Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,215
1706070145956.jpg

Ukishazaliwa Kigoma au ukiwa na asili ya Kigoma jambo la kwanza unalotakiwa kuwa nalo (kichwani) kabla ya yote unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa maswala ya elimu ya uraia na utaifa. Kwasababu hiyo ndio fitina ya kwanza utakutana nayo pindi tu ukihitaji kujitanua kihimaya. Uraia ndio fimbo ya kwanza utayocharazwa nayo.

Mambo muhimu ni kuhakikisha kwamba makaburi ya wazee wako yanahifadhika kwa pande zote (ubabani na umamani). Hakikisha kwamba nyumba za wazee wako zinahifadhika haziuzwi wala kuvunjwa. Hakikisha kwamba ardhi yenu mnaitunza vyema, kumbukumbu za picha na mabaki ya historia muyahifadhi ipasavyo.

Watoto zenu anzeni kuwafundisha mapema namna ya kukabiliana na kasumba hii ya uraia inayotumiwa kama silaha kuwadhoofisha watu wa Kigoma.

Kwanini tunashauri mambo haya? Ni kwasababu nchi yetu pendwa bado haina njia sahihi ya kufanya verification ya uraia hususan kwa watu walio mipakani. Usumbufu umekithiri mno, na sasa imekua kasumba endelevu.

Sio ajabu tena muhamiaji haramu kuingia nchini, kupata haki zote kinyemela ikiwemo kuajiriwa na kuteuliwa katika nafasi za maamuzi.

Hawa watu wanapataje nguvu hiyo?
...........
Hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mifumo mizuri kwa watu wa mipakani, hususan huku kwetu Kigoma na watu wenye asili ya Kigoma.

Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopewa uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huu kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kama tunawapa watu uraia kwanini hakuna mifumo mizuri ya utambuzi kwa watu hawa? Kwanini bado wenyeji wenye asili ya Kigoma wanapitia madhila na kasumba ya uraia hadi sasa?

Kasumba hii imepelekea hofu kwa watu wa Kigoma, leo mtu wa Kigoma hawezi kuthubutu kusema kwamba ana ndugu Congo au Burundi.

Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi wamesoma hadi shule za Kenya, wana ndugu zao Kenya na Tanzania na wala hawapati usumbufu au ukakasi wowote.

Ukienda Mtwara, Wamakonde na Wayao wapo pande zote mbili za Msumbiji na Tanzania, wala hakuna shida.

Ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na Wazambia na Wamalawi, wameoleana mno, wafanyabiashara wengi wa Lusaka ni Wakinga na Wanyakyusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule Zambia.

Leo hapa mwanakigoma apite mpakani aseme naenda kusalimu ndugu zangu Burundi au naenda kwa ndugu zangu Congo. Basi na yeye atajumuishwa kuwa ni Mrundi au Mkongo.

Ukienda Moshi kwa Wachagga, na Wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili Tanzania na Kenya, nchi ya Kenya kuna eneo na kabila la Wameru.

Ni kawaida sana kumkuta mtu wa Tanga au Zanzibar ana ukoo wa mashangazi na wajomba huko Mombasa Kenya.

Mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote kwasababu watu wanaoleana, wanafanya biashara pamoja, wanazaliana na wengine wanahamia kabisa. Lakini huku kwetu Kigoma mambo yanakua ni tofauti. Dhiki na manyanyaso ya uraia yanazidi.

Je! serikali inasubiri nini kutatua fumbo hili la muda mrefu kwa wakazi wa asili ya Kigoma?

Ukijitambulisha wewe ni mtu wa Kigoma chakwanza kabisa mtu anakufikiria kunako uraia. Kanakwamba watu wa Kigoma ni raia daraja la pili. (Inaumiza sana kihisia na kiakili pindi unapowekewa mashaka).

Kigoma Region Tanzania
 
View attachment 2881093

Ati wamepewa uraia watu zaidi ya 200,000? Huo ni uraia hewa ndugu yangu kutengwa kupo pale pale miaka ya 70's watusi waliokuwepo kagera hasa kambi ya kimuli walipewa uraia na nyerere basi wakaishi mpaka wakazeeka na kufia hapo kagera sasa mwaka 2006 vizazi vyao vilivyobaki vikasombwa na kupelekwa Rwanda kwamba ni wahamiaji haramu wanarudishwa kwao, wengi wao hajui hata lugha ya kinyarwanda hawana ndugu huko ila ikabidi wapekwe tu bila kujali lolote.

Utajiri wa kwanza ni watu sasa inakuwaje nchi inakataa watu? Tutapataje maendeleo bila watu? Na hii kasumba ya ukitaka kumdhoofisha mtu unamuita mkimbizi itaisha lini? Hayo tumeyaona na yanazidi kuongezeka ilikuwaga kigoma na kagera sasa hata geita na shinyanga ukizaliwa huko unaonekana ni raia wa mashaka, mwisho wa haya mambo lini? Yanafaida kwa nani?
 
Mbona sijaishi Kigoma na naona waha wanasumbuliwa hata huku kwetu? akionekana tu anaitwa Ndikumana anaitwa uhamiaji, hata mimi kwetu ni mpakani sn lakini hakuna usumbufu wowote na tuna vuka na kurudi salama
Kuna wahaya wenye pua ndefu kama watusi hao ndo hupata usumbufu sasa, lakini kuna wahaya walioa watusi wakazaa watoto sasa hao watoto ndo husumbuliwa na kuonekana wahamiaji haramu wakimbizi, wanatengwa na kunyoshewa vidole kuanzia siasa nk.
 
Ati wamepewa uraia watu zaidi ya 200,000? Huo ni uraia hewa ndugu yangu kutengwa kupo pale pale miaka ya 70's watusi waliokuwepo kagera hasa kambi ya kimuli walipewa uraia na nyerere basi wakaishi mpaka wakazeeka na kufia hapo kagera sasa mwaka 2006 vizazi vyao vilivyobaki vikasombwa na kupelekwa Rwanda kwamba ni wahamiaji haramu wanarudishwa kwao, wengi wao hajui hata lugha ya kinyarwanda hawana ndugu huko ila ikabidi wapekwe tu bila kujali lolote. Utajiri wa kwanza ni watu sasa inakuwaje nchi inakataa watu? Tutapataje maendeleo bila watu? Na hii kasumba ya ukitaka kumdhoofisha mtu unamuita mkimbizi itaisha lini? Hayo tumeyaona na yanazidi kuongezeka ilikuwaga kigoma na kagera sasa hata geita na shinyanga ukizaliwa huko unaonekana ni raia wa mashaka, mwisho wa haya mambo lini? Yanafaida kwa nani?
Eti utajiri ni watu, kawachukue M23 na hamas wale pia si watu kawachukue ili waanzishe makazi makazi tupate maendeleo.

Yaani hali hii akili ndo tumepewa Bure ingekua tunalipia sijui ingekuaje
 
Kuna wahaya wenye pua ndefu kama watusi hao ndo hupata usumbufu sasa, lakini kuna wahaya walioa watusi wakazaa watoto sasa hao watoto ndo husumbuliwa na kuonekana wahamiaji haramu wakimbizi, wanatengwa na kunyoshewa vidole kuanzia siasa nk.
Mbeya, Songwe, Mara na Kilimanjaro nazo zimepakana na nchi jirani na kuoa na kuolewa ni jambo la kawaida sn, mbona hakuna usumbufu wowote?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom