[B]Ripoti ya Benki Kuu sio Wiki Ijayo sasa imekuwa JANUARI/08,Kwa nini kila siku Tarehe zinapelekwa mbele! Kuna nini kinafichwa hapa,endelea kusoma maneno ya CAG,kama yalivyonukuliwa kwenye gazeti la majira;
[/B]
*CAG akadhiwa ripoti ya mwisho ya uchunguzi
*Aahidi kutobadili chochote kilichoainishwa
*Asema ataifikisha kwa Rais Kikwete kama ilivyo
* Kukadhiwa wiki ya kwanza Januari mwakani
Na Mwandishi Wetu
WAKATI utata wa kujiuzulu kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Daudi Balali ukiendelea kutanda, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amepokea ripoti ya mwisho ya uchunguzi wa ubadhirifu ndani ya benki hiyo uliofanywa na Kampuni ya Ennst & Young.
Taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na kusainiwa na CAG, Bw. Ludovic Utouh, ilieleza kwamba ripoti hiyo imepokelewa baada ya rasimu ya awali ya uchunguzi huo kupokelewa Novemba 27 mwaka huu.
"Kama ilivyoelezwa kwenye taarifa hiyo, ripoti iliyopokelewa ilikuwa ni ripoti ya awali ambayo ilifanyiwa kazi na ofisi yangu na kurudishwa kwa wataalamu walioifanya kazi hii ili kukamilisha ripoti hii. Huu ni utaratibu wa kawaida wa kufanya kazi za ukaguzi hasa ikichukuliwa maanani kuwa Kampuni ya Ernst & Young, imefanya kazi hii kwa niaba yangu," alisema Bw, Utouh.
Katika taarifa hiyo, Bw. Utouh, alisema mbali na uchunguzi wa 'EPA Account'ya Benki ya Tanzania, hadidu za rejea za kazi hiyo ziliwataka wachunguzi kurejea ukaguzi wa hesabu za BoT za mwaka 2005/06, kazi iliyofanywa na Kampuni ya Hesabu ya TAC Associates ikishirikiana na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Alisema wachunguzi hao wametakiwa kutoa ripoti mbili tofauti moja ikiwa ni ya 'EPA Account' na nyingine ikihusu rejea ya ukaguzi wa hesabu za BoT kwa hesabu za mwaka 2005/06.
" Hivyo basi, napenda kutoa taarifa rasmi kwa Watanzania wenzangu ya kuwa nimepokea kutoka Kampuni ya Ernst & Young taarifa za mwisho za uchunguzi, siku ya Jumapili Desemba 23 (jana ). Kwa sasa nazipitia ripoti hizi mbili ili kujihakikishia usahihi wa yaliyomo kabla ya kuwasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete katika juma la kwanza la Januari, 2008 baada ya kumaliza likizo yake, alisema Bw. Utouh.