Gavana Balali Ajiuzulu!

Gavana Balali Ajiuzulu!

Tusisahau ya Kabwe kunusurika na kombeo kumchota Mbatia!

According to dataz, mama wakati anafariki alikuwa na shillingi millioni 200 cash, ndani ya gari ambazo zilkuwa ni mabaki ya alizokwisha zigawa mikoa kama 20, ambako alikuwa tayari ameshapitia katika kupiga kampeni ya NEC, na alikuwa amekbakiza mikoa sita zaidi akizunguka kugawa rushwa,

Kumbe kisa na mkasa wa safari, ilikuwa ni kampeni za NEC, I mean Mungu emuweke mahali pema huko mbinguni, lakini damn it!
K**leki walai! Sasa haya mahela yote yaliishia wapi au ndo wajanja walijichotea? Hii nchi ni crisis kwa kweli, sasa mpaka hapo FMES hujakubali tu kwamba tunahitaji kuanza upya nikiimanisha bila CCM?
 
Hivi kuna watu wanaamini wanaweza kumtetea Balali? Huyu naona hateeki, hata huruma ya mgonjwa hawezi kupata-yaani ndo imetoka hivyo. Tena sidhani kama kuna mtu mwenye akili atazaa mtoto akubali kumwita Balali, utakuwa uwenda wazimu!
 
Kalamu,
Uchunguzi wa BoT ulianza toka JK alipoingia madarakani. Nina hakika mada na BoT na kina Balali imekuja JF baada ya hotuba ya mama Meghji kuzungumzia wizi BoT bungeni, tena uchunguzi unaofanyika unahusiana na fedha za misaada ikiwa ni pamoja na World Bank. Kuna wizi uliotangulia huu wa Dr. Slaa na mada yake ilikuwepo hapa JF mapema tu bunge a kwanza.
Hizi kamba za JK kuwa uchunguzi unafanyika ni kutafuta muda Wadanganyika msahau kwani hakuna anayetazama ama kufuatilia madai ya Dr. Slaa ambayo rais mwenyewe alisema kuwa hazina ushahidi, mwenye ushahidi aulete.. kisha msisitizo zaidi umekuja pale JK alipotembelea US ndipo katoa hadi ya kulitupia jicho swala hilo.
Kwa taarifa za mjini mzee wangu hakuna mtu anayefuatilia swala la Dr. Slaa kuhusu BoT kama orodha tuliyoiweka hapa JF akaiwakilisha hadi hili swala la orodha ya mafisadi.
Huu ni wizi mwingine kabisa ambao ushahidi wake ulipatikana ktk vitabu vya benki hiyo kuu ndio unachunguzwa hadi kesho na hauhusiani kabisa na madai ya Dr. Slaa ama sivyo tungemsikia JK akichagua kamati maalum ya kuchunguza swala hilo bila kumsahau Dr. Slaa mwenyewe. ndugu yangu usisikie kabisa habari za magazeti yetu wanafiki wakubwa na wajuzi wa tungo na simulizi.
 
Barua ilifika Ikulu tangu Jumatano, wao walikuwa wamekusudia kumsimamisha kazi ambako kungeendana na kutolewa ripoti ya BoT, mwenzao kawawahi.. now its their move! Miye niko hapa napiga mluzi tu.. !


Kujifunga goli, kwa sababu zipi?
Huu mwaka hawatausahau; yaani unavyoendelea kuisha taratibu, utadhani ni movie iliyopunguzwa spidi hivi......!
 
Mtanzania,
nadhani bado hujanielewa. Mtu kama Dr. Slaa hana ushahidi zaidi ya kukusanya makaratasi ambayo kwa mswahili hayana nguvu kortini wala kwa rais. Huyu hana madhara zaidi ya watu kusema sana vijiweni lakini mafisadi wenyewe wanazidi kutesa. Ni korti za migahawani ambako mtu akisema na watu wakisha jua basi inatosha. Hii ndio sifa ya Dr. Slaa ambayo imetumika Kisiasa sio kwa manufaa mengine zaidi, na wananchi tumempa sifa hiyo kisiasa. Alistahii hizo sifa kisiasa nothing else!
Balali is smart that hiyo scenerio ya kiswahili...pili yeye sio mwana siasa na kesha lala na huyo mwanamke malaya. Nimekuuliza vizuri akisha sema then what?... wewe nambie kwa jinsi unavyoifahamu serikali ya TZ pamoja na sisi wenyewe ni kipi kitafuata?
Jamani Mkapa na rada yule pale anadunda na kutuita wajinga. Lowassa na Richmond ni waziri mkuu hadi 2015 atakapo gombea urais. Karamagi ndio kwanza anatafuta wawekeshaji wengine wenye deal nene. What have we done? nothing isipokuwa kuwaona hawa watu heroes na kuwaunga mkono kama vile thanks za JF. Zitto hadi leo hayupo bungeni na wananchi tumekwisha sahau na kamati mpya imeshateuliwa akiwamo Zitto mwenyewe hali bunge na baadhi wananchi bado wanaamini kalidanganya bunge!..
I mean huu mchezo wa kuzungukana mbuyu utakwisha lini! when are gonna be serious.

Deja' Vu!! But what do we do?! OOh dear, Hivi Tanzania yetu tumelaaniwa?... Siongopi, mbona Ndg. Mkandara kwa hayo uliyosema naanza kujisikia kichefuchefu.... Duuh, najisikia kizunguzungu, Inatisha kwa kweli, na naanza kuona Tanzania yetu on a self catastrophic collision course, na hapo ndipo maneno ya Mwl. Nyerere (RIP) yatatimia - maana hii itakuwa "UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA!!

EEH MOLA, TUNUSURU!

SteveD.
 
Jamani,

Nakubaliana na Mkandara, pasipo ushahidi wa kuwasilishwa mahakamani, kelele zote ni bure!

Tunafukuta kama fuko, mishipa ya damu na misuliimevimba na mapigo ya moyo yanakwenda kasi ya sungura, lakini tukiambiwa leteni basi huo ushahidi hata kama ni mahakama ya Ubelgiji, ushahidi wa kweli hatuna zaidi ya "inasemekana" "inaaminika"!

Ukiangalia mtiririko wa maneno ya Slaa na orodha yake, hakuna hata kimoja kinachowezakupitika mahakamani zaidi ya kurutubisha gumzo mtaani!

Jambo pekee ambalo nina angalau tumaini kupatiwa ufumbuzi japo waweza kuwa mdogo, ni kamati ya Bunge ya RDC. Ushahidi wa udhaifu wa kuwa makini katika utendaji ni mkubwa sana, ingawa mazingira ya Rushwa yanaweza kutoka patupu kama maneno ya Hosea.

Tujiulize, je mfumo wetu wa Tanzania na sheria zake ni makini kama siye tuishi ughauibuni? iwe ni UK, USA, Japan au China?

Balali, kamwe hatafikishwa mahakamani! sana sana ni kujiuzulu (kama Ikulu inakana hajajiuzulu), kufukuzwa kazi ama kurudi mavumbini.

Je mmesahau kesi ya Kiula ilikwisha vipi? Mnyiramba yule he was smart! Vi-memo vyote alikuwanavyo, akawasilisha mahakamani(kwa mwendesha mashtaka), kesi ikafutwa, kabakia mkulima wa Karanga kwao Kinampanda! waliohusika baada ya Kuhara, leo wanapigia kelele Waandishi wa habari kuwa wamejaa Rushwa!

Changes to bring justice will happen once we are more organized and competent in our investigaions!
 
Mkandara,

Yes investigation of BOT is on debt structure bonds stuff and not Majengo or Meremeta!
 
Kalamu,
Uchunguzi wa BoT ulianza toka JK alipoingia madarakani. Nina hakika mada na BoT na kina Balali imekuja JF baada ya hotuba ya mama Meghji kuzungumzia wizi BoT bungeni, tena uchunguzi unaofanyika unahusiana na fedha za misaada ikiwa ni pamoja na World Bank. Kuna wizi uliotangulia huu wa Dr. Slaa na mada yake ilikuwepo hapa JF mapema tu bunge a kwanza.
Hizi kamba za JK kuwa uchunguzi unafanyika ni kutafuta muda Wadanganyika msahau kwani hakuna anayetazama ama kufuatilia madai ya Dr. Slaa ambayo rais mwenyewe alisema kuwa hazina ushahidi, mwenye ushahidi aulete.. kisha msisitizo zaidi umekuja pale JK alipotembelea US ndipo katoa hadi ya kulitupia jicho swala hilo.
Kwa taarifa za mjini mzee wangu hakuna mtu anayefuatilia swala la Dr. Slaa kuhusu BoT kama orodha tuliyoiweka hapa JF akaiwakilisha hadi hili swala la orodha ya mafisadi.
Huu ni wizi mwingine kabisa ambao ushahidi wake ulipatikana ktk vitabu vya benki hiyo kuu ndio unachunguzwa hadi kesho na hauhusiani kabisa na madai ya Dr. Slaa ama sivyo tungemsikia JK akichagua kamati maalum ya kuchunguza swala hilo bila kumsahau Dr. Slaa mwenyewe. ndugu yangu usisikie kabisa habari za magazeti yetu wanafiki wakubwa na wajuzi wa tungo na simulizi.

Ninakubaliana na mengi uliyoyasema humu, hasa ukweli kuhusu uchunguzi wa BOT.

Pamoja na hayo, Slaa bado ametoa mchango, hata kama sisi mitaani ni wasahaulifu kiasi hicho. Na hapo ndipo ninaposema kuwa wapinzani wachukue jukumu hilo la kutukumbusha, mara kwa mara sisi wananchi, pengine siku moja tutazinduka na kuanza kuona mambo yalivyo. Hilo litakuwa limesaidia kutuondolea wadharimu hawa.

Tusilokubaliana, ni hilo la kutokuwepo na faida inayotokana na akina Slaa kuendelea kuibua mambo kisiasa.
 
Rev. Kishoka,
Balali, kamwe hatafikishwa mahakamani! sana sana ni kujiuzulu (kama Ikulu inakana hajajiuzulu), kufukuzwa kazi ama kurudi mavumbini
Shukran mkuu wangu ebu tazama hilo hasara alilotuweka Karamagi, wananchi wanaomba rais amsastaafishe! - What a crap, hivi kweli tunaridhika na kustaafu kwake. That's all wadanganyika mnaliomba?

Kalamu,
Kweli kabisa Dr. Slaa anastahili sifa sanaaa lakini kisheria haimsaidii kitu Mdanganyika kufahamu hayo while nothing changes - Bora nusu shari kuliko shari kamili.
 
Tusisahau ya Kabwe kunusurika na kombeo kumchota Mbatia!

According to dataz, mama wakati anafariki alikuwa na shillingi millioni 200 cash, ndani ya gari ambazo zilkuwa ni mabaki ya alizokwisha zigawa mikoa kama 20, ambako alikuwa tayari ameshapitia katika kupiga kampeni ya NEC, na alikuwa amekbakiza mikoa sita zaidi akizunguka kugawa rushwa,

Kumbe kisa na mkasa wa safari, ilikuwa ni kampeni za NEC, I mean Mungu emuweke mahali pema huko mbinguni, lakini damn it!

Wakuu,

Labda mie ni umaskini wangu unanisumbua, lakini ningekuwa na hela kama hiyo nisingetoa rushwa hata kidogo kwa ajili ya ujumbe wa NEC, ningeitumia kuimarisha shamba langu na ningepata hela nzuri zaidi. Kumbe tunatofautiana sana na hawa jamaa katika kufikiri!
 
Dua,
Chukueni mali zote za Balali lakini bado mtakuwa hamja solve problem ambayo ni virus ndani ya uchumi wa nchi yetu. wajomba wanaotumaliza bado wamo ktk system na mkichukua mali zake kesho zitarudi palepale maanake Mafia watamwona kaweza ku keep ahadi.
Kitu muhimu kwetu ni kutafuta mbinu ya kuweza kuyajua yote na kisha kuyafanyia kazi, lakini kama tumeshindwa huko nyuma Balali hawezi kuwa mhanga!...na nani yupo tayari kumtoa mhanga ama ndio maneno yetu ya mtaani tu.

Pamoja na kukubaliana na hilo kwamba hana mali ya kuweza kulipa hasara lakini ni vizuri hata kile kidogo ambacho atawaachia watoto wake au ndugu kichukuliwe kwani sio kidogo cha kutokuweza hata kuwasomesha wabongo 10 au ishirini kwenye vyuo vikuu Tanzania au nje.
 
Dua,
Hujanielewa maana yangu. Mkichukua leo kesho account yake itarudi pale pale kwani virus ni vigogo wenyewe wamo serikalini ndani ya uchumi wetu. Na pengine atapewa zaidi kuondoa Wabongo wengine 10 ama 20 vyuoni. Hii ndio Bongo mjomba matanuzi hayana mpaka wala haogopwi Mungu sembuse binadam.
Ukichukua nyumba yake kesho atapewa Polisi Oficers mess yote!
 
Kithuku:
Na ndio sababu tunasema, sasa hivi CCM inakopi kila kitu kilichokuwa kinafanywa na KANU. Tegemeo letu ni kuwa pengine, muda si mwingi na sisi tutalokoka.

Hata hivyo, sioni ni jinsi gani tutaondokana tena na rushwa katika siasa tena, iwapo kuwa kupata uongozi ni lazima uwe na nyenzo ya kuupatia huo uongozi. Chukulia mfano wa mapesa yaliyomwagika katika uchaguzi huu wa Kenya wa hii kesho kutwa!
 
Wakuu,

Labda mie ni umaskini wangu unanisumbua, lakini ningekuwa na hela kama hiyo nisingetoa rushwa hata kidogo kwa ajili ya ujumbe wa NEC, ningeitumia kuimarisha shamba langu na ningepata hela nzuri zaidi. Kumbe tunatofautiana sana na hawa jamaa katika kufikiri!

Wenzako mashamba yao ni madaraka na mengine yote yanaanzia hapo. Hawa ukiwanyanganya madaraka hawana pakuanzia maana mishipa ya fikra ilishazibwa na hayo madaraka kwa ulevi
 
Jamani, Accountability! Accountability! Accountability!

Balali lazima a-take responsibility of his actions. Amevunja miiko ya kiongozi na ame-misuse office yake. Nyinyi mnaomtetea, inawezekana kunakosekana ushahidi wa some allegations, BUT; facts is; zaidi ya dola milioni mia tatu na nyongeza zimepotea kiajabu ajabu chini ya uongozi wake akiwa kama gavana! Mnataka facts na shutuma gani zaidi ya hiyo ili Balali awe accountable for? Isn't that enought? Mnataka nini tena jamani? Acha mimi niende zangu, maana naona haya ya sasa yananishinda! Xmas njema wazalendo.
 
Serikali kwa kupitia Waziri Meghji imethibitisha kuwa Ripoti ya E&Y Itatolewa public wiki ijayo;

Balali akamatwe - Dr.Slaa

Na Salehe Mohamed.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali.
Dk. Slaa ametoa kauli hiyo jana siku moja tu baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo hazijathibitika kuwa gavana huyo, ambaye yupo Marekani kwa matibabu, ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo, akitaja maradhi yanayomsumbua kama sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo.

Akizungumzia taarifa za kujiuzulu kwa Dk. Balali, Dk. Slaa kwanza alimpa pole kutokana na maradhi yanayomkabili, lakini akamtaka Rais Kikwete kuamuru kukamatwa kwa gavana huyo mara moja ili ajibu tuhuma zote zinazomkabili.

Akiandika ujumbe mrefu wa simu ya mkononi, Dk. Slaa aliorodhesha baadhi ya tuhuma ambazo Dk. Balali anatakiwa kuzijibu kuwa ni kughushi taarifa ya BoT ya 2005 aliyowasilisha kwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji Septemba 20, 2005 katika kitabu ambacho ndani yake taarifa ya fedha ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imesainiwa Juni 21, 2007.

"Isitoshe yeye mwenyewe amesaini kama Mwenyekiti wa BoT Juni 21, 2007. Balali pia amesaini balance sheet (mizania) ndani ya kitabu hicho hicho. Taarifa zinazohusika ni hizo hizo za 2005/2006 zenye migogoro. Ni dhahiri kuna kughushi.

"Meghji kakaa kimya. Kughushi au ku-back-date (kurudisha nyuma tarehe) ni kosa la jinai. Kuna kirusi gani nchini? Raia wa kawaida hata angeumwa saa hizi angekuwa analindwa na askari magereza hospitalini… hakuna mwenye kibali kuvunja sheria," alisema.

Alizitaja tuhuma nyingine kuwa ni matumizi yenye kutia shaka katika malipo ya akaunti ya nje (EPA), fedha zilizolipwa KAGODA Co bila maelezo, fedha zilizopelekwa Deep Green na zile za Tangold Ltd.Aidha, alimtaka Rais Kikwete kumchukulia hatua za kisheria na ikiwezekana kumfikisha mahakamani Balali akimtuhumu kufuja fedha za wavuja jasho, ambao kila kukicha maisha yao yanazidi kudidimia kwa sababu ya watu wachache wanaotumia rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi.

"Serikali inaogopa nini kumchukulia hatua mtu anayefuja mabilioni ili hali mjamzito anajifungulia bila huruma ofisi ya WEO kwa ajili ya kukosa sh 20,000?" alihoji Dk. Slaa. Hata hivyo, madai hayo ya Slaa yalipata kukanushwa wakati fulani na Balali wakati alipoitisha mkutano nadra na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya watu kadhaa kumhusisha na tuhuma za ubadhirifu wa BoT alizozielezea kuwa zisizo na msingi.

Wakati Slaa akitoa madai hayo, ripoti ya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha BoT uliofanywa na kampuni ya ukaguzi wa mahesanu ya Ernst & Young kwa maagizo ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), itawekwa hadharani wiki ijayo.Hayo yalithibitishwa jijini Dar es Salaam jana na Waziri Meghji, aliyewaambia waandishi wa habari kuwa ripoti hiyo ndiyo kwa kiasi kikubwa itakayoisaidia serikali kushughulikia kile kitakachoonekana kina tatizo.

Akifafanua, Meghji alisema kuwa, ushughulikiaji huo wa matatizo yatakayoainishwa katika ripoti hiyo, kutahusisha pia kuwachukulia hatua stahili, wale wote watakaobainika kufanya makosa, kulingana na taratibu za kazi na sheria za nchi.Alisema hivi sasa ni vigumu kuanza kuzungumzia suala la ubadhirifu wa fedha au kumnyooshea mtu kidole, hadi hapo ripoti hiyo itakapokamilika, hivyo ni vema kwa wakati huu jamii ikaendelea kuvuta subira.

"Тuvute subira jamani kwani ripoti itatolewa ‘next week' (wiki ijayo) na ndipo hapo tutaangalia cha kufanya kwa yale yatakayobainika na kuwachukulia hatua wale wote watakatajwa na ripoti hiyo," alisema Meghji.Serikali iliiagiza CAG kuyafanyia uchunguzi madai ya viongozi wa upinzani kuwapo kwa matumizi mabaya (ufisadi) ya fedha za wavuja jasho katika BoT.Viongozi hao wa upinzani wakiongozwa na Dk. Slaa, ndio walioibua sakata hilo bungeni na kudai kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na matumizi ya fedha yenye kutia shaka ndani ya BoT.

Awali, madai hayo ya wapinzani yalipingwa vikali na serikali, lakini baadaye, ilibainika kuwepo kwa kasoro katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na ndipo serikali ilipoiagiza ofisi ya CAG kufanya ukaguzi huo.

Meghji anatoa kauli hiyo siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuhoji sababu za serikali kuikalia ripoti hiyo kwa muda mrefu hata baada ya kazi kukamilika.Kwa upande wake, Dk. Slaa bado anaendelea kudai kuwa, ukaguzi huo umefanywa katika sehemu ndogo sana kwani ubadhirifu ndani ya BoT unahusisha vitengo vingi zaidi ya EPA.

Katika hatua nyingine, Meghji, alisema mpaka sasa ofisi yake haijapata taarifa ya kujiuzulu kwa Dk. Balali na kusema kuwa taarifa hizo alizisoma kwenye magazeti jana.

Alisema anachokijua ni kuumwa kwa Dk. Balali na yupo nchini Marekani akipatiwa matatibu ya maradhi yake na si kujiuzulu wadhifa wake kama ilivyoripotiwa kwenye magazeti kadhaa ya hapa nchini."Mimi sijapata barua ya Balali kujiuzulu na kama amefanya hivyo, anapaswa kuandika barua na mara tutakapoipata tutaueleza umma kuhusiana na uamuzi huo," alisema Meghji.Kujiuzulu kwa Dk. Balali bado ni kitendawili kikubwa kutokana na kauli ya Waziri Meghji pamoja na ile iliyotolewa na Rais Kikwete majuzi wakati alipozungumza na wahariri kuwa, anachofahamu ni kuwa gavana huyo yupo katika matibabu.

Hata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alipoulizwa juzi, naye alishindwa kukubali au kukanusha iwapo Dk. Balali ameandika barua hiyo ya kujiuzulu.

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, Dk. Balali yupo nchini Marekani, inakoelezwa kuwa amelazwa katika hospitali moja baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Huku nyuma, ameacha wingu zito la tuhuma dhidi yake na taasisi anayoiongoza, kutokana na matumizi yenye kutia shaka ya fedha, hasa zile zilizotumika katika malipo kwa kampuni kadhaa na ujenzi wa majengo mapya ya BoT.
source:Tanzaia Daima.
 
Govt mum on fate of BoT chief

By The Citizen reporter


Uncertainty persisted yesterday on the resignation of Bank of Tanzania Governor Daudi Ballali. Mr Salva Rweyemamu, the director of communications at the State House, still maintained that no official communication had reached the president regarding such a move by the governor. "So far we have no official communication about this matter," he said, elaborating that information about his resignation was only seen in some sections of the media. "That's what I can say," he told The Citizen yesterday.

Finance Minister Zakia Meghji also divulged no new ground on the issue, saying she wasn't aware the BoT governor had resigned. "I have no clue about what's going on," she said, promising yet another follow-up about the matter. Credible sources in the central bank were affirmative mid this week that the governor had resigned.

"The government was struggling to establish who leaked the information about the resignation of Mr Ballali," reliable sources indicated. Certain BoT officials were under pressure on the leakage, an official said, declining to be named.

"They (government) also want to establish the motive behind the leakage?we are terrified following the situation." Sharp divisions were being reported among top BoT officials, with some dejected that the governor "had been made a sacrificial lamb" to level off political pressures.

The group sympathetic with the outgoing governor says that huge payments at the central bank were done under orders of the government, not by the governor's discretion. "They used him when they were in deep financial straits but now having succeeded in their mission, the governor is becoming a liability. He has been made a scapegoat," a sad official snorted to The Citizen.

A less visible group comprising largely of non-sympathisers asserted that the governor had "failed to manage the central bank effectively during his tenure, paving the way for shady deals to take place within the institution." "The central bank's image has suffered during his leadership, with ghost projects mushrooming dramatically. He has made himself a sacrificial lamb," one of them disparagingly remarked.

Mr Ballali's resignation including details that a letter was received at the State House late Tuesday this week to that effect was top rumour in downtown Dar es Salaam. Other affirmative reports say his medical condition wasn't improving, after he was hospitalized in Boston, Massachusetts in a medical trip that has taken the better part of three months.

During a meeting with editors of print and audiovisual media, President Kikwete brushed aside suggestions that the governor had apparently found the controversy on the central bank unbearable, switching to the United States for a while.

The president affirmed that he was only aware of the governor's medical condition, and that it wasn't improving quickly enough. Some reports even suggested his health situation had declined in a 'dramatic' way.

The governor has been under pressure from opposition MPs led by Dr Wilibrod Slaa, the Chadema secretary general, whose entire political programme is focused on verifying payments at the central bank.

The bill for constructing the central bank twin towers, several times higher than putting up a similar building in New York, has used up countless hours in Parliament as far back as mid 2005 Budget session. Equally engaging is the situation in the external payments accounts, where the government pays arrears on the country's foreign debt.

With the twin towers bill put at around $400 million and EPAs payments chalking up twice as much according to internet documents, explaining all this has been a problem for the governor during the past half year.
 
Maswali zaidi yamkabili Balali, serikali kuhusu BoT

Na Waandishi Wetu


UVUMI kuhusu kujiuzulu kwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT)Daudi Ballali kunazidisha maswali kufuatia pia kutokuwepo taarifa za wazi kutoka Ikulu ambako ndipo kwa mujibu wa taratibu alipo muajiri wa gavana huyo.

Taarifa za Ikulu zilizotolewa kwenye vyombo vya habari juzi zilieleza kutokuwepo na ukweli au uongo kuhusu Balali kuandika barua ya kuomba kujiuzulu. Taarifa hiyo ilieleza pia kuwa, Rais ambaye ndiye mwenye mamlaka kuhusu kukubali au kukataa kujiuzulu kwa Balali hakuwepo kufuatia kuwa likizo ya mwisho wa mwaka.

Taarifa kuhusu Balali kukimbia nchi kwenda nchini Marekani ambazo zilitolewa na viongozi wa upinzani, ambao kwa kipindi kirefu zaidi cha mwaka huu 2007 unaelekea ukingoni, walikuwa wakimtuhumu kutokana na matumizi mabaya ya fedha katika chombo hicho muhimu katika kudhibiti na kukuza uchumi wa nchi.

Mara kadhaa Balali amekuwa akikanusha tuhuma dhidi yake huku akifafanua kuwa, wanaomtuhumu wanafanya hivyo kutokana na wivu ama kufuatia kukosa baadhi ya mambo waliyotaka awafanyie bila kufuata taratibu.

Hata hivyo taarifa za ugonjwa wa Balali zinathibitisha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Grey Mgonja na Waziri wake Zakhia Meghji Septemba 09, 2007 ikiwa ni kauli ya kwanza kabisa kutolewa na uongozi wa serikali kuhusu afya ya Balali. Taarifa zilizofuata baada ya wiki moja zilieleza pia kuwa, Gavana Balali alikuwa anaendelea vema, licha ya kwamba hazikueleza kuwa anasumbuliwa na nini.

Swali gumu linalowaumiza wachambuzi wa mambo ni kuhusu kuwepo tetesi juu ya matumizi ya fedha za BoT zinazohusishwa na kuchangia gharama za uchaguzi kwa chama tawala. Kama jibu la aina hiyo litakuwa la kweli, ni vigumu kwa Balali kuwekwa kitanzi wakati alikuwa akifanya kazi kwa maslahi ya dola.

Taarifa hizo mara kadhaa zimepingwa na uongozi wa CCM ambao umekuwa ukielezea kuwa, una mtaji mkubwa wa wanachama wenye uwezo mbalimbali hivyo hauwezi kutumia njia za panya kusaka fedha za kampeni.

Jambo la wazi ni kuwa, Balali ni mgonjwa lakini swali lingine ni hili la kuhusu uwepo wa Jakaya Kikwete nchini Marekani wiki iliyopita, safari ambayo anaelezwa kuwa alimtembelea Balali kumjulia hali.

Baada ya Kikwete kufika nchini siku mbili baadaye, ndipo kunaanza kuwepo uvumi wa Balali kuandika barua ya kujiuzulu huku akipinga kauli yake aliyowahi kuitoa Julai 12, 2007 alipowaambia waandishi wa habari kuwa hajiuzulu ng'o, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na wapinzani.

Lakini swali lingine ni lile la kupewa wasaidizi wengi tofauti na ilivyotarajiwa kwamba Rais Kikwete angempumzisha kazi. Julai 11, 2007 kulipatikana taarifa kutoka Ikulu ikieleza kuwa Rais Kikwete ameteua Manaibu Gavana watatu ambao aliwapanga kuwa chini ya Balali.

Taarifa hii ilielezwa kama njia ya kuanza mkakati wa kumuondoa Balali lakini Ikulu ikafafanua kuwa, malengo ya rais yalikuwa kuifanya BoT kufanya kazi vema zaidi.

Manaibu Gavana walioteuliwa ni; Profesa Benno Ndullu, Lila Mkila na Juma Reli. Lakini jambo lililojionyesha wakati huo baada ya uteuzi ni hili la Balali kwenda matibabu ambayo yupo hata sasa.

Lakini jambo jinginr ni kama Rais Kikwete atapokea kujiuzulu kwa Balali huku ikitangazwa kuwa wiki ijayo ripoti ya ukaguzi wa BoT itakuwa inawekwa hadharani. Ni wazi kama Balali atahusishwa moja kwa moja na tuhuma zinazomkabili ama zile zilizoko chini yake kama Gavana atatakiwa kuwajibishwa.

Pia inawezekana Ikulu ikawa tayari na taarifa kuhusu ripoti hiyo ya ukaguzi na hivyo safari ya Kikwete Marekani ikaambatana na kumtaka Balali kujiuzulu ili kupoza mambo. Bado kuna ugumu maana ripoti hiyo inayotangazwa kutoka wiki ijayo, inaelezwa pia kuwa imekuwa ikijadiliwa kimya kimya na taasisi mbalimbali za serikali hali inayotoa maswali kuhusu usafi wake na kama itabakia ile ile iliyoandaliwa na kampuni la kigeni la Ernst&Young.

Baadhi ya tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa Balali na BoT ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Benki Kuu (Twin towers) kwa gharama kubwa.

Baadhi ya wabunge walitaka maelezo ya kina kuhusu sababu za matumizi ya dola za Marekani 340 milioni sawa na Sh425 bilioni kujenga jengo hilo, wakati lingeweza kujengwa kwa gharama ndogo zaidi.

Tathmini ya wataalam wa ujenzi zinasema kuwa gharama za ujenzi huo ni zaidi ya mara mbili ya gharama za kujenga jengo la aina hiyo katika miji maarufu ya nchi zilizoendelea kama London, New York au Tokyo.

Pia zipo tuhuma kuhusu uidhinishaji wa malipo ya dola za Marekani milioni 200 sawa na Sh250 bilioni, kwa ajili ya miradi isiyoeleweka na kuidhinisha ada kubwa za mawakili wa kutetea kesi za Benki Kuu.

Tuhuma zingine ni kuidhinisha malipo hewa ya madeni ya nje (EPA) na matumizi ya kampuni ya Deep Green Finance ya Afrika Kusini.


MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU TAARIFA ZA BoT

Desemba 20: Inaripotiwa kuwa Gavana Balali ameandika barua ya kujiuzulu akiwa nje ya nchi, Ikulu na Wizara ya Fedha zinasema kuwa hazina taarifa.

Desemba 19: Meghji anatetea kuchelewa kwa ripoti ya BOT.

Desemba 01: Dk Wilbrod Slaa anaelezea kukerwa na usiri wa Ripoti ya ukaguzi wa hesabu za BoT.

Novemba 29: ukaguzi wa hesabu za BoT unakamilika na inaelezwa ripoti hiyo kufika kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali.

Septemba 22: wafadhili wanadai ufafanuzi wa tuhuma za ufisadi zinazoihusu BoT.

Septemba 20: Hali ya Gavana Balali inaripotiwa kuendelea vizuri.

Septemba 16: Wananchi wataka msimamo wa tuhuma za BoT na nyinginezo kutoka kwa Rais Kikwete.

Sept 15: Dk Slaa wanahutubia mkutano wa hadhara Mwembe Yanga Temeke, kisha anataja orodha ya waliowaita mafisani wanaotafuna nchi, akimjumuisha na Balali.

Septemba 14: Afya ya Gavana Balali inagubikwa na utata, lakini inaelezwa kuwa yuko nje nchi kwa matibabu.

Septemba 11: Kampuni ya Ernst&Young iliyoteuliwa kupitia hesabu za BOT katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ili kubaini ukweli kuhusu ubadhirifu wa fedha, inaanza kazi.

Septemba 09: Inaripotiwa kuwa hali ya Gavana si nzuri, hivyo amepelekwa nje ya nchi kwa uchunguzi na matibabu.

Agosti 19: CHADEMA inajibu mapigo ya Spika dhidi ya Slaa na hoja ya BoT.

Agosti 18: Spika anamtuhumu Dk Slaa kuwa ameghushi nyaraka alizotaka kuzitumia dhidi ya BoT na kutishia kumshitaki.

Agosti 16: Slaa anachomoa hoja binafsi ya BoT Bungeni akidai kuwa inaonekana hakuna nia njema, hasa baada ya mbunge mwenzake Zitto Kabwe kusimamishwa baada ya kuwasilisha hoja yake iliyokataliwa na wabunge wa CCM. Anaahidi kuipeleka kwa wananchi na kwa wafadhili, lakini pia anadai kutishiwa maisha.

Agosti 12: Muda wa Balali kustaafu uliainishwa kupitia vyombo vya habari, muda huo uliainishwa kuwa ni Juni mwaka 2008.
Julai 13: Gavana Balali anakataa hoja iliyoelekezwa kwake na wapinzani waliomtaka kujiuzulu kwa manufaa ya umma. Yeye anasema hajiuzulu kamwe.

Julai 12: Balali anapunguziwa mzigo na alipewa manaibu watatu kumsaidia.

29 Juni: Serikali kupitia kwa Waziri wake wa Madini na Nishati inamsafisha mke wa Gavana Daudi Balali aitwaye Ana Muganda kuhusu tuhuma ya yeye kutumia nafasi ya mumewe na kisha kuwa mkurugenzi katika moja ya makampuni ya madini ya dhahabu hapa nchini.

27 Juni: IMF inatoa taarifa kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wake Murilo Portugal akitaka uwazi uwepo katika suala la kuichunguza BoT.

Juni 26: Mjadala unatanuka kuhusu tuhuma za ufujaji fedha BoT na safari hii mbunge wa CCM Ole Sendeka anataka iundwe tume ya kuichunguza BoT.

Juni 25: Mbunge wa Karatu Dk Wilbrod Slaa anatoa dai Bungeni akitaka Gavana wa Benki Kuu David Balali ajiuzulu.

Juni 15 Bunge la Bajeti linakaa na Bajeti ya mwaka 2007/08 inasomwa na Waziri wa Fedha Zakhia Meghji.

Source: Mwananchi Jumapili
 
Haya na hii VP? mbona wanauma uma maneno?


WAKATI UTATA WAGUBIKA KUJIZULU KWAKE
Gavana Ballali harudi

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

WAKATI taarifa za kujiuzulu na hali ya afya ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinazidi kutatanisha, imefahamika kwamba Gavana huyo, Dk.Daudi Ballali, hatorejea nchini.

Imeelezwa kwamba Gavana Ballali ameshauriwa kuendelea kupata matibabu huko Boston, Marekani hadi hapo hali yake ya afya itakapotengemaa kabisa ili kuepuka ‘mazonge' akiwa nchini Tanzania.

Tayari, Ofisi ya Rais, kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu, imekwisha kusema kwamba haina taarifa ‘rasmi' kuhusu kujiuzulu kwa Dk. Ballali na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji naye amesema hana taarifa.

Hali ya Ballali bado ni ya kutatanisha baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa na Rais Jakaya Kikwete, amethibitisha kufahamu kwake kuhusu ugonjwa wa Dk. Ballali alipozungumza na waandishi wa habari Ikulu, Jumatano wiki hii.

Habari kutoka BoT, zinaeleza kwamba kabla hata ya taarifa za kujiuzulu kwake, Dk. Ballali aliondoka nchini akijua kwamba hatarejea tena nchini hasa baada ya serikali kuteua Manaibu Gavana wawili, Juma Reli aliyekuwapo na Prof. Benno Ndulu.

"Alipondoka sisi wote hapa BoT tulijua kwamba hatorudi tena nchini kwani, mbali ya maofisa wa serikali, hata jamaa zake walimshauri asirudi tena nchini kutokana na jina lake kuchafuliwa mno na vyombo vya habari," alisema ofisa mmoja mwandamizi wa BoT.

Ofisa huyo alisema baada ya kufanya kazi ndani na nje ya nchi kwa miaka mingi na kujijengea heshima kubwa, watu walio karibu na Gavana Ballali, walimshauri aende kupumzika na kuangalia zaidi afya yake nje ya nchi na zaidi Marekani ambako tayari alikwishakupazoea.

"Hivi unadhani hata kama ni wewe, watu wengi wamehusika na ulaji wa BoT, halafu wewe ndiye unabebeshwa lawama na kuharibiwa jina kwa hiyo kwa kuwa ni mgonjwa ni bora akapumzike na kupata matibabu akiwa na familia yake bila kupata bughudha," anasema ofisa huyo wa BoT.

Hata hivyo, Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, ameliambia KULIKONI kwa simu jana kwamba suala la Ballali kutorejea alikwishalizungumzia Juni 15, 2007 na hivyo haoni ajabu kusikia Gavana amejiuzulu akiwa nje ya nchi.

Hata hivyo, Dk. Slaa anasema kama kweli serikali inaendeshwa kwa haki, Ballali anastahili kurejea ama kurejeshwa nchini na kujibu tuhuma ama kushitakiwa.

"Kama kuna watuhumiwa na washitakiwa wanaolazwa pale Muhimbili (Hospitali ya Taifa ya Muhimbili) wakiwa na pingu mikononi na miguuni, kwanini hawa wakubwa nao wasifungwe pingu hata kama wanaumwa? Hatuwezi kuwa na huruma kwa wakubwa na kuwahukumu wadogo," alisema Dk. Slaa.

Alisema Ballali anashauriwa asirejee nchini kwa kuwa mbali ya yeye binafsi kuhusika na tuhuma mbalimbali, wako watu wazito ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaohusika na ufisadi ndani ya BoT na hivyo kurejea kwake nchini kunaweza kuibua mambo mengi zaidi.

"Mbali ya hayo, kuna kosa la jinai ambalo Ballali amelifanya kwa kughushi taarifa aliyoiwasilisha kwa Waziri wa Fedha, , taarifa ambayo ilikabidhiwa kwa wabunge, sasa hilo ni kosa la mtu kufungwa kwanini aachwe huko nje?" alihoji Dk. Slaa.


Habari za awali zilizoifikia KULIKONI juzi zilieleza kwamba Gavana Ballali ameomba kujiuzulu rasmi wadhifa wake, kupitia barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Kikwete Jumatano wiki hii akitoa sababu za matatizo ya kiafya kuwa ndio zimemfanya achukue hatua hiyo.

Ballali ambaye amekuwa Gavana wa Benki Kuu kwa miaka saba sasa amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali moja mjini Boston, huko Marekani kwa takriban miezi mitatu iliyopita, lakini kabla ya kuanza tiba alikuwa nchini akipambana na shutuma nzito za ufisadi dhidi yake na taasisi ya umma anayoongoza.

"Gavana ametaja sababu za matatizo ya kiafya kufuatia operesheni ya upasuaji aliyofanyiwa kuwa ndio sababu kuu ya kujiuzulu kwake," chanza cha habari serikalini kimesema.


Chanzo hicho kiliongeza: "Tunatarajia Rais atakubali kujiuzulu kwake kwa kuwa tunatambua shutuma za ufisadi zilizokuwa zinamkabili pia."

Vyanzo vya uhakika vinasema, Dk. Ballali alikutana na Rais Kikwete wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani hivi karibuni ambapo alisisitiza nia yake ya kujiuzulu. Pia watendaji waandamizi wa serikali wamefanya mazungumzo ya siri na Dk. Ballali nchini Marekani.

Inafahamika pia kwamba Dk. Ballali, ambaye amekuwa nje ya nchi kabla ya mchakato wa kuchunguza ufisadi ndani ya Benki Kuu haujaanza rasmi, atakuwa anakamilisha tu hatua ambayo ilitarajiwa kwani isingekuwa rahisi kwake kujisafisha dhidi ya shutuma nzito zilizokuwa zinamkabili.

Serikali nayo kwa upande mwingine imekuwa ikishinikizwa sana na wafadhili na wahisani wa nje ili kuchukua hatua dhidi ya tuhuma za ufisadi ndani ya Benki Kuu na sehemu nyingine za sekta mbalimbali.

Baadhi ya wafadhili wakubwa wa serikali wamefikia hatua ya kutishia kuchelewesha utekelezaji wa ahadi zao za misaada kwa Tanzania wakitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya mafisadi.

Kwa miezi kadhaa sasa, Ballali amekuwa akikataa kujiuzulu wadhifa wake licha ya kutakiwa kufanya hivyo na raia kadhaa wakiwemo pia wabunge.


Katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya Benki Kuu Julai mwaka huu, Ballali alisema hawezi kujiuzulu na kwamba tuhuma dhidi yake ni za "uzushi na uongo mtupu."

Tuhuma mojawapo inayomkabili, Dk. Ballali ni ujenzi wa jengo jipya la Benku Kuu - BoT Twin Tower – kwa gharama kubwa kuliko gharama halisi.

Dk. Ballali anatuhumiwa pia kwa kuidhinisha malipo ya dola za Marekani milioni 200 (takriban bilioni 250/-) kwa ajili ‘miradi isiyoeleweka' na kuidhinisha ada kubwa za mawakili wa kutetea kesi za Benki Kuu.


Kujiuzulu kwa Gavana Ballali bado kutaacha tatizo kuhusu gharama za jengo jipya ‘BoT Twin Tower' zinazokadiriwa kufikia dola milioni 340 (takriban bilioni 425/-). Tathmini ya wataalamu wa ujenzi zinasema gharama hizo ni mara mbili ya gharama za kujenga jengo la aina hiyo katika miji maarufu ya nchi zilizoendelea kama London, New York au Tokyo.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekuwa inachunguza tuhuma hizi pamoja na malipo ya mamilioni ya dola kwa kampuni mfu za Meremeta Gold Mine Company Limited, Tangold, Mwananchi Gold Company, Alex Stewart Asseyors na kadhalika.

Wakati Dk. Ballali anataka kujiuzulu Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utuoh, anatarajia kuwasilisha serikalini taarifa rasmi kuhusu ukaguzi aliofanya ndani ya Benki Kuu hususan katika kijengo cha malipo ya madeni ya nje, kinachoshutumiwa zaidi kwa ufisadi.

Source: Kulikoni, Jumamosi Desemba 11, 2007.

N.B.
Kama kuna makosa ya uchapaji ni ya kwangu kwani nimechukua muda mrefu kuchapa hii habari kwani haipo katika web
 
Back
Top Bottom