Hata Tundu Lissu hawezi shinda kesi ya Bil 260 ICSID. Wanaohusika na kuingia mikataba mibovu wanyongwe

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Hivi ni nani akipewa Bil 2 kati ya hizo bil 260 atasimama imara kutetea taifa letu? Hata Tundu Lissu pamoja na Uzalendo wake hawezi shinda.

Tumeshuhudia mlolongo wa kesi nyingi serikali ikishindwa hata mahakama za hapa kwetu.

Mtu anaelipwa chini ya 5M akasimamie kesi ya billions unategemea nini?

Suluhisho la haya mambo ni tushughulike huku kwetu hasa tunapoingia mikataba na tenda mtu akiingi mkataba mbovu ni anyongwe tu awe mfano maana hizo pesa zinazopotea zingeweza okoa maisha ya Watanzania wengi.

Na Watanzania tufunguke mtu kaingia mkataba mbovu 2013 /2014 unakuja unavunjwa 2017 analaumiwa alievunja alie ingia katulia anaejoy life, tuko serious kweli?

Lissu aliwahi kushinda kesi gani kwenye uga wa kimataifa, kelele zake ni kwa wapuuzi wa hapa ndani

USSR
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Mtu anaelipwa chini ya 5M akasimamie kesi ya billions unategemea nini ?

suluhisho la haya mambo ni tushughulike huku kwetu hasa tunapoingia mikataba na tenda mtu akiingi mkataba mbovu ni anyongwe tu awe mfano maana hizo pesa zinazopotea zingeweza okoa maisha ya watanzania wengi .
Mkuu, suluhisho ingekuwa ni kuwalipa wanasheria bilioni 2 au asilimia hata 4 ya fedha inayogombaniwa. Wangeshinda vishawishi
 
Serikali inaingia mikataba mibovu ikiwa inajua kuwa ni mibovu.

Ona mkataba kama wa DP WORLD mkataba mbovu lakini serikali na bunge linaung'ang'ania.

Kama sio rushwa ni nini

Baada ya miaka mitano mkataba unavunjika tunaambiwa tulipe fidia.

Wananchi tusikubali tena kodi zetu zilipe fidia.

Mali za CCM ziuzwe zilipe fidia haiwezekani serikali ya CCM iliingize taifa Kwenye mikataba ya kipumbavu ikivunjika watanzania tulipe fidia.
 
Serikali inaingia mikataba mibovu ikiwa inajua kuwa ni mibovu
Ona mkataba kama wa DP WORLD mkataba mbovu lakini serikali na bunge linaung'ang'ania..
Wanajali maslahi yao
 
Hivi ni nani akipewa Bil 2 kati ya hizo bil 260 atasimama imara kutetea taifa letu ? Hata Tundu lissu pamoja na Uzalendo wake hawezi shinda...

Una fikra potofu na mbaya kabisa.

Siyo kila mtu hula rushwa au kuhongwa.

Ushindi kwenye kesi unatolewa kwa kufuata facts na logic.

Siyo sura au jina la wakili linalotoa ushindi.

Tunatakiwa kuwafundisha watoto wetu na vizazi vijavyo kutumia akili zao ili kupata ufanisi katika haki.

Samahani kama nimekukwaza lakini lazima tuwe wakweli kwa kuwafundisha watu wetu fikra chanya ili waondokane na ujinga.
 
Una

Huo ndio ukweli mchungu wewe ni mfuasi wa uongo mtamu
 
Hivi ni nani akipewa Bil 2 kati ya hizo bil 260 atasimama imara kutetea taifa letu? Hata Tundu Lissu pamoja na Uzalendo wake hawezi shinda.

Tumeshuhudia mlolongo wa kesi nyingi serikali ikishindwa hata mahakama za hapa kwetu.

Mtu anaelipwa chini ya 5M akasimamie kesi ya billions unategemea nini?

Suluhisho la haya mambo ni tushughulike huku kwetu hasa tunapoingia mikataba na tenda mtu akiingi mkataba mbovu ni anyongwe tu awe mfano maana hizo pesa zinazopotea zingeweza okoa maisha ya Watanzania wengi.

Na Watanzania tufunguke mtu kaingia mkataba mbovu 2013 /2014 unakuja unavunjwa 2017 analaumiwa alievunja alie ingia katulia anaejoy life, tuko serious kweli?

Watanzania tujiulize mwaka 2013/14
1. Ni nani alikuwa Rais wa Nchi?

2. Ni nani alikuwa waziri wa madini na nishati?

3. Ni nani alikuwa katibu mkuu wizara ya madini na nishati?

4. Ni nani alikuwa naibu waziri wa madini na nishati?

Ukipata majibu ujue hawa watu ndio wanaohitajika kunyongwa kwa kuliinhiza taifa kwenye mikataba mibovu.

2. Kama bado wapo serikalini waondolewe haraka.
 
Attachments

  • 15539BFE-670A-496E-A63F-094792B76E36.jpeg
    15539BFE-670A-496E-A63F-094792B76E36.jpeg
    47.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom