Ni ngumu sana kumpata Mwanamke kama Tulia Ackson. Ana uwezo mkubwa, anafaa kuwa Rais

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Habari za Sabato!

Sijawahi kumfahamu Mwanamke yeyote kwa hapa Tanzania mwenye uwezo kama Tulia Akson. Sisemi ili wengine wamuonee Wivu, wala sisemi ili yeye awe na Kiburi. Ila naongea kila ambacho ninaokiona Kwa Tulia mwenyewe.

Kama utapata Nafasi ya Kumsikia Tulia Akson akizungumza iwe kwa kuhojiwa au kuhutubia, utagundua kuwa hana tofauti na kina Kamala Harris au kina Hilary Clinton.

Utulivu!
Kujiamini!
Umahiri!
Hoja!
Ubobevu!,

Nimeona Watu wengi wanapokutana na Tulia katika mijadala wakimshindwa kwa Hoja. Unapozungumzia hoja Unazungumzia uwezo wa akili ya mtu kujenga mantiki, yaani kitu kieleweke. Wakati mwingine kwa lugha rahisi.

Tulia sijawahi kumsikia akijali uanamke wake au maumbile yake kama sehemu 6a kikwazo katika kazi zake.
Tena yeye hupendelea changamoto anapokutana na sisi wanaume.

Tulia hatajali kama wewe ni Waziri au Mheshimiwa, ukiwa bungeni kama ataona kuna jambo hujalitolea maelezo yaliyonyooka au hakuna hoja anauthubutu wa kukukosoa au kutaka kukuweka Sawa.
Kujadiliana na Tulia Akson itakupasa uwe na uwezo mkubwa kama yeye au umzidi ili usije ukaaibika.

Kwa mwanaume mwenye upeo mdogo lazima amwone Tulia kama Mjuaji, hasa pale atakaposhindwa kwa Hoja.

Tunaposema Wanawake wapewe nafasi tunahitaji wanawake wa mfano wa Tulia Akson. Wanawake wenye uwezo.

Sio Mwanamke anayelalamika hajapewa haki yake. Tunahitaji Wanawake wenye uwezo wa kudai haki zao wenyewe bila kusaidiwa. Hao ndio watakuwa na uwezo wa kuongoza.

Tulia Akson anauwezo wa kushika nafasi ya Urais katika nchi yetu na sio hivyo tuu hata kuongoza Nchi yoyote hapa Duniani. Kwa sababu anasifa za level za kimataifa.

Nimemaliza
 
Kwa lile bunge legelege sijui umetumia kigezo gani kupima uwezo wa Tulia kwenye kujenga hoja.

Nina wasiwasi unamchukulia Tulia vile alivyo na tabia za kidikteta, kuingilia mazungumzo ya wale anaozungumza nao, ndio unamuona ana uwezo wa kujenga hoja.

Sijui kama uliwahi kumuona yule Tulia aliyeliongoza bunge kupitisha ule mkataba haramu na DPW unaolalamikiwa na wengi mpaka leo, yule alikuwa kuwadi wa watanganyika aliyejipendekeza kwa serikali ili kufanya kile serikali inachotaka.

Akiwa kama spika wa bunge alitakiwa kuwa kama refarii, awaongoze wote wanaopinga hoja na kuunga mkono hoja, lakini badala yake Tulia bila aibu akasimama na wale wanaounga mkono hoja kutoa bandari zetu, huyu ni kiongozi wa hovyo kabisa nina wasiwasi na upeo wako kumsifia.

Watu waliokuwa wakipinga kama Mpina ndio hawakupewa hata hiyo nafasi ya kutoa mchango wao kwa mdomo, kama Tulia anajiamini kwenye kujenga hoja kwanini akawazuia wale wenye kupinga uuzwaji wa bandari zetu wasiongee bungeni siku ile?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Lile bunge legelege sijui unetumia kigezo gani kupima uwezo wa Tulia kwenye kujenga hoja.

Nina wasiwasi unamchukulia Tulia vile alivyo na tabia za kidikteta, kuingilia mazungumzo ya wale anaozungumza nao, ndio unamuona ana uwezo wa kujenga hoja.

Sijui kama uliwahi kumuona yule Tulia aliyeliongoza bunge kupitisha ule mkataba haramu na DPW, yule alikuwa kuwadi wa watanganyika aliyejipendekeza kwa serikali ili kufanya kile serikali inachotaka.

Akiwa kama spika wa bunge alitakiwa kuwa kama refarii, awaongoze wote wanaopinga hoja na kuunga mkono hoja, lakini badala yake Tulia bila aibu akasimama na wale wanaounga mkono hoja kutoa bandari zetu, huyu ni kiongozi wa hovyo kabisa nina wasiwasi na upeo wako kumsifia.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Shida ninayoona anayo, ni kuna muda anafanyaga mambo kukomoa yani ni kwamba utafanya nini sasa nimefanya.
Hana tofauti sana na ndungai.
Yani kama hakupendi basi atakukomoa hata kama anajua anachofanya si sahihi.
 
Habari za Sabato!

Sijawahi kumfahamu Mwanamke yeyote kwa hapa Tanzania mwenye uwezo kama Tulia Akson. Sisemi ili wengine wamuonee Wivu, wala sisemi ili yeye awe na Kiburi. Ila naongea kila ambacho ninaokiona Kwa Tulia mwenyewe.

Kama utapata Nafasi ya Kumsikia Tulia Akson akizungumza iwe kwa kuhojiwa au kuhutubia, utagundua kuwa hana tofauti na kina Kamala Harris au kina Hilary Clinton.

Utulivu!
Kujiamini!
Umahiri!
Hoja!
Ubobevu!,

Nimeona Watu wengi wanapokutana na Tulia katika mijadala wakimshindwa kwa Hoja. Unapozungumzia hoja Unazungumzia uwezo wa akili ya mtu kujenga mantiki, yaani kitu kieleweke. Wakati mwingine kwa lugha rahisi.

Tulia sijawahi kumsikia akijali uanamke wake au maumbile yake kama sehemu 6a kikwazo katika kazi zake.
Tena yeye hupendelea changamoto anapokutana na sisi wanaume.

Tulia hatajali kama wewe ni Waziri au Mheshimiwa, ukiwa bungeni kama ataona kuna jambo hujalitolea maelezo yaliyonyooka au hakuna hoja anauthubutu wa kukukosoa au kutaka kukuweka Sawa.
Kujadiliana na Tulia Akson itakupasa uwe na uwezo mkubwa kama yeye au umzidi ili usije ukaaibika.

Kwa mwanaume mwenye upeo mdogo lazima amwone Tulia kama Mjuaji, hasa pale atakaposhindwa kwa Hoja.

Tunaposema Wanawake wapewe nafasi tunahitaji wanawake wa mfano wa Tulia Akson. Wanawake wenye uwezo.

Sio Mwanamke anayelalamika hajapewa haki yake. Tunahitaji Wanawake wenye uwezo wa kudai haki zao wenyewe bila kusaidiwa. Hao ndio watakuwa na uwezo wa kuongoza.

Tulia Akson anauwezo wa kushika nafasi ya Urais katika nchi yetu na sio hivyo tuu hata kuongoza Nchi yoyote hapa Duniani. Kwa sababu anasifa za level za kimataifa.

Nimemaliza
Hamna kitu hapo. Watu mnasifia ujinga tu sijui mumelipwa Shillingi ngapi? Huyo Tulia bila LIFT ya Magufuli asingefika hapo alipofika. Alimfanyia nini Magufuli hadi akampa u Naibu Spika, ni siri yao

Kwenye duru za sheria wala siyo nguli kihivyo, nenda kaulize UDSM uone kama ana machapisho. Ukikuta ana machapisho nenda kayatest kwa Plagiarism application ndiyo uje hapa.

Watu eti wanamsifia kushinda kesi ya muta 200 mwaka 2015. Ile kesi hata mwanafunzi wa first year Law School angeshinda tu kwa kuwa tayari Jaji wa High Court alikuwa na maelekezo.
 
Back
Top Bottom