Gavana Balali Ajiuzulu!

Gavana Balali Ajiuzulu!

Mama Lao,

Apende asipende he had no choice but to give out money to bail out serikali (CCM)! hata kama angekataa, the next guy was going to face the same dillema and had to either accept what the Government wants or surrender!

Nyinyi mwafikiri ni pesa zinazotoka kirahisi bila ruhusa ya Raisi na Waziri wa Fedha? Nope! Ukirudia mada yangu kuhusu Meremeta utaelewa ni nini kilichotokea. Kibaya zaidi ni kuwa Uchunguzi huu utaleta vurugu mechi ambayo hatutataka kuina kamwe.

When did you see Jeshi being investigated? who has balls to investigate CCM and its arms?

Mwacheni Kondoo wa Kafara atulie huko unyamwezini! The only way for the truth to come out is for CCM loosing the control of parliament in 2010!

Hiyo ripoti itakaliwa Ikulu na Rais atasema kwa Taifa hakuna ushahidi wa Wizi na Sifukuzi Mawaziri!

But collectivelly, we can make the thruth even partial to come out 2011 if we vote more seats to opposition in the parliament!

Kweli kabisa Rev hata mimi nakubaliana nawe kwa kiasi fulani kuwa Balali ni kafara hapa. Pesa zilizatikiwa kutoka ili zilipie uchaguzi wa ccm na kuwanunua wanajeshi wazidi kuwa watiifu.

Pesa nyingine zimetoka kumlipa mwizi na mkoloni Rostam Aziz kwa mapesa aliyogawa kwa wajumbe wa NEC wakati wa kampeni za CCM mwaka 2005. Balali hakuwa na choice lasivyo wangemrutihinda kama kipindi kipindi kile cha kesi Rutihinda+Kibona dhidi ya CCM ya Malecela.

Hata hivyo, kwanini jamaa wanataka Balali afe so bad? hili ndilo swali najiuliza. Mimi sina msahama kwa Balali, kama ni mwema angefanya alichofanya yule Githongo wa Kenya kwa kurekodi mazungumzo na baadae akimbilie huku na kuwashikia bango jamaa.

Yeye atahusishwa tu na wizi huu labda kama anataka light sentensi kwa kushirikiana na waendesha mashtaka. Hata hivyo ujenzi wa majengo ya BOT una kashfa kibao na Balali aliutetea hadharani. Kwa hili the guy naye ni mwizi na anastahili kuwa na special tanuru ya kumchoma vizuri huko jehanum siku akifa rasmi
 
Asante Mwanakijiji kwa hii barua!

This is JF, kila kitu kinapatikana kikiwa bado moto kabisaaa!
Wenye vikorosho wajinyonge but this baby will be here to win.

Kuhusu Balali, Nimesema mengi ya kutosha!

BTW. Hii barua si inaweza kupunguzwa ukubwa. Mkjj jaribu kuadjust size kidogo
ok ngoja niifanyie kazi wangu. Na wewe na huku kupotea ndio imekuwaje hadi watu wananiuliza nini kimekusibu.
 
Hivi kweli wanataka tuamini kuwa RO na Kikwete kumtembelea Balali ilikuwa ni kumjulia hali tu. Kulichosemwa sijui, ila kilichosikika ni kama hivi "uchunguzi bwana si mzuri sana, na tutaweka hadharani lakini haitakuwa nzuri tukifanya hivyo wewe ukiwa nchini. Tunakupa deal you resign and we..."
 
Bravo JF, kwa kutupakulia vya moto haswaaa,Ila bado njaa inauma ya muziki wa repoti ya BOT .. yaani huo tu!
 
ok ngoja niifanyie kazi wangu. Na wewe na huku kupotea ndio imekuwaje hadi watu wananiuliza nini kimekusibu.

Haya miye nasubiri,

Mwenzako mimi niko likizo ya krismass huku Trinidad and Tobago. Nilitaka kwenda bongo ila nilivyosikia kuwa RO (mzee wa usalama mwenyewe) anakwenda Marekani "kumjulia hali Balali" ikabidi nibadili plan zote.

Bado mwaliko wako wa kuja huku Tuesday unastand - haitakuwa sherehe ya kidini kwa hiyo usiwe na wasiwasi kuwa utalishwa nguruwe so kazi yako ya ushehe itabaki salama.
 
Kwa kuipunguza size, select it then copy it to microsoft word. There you can adjust its size.

Mambo moto haya!
 
Barua hiyo ilivyoandikwa ni dalili tosha kwamba kasukumwa. Sasa je ataamua kuondoka kama mwewe aliyeloa au atapigana kusafisha jina lake?
 
Re: KLHN/JF Exclusive: Barua ya Balali Kujiuzulu

--------------------------------------------------------------------------------



Bowbow, kwanza naona kama "UNAGUSWA" sana na hii mada, toka juzi. ila kwa taarifa ni kwamba:

Ni kwamba nafurahi sana lakini maswali ya itifaki ni muhimu kuuliza maana kama uliwahi kuhusika na maswala ya ajira au kuwa mwajiri nadhani unaweza kuona kwenye barua kuna kasoro.

Na mara nyingi barua iliyoandikwa mazingira kama hayo unaweza kuhisi kuna jambo.

Mimi bado nahisi kalazimiashwa kuresign katika mazingira haya:
1. Amejengewawa Mazingira na mafisadi wenzie kwa maslahi yao.
2. Kwa kitendo chake cha kuwa njee ya ofisi zaidi ya 3months.
3. Alijichukulia madaraka kwenda kutibiwa njee bila idhini ya wakuu wake so wamemshinikiza kuresign.
4. Kapata shinikizo kwa wananchi wanaolilia fedha zao za kodi walizoiba
5. Mengineyo
 
Ila yeye, balali kwanini akubali kubeba mzigo peke yake?? si aseme tu ukweli? wanao weza mfikia muombeni kabisa na mmrekodi ili hata kama si leo ushahidi wake wa kipi kilitokea uwepo na hawa wezi warudishie, narudia kusema waturudishie, hata kama ni karne ijayo, walau wajukuu zetu watafaidi!
 
Kinachonishangaza ni kuwa habari hizi, ukiacha magazeti ya this day na majira, hakuna mengine ambayo yamechapisha. Majira waliitoa jana, na leo nzima nimeangalia walau mtanzania, tanzania daima na mwananchi hii habari siioni zaidi ni za hotuba ya kikwete kwa waandishi wa habari.

What is this? nilidhani hii ingekuwa big news kwa vyombo vya habari...anyway mi sio mwandishi wa habari labda wana vigezo vyao vya ipi habari na ipi si habari
 
Wote wanahusika na kama Balali alilazimishwa sasa huu ndio muda wa kusema.

Pia ikumbukwe hizo pesa zilichotwa wakati JK ni waziri tu kwahiyo
kama kuna watu walihusika ni Mkapa pamoja na waziri wa fedha ambaye nafikiri alikuwa Mramba.

Balali hawezi kutumia kisingizio cha kulazimishwa, yeye ndiye alipewa majukumu ya kulinda hiyo BOT, kitu pekee anachoweza kufanya ni kujiona yuko shimoni, hakuna sababu ya kuendelea kuchimba mpaka anafunikwa. Inabidi atoke clean, vinginevyo Watanzania tutakuwa naye tu mpaka siku anaenda kaburini na wala hapo haitakuwa mwisho.

Inabidi ifike mahali tuseme haya mambo sasa basi.
 
vyombo vya habari vina tabia ya kutodandia habari kama mmoja anaijua vema inatosha kuimwaga ila kuna vyombo vingine ni fisadi tu angalia gazeti la MTANZANIA haifai isipokuwa mtu mmoja tu Manyerere anandika ukweli ila UHURU MZALENDO na hata kibaraka MAJIRA bomu tu!!!!!
 
Hii barua ya sentenso mbili tu bila kichwa cha habari, mie naona kama imeharakishwa, kama vile kuna mtu alikuwa anamsimamia aiandike harakaharaka.

Tunaodhani tunamdai hela zetu tuna kazi ngumu ya kufanya. Tukimshitaki, haohao mafisadi wenzie waliomtosa watamtetea "tooth and nail" ili asije akatoboa siri zao. Tukinyamaza ndio imetoka hiyo, hakuna atakayemchukulia hatua yoyote. Na bado hamjasikia mhe Rais atakavyojibu ni jinsi gani alivyopokea barua hiyo ya kujiuzulu kwa "moyo mzito" kwani taifa bado lilikuwa linahitaji "utumishi wake".
 
naomba ushauri kwa wanasheria njia ya kumshtaki huyu balali huko huko kwa kuzingatia itifaki za kisheria zilizoridhiwa na bunge letu ili tuone cha kufanya safari hii hili kamwe tusijisahau kabisa tuweke rekodi mbona nchi zingine zinaweza???
 
Hii barua ya sentenso mbili tu bila kichwa cha habari, mie naona kama imeharakishwa, kama vile kuna mtu alikuwa anamsimamia aiandike harakaharaka.
...........

Kithuku, you have a point there.
Hiyo barua imechapwa katika stationary yenye heading ya BOT. Ukifikiria pia kuwa Balali wakati akienda Boston kwa 'check-up' hakujua kuwa itabidi ajiuzulu katika mazingira haya, hivyo si rahisi kuwa alienda na stationary za BOT.

Kwa hiyo mtazamo mzuri ni kuwa hiyo barua ilitayarishwa na kuchapwa Dar halafu akapelekewa huko Boston na kuambiwa ai-sign, mtu akaondoka nayo au ikatumwa kurudi Bongo. Kwa kufanya hivyo inaongeza pia uwezekano wa ku-leak, which is what happened.
 
shamba wa kijijini

Tatizo watu hapa ni waoga kwenda front ni mabingwa wa kbonyesh keyboard.

lakini the only njia ya kuonyesha uzaalendo kuenda mahakamani.
 
Mimi bado nahisi kalazimiashwa kuresign katika mazingira haya:
1. Amejengewawa Mazingira na mafisadi wenzie kwa maslahi yao.
2. Kwa kitendo chake cha kuwa njee ya ofisi zaidi ya 3months.
3. Alijichukulia madaraka kwenda kutibiwa njee bila idhini ya wakuu wake so wamemshinikiza kuresign.
4. Kapata shinikizo kwa wananchi wanaolilia fedha zao za kodi walizoiba
5. Mengineyo

Sikubaliani na hoja zako kwa sababu zifuatazo:

1. Hayo mazingira ajijengea mwenyewe. Nimeona watu wanamtetea sana kwamba anatolewa kafara. Kinachomsukuma kutoka ni report ya Ernst & Young. Hapo bado tuhuma za Twin Towers hazijachunguzwa, una uhakikka gani kwamba jamaa ni msafi? Kama jamaa angekuwa msafi wala asingetoka "eti kwa sababu ya ugonjwa" wakati watu wanakutana nae mara kwa mara!

2. Kuwa nje ya nchi kwa miezi mitatu kuna husiana nini na ku-resign? Sioni uhusiano wowote maana chini yake kuna manaibu gavana watatu na wote wako ofisini. Kwa hiyo bado kazi zinaendelea kama kawaida.

3. Una uhakika gani kwamba alijichukulia madaraka ya kwenda kutibiwa nje bila idhini ya wakuu wake? Hivi unaelewa kwamba Gavana akiondoka nchini lazima Rais na Waziri wa Fedha wataarifiwe kwamba jamaa hayuko ofisini. Sasa hayo madaraka alijichukulia vipi? Kama alijichukulia madaraka basi wangem-fire baada ya wiki 2 tu kupita.

4. Shinikizo ni report iliyokuwa inasubiliwa, wala si wananchi. Kama ni kulialia kwa wananchi basi angeondoka wakati ule wa kikao cha Bunge. Mbona alipokutana na wanahabari aliwaambia yuko comfortable, hiyo comfortability imeishia wapi? Kama angekuwa anaogopa shinikizo la wananchi angeachia madaraka wakati ule ambapo kila kukicha magazeti yalikuwa na news za Ufisadi ndani ya BoT, Twin Towers, EPA na mengineyo kibao.
 
lakini the only njia ya kuonyesha uzaalendo kuenda mahakamani.

Mahakama za Tanzania? Ambazo mtuhumiwa anapitishwa kwenye mlango wa majaji na jaji mkuu hasemi lolote?

Akishitakiwa mahakama za nje naweza kuwa na imani kwamba haki itatendeka. Lakini kama ni mahakama za Bongo kuanzia Ikulu mpaka BoT wote watajipanga kumtetea mtu mmoja ili asije akamwaga siri zaidi. Siri zikitoka unaweza kushangaa mpaka JK ana mgao wake kwenye hizo pesa za EPA!
 
Back
Top Bottom