Serikali imefuta Tozo Kwa muamala ya kutuma na sio miamala ya kutoa kama wanavyojinasibu

Rurakha

Senior Member
Oct 20, 2019
121
209
Napenda kuwataarifu kuwa Tozo zilizofutwa ni Kwa miamala ya kutuma pesa pekee

Mfano umeweka pesa kwa Wakala na umahitaji kufanya transfer kwa nature ya maumala huo Hauna Tozo

Ila ukienda Kwa Wakala au Benki kutoa pesa utakatwa Tozo

Mfano nimeambatisha makato ya mtu anaetoa 70k Kwa Wakala wa CRDB atakatwa kama ifuatavyo
1. Ada ya muamala ni 3284.86
2. Tozo ya Serikali 573

Jumla ya Makato ni 3857.86

Lakini Kwa taarifa nimezopata wakati mteja akiwa anatoa hatokua na access ya kuona haya makato ila Wakala atayaona

Makato haya yako applicable Kwa wanaotumia Benki na Mitandao ya simu

Binafsi naona ni makato makubwa sana ndio maana Benk zinapata faida kubwa sana tuendelee kupaza sauti hizi Tozo za kinyonyaji zifutwe
 

Attachments

  • Screenshot_20230707-111845.jpg
    Screenshot_20230707-111845.jpg
    61.8 KB · Views: 4
Hata kutuma hazijafutwa mimi nimetoka kutuma hela sasa hivi miamala hipo pale pale
 
Kabla viongozi hawajaficha sura zao kwa hii aibu ya kutudangaya kuna wale wapambe walikuwa wanaropoka kwa nguvu wakisoma vichwa vya habari kwenye magazeti
 
Back
Top Bottom