Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, leo Julai 8, 2023 amesema kuwa tozo kwenye miamala ya kutoa pesa haijafutwa.
"Tozo imefutwa kwenye utumaji ama usafirishaji wa fedha kupitia kwenye mifumo, ukituma wewe fedha kupitia kwenye simu yako kwenda kwenye simu nyingine, ile tozo tuliyokuwa tunaipigia kelele imefutwa, lakini ukienda kutoa fedha kwenye ATM ama kwa wakala ipo" amesema Msigwa.
Pia, amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhamasisha uchumi usiotumia fedha taslimu ambao dunia ya sasa inahama huko pamoja na kupunguza gharama za uchapishaji wa noti ambapo serikali hutumia fedha nyingi.
Awali, JamiiForums kupitia jukwaa lake la Jamii Check, Julai 6, 2023, ilitoa pia ufafanuzi huu ulioungwa mkono na msemaji wa Serikali hii leo.
Tozo za miamala ya kieletroniki zilizofutwa ni;
- Unapomtumia mtu muamala kutoka simu yako kwenda simu ya mtu mwingine.
- Unapohamisha fedha kutoka akaunti yako ya Benki kwenda akaunti nyingine.
- Unapohamisha fedha kutoka akaunti yako ya Benki kwenda kwenye simu yako.