Full mipasho bungeni

Lissu alishawatukana wazanzibari jana wakati wa hotuba yake, vipi mkuki kwa nguruwe eeeeh!
Kama kuna kosa ambalo hatutamsamehe mwalimu Nyerer ni huu muungano na watu waajabu wenye matusi na majivuno kama wazanzibari,wakati umefika,sasa wakutengana kila mtu aingie kivyake kwenye shirikisho la Africa Mashariki
 
Lissu alishawatukana wazanzibari jana wakati wa hotuba yake, vipi mkuki kwa nguruwe eeeeh!

Wa Zenji wala hawajamtukana zaidi ya kumpa ukweli ulivyo. Ila inaonenaka Chadema wanaogopa vivuli vyao wenyewe.

Yetu macho.
 
Kwa wale watu makini, nadhani mmeshajua kuwa hawa watu waliandaliwa kutoka jana, mbona wale wabunge waliokuwa wanauponda muungano sikuwaona wakichangia, kama ni kweli hawa wabunge walikuwa wanawakilisha sauti ya wazanzibar wote sasa hizi roho za kwanini juu ya muungano zinatoka wapi? Lakini msiwe na wasiwasi juu ya hili hivi punde mtayasikia mengine kuhusu huu muungano na ninawahakikishia hili

Michango ya wabunge hao imesikitisha sana, kwanza wachangiaji wote 4 wa leo ni wa kutoka upande wa pili wa Muungano (zbr), 3 ni wa CCM na 1 ni wa Chadema kama sikosei anaitwa Mhe. Raya, huyo peke yake hakuzungumzia udini wala uzanzibar. lkn wale 3 wa CCM wametumia lugha ya kuudhi sana na kufanya personal attack kwa Lissu. Lugha hiyo angezungumza mbunge wa upinzanii nina hakika angetolewa na polisi mjengoni! maneno kama Tundu Lissu ni Mpuuzi, Muongo, Fitina na zaidi kulitangazia bunge kuwa Tundu Lissu Kizanzibar ni "Tundu Lussu", kwa tafsiri tuliyopewa ni matusi na kumdhalilisha mbunge mwenzao!

Wabunge wa upinzani akiwamo Lissu mwenyewe walipotaka kuomba mwongozo wa Spika, makinda aliwakatalia na kuwaambia wavumiliane! lkn kikubwa ambacho wabunge 3 wa CCM wamechangia ni kuhusu hotuba ya Lissu aliposema ktk mchakato wa Katiba ujao, rais wa Zbr ashirikishwe kwenye mambo ya muungano tu si kama rasimu iliyopo inavyosema kuwa atashiriki ktk kila hatua. Swali la Tundu Lissu hapa ni mbona wao wana Katiba yao na ktk mchakato wao hawakuwashirikisha wa TZ bara?

Lissu ktk hotuba yake jana aliainisha mapungufu makubwa ktk rasimu ya marekebisho ya katiba ambayo kama kweli yapo hivyo ni tatizo kubwa na ninaamini ikipelekwa kwa wananchi ikajadiliwe watayakataa! labda yatumike mabavu, kitu ambacho kinaweza kuleta vurugu. Kwa ukali wabunge hao wanaitetea Zbr kuwa ni nchi kamili na anayetaka kuwachokoa kuhusu hilo hawatakubali. Mwingine akasemea suala la Waislamu bara wananyanyaswa na sheria ya ndoa ya 1971. Kuwa dini ya kiislamu inaruhusu kijana wa miaka 18 kuoana na binti wa miaka 15 na sheria hiyo inakataza...kwanini? Anasisitiza waislamu bara wanaonewa pia kwa kutokuwa na mahakama ya kadhi. Cha kujiuliza hapa anataka watoto wa ikaka 18 na 15 waoane hivi wataenda shule saa ngapi? ndio maana kuna kundi huwa linalalamika kuwa wanaonewa kupewa fursa sawa na wenzao na kwamba dini fulani inapendelewa.....wanasahau kuwa wakati wengine wanaoana wenzao wanaenda shule na matokeo yake wanaopata fursa hizo ni wale walioenda shule. I might be wrong but this is it! Mbunge huyo ameapa kwa miungu kuwa mwakani ataongoza maandamano makubwa ya kupinga waislamu kuonewa.

Kaaazi kwelikweli!
 
woooooooteeeeeeeee hamna tofauti na mletaji mada hakuna mtu aliyetujuza kwa undani tukaelewa
 
Wabunge wa znz kitu gani???shule ipo????au skuli??ati wabunge? wamshuru Nyerere,wanaongoza vitongoji leo wanajifanyamuch know,leteni cv hapa ubaoni tuwaone.
<br /> <br / hawana lolote hawa tena waendezao hawajui wanafanyaje bungeni kazi yao ni kuongea kishogashoga na sijui kelele zao ni za nini wakati alichoongea lisu ni ukweli m2pu kw RAIS WA ZANZIBAR ASHIRIKISHWE KWENYE MAMBO YANAYOHUSU MUUNGANO TU.
 
Haya ndio madhara ya kuwafanya w/viti wa vitongoji kuwa wabunge.
Sijui hizo hansadi zenu mtarekodi huo upupu kama kumbukumbu kwa baadae ama vipi.
.
 
Kwa wale watu makini, nadhani mmeshajua kuwa hawa watu waliandaliwa kutoka jana, mbona wale wabunge waliokuwa wanauponda muungano sikuwaona wakichangia, kama ni kweli hawa wabunge walikuwa wanawakilisha sauti ya wazanzibar wote sasa hizi roho za kwanini juu ya muungano zinatoka wapi? Lakini msiwe na wasiwasi juu ya hili hivi punde mtayasikia mengine kuhusu huu muungano na ninawahakikishia hili

Ninafikiria hivyo pia, kwanza waliyachukia yaliyowasilishwa na Lisu wakapanga kabisa- watu wangapi watakaozungumza na watakuwa na uelekeo gani, yawezekana na wabunge hao walikuwa tayari wana uelekeo huo au waliandaliwa. Lakini kinachoshangaza, wabunge wengi wa Zanzibar hii ilikuwa ajenda yao hapo nyuma kidogo sasa hivi wameifukia, mimi nadhani huu ni moto ambao unangoja kulipuka na utakua mkubwa mno.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
wanzibari wamesema watashiriki kwa kila jambo linalohusu Tanzania liwe la Muungano au lisiwe la Muungano.hakuna serikali ya Tanganyika kokote. tusiwaonee kwa udogo wao wa idadi ya watu. Akaja mwingine akasema Waislam wa Tz Bara wamekosa haki kwenye mambo mengi tuu yanayowahusu mfano mahakama ya KADHI, haki ya kuoa au kuolewa mara tu unapovunja UNGO au KUBALEHE haki hii wameikosa Wanataka Katiba Iwarudishie. nilishindwa kuvumilia kusikiliza hoja za aina hii za kutetea kutaka kuoa au kuolewa kwenye umri wa Kitoto.
 
Sikujua Waziri Wa Sheria Selina KOmbani anaweza akapersonalise Hotuba ya Upinzani Kwa sababu nimeona anajibu vifungu kama vile anamsuta Tundu Lissu,Na yeye pia ana shaka na uwezo na wake wa ufahamu,staha na matumizi ya lugha,nadhani hilo la uraisi wa kifalme na kuita mahakama kuendeshwa kifisadi limemuuzi zaidi,amesema Tundu Lissu ni mchochezi kwa kusema wazanzibari sasa waangalie nafasi yao kwenye muungano,washiriki mambo ya muungano tuu
Kasema Tundu Lissu anaharaka kwa kuongelea mambo ya Katiba bila ruhusa yake anasema Tundu Lissu kapeleka mswaada wa Katiba wakati bado wizara wako kwenye mchakato,anatuonya watanzania tusije tukaingizwa mkenge na mtu mmoja kwa maana (Tundu Lissu ) kama ilivyokuwa kwenye mswaada
Mytake : Nimesikitishwa na kukasirishwa jinsi Selina Kombani anavyomshushia hadhi Tundu Lissu kwa kumuona si mtu wa kuaminika kwamba hotuba amejiandikia mwenyewe bila mawazo ya upinzani ,halafu kitendo cha waziri mwenye dhamana ya wizara kuwaunga mkono wabunge waliokuwa wanamtukana Tundu Lissu matusi ya nguoni kinaonyesha kwamba kama kawaida yao CCM walijipanga

Unajua Secina Kombani alikotokea? Alikuwa secretary wa SUA kwa miaka mingi akajiendeleza kidogo na kuingia kwenye siasa. Pamoja na kujiendeleza kwake na kupewa wizara nzito ya masuala ya sheria wakati hata taaluma ya sheria japo certificate hana unategemea nini? kashindwa tu hata kuchanganya na za kwake ili hekima imtawale anazungumzia ushabiki wa chama! kwa mtaji huu hatuwezi kufika popote.

Mchakato wa Katiba wapelekewe wananchi waamue wanataka muungano wa namna gani? Maana Wazanzibar wanataka haki yao kama nchi sasa muungano wa nini tena? Wana Rais wao, bendere yao, mwimbo wao wa taifa na Katiba yao ambayo bara hatukushirikishwa. Hivi huu muungano kwa maslahi ya nani? kwanini wa bara tunatukanwa na kudhalilishwa kiasi hiki as if sisi ndio tunaung'ang'ania? Mwl. Nyerere alikuwa na nia nzuri sana kwa wakati huo, naamini angekuwepo hii leo kwa upepo unavyoenda hata yeye angetaka mabadiliko makubwa yafanyike kama si kuuvunja. They need us more than we need them! Wengi wetu tumeuchoka sana huu muungano, vinginevyo tuwe na serikali ya Zbr, ya Tanganyika na hiyo ya Muungano, vinginevyo tunacheza makidamakida na huu muungano fake!
 
Hivi kusema Zanzibar kwenye katiba isihusike kwenye mambo yatakayohusu Tanganyika (bali wahusike kwenye mambo ya muungano tu) kama ambavyo Tanganyika haikuhusika kwenye katiba ya Zanzibar ni tusi?
 
woooooooteeeeeeeee hamna tofauti na mletaji mada hakuna mtu aliyetujuza kwa undani tukaelewa

U R NOT SERIOUS...INGEKUWA SKYPE TUNGEKUSIMULIA!
Umesoma kweli wewe/ au unatak autafuniwe namna gani....?Kama uelewa wako ni mdogo hivyo sijui tukusaidieje!
 
[COLOR=#ff0000 said:
Nduka[/COLOR];2405272]Haina majotroo bana, hivi unajua maana ya Tundu Lissu kule Unguja?

Haina majotroo pia....we unajua maana ya neno 'Nduka' kwetu uChagani? Muombe 'Paw' hasinipe ban nikuambie!
 
Uzuri wa muungani ni mmoja tu, kwa sisi wafanyakazi wa kuajiriwa tunapumzika kila terehe 26 April. tudumishe muungano wapendwa.
 
Hebu ngoja na mimi nijaribu kusema hivi....hao wapuuzi wenye vyeti feki wanaowaza kwa kutumia makalio wanajipya gani? haha hahaa ina utamu kumbe, hizo ni sifa sio matusi
 
Sijui hizo hansadi zenu mtarekodi huo upupu kama kumbukumbu kwa baadae ama vipi.
.
hivi zinapatikanaje? Wana wetu watakuja kutuumbua kwamba uwezo wetu wa kupambanua mambo ulikuwa mdogo sana.
 
Back
Top Bottom