Gavana Balali Ajiuzulu!

Gavana Balali Ajiuzulu!

WanaJF tusisahau kwa kumsakama balali peke yake.Iweje balali aonekane kama ndio msaliti mkubwa? Kuna game anachezewa jamaa huyu na JK.
Mimi naona kama Balali akijiuzulu na JK aachie ngazi mara moja woote ni wezi hawa balali hakuiba peke yake.
Namtaka fashisti Jakaya Kikwete aachie ngazi amfate balali.Wezi woote hawa
 
Apende asipende he had no choice but to give out money to bail out serikali (CCM)! hata kama angekataa, the next guy was going to face the same dillema and had to either accept what the Government wants or surrender!
Nakubaliana na wewe Rev kuna game inachezwa na JK aonekane Mr Clean hapa kwa kumtoa mwanakondoo balali kafara
Nyinyi mwafikiri ni pesa zinazotoka kirahisi bila ruhusa ya Raisi na Waziri wa Fedha? Nope! Ukirudia mada yangu kuhusu Meremeta utaelewa ni nini kilichotokea. Kibaya zaidi ni kuwa Uchunguzi huu utaleta vurugu mechi ambayo hatutataka kuina kamwe
.
Lazima kuna sahihi ya JK na Meghji bwana mdogo sana balali hana ubavu wa kukataa analosema Mkubwa wake.Ikumbikwe kuwa balali anafanya kazi kitalaam na Jk kisiasa lazima migongano itokee
 
Jamani yawezekana tumeshapigwa changa la macho kama kawaida yetu wadanganyika!
 
Balali akamatwe - Slaa

na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo jana siku moja tu baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo hazijathibitika kuwa gavana huyo, ambaye yupo Marekani kwa matibabu, ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo, akitaja maradhi yanayomsumbua kama sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo.

Akizungumzia taarifa za kujiuzulu kwa Dk. Balali, Dk. Slaa kwanza alimpa pole kutokana na maradhi yanayomkabili, lakini akamtaka Rais Kikwete kuamuru kukamatwa kwa gavana huyo mara moja ili ajibu tuhuma zote zinazomkabili.

Akiandika ujumbe mrefu wa simu ya mkononi, Dk. Slaa aliorodhesha baadhi ya tuhuma ambazo Dk. Balali anatakiwa kuzijibu kuwa ni kughushi taarifa ya BoT ya 2005 aliyowasilisha kwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji Septemba 20, 2005 katika kitabu ambacho ndani yake taarifa ya fedha ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imesainiwa Juni 21, 2007.

"Isitoshe yeye mwenyewe amesaini kama Mwenyekiti wa BoT Juni 21, 2007. Balali pia amesaini balance sheet (mizania) ndani ya kitabu hicho hicho. Taarifa zinazohusika ni hizo hizo za 2005/2006 zenye migogoro. Ni dhahiri kuna kughushi.

"Meghji kakaa kimya. Kughushi au ku-back-date (kurudisha nyuma tarehe) ni kosa la jinai. Kuna kirusi gani nchini? Raia wa kawaida hata angeumwa saa hizi angekuwa analindwa na askari magereza hospitalini… hakuna mwenye kibali kuvunja sheria," alisema.

Alizitaja tuhuma nyingine kuwa ni matumizi yenye kutia shaka katika malipo ya akaunti ya nje (EPA), fedha zilizolipwa KAGODA Co bila maelezo, fedha zilizopelekwa Deep Green na zile za Tangold Ltd.Aidha, alimtaka Rais Kikwete kumchukulia hatua za kisheria na ikiwezekana kumfikisha mahakamani Balali akimtuhumu kufuja fedha za wavuja jasho, ambao kila kukicha maisha yao yanazidi kudidimia kwa sababu ya watu wachache wanaotumia rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi.

"Serikali inaogopa nini kumchukulia hatua mtu anayefuja mabilioni ili hali mjamzito anajifungulia bila huruma ofisi ya WEO kwa ajili ya kukosa sh 20,000?" alihoji Dk. Slaa. Hata hivyo, madai hayo ya Slaa yalipata kukanushwa wakati fulani na Balali wakati alipoitisha mkutano nadra na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya watu kadhaa kumhusisha na tuhuma za ubadhirifu wa BoT alizozielezea kuwa zisizo na msingi.

Wakati Slaa akitoa madai hayo, ripoti ya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha BoT uliofanywa na kampuni ya ukaguzi wa mahesanu ya Ernst & Young kwa maagizo ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), itawekwa hadharani wiki ijayo.Hayo yalithibitishwa jijini Dar es Salaam jana na Waziri Meghji, aliyewaambia waandishi wa habari kuwa ripoti hiyo ndiyo kwa kiasi kikubwa itakayoisaidia serikali kushughulikia kile kitakachoonekana kina tatizo.

Akifafanua, Meghji alisema kuwa, ushughulikiaji huo wa matatizo yatakayoainishwa katika ripoti hiyo, kutahusisha pia kuwachukulia hatua stahili, wale wote watakaobainika kufanya makosa, kulingana na taratibu za kazi na sheria za nchi.Alisema hivi sasa ni vigumu kuanza kuzungumzia suala la ubadhirifu wa fedha au kumnyooshea mtu kidole, hadi hapo ripoti hiyo itakapokamilika, hivyo ni vema kwa wakati huu jamii ikaendelea kuvuta subira.

"Тuvute subira jamani kwani ripoti itatolewa ‘next week' (wiki ijayo) na ndipo hapo tutaangalia cha kufanya kwa yale yatakayobainika na kuwachukulia hatua wale wote watakatajwa na ripoti hiyo," alisema Meghji.Serikali iliiagiza CAG kuyafanyia uchunguzi madai ya viongozi wa upinzani kuwapo kwa matumizi mabaya (ufisadi) ya fedha za wavuja jasho katika BoT.Viongozi hao wa upinzani wakiongozwa na Dk. Slaa, ndio walioibua sakata hilo bungeni na kudai kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na matumizi ya fedha yenye kutia shaka ndani ya BoT.

Awali, madai hayo ya wapinzani yalipingwa vikali na serikali, lakini baadaye, ilibainika kuwepo kwa kasoro katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na ndipo serikali ilipoiagiza ofisi ya CAG kufanya ukaguzi huo.

Meghji anatoa kauli hiyo siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuhoji sababu za serikali kuikalia ripoti hiyo kwa muda mrefu hata baada ya kazi kukamilika.Kwa upande wake, Dk. Slaa bado anaendelea kudai kuwa, ukaguzi huo umefanywa katika sehemu ndogo sana kwani ubadhirifu ndani ya BoT unahusisha vitengo vingi zaidi ya EPA.

Katika hatua nyingine, Meghji, alisema mpaka sasa ofisi yake haijapata taarifa ya kujiuzulu kwa Dk. Balali na kusema kuwa taarifa hizo alizisoma kwenye magazeti jana.

Alisema anachokijua ni kuumwa kwa Dk. Balali na yupo nchini Marekani akipatiwa matatibu ya maradhi yake na si kujiuzulu wadhifa wake kama ilivyoripotiwa kwenye magazeti kadhaa ya hapa nchini."Mimi sijapata barua ya Balali kujiuzulu na kama amefanya hivyo, anapaswa kuandika barua na mara tutakapoipata tutaueleza umma kuhusiana na uamuzi huo," alisema Meghji.Kujiuzulu kwa Dk. Balali bado ni kitendawili kikubwa kutokana na kauli ya Waziri Meghji pamoja na ile iliyotolewa na Rais Kikwete majuzi wakati alipozungumza na wahariri kuwa, anachofahamu ni kuwa gavana huyo yupo katika matibabu.

Hata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alipoulizwa juzi, naye alishindwa kukubali au kukanusha iwapo Dk. Balali ameandika barua hiyo ya kujiuzulu.

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, Dk. Balali yupo nchini Marekani, inakoelezwa kuwa amelazwa katika hospitali moja baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Huku nyuma, ameacha wingu zito la tuhuma dhidi yake na taasisi anayoiongoza, kutokana na matumizi yenye kutia shaka ya fedha, hasa zile zilizotumika katika malipo kwa kampuni kadhaa na ujenzi wa majengo mapya ya BoT.

Source: Tanzania Daima
 
Ukisoma kwa makini maneno ya Mama Meghji unagundua kwamba Mwanakijiji hakuwa mbali sana aliposema kwamba Ballali amewa-time hawa jamaa. Sasa sijui hiyo next week watakuja na lipi jipya?
 
Balali akamatwe - Slaa

na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo jana siku moja tu baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo hazijathibitika kuwa gavana huyo, ambaye yupo Marekani kwa matibabu, ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo, akitaja maradhi yanayomsumbua kama sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo.

Akizungumzia taarifa za kujiuzulu kwa Dk. Balali, Dk. Slaa kwanza alimpa pole kutokana na maradhi yanayomkabili, lakini akamtaka Rais Kikwete kuamuru kukamatwa kwa gavana huyo mara moja ili ajibu tuhuma zote zinazomkabili.

Akiandika ujumbe mrefu wa simu ya mkononi, Dk. Slaa aliorodhesha baadhi ya tuhuma ambazo Dk. Balali anatakiwa kuzijibu kuwa ni kughushi taarifa ya BoT ya 2005 aliyowasilisha kwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji Septemba 20, 2005 katika kitabu ambacho ndani yake taarifa ya fedha ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imesainiwa Juni 21, 2007.

“Isitoshe yeye mwenyewe amesaini kama Mwenyekiti wa BoT Juni 21, 2007. Balali pia amesaini balance sheet (mizania) ndani ya kitabu hicho hicho. Taarifa zinazohusika ni hizo hizo za 2005/2006 zenye migogoro. Ni dhahiri kuna kughushi.

“Meghji kakaa kimya. Kughushi au ku-back-date (kurudisha nyuma tarehe) ni kosa la jinai. Kuna kirusi gani nchini? Raia wa kawaida hata angeumwa saa hizi angekuwa analindwa na askari magereza hospitalini… hakuna mwenye kibali kuvunja sheria,” alisema.

Alizitaja tuhuma nyingine kuwa ni matumizi yenye kutia shaka katika malipo ya akaunti ya nje (EPA), fedha zilizolipwa KAGODA Co bila maelezo, fedha zilizopelekwa Deep Green na zile za Tangold Ltd.Aidha, alimtaka Rais Kikwete kumchukulia hatua za kisheria na ikiwezekana kumfikisha mahakamani Balali akimtuhumu kufuja fedha za wavuja jasho, ambao kila kukicha maisha yao yanazidi kudidimia kwa sababu ya watu wachache wanaotumia rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi.

“Serikali inaogopa nini kumchukulia hatua mtu anayefuja mabilioni ili hali mjamzito anajifungulia bila huruma ofisi ya WEO kwa ajili ya kukosa sh 20,000?” alihoji Dk. Slaa. Hata hivyo, madai hayo ya Slaa yalipata kukanushwa wakati fulani na Balali wakati alipoitisha mkutano nadra na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya watu kadhaa kumhusisha na tuhuma za ubadhirifu wa BoT alizozielezea kuwa zisizo na msingi.

Wakati Slaa akitoa madai hayo, ripoti ya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha BoT uliofanywa na kampuni ya ukaguzi wa mahesanu ya Ernst & Young kwa maagizo ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), itawekwa hadharani wiki ijayo.Hayo yalithibitishwa jijini Dar es Salaam jana na Waziri Meghji, aliyewaambia waandishi wa habari kuwa ripoti hiyo ndiyo kwa kiasi kikubwa itakayoisaidia serikali kushughulikia kile kitakachoonekana kina tatizo.

Akifafanua, Meghji alisema kuwa, ushughulikiaji huo wa matatizo yatakayoainishwa katika ripoti hiyo, kutahusisha pia kuwachukulia hatua stahili, wale wote watakaobainika kufanya makosa, kulingana na taratibu za kazi na sheria za nchi.Alisema hivi sasa ni vigumu kuanza kuzungumzia suala la ubadhirifu wa fedha au kumnyooshea mtu kidole, hadi hapo ripoti hiyo itakapokamilika, hivyo ni vema kwa wakati huu jamii ikaendelea kuvuta subira.

“Тuvute subira jamani kwani ripoti itatolewa ‘next week’ (wiki ijayo) na ndipo hapo tutaangalia cha kufanya kwa yale yatakayobainika na kuwachukulia hatua wale wote watakatajwa na ripoti hiyo,” alisema Meghji.Serikali iliiagiza CAG kuyafanyia uchunguzi madai ya viongozi wa upinzani kuwapo kwa matumizi mabaya (ufisadi) ya fedha za wavuja jasho katika BoT.Viongozi hao wa upinzani wakiongozwa na Dk. Slaa, ndio walioibua sakata hilo bungeni na kudai kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na matumizi ya fedha yenye kutia shaka ndani ya BoT.

Awali, madai hayo ya wapinzani yalipingwa vikali na serikali, lakini baadaye, ilibainika kuwepo kwa kasoro katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na ndipo serikali ilipoiagiza ofisi ya CAG kufanya ukaguzi huo.

Meghji anatoa kauli hiyo siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuhoji sababu za serikali kuikalia ripoti hiyo kwa muda mrefu hata baada ya kazi kukamilika.Kwa upande wake, Dk. Slaa bado anaendelea kudai kuwa, ukaguzi huo umefanywa katika sehemu ndogo sana kwani ubadhirifu ndani ya BoT unahusisha vitengo vingi zaidi ya EPA.

Katika hatua nyingine, Meghji, alisema mpaka sasa ofisi yake haijapata taarifa ya kujiuzulu kwa Dk. Balali na kusema kuwa taarifa hizo alizisoma kwenye magazeti jana.

Alisema anachokijua ni kuumwa kwa Dk. Balali na yupo nchini Marekani akipatiwa matatibu ya maradhi yake na si kujiuzulu wadhifa wake kama ilivyoripotiwa kwenye magazeti kadhaa ya hapa nchini.“Mimi sijapata barua ya Balali kujiuzulu na kama amefanya hivyo, anapaswa kuandika barua na mara tutakapoipata tutaueleza umma kuhusiana na uamuzi huo,” alisema Meghji.Kujiuzulu kwa Dk. Balali bado ni kitendawili kikubwa kutokana na kauli ya Waziri Meghji pamoja na ile iliyotolewa na Rais Kikwete majuzi wakati alipozungumza na wahariri kuwa, anachofahamu ni kuwa gavana huyo yupo katika matibabu.

Hata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alipoulizwa juzi, naye alishindwa kukubali au kukanusha iwapo Dk. Balali ameandika barua hiyo ya kujiuzulu.

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, Dk. Balali yupo nchini Marekani, inakoelezwa kuwa amelazwa katika hospitali moja baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Huku nyuma, ameacha wingu zito la tuhuma dhidi yake na taasisi anayoiongoza, kutokana na matumizi yenye kutia shaka ya fedha, hasa zile zilizotumika katika malipo kwa kampuni kadhaa na ujenzi wa majengo mapya ya BoT.
Mkuu tuwekee Source ya habari hii
 
Ukisoma kwa makini maneno ya Mama Meghji unagundua kwamba Mwanakijiji hakuwa mbali sana aliposema kwamba Ballali amewa-time hawa jamaa. Sasa sijui hiyo next week watakuja na lipi jipya?
Mkuu hapa jamaa wanatuchezea tu hawa mafisadi.Wamegeukana naona Jakaya anataka kujisafisha kwa kumlipua Balali,na yeye lazima ajibu tuhuma hizi Balali hayupo peke yake
 
TANZANIA DAIMA
Balali akamatwe - Slaa

na Mwandishi Wetu​

Na Salehe MohamedKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali.
Dk. Slaa ametoa kauli hiyo jana siku moja tu baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo hazijathibitika kuwa gavana huyo, ambaye yupo Marekani kwa matibabu, ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo, akitaja maradhi yanayomsumbua kama sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo.

Akizungumzia taarifa za kujiuzulu kwa Dk. Balali, Dk. Slaa kwanza alimpa pole kutokana na maradhi yanayomkabili, lakini akamtaka Rais Kikwete kuamuru kukamatwa kwa gavana huyo mara moja ili ajibu tuhuma zote zinazomkabili.

Akiandika ujumbe mrefu wa simu ya mkononi, Dk. Slaa aliorodhesha baadhi ya tuhuma ambazo Dk. Balali anatakiwa kuzijibu kuwa ni kughushi taarifa ya BoT ya 2005 aliyowasilisha kwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji Septemba 20, 2005 katika kitabu ambacho ndani yake taarifa ya fedha ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imesainiwa Juni 21, 2007.

“Isitoshe yeye mwenyewe amesaini kama Mwenyekiti wa BoT Juni 21, 2007. Balali pia amesaini balance sheet (mizania) ndani ya kitabu hicho hicho. Taarifa zinazohusika ni hizo hizo za 2005/2006 zenye migogoro. Ni dhahiri kuna kughushi.

“Meghji kakaa kimya. Kughushi au ku-back-date (kurudisha nyuma tarehe) ni kosa la jinai. Kuna kirusi gani nchini? Raia wa kawaida hata angeumwa saa hizi angekuwa analindwa na askari magereza hospitalini… hakuna mwenye kibali kuvunja sheria,” alisema.

Alizitaja tuhuma nyingine kuwa ni matumizi yenye kutia shaka katika malipo ya akaunti ya nje (EPA), fedha zilizolipwa KAGODA Co bila maelezo, fedha zilizopelekwa Deep Green na zile za Tangold Ltd.Aidha, alimtaka Rais Kikwete kumchukulia hatua za kisheria na ikiwezekana kumfikisha mahakamani Balali akimtuhumu kufuja fedha za wavuja jasho, ambao kila kukicha maisha yao yanazidi kudidimia kwa sababu ya watu wachache wanaotumia rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi.

“Serikali inaogopa nini kumchukulia hatua mtu anayefuja mabilioni ili hali mjamzito anajifungulia bila huruma ofisi ya WEO kwa ajili ya kukosa sh 20,000?” alihoji Dk. Slaa. Hata hivyo, madai hayo ya Slaa yalipata kukanushwa wakati fulani na Balali wakati alipoitisha mkutano nadra na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya watu kadhaa kumhusisha na tuhuma za ubadhirifu wa BoT alizozielezea kuwa zisizo na msingi.

Wakati Slaa akitoa madai hayo, ripoti ya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha BoT uliofanywa na kampuni ya ukaguzi wa mahesanu ya Ernst & Young kwa maagizo ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), itawekwa hadharani wiki ijayo.Hayo yalithibitishwa jijini Dar es Salaam jana na Waziri Meghji, aliyewaambia waandishi wa habari kuwa ripoti hiyo ndiyo kwa kiasi kikubwa itakayoisaidia serikali kushughulikia kile kitakachoonekana kina tatizo.

Akifafanua, Meghji alisema kuwa, ushughulikiaji huo wa matatizo yatakayoainishwa katika ripoti hiyo, kutahusisha pia kuwachukulia hatua stahili, wale wote watakaobainika kufanya makosa, kulingana na taratibu za kazi na sheria za nchi.Alisema hivi sasa ni vigumu kuanza kuzungumzia suala la ubadhirifu wa fedha au kumnyooshea mtu kidole, hadi hapo ripoti hiyo itakapokamilika, hivyo ni vema kwa wakati huu jamii ikaendelea kuvuta subira.

“Тuvute subira jamani kwani ripoti itatolewa ‘next week’ (wiki ijayo) na ndipo hapo tutaangalia cha kufanya kwa yale yatakayobainika na kuwachukulia hatua wale wote watakatajwa na ripoti hiyo,” alisema Meghji.Serikali iliiagiza CAG kuyafanyia uchunguzi madai ya viongozi wa upinzani kuwapo kwa matumizi mabaya (ufisadi) ya fedha za wavuja jasho katika BoT.Viongozi hao wa upinzani wakiongozwa na Dk. Slaa, ndio walioibua sakata hilo bungeni na kudai kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na matumizi ya fedha yenye kutia shaka ndani ya BoT.

Awali, madai hayo ya wapinzani yalipingwa vikali na serikali, lakini baadaye, ilibainika kuwepo kwa kasoro katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na ndipo serikali ilipoiagiza ofisi ya CAG kufanya ukaguzi huo.

Meghji anatoa kauli hiyo siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuhoji sababu za serikali kuikalia ripoti hiyo kwa muda mrefu hata baada ya kazi kukamilika.Kwa upande wake, Dk. Slaa bado anaendelea kudai kuwa, ukaguzi huo umefanywa katika sehemu ndogo sana kwani ubadhirifu ndani ya BoT unahusisha vitengo vingi zaidi ya EPA.

Katika hatua nyingine, Meghji, alisema mpaka sasa ofisi yake haijapata taarifa ya kujiuzulu kwa Dk. Balali na kusema kuwa taarifa hizo alizisoma kwenye magazeti jana.

Alisema anachokijua ni kuumwa kwa Dk. Balali na yupo nchini Marekani akipatiwa matatibu ya maradhi yake na si kujiuzulu wadhifa wake kama ilivyoripotiwa kwenye magazeti kadhaa ya hapa nchini.“Mimi sijapata barua ya Balali kujiuzulu na kama amefanya hivyo, anapaswa kuandika barua na mara tutakapoipata tutaueleza umma kuhusiana na uamuzi huo,” alisema Meghji.Kujiuzulu kwa Dk. Balali bado ni kitendawili kikubwa kutokana na kauli ya Waziri Meghji pamoja na ile iliyotolewa na Rais Kikwete majuzi wakati alipozungumza na wahariri kuwa, anachofahamu ni kuwa gavana huyo yupo katika matibabu.

Hata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alipoulizwa juzi, naye alishindwa kukubali au kukanusha iwapo Dk. Balali ameandika barua hiyo ya kujiuzulu.

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, Dk. Balali yupo nchini Marekani, inakoelezwa kuwa amelazwa katika hospitali moja baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Huku nyuma, ameacha wingu zito la tuhuma dhidi yake na taasisi anayoiongoza, kutokana na matumizi yenye kutia shaka ya fedha, hasa zile zilizotumika katika malipo kwa kampuni kadhaa na ujenzi wa majengo mapya ya BoT.

Personaly sioni kama tumeshapigwa goli...! Its true state house ndio wamekamatwa...pants down! Slaa is right
 
Bravo Slaa.. washa washa.. hakuna Tembo kulala hapa, kama wanadhani kwamba kajiuzuru na wanamtisha abaki huko kwa kumfanaya kafara ili wao waonekane clean.. lazima tushinikize ashitakiwe, sasa huko huko kwenye sheria atasema tu!

Sema hapa watanzania wote tumuombee afya njema huyu balali asife na siri kubwa moyoni! Make hapa wanaweza hadi mkolimba hivi hivi pamoja na kwamba ana maradhi yake!
 
Akizungumzia taarifa za kujiuzulu kwa Dk. Balali, Dk. Slaa kwanza alimpa pole kutokana na maradhi yanayomkabili, lakini akamtaka Rais Kikwete kuamuru kukamatwa kwa gavana huyo mara moja ili ajibu tuhuma zote zinazomkabili.

Akiandika ujumbe mrefu wa simu ya mkononi, Dk. Slaa aliorodhesha baadhi ya tuhuma ambazo Dk. Balali anatakiwa kuzijibu kuwa ni kughushi taarifa ya BoT ya 2005 aliyowasilisha kwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji Septemba 20, 2005 katika kitabu ambacho ndani yake taarifa ya fedha ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imesainiwa Juni 21, 2007.

"Isitoshe yeye mwenyewe amesaini kama Mwenyekiti wa BoT Juni 21, 2007. Balali pia amesaini balance sheet (mizania) ndani ya kitabu hicho hicho. Taarifa zinazohusika ni hizo hizo za 2005/2006 zenye migogoro. Ni dhahiri kuna kughushi.

"Meghji kakaa kimya. Kughushi au ku-back-date (kurudisha nyuma tarehe) ni kosa la jinai. Kuna kirusi gani nchini? Raia wa kawaida hata angeumwa saa hizi angekuwa analindwa na askari magereza hospitalini… hakuna mwenye kibali kuvunja sheria," alisema.

DR. slaa anaoujumbe mzito sana hapa kuwa kama mtu anatuhumiwa kwa kosa la jinai kwa nini awe huru ama sheria ni kwa wale masikini tuu kwenye taifa hili?
 
Hatua kali ya kinidhamu imeota mbawa, sasa sijui watasema wanamfungulia mashitaka? Maana kumsimamisha kazi ingeonyesha kwamba kuna hatua imechukuliwa, lakini kujiuzulu tena kwa ridhaa yake mwenyewe hapo amewapiga 2 - 0!

Nimekubali Ballali ni mtaalam wa game, na amefanya the right move ili kulinda heshima yake na ndiyo maana Ikulu na Hazina wanajikanyaga, hawajui waseme nini. JK alitutamkia kwamba once report ikitoka yeyote atakayehusika na utafunaji na ma-dollar ya wafadhili atachukuliwa hatua za kinidhamu bila kujali wadhifa wake. Ngoja tusubiri hatua ya kinidhamu itakayochukuliwa just in case Ernst & Young watakuwa wamem-implicate Ballali!

Kama MMJ yuko right, basi barua hiyo ilivujishwa kwa makusudi ili habari itoke mapema kabla serikali haijajua ijibu nini. Kama hii barua isingevuja basi serikali ingekaa kimya na baadaye kuamua kutangaza kwamba Rais amesitisha uteuzi wa Gavana kwa maslahi ya umma ili JK ajizolee ujiko kwamba amefanya kweli na kumbe hakuna kitu! Msanii kakutana na msanii mwenzake na tena mtoto wa mjini!

Keil,

Kwa kuwa Rais ana haki ya kukubali au kukataa mtu kujiuzulu na kama walikuwa na nia ya kumsimamisha kazi!!! hilo ni jambo rahisi sana,,, wakati wa kujibu barua ya kujiuzulu kwa Gavana, Rais anakataa kujiuzulu kwake na badala yake kumfukuza!!!

Ushindi wa 2 - 0 ingekuwa kama Rais angekuwa tayari ameridhia kujiuzulu kwake!!!
 
MK,
huyu ndugu yetu wameshamkatalia kijiuzulu kwake hivyo bado ataendelea kuwa gavana wetu na kufanyakazi kwa kutumia remort control.
 
I dont think at this time we need to care anaumwa nini. Tunataka kujua kwanza alihusika kwa kiasi gani kuitia BOT katika hii turmoil. Watu wengi mnaangalia from wizi point of view, mimi nasema the guy is responsible for the whole poor monetery system and fisical policy. Yaani kuanzia his bad decisions on control inflations, interest rates and all that mess he made. He need to be responsible as soon as the report come out.

Enzi za zamani anasomewa mashitaka akiwa kitandani, ili kuonyesha kwamba people don't play. Unapokubali cheo katika kazi za jamii maana yake unakubali majukumu ya cheo na madhara yake unayafahamu kama upuuzi utafanyika.

So, kusema kwamba inabidi aachiwe sijui nini, that will be non sense. He need to be responsible for every bad move he made to put the country on turmoil economic system.
 
What?????????????

Wewe unajua maana ya haki??? Yale yale ya CCM mtu akiiba anahamisha kitengo/wizara na kupewa kitengo kipya. Kama huo sio ufisadi ni nini?

Haki anayostahili BALAA BALALI ni kufikishwa mahakamani na kuchezea mvua zisizopungua 50.
 
Jamani kama kuna mtu ana contact zozote za DR. Slaa naziomba. Tafadhali sana. Huyu mtu anahitaji TUZO ya hali ya juu kwa kuzidi kupigania maslahi yetu.
 
Jamani jamani mwogopeni Mungu kidogo na muwe na huruma ya kulinda shahidi wa taifa badala ya kumshutumu.
Kutoka mitaani, kuna ushahidi mkubwa kuwa Dr. Balali kakimbia Bongo kwa usalama wa maisha yake baada ya kuombwa na baadhi ya watu waliokuwa karibu naye hasa navyosikia baada ya yeye kutoa madai kama ya dada yetu marehemu AC kuwa yupo tayari kuyataja majina ya viongozi waliohusika.
Kwa hiyo twende taratibu na swala hili na kama kweli kuna uwezekano Dr. Bilali ahojiwe akiwa huko aliko na sio kuvuta hasira zetu ovyo.
Dr. Balali ni wanted na Mafia ya Bongo na kumtakia mabaya yeye ni kupoteza kabisa uwezekano wa kufahamu kilichotokea benki kuu.
 
kama analakusema angekwisha sema,lakini hakuna kitu kama hicho yeye ni shirika moja na mkuu wa kaya.hapa sisi utanachezewa nanihiii zetu tu.ulisikia wapi maiti kafufuka ?
 
Back
Top Bottom