Huwezi kuficha siri ya wizi! Any plot that is against national interest does not qualify to be a national secret. Hao usalama waulizwe, kwa nini mkataba wa Buzwagi, Richmond nk nayo ilikuwa siri lakini tulipoitoa hawajatukamata? Kwani nyaraka za BOT alizoanza kuanika Dr Slaa nyingine si siri, mbona usalama wa taifa hawamkamati hususani kwa kuwa na ripoti yao ya usalama wa taifa waliyompelekea Lowassa ambayo imeandikwa SIRI kwa herufi kubwa? Siri inaweza kuwa kati ya wezi na wezi, lakini hakuwezi kuwa na siri kati ya wezi na wenye mali! Binafsi sijaipata hiyo ripoti, ila nimepata shauku zaidi ya kuitafuta.
Nami nawatakia wote Noeli na Mwaka mpya wenye upendo, furaha, jitihada na mafanikio.
JJ