilizopatikana. Kaji huhifadhiwa peke yake na kamba peke yake kwenye matenga makubwa ambapo nyumbani tena hufungwa upya na kuwekewa barafu mpya tayari kwa safari ya kwenda Dar es Salaam alfajiri kwa kutumia mabasi ya SIKINDE na CHAMPSI MULJI.

Wale samaki wengine pia Mwinyi Mkila alipatana na wavuvi na kujuwa bei.

Baadhi ya wachuuzi waliomba wauziwe wale Jodari na Sehewa kwa ajili ya vitoweo, na ilifanyika hivyo.

Injini ilibebwa kwa toroli kurudishwa nyumbani, matenga ya samaki nayo vivyo hivyo. Mashua alikabidhiwa kijana mwingine ambaye hakwenda dagoni kwa ajili ya ukaguzi na kuiweka sehemu salama.

Wavuvi wote pamoja nami tulifika nyumbani salama na zoezi la kupewa ujira likaendelea.

Baada ya hilo zoezi wavuvi wote wakiwa na tabasamu walielekea kupumzika majumbani kwao, mimi nikabaki na baba huku akinidadisi uzoefu nilioupata huko dagoni.
****

Siku ilienda vyema na muda mwingi niliutumia kupumzika, lakini jua lilivyoanza kuzama tu nikaanza kusikia (kuhisi) baridi isiyo ya kawaida. Nilihisi homa maana tulivyokuwa dagoni tuliumwa na mbu pamoja na usubi ingawaje nyavu (mosquito net) za kuzuia mbu tulikuwa nazo.

Nilipewa panadol ili kujaribu kutuliza homa lakini kadri muda ukivyokuwa unakwenda ndivyo homa ikawa inazidi.

Baba aliamuru kaka yangu mkubwa anipeleke hospitali, hapakuwa mbali sana maana ni mwendo wa kutembea kiasi cha robo saa tu.

Nilifika hospitali giza likiwa limeshaingia nikiwa natetemeka sana, nikapelekwa kuonana na daktari wa zamu, akaniandikia kwenda kupima damu kwa ajili ya malaria na homa ya matumbo.
*****

Nilipata matibabu sawia na vipimo vilivyoonesha, sikuwa na malaira kali, ilionekana kwa mbaali tu (scanty) na sikuwa na homa ya matumbo wala maradhi mengine kwa mujibu wa vipimo.

Nilipewa dawa za kushusha homa pamoja na kuanzishiwa dozi ya klorokwini (chloroquine) kwa ajili ya kutibu malaria iliyoonekana kidogo.

Baada ya siku 3 nilipata nafuu kiasi, bahati nzuri sikuwa mvivu wa kumeza dawa, hata hizo klorokwini nilizimeza kwa kuweka kidonge kwenye ndizi mbivu ndogo na kupita kooni bila tabu hadi nilipo maliza dozi ya 4-4-2. Wakati mwingine pia nilitumia tonge la ugali kuweka dawa na kumeza.

Siku ya nne nikazidiwa tena, safari hii sikuwa na homa bali nilikuwa napata gumbizi mara kwa mara. Nikapelekwa tena hospitali na kupimwa wingi wa damu lakini nilikuwa na damu ya kutosha (13 na) hivyo daktari alishauri nipelekwe Muhimbili kwa ajili ya vipimo vya magonjwa ya moyo.
*****

Muhimbili walianza upya kunipima vipimo vyote muhimu lakini hawakuona ugonjwa wowote wa kuweza kunipa kuzunguzungu ninachojisikia.

Ikashauriwa nipimwe kipimo cha mionzi kwenye kichwa ili kuangalia kama kuna tofauti yoyote humo.

Vipimo vyote vilionesha nipo kawaida, lakini wakaamua kunitoa damu na kuipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi nikaambiwa majibu yatapatikana baada ya siku thelathini.
***

Ndani ya siku 30 za kusubiri majibu kutoka maabara nilikuwa napitia nyakati ngumu na za ajabu ajabu mara kizunguzungu, mara homa lakini havidumu sana kwa maana inakuwa kama homa ya vipindi.

Majibu yalikuja kuwa sina tatizo lolote, na ndipo daktari mmoja wakati wa 'clinic' akatushauri tujaribu dawa za mitishamba.

"Jaribuni kienyeji inawezekana huu siyo ugonjwa wa hospitalini" alisikika yule daktari mtu mzima hivi.

Pilika zikaanza sasa, baada ya kikao vya kifamilia Bagamoyo.

Katika kile kikao ndio nikaelezea kuwa wakati nipo dagoni nilipatwa na gumbizi na kuanguka na kupoteza fahamu.

Ikaamuliwa tuende kwa Zahiri aliyekuwa akiishi Mangesani.

Baada ya kuelezewa hali ilivyonitokea, atatuambia tuende siku ya alhamisi ambapo pia kuna wagonjwa wengine wengi watakuja siku hiyo ili kufanya tiba ya pamoja.

Zahiri (R.I.P) ni tabibu aliyekuwa akitibu maradhi yahusianayo na 'mashetani' ya kijini.

(Alikuwa maarufu sana Bagamoyo na alikuwa shabiki (mwanachama) wa Simba sports club. Mara nyingi Simba wakienda Bagamoyo lazima wafike kwake).

Siku ya alhamisi ilipowadia nilienda kwa Zahiri nikisindikizwa na kaka yangu mkubwa, wagonjwa tukatengwa peke yetu eneo la uani (kwenye uzio wa nyumba) uliozungushiwa kwa makuti, na wasindikizaji waliamriwa wakae pembeni lakini ndani ya uzio huo huo.

Maandalizi ya utabibu yakawa tayari nikaona vigoma (vyapuo) vikipigwa kwa mdundo wa aina yake mara wagonjwa ambao wengi wao walikuwa akina mama walianza kutikisa vichwa, mie nilikuwa dhahiri bila kupata athari za midundo hiyo.

Hali ya ngoma na kucheza iliendelea hadi wengine walianza kugalagala na wengine kuanza kuzungumza maneno yasiyoeleweka, kiarabu si kiarabu, kihindi si kihindi ilimradi vurugu ya mchanganyiko wa lugha, mie nikishuhudia yoye kwa macho.

Nashangaa siku hiyo sikupatwa na homa wa gumbizi badala yake nilikuwa nipo kawaida tu nikishuhudia yote yaliyokuwa yakiendelea.

Baada ya muda fulani kupita, Zahiri alimfuata mgojwa mmoja mmoja na kumshika sikio na kuzungumza sikioni mwa mgonjwa huyo kwa kiswahili na kiarabu.

Wagonjwa wengine walijibu, wengine walipiga kelele tu, wengine walikaa kimya, na alipofika kwangu akanishika sikio nikasisimka lakini nikarudi kawaida.

Alizungumza maneno mengi ya kiarabu na kiswahili lakini mie nilikuwa namuangalia tu.

Mwishowe akamuambia kaka kuwa turudi jumamosi kwa ajili ya tiba zaidi.

Hatukupewa dawa yoyote wala kuombwa pesa.
****

Jumamosi tulifika pale wagonjwa wachache maana wengi siku ya alhamisi walipatiwa dawa za kutumia.

Tukakuta kumeandaliwa sinia zenye vyakula vitamu vitamu vya aina mbalimbali ikiwemo tende, halua, peremende, ndizi mbivu (kisukari), sharubati nk.

"Leo ni siku ya 'chanu' maalum" alisema tabibu Zahiri.

Akashika kitabu na kusoma meneno ambayo sikuyaelewa na vigoma vidogo viaanza kupigwa huku yeye akiendelea kusoma maeno katika lugha isiyokuwa kiswahili wa kiarabu.

Wale wagonjwa wengine mara nikaona wanajongea kwa mitindo tofauti kwenye sinia za vyakula na kuanza kula, lakini mimi nilikuwa nimekaa tu kwenye jamvi pale chini huku nikiziangalia zile ndizi maana napendaGa sana ndizi.

Hali ile iliendelea na mara wale wagonjwa wakawa kawaida, wakapewa dawa zao za kutumia majumbani mwao ikiwemo dawa kama karatasi nyeupe iliyoandikwa maneno na namba za ajabu ajabu kwa wino kama wa rangi ya machungwa hivi (zafarani?) Kwa ajili ya kuloweka kwenye maji kwa ajili ya kunywa na mengine kuogea.

Wakaondoka wagonjwa wote nikabakia mimi na kaka.

Tabibu Zahiri akanisogelea, akaniangalia usoni kwa kunikazia macho na kuzungumza lugha mbalimbali lakini nilikuwa nimetulia tu.

Akachukuwa karatasi nyeupe na peni nyekundu akaanza kuandika andika kwenye karatasi mfano wa kuchora chora kisha akawa kama anakatakata aliyoyaandika na hatimaye akaja na kauli kwamba nipelekwe kwenye kitabu.

"Huyu si wa hapa, mpelekeni kwa Sheikh Mohamed"

Sheikh Mohamed (Allah amwie radhi) wakati huo alikuwa ni kiongozi mkubwa wa dini hapo Bagamoyo na alikuwa ana wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwafundisha elimu ya dini ya kiislamu.

Ilikuwa ni kawaida ya Sheikh Mohamed kukaa nje ya baraza yake kila siku asubuhi baada ya kuswali na kuendea kufanya ibada mbalimbali ikiwemo kupokea salamu za wapita njia.

Hivyo haikuwa vigumu kumpata Sheikh Mohamed kama alivyokusudia tabibu Zahiri.

Jumapili asubuhi mimi na kaka yangu tulifika nyumbani kwa Sheikh Mohamed si mbali sana kutoka kwa tabibu Zahiri ambapo ni umbali wa kuvuka barabara moja ya lami tu.

"Assalaam aleikum" tulimsalimia kwa pamoja

"Wa aleikum salaam, karibuni" alijibu kwa sauti yake nzito huku akituonyeaha sehemu ya kukaa kwenye kibaraza kando ya 'kiambaza' cha nyumba yake, maana dalili zote tulikuwa tunaonesha sisi siyo wa kusalimia na kupita.

"Sheikh tumekuja tuna shida, ndugu yangu huyu anasumbuliwa na maradhi tusiyoyajuwa..." Kaka alieleza historia nzima.

"Haya karibuni ndani" Sheikh alijibu huku akiinuka na kuelekea sebuleni ambapo kulikuwa na busati.

Wakati huo wote mimi nipo kawaida kabisa, sina dalili zozote za maradhi.

Baada ya utangulizi wa kaka, Sheikh akasema "al faat'ha"

Tukaanza kusoma sura ya ufunguzi kutoka kitabu cha Qur’an.

Hii sura waumini wote wa kiislam wanaijuwa maana ndiyo hutumika katika ibada ya swala mara kwa mara.

Baada ya kumaliza kusoma sura ya ufunguzi, akaanza kusoma yeye sura mbalimbali kwa ufupi ufupi na kwa haraka haraka sana, kisha akaagiza yaletwe maji kwenye bilauli akayasomea kisha akaniamuru niyanywe palepale.

Baada ya kunywa akasema turudi Jumatatu baada ya swala ya alasiri kwa ajili ya kisomo maalum.

Siku hazikuganda, Jumatatu ikafika na muda ukawadia tukaenda kwa Sheikh.

Tulivyofika alitukaribisha na kutuambia kuwa amefanya dua kisha akasema:-

“Maradhi haya ni ya bara huko, inabidi tiba aanzie huko”

Neno Bara kwa wakazi wa Pwani hulitumia kama vile kusema ‘mikoani’

Tukaangaliana na kaka pale kisha tukaaga na kuondoka.
***********

Inaendelea
Maradhi ya bara doh!
Wewe ulikua umeshindikana yani wenzio wanaswaliwa swalaa wewe hata unywele hautikisiki 😂 wanaimbiwa vigomaa weee hata hushtuki😂 ulishindikana kwa mganga na kwa shehe pia🙌🙌😁😁!
leadermoe naendelea kujifunza🙇
 
Nimeiangalia

Lakini inaelezea kwa uchache sana juu ya jinni mzuri, ambaye alikuwa kifungoni kwa miaka kadhaa tangia wakati wa Suleiman mwana wa Daud, Jinni huyo alikuwa mtumishi wa Malkia wa Sheba, na kupitia vifungo na utumishi kwa binadamu mbalimbali.

Okay

Hao ni sehemu moja ya majini.

Lakini kama nilivyosema awali, majinni wapo wa species nyingi na wenye fani mbalimali.

Mfano Wajapani wanawatumia kwenye fani ya Ninjitsu! nk

Wachina kwenye fani mbalimbali...

Wahindi, Wazungu, Waarabu na hata sisi waafrika.

Kuna kijana hapa Tz ni fundi wa mifumo ya hydraulic na mitambo, huyu jamaa ana rafiki yake Jinni Mwanamke. 'Wameolewa' mitala na jamaa, ilikuwa siri hadi mkewe (binadamu) akajuwa na wanakula maisha...

Sasa huyu fundi wakati wa JPM akiwa Ujenzi, alimtumia sana kutatua changamoto zilizoshindikana kutatuliwa na mafundi wengine, akija yeye anaangalia tatizo kisha anaenda pembeni anawasha 'udi wake', whatsoever kitu kama udi, basi jinni anakuja kumuelekeza exactly tatizo lilipo na suluhisho.

So huo ni mfano wa kuwatumia vizuri hao viumbe, hehehehe na mzigo anakula, da!

Na mimi binafsi nimeshakaa kwa saa kadhaa chumba kimoja na kajini katoto kaitwako Jeni (mara ajiite Jenifer mara Jannet, mara aseme wao ni tofauti...) vyovyote vile iwavyo, lakini huyu hakuwa mzuri kwa huyo mtoto aliyemvaa...

Alikuwa anamzuia asiende shule...

Akienda tu mtoto (10-11yrs old) anaanguka na kupoteza fahamu, akirudishwa nyumbani kwao anakuwa mzima...

Hapa nilishuhudia jinni akiandika kupitia kwa huyo mtoto (mtoto akiwa hajitambui), yaani Sheikh alikiwa anajibizana naye sheikh kwa kusema, jini kwa kuandika... Mimi na baba wa mtoto tukishuhudia...

Hatimaye aliacha alama ya uwepo wake (huyo Jinni) kwenye kiganja cha huyo mtoto kwa kumchora chora kwa mana isiyoelezeka (bila peni wa nini) wakati awali hakuwa hivyo.

Huyu Jeni ni mfano wa majini wabaya!

Kuna wengine wapo kama dragons , wengine kama magombalima makubwa (bats / popo), wengine kama majoka tu, wapo aina nyingi.
Mh nawe unanitisha
 
Back
Top Bottom