MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Nilimsikia Tundu Lissu akisema eti kabla ya serikali kuzuia makontena ya mchanga ilitakiwa kwanza ikajitoe kwenye uanachama wa Investment Guarantee Agency (MIGA) na Bilateral investment treaties (BITs). Tundu Lissu alienda mbele zaidi na kudai eti serikali inapaswa kufanya kile ambacho nchi ya Bolivia chini ya Rais Evo Morales ilifanya kwa kujitoa kwanza kwenye uanachama wa MIGA na BIT’s kabla ya kuanza ubinafsishaji wa mashirika mbali mbali.
Kwa wale ambao hawakuzisoma hoja za Tundu Lissu wanaweza kugonga hapa na kusoma.
GONGA LINK>>Tundu Lissu: Rais Magufuli anapotosha kuhusu Magwangala ajifunze kwa Rais wa Bolivia
Huu ni ushauri wa kijinga na serikali ikiukubali itakuwa serikali ya kijinga.
Kwanza ieleweke kuwa nchi ya Bolivia haikujitoa kwanza kwenye The International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID) kabla ya kuanza ubinafsishaji. Ikumbukwe kuwa Rais Evo Morales aliapishwa kuwa Rais tarehe 22 January 2006 na siku ya tarehe 1 May 2006 katika sherehe ya wafanyakazi akatangaza kubinafsisha oil and gas industries kwa kuyapa makampuni siku 180 za ku-renegotiate mikataba na serikali au yaondoke nchini ambao baada ya hotuba wanajeshi walienda kuzingira viwanda vya sekta ya mafuta na gesi.
Bolivia ilijiondoa katika ICSID mwezi May 2007, mwaka mmoja baada ya zoezi la ubinafsishaji kuanza.
Tokea aingie madarakani, Rais Morales amebinafsisha oil and gas industry, Zinc industries, Telecoms, tin mining na sehemu kubwa ya usambazaji wa umeme.
Tanzania haiwezi kwenda kujitoa MIGA na BIT’s kwa gharama ya kampuni moja tu ya kimataifa ambayo hata kujitoa kwetu hakutaathiri mkataba wake wakati faida ni kubwa kiuwekezaji kama nchi itaendelea kuwa mwanachama na pia tutakuwa na watanzania ambao ni wazalendo wakati wa kuingia mikataba.
Ikumbukwe kuwa hata kama Tanzania itajitoa, mikataba iliyoingia kabla ya kujitoa haitaathiriwa na uamuzi wa kujitoa kwa sababu ya masharti ya Article 72 ya ICSID Convention.
Article 72 ya ICSID inasema:
“Notice by a Contracting State pursuant to Articles 70 or 71 shall not affect the rights or obligations under this Convention of that State or of any of its constituent subdivisions or agencies or of any national of that State arising out of consent to the jurisdiction of the Centre given by one of them before such notice was received by the depositary.”
Wataalam wa Retrospective law nadhani wanaielewa vizuri hiyo article.
Wataalam wa conflict resolution wanafahamu kuwa huwezi kufanikiwa katika kutatua mgogoro kama upande mmoja una nguvu zaidi ya upande mwingine. Mafanikio hupatikana mara nyingi kama pande zote zitakuwa na nguvu sawa au kama zote kwa pamoja zitafahamu kuwa zinapoteza badala ya kufaidika.
Rais Magufuli anafahamu hawezi kuwashinikiza ACACIA kuipitia(review) mkataba na kufanikiwa wakati ACACIA wanaamini kuwa wanafanya kazi zao ndani ya mkataba. Hii ina maana kuwa ACACIA wanaamini wana nguvu kimkataba zaidi ya serikali. Kwa mantiki hii, serikali haiwezi kuwa na ushawishi na nguvu katika meza ya mazungumzo.
Rais Magufuli anachofanya ni kuibua madhaifu yao ili kupunguza ushawishi na nguvu zao kimkataba na kwa kufanya hivyo itakuwa ni bargaining power ya serikali pindi watakapokaa mezani kujadili hatima ya mikataba baada ya kuipitia kama inavyoelekezwa kwenye sheria ya Madini 2010. Ieleweke kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha sheria ya madini 2010 kinaitaka serikali kufanya mapitio ya mikataba ya madini kila baada ya miaka 5. Serikali haijawahi kufanya mapitio ya mikataba ya madini tokea sheria ya madini 2010 ipitishwe.
Mpaka sasa serikali imeibua madhaifu makuu mawili ya ACACIA,
Udhaifu wa kwanza ni kukwepa kulipa kodi zaidi ya shilingi bilioni 160.
Kuhusu ukwepaji wa kodi, gonga hapa,
GONGA LINK>>Barrick Gold loses appeal vs 160bn tax evasion ruling
GONGA LINK>>Mahakama ya rufaa: Barrick Gold Acacia mining wana hatia kukwepa kodi
Unaweza pia kusoma hapa kuhusu ''madudu'' ya Acacia;
GONGA LINK>>Acacia Mining-Buzwagi mine deception scam in President Magufuli's face
GONGA LINK>>Barrick Gold Acacia: Better the devil you know than the devil you don't
Udhaifu wa pili ni sakata la mchanga(makinikia) ambalo limebeba makosa ya under-invoicing and under-stating values ambayo pia yamebeba makosa kama ya corruption na price transferring.
Haya ni makosa ambayo yanaipa nguvu kubwa serikali itakapoanza kufanya mapitio ya mikataba kwa sababu ACACIA watakuwa wamepunguzwa nguvu za kimkataba. Kamati ya pili ya Rais Magufuli itabainisha ukweli.
Nimedokezwa ACACIA wamefahamu na kuyaona madhaifu yao na kwa sasa wanahangaika kutaka mazungumzo na serikali huku wakidai wako tayari kutoa pesa kwa ajili ya kufanya utafiti wa kuanzisha kiwanda cha kuchengua mchanga (makanikia) nchini.
A Chinese military general, strategist and philosopher, Sun Tzu once said, If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle.