Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 20,517
- 30,587
Huyu Motivation Speaker kama umemlipa hela kamwambie arudishe na mangumi juu.Wajasilimali wenzangu msije mkasema sijawaambia,iko hivi kama una shamba karibu na Dar,maana ya Mkuranga, Bagamoyo nk fikiria mradi huu unalipa.Nimeiba idea hii kwa jirani yangu kupitia meneja wake nikaone ni FURSA muhimu.
Iko hivi kwa mfano;
Kama una eneo lako hata kama ni ekari moja tu ya shamba na uko eneo ambalo jirani zako wana shamba ambalo hawaliendelezi, basi unaweza kutumia fusra hii kubadili maisha yako.
Mchanganuo wa biashara hii ni kama ifauatvyo
A: INVESTMENT COST
1.Nenda Mikoani nunua mitamba 80,000 kwa 250,000@ = = 20,000,000
2.Nunua madume 4 ya kisasa au Boran ambayo yataanza kupanda baada ya mwaka @ 300,000 = 1,200,000
3.Ujenzi wa Zizi na Nyumba ya mfanyakazi (Lumpsum) = 2,000,000
4.Mabomba ya kuogeshea 2 na Vifaa tiba @ (Lumpusm) = 200,000
JUMLA = 23,400,000
B: RUNNING COST
1.Mishahara ya wachungaji 2 Sh 200,000 X miezi 12 = 2,400,000
2.Walinzi 2 x 200,000 X Miezi 12 = 2,400,000
3.Madawa ya kuogesha na Tiba 50,000 X Miezi 12 = 600,000
4.Chakula wafanyakazi (Sembe +maharage) 100,000 Miezi 12 = 1,200,000
5. Supervisor 300,000 x miezi 12 = 3,600,000
6.Dharula 50,000 X miezi 12 = 600,000
JUMLA 10,800,000
JUMLA KUU A + B 34,200,000
BAADA YA MWAKA MMOJA
-Ngombe 70 watatoa 140 litres X 1000/= Sawa na 140,000/day 4,200,000 /month sawa na Tsh 50,400,000/YR
-Baada ya Miaka 3 utauza ng'ombe 50 X 700,000 35,000,000/YR
NOTE
Hii ina maana baada ya mwaka 1 unarejesha hela yako imerudi na faida ya kutosha. Hakikisha unampata meneja/Supervisor mzuri na umpe motisha ukifika hatua ya kutengeneza faida. Swala la ulinzi na afya ya mifugo lichukulie kwa umakini mkubwa sana. Ninae andika hii hoja ni mtoto wa mfugaji wa ng'ombe wa asili na sasa mfugaji wa ng'ombe wa kisasa..Uzoefu 100%
Hayo ni maoni yangu.
Karibuni kwa maoni.
Kakudanganya sana tu tafuta wafugaji tukueleze siyo huyo motivation atakudanganya utupie mtaji wako wote ujinyonge bure.
Kwanza mtamba wa 250000/=unaupata wapi ?
Zagamba la Boran upate kwa 300000/=?