Pamoja na kwamba wabunge wengi wameonekana kupiga makofi wakati baadhi ya wabunge wakimponda Mh Lissu kuhusu hoja yake kuwa Zanzibar ishiriki kwenye masuala ya Muunngano na sio vinginevyo, nahisi wabunge wengi (including wa ccm) kichinichini wanakubalina naye (Lissu). Wanzazibari wenyewe wamekuwa wanauliza serikali ya Tanganyika iko wapi lakini majibu yako techinical siku zote.
Hata wakati wa mojadala bungeni, wabunge wengi wa toka Zanzibar wanapata shida kuchangia maana kusema kweli mambo mengi hayagusi Zanzibar ila wanafanya hivyo kwa sababu ya mfumo uliopo. Mfano, mijadala ya wizara mifugo, ujenzi, kilimo n.k Hizi haziko kwenye mambo ya muungano.
Iko haja ya kuangalia haya mambo kwa busara na umakini na sio kumshambulia Tundu Lissu (personally) maana wanaweza kukuta wako watanzania wengi (pande zote za muungano) wenye mawazo kama yake lakini hawapati majibu. Don't kill the messanger!