Gavana Balali Ajiuzulu!

Gavana Balali Ajiuzulu!

Very interesting indeed; serikali hii inafikiri inaweza kuendelea kuwa ya kisiri katika kila jambo. Hili jambo haliwezekani katika ulimwengu wa leo.
 
Tatizo ni kuwa barua hii ilikuwa imetumwa Ikulu; sasa mjanja mmoja akaamua kuilikisha kwa waandishi kabla haijafika Ikulu/haijatangazwa rasmi.

Haya mambo ni kawaida sana kwa Tanzania, ndio maana pia Rais anaweza kumsataafisha mtu kazi bila ya hata wao kutopokea barua ya maelezo in the first place, let alone hao mabosi wao wa kutojua what is happening. Waacheni waandishe wapeleke habari, maana they learned from the best!

Na binafsi kitu kimoja kinachoweza kutokea na msishangae ni kuwa Rais akiamua kukataa kujiuzulu kwa Balali kuwakomoa wale waliolikisha barua hii.

Sijui kama ni kukomoa, but niko nawe katika kutokubali kujiuzulu kwa huyu Mzee wa Kashfa! Sitashangaa, kabisa...matter of fact, I almost see it coming.

Hata hivyo kuna jambo jingine hapa kuhusu mama Meghji, Balali hayuko chini ya Meghji (at least not directly) ndiyo maana barua imeelekezwa kwa Rais na ni jukumu la Ikulu kuvitangazia vyombo vyake kuwa Balali amejiuzulu.

Bongo bwana, hata kama hayuko chini yake directly, Benki kuu si iko Chini ya Wizara ya Fedha, one way or the other Mama Meghji alitakiwa awe na taarifa hii kwa sasa...ndio maana naamini kabisa Mama Zakia hajaona hiyo barua! Na yeye kusema hana taarifa hizo, sidhani kama amekosea.
 
Panatisha! sasa hivi naamini kabisa kuwa mtu aliyepewa barua hiyo kuipeleka Ikulu alikuwa na hakika kuwa imefika ndipo ikasambazwa kwa vyombo vya habari. La msingi ni kuuliza nani aliipata barua hiyo kule Ikulu na ni lini alimwambia Rais kuwa Balali ameomba kujiuzulu. Yawezekana kabisa kuwa wakati Rais anazungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano Barua ilikuwa tayari imeshafika Ikulu lakini kutokana na uzembe wa mtu fulani, Rais hakuambiwa hadi pale aliposikia kwenye maswali ya waandishi. Kama hilo ni kweli (and I have no reason to believe otherwise), kuna mtu anatakiwa atimuliwe kazi!!
 
Yaani hii nchi inaendeshwa kidizaini dizaini utadhani ka kampuni ka mtu binafsi na si major corporation....where is the professionalism?
 
Tatizo ni kuwa barua hii ilikuwa imetumwa Ikulu; sasa mjanja mmoja akaamua kuilikisha kwa waandishi kabla haijafika Ikulu/haijatangazwa rasmi. Na binafsi kitu kimoja kinachoweza kutokea na msishangae ni kuwa Rais akiamua kukataa kujiuzulu kwa Balali kuwakomoa wale waliolikisha barua hii. Hata hivyo kuna jambo jingine hapa kuhusu mama Meghji, Balali hayuko chini ya Meghji (at least not directly) ndiyo maana barua imeelekezwa kwa Rais na ni jukumu la Ikulu kuvitangazia vyombo vyake kuwa Balali amejiuzulu.

Atafanya hivyo iff bomu la Ernst & Young linabebeka for sometime kabla halijalipuka, lakini vinginevyo lazima akubaliane na hiyo barua hata kama imevuja. Kuhusu Mama Meghji kuwa in dark wala sishangai kwa kuwa barua ya resignation ya Gavana siyo lazima ipitie kwake. Gavana huteliuliwa na Rais na hata barua ya uteuzi hutoka Ikulu na siyo Hazina, kwa hiyo hata resignation letter inapelekwa Ikulu.
 
Tatizo ni kuwa barua hii ilikuwa imetumwa Ikulu; sasa mjanja mmoja akaamua kuilikisha kwa waandishi kabla haijafika Ikulu/haijatangazwa rasmi. Na binafsi kitu kimoja kinachoweza kutokea na msishangae ni kuwa Rais akiamua kukataa kujiuzulu kwa Balali kuwakomoa wale waliolikisha barua hii. Hata hivyo kuna jambo jingine hapa kuhusu mama Meghji, Balali hayuko chini ya Meghji (at least not directly) ndiyo maana barua imeelekezwa kwa Rais na ni jukumu la Ikulu kuvitangazia vyombo vyake kuwa Balali amejiuzulu.

Mkjj,

Usisahau kuwa Kikwete anakopi vitu vingi toka kwa hero ana ido wake Joji Kichaka. Huu usanii wote ni kama wa Joji Kichaka na serikali yake. Hiyo barua wote Kikwete na Meghji wanaijua ili wanafanya ya Gonzales kuwa hawana rekoleksheni yake.

Usanii kila mahali mpaka kwenye mambo muhimu ya Taifa.

Hapa ndipo naipendea JF, mambo ya siri kabisa hata ndani ya ikulu yanamwagwa hapa hadharani. Kikwete jiandae kukimbia nchi maana hao wasaidizi wako wote hawakupendi.....mweh
 
Professionalism itatoka wapi wakati watu walio kwenye system walishachoka? Hivi mnadhani watu wanao ona ufisadi mkubwa kiasi hicho wakati wao wanaishi kwa kutegemea mshahara wa mwisho wa mwezi ambao hautoshi pia, kwanini wasifurahie kuvujisha nyeti kama hizo? Kosa liko kwa mtu aliyepokea barua, maana barua zote huwa zinafikia getini na baada ya hapo zinapelekwa kunako husika. May be wazee wa pale getini wamechoka kazi na hivyo wanahitaji kupumzika. Ngoja tusubiri mwisho wa hili saga rhumba ili tuone nini kitatokea. Dalili za kwamba watu tutapewa zawadi ya kiporo cha X-Mas ninaiona iko wazi zaidi. JK atakubali kujiuzulu kwa mshikaji baada ya sikukuu ya X-Mas kupita!
 
Yaani hii nchi inaendeshwa kidizaini dizaini utadhani ka kampuni ka mtu binafsi na si major corporation....where is the professionalism?

Wapinzani nao ni kama hii Camera na huo ukuta:

2043-fail-camera.jpg
 
Ktk chokonoa yangu ambayo ni "amateur" Balali hayupo kwenye city of champions(Boston)...........kapotelea NYC au DC.

Kuna kinda moja la "ki-ccm" nitakuwa nalo kesho, lazima litakuwa na insides za whereabouts ya huyu bingwa!!.
 
Hivi huyu mwenzetu Balali anasafirigi na letter heads? Au hii barua iliandikwa Tanzania, akapelekewa kui-sign na baadae kui-fedex back to TZ? Si mchezo!
 
Kisura.. mwenzio alitembelea na RO na Rais mwenyewe... na kwa vile alikuwa bado ni gavana kwa sababu sikusikia kama amekaimiwa basi bila ya shaka alikuwa anapata taarifa taka ndani.
 
Kisura.. mwenzio alitembelea na RO na Rais mwenyewe... na kwa vile alikuwa bado ni gavana kwa sababu sikusikia kama amekaimiwa basi bila ya shaka alikuwa anapata taarifa taka ndani.

I love this country man!

Ama kweli aliyekuja na notion ya "Bongoland" ana-deserve kuwekwa kwenye kitabu cha ma-genius wa dunia hii!
 
hivi kwa utaalamu uliopo huyu mkuu hawezi kutembea
na "template" ya barua official za benki kuu kwenye
laptop yake? kama hilo lawezekana kulikuwa hakuna haja
ya huyu mkuu kutembea na headed paper ya bot.
 
Yeah...nadhani wanatumia template ila labda inabadilishwa kidogo kuendena na situation...halafu yeye anatia sahihi tu
 
hapa ni kumkoma nyani mchana kweupeeee... and we dare to talk openly!!

Heshima mbele wakuu, mzee mwenzangu MMJ heshima mkuu yaani hii barua ndio hasa kumkoma nyani mpaka Giladi kupitia milima ya Golani, mambo ya maisha yamenizidi kidogo lakini ninaona kwa mbali vitu vizito hapa JF, lakini niko njiani kurudi, tena na vitu vya moto sana, tena hatimaye nimeipata fresh habari ya Mama Mongella, yaliyojiri mpaka Msekwa kuchaguliwa, yaliyojiri mpaka air uchumi kutemwa umakamu, yaliyojiri na kifo cha Mbatia, na mengineyo.....!

Stay Tuned, I will be right back soon, mambo yote hadharani hapa JF! Ninarudi karibuni sana...!
 
Wakuu nakuombeni pia msome ombi langu nililokuwekeeni kwenye Forum ya "Hoja Mchanganyiko" au Miscellaneous. Asanteni.
 
GAZETI MAJIRA

::Habari za Tanzania Jumamosi Des 22, 2007

•
Sina taarifa ya Balali kujiuzulu-Meghji

Habari Zinazoshabihiana
• Gavana Daudi Balali ajiuzulu 21.12.2007 [Soma]
• Balali: Kushuka thamani ya shilingi hakutaathiri uchumi 27.10.2006 [Soma]
• Na Rehema Mohamed

WIZARA ya Fedha imesema haina taarifa rasmi za kujiuzulu kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Daudi Balali.

Jana baadhi ya magazeti yalinukuu barua ya Bw. Balali kwa Rais Jakaya Kikwete, akiomba kujiuzulu wadhifa huo akiwa Boston, Marekani alikolazwa kwa miezi mitatu sasa baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Akizungumza jana baada ya kuzindua Bodi ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Waziri wa Fedha, Bibi Zakia Meghji, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hana taarifa hizo ila alizisoma magazetini.

Waziri Meghji alisema mpaka sasa hajapokea barua yoyote ya kujiuzulu kutoka kwa Gavana Balali.

"Mimi Waziri wa Fedha sina taarifa hiyo, kwa kawaida katika ofisi yetu na hata nyingine, mtu akitaka kuchukua hatua hiyo kuna utaratibu wa kuandikiana barua.

"Mimi ofisini kwangu sikuletewa na sina barua hiyo, subirini ripoti ya Mkurugenzi wiki ijayo," alisema Bibi Meghji.

Kuhusu kubadilishwa kwa Gavana huyo kutokana na matatizo yake ya kiafya, Bibi Meghji alisema Wizara yake haijazungumzia juu ya suala hilo.

Akijibu swali kuhusu ugonjwa na tuhuma zake ndani ya BoT, alisema hana uhakika na hilo, ila anachojua anaumwa na yuko Marekani kwa matibabu.

Magazeti ya jana yalieleza kwamba kujiuzulu kwa Gavana Balali kumekuja huku ripoti ya tuhuma za ufisadi ndani ya BoT ikiwa imeshakabidhiwa kwa Rais Kikwete na inapitiwa.

Uchunguzi huo uliagizwa na Serikali ili kubaini kama kulikuwa na ubadhirifu ndani ya BoT hususan kuhusu ujenzi wa majengo mawili 'twin tower 'ya benki hiyo.

Ulifanywa kupitia kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo kampuni binafsi ya Uingereza ya Ernst & Young, iliufanya na kuwasilisha ripoti yake kwa Rais.

Uchunguzi huo ulitokana na shinikizo kutoka kambi ya upinzani kupitia Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa, baada ya kutangaza ilichokiita orodha ya mafisadi, huku akimtaja Bw. Balali kuhusika na ubadhirifu ndani ya BoT.

Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
 
Hapa kuna harufu ya samaki aliyeoza; watu hatupati hewa safi.
 
Barua ilifika Ikulu tangu Jumatano, wao walikuwa wamekusudia kumsimamisha kazi ambako kungeendana na kutolewa ripoti ya BoT, mwenzao kawawahi.. now its their move! Miye niko hapa napiga mluzi tu.. !
 
Barua ilifika Ikulu tangu Jumatano, wao walikuwa wamekusudia kumsimamisha kazi ambako kungeendana na kutolewa ripoti ya BoT, mwenzao kawawahi.. now its their move! Miye niko hapa napiga mluzi tu.. !

Hatua kali ya kinidhamu imeota mbawa, sasa sijui watasema wanamfungulia mashitaka? Maana kumsimamisha kazi ingeonyesha kwamba kuna hatua imechukuliwa, lakini kujiuzulu tena kwa ridhaa yake mwenyewe hapo amewapiga 2 - 0!

Nimekubali Ballali ni mtaalam wa game, na amefanya the right move ili kulinda heshima yake na ndiyo maana Ikulu na Hazina wanajikanyaga, hawajui waseme nini. JK alitutamkia kwamba once report ikitoka yeyote atakayehusika na utafunaji na ma-dollar ya wafadhili atachukuliwa hatua za kinidhamu bila kujali wadhifa wake. Ngoja tusubiri hatua ya kinidhamu itakayochukuliwa just in case Ernst & Young watakuwa wamem-implicate Ballali!

Kama MMJ yuko right, basi barua hiyo ilivujishwa kwa makusudi ili habari itoke mapema kabla serikali haijajua ijibu nini. Kama hii barua isingevuja basi serikali ingekaa kimya na baadaye kuamua kutangaza kwamba Rais amesitisha uteuzi wa Gavana kwa maslahi ya umma ili JK ajizolee ujiko kwamba amefanya kweli na kumbe hakuna kitu! Msanii kakutana na msanii mwenzake na tena mtoto wa mjini!
 
Back
Top Bottom