Full mipasho bungeni

Maneno ya huyo chambo ni makali kiubinadamu kwan hata kama hoja za lissu zilikukwaza si naye angepaswa kujibu kwa hoja?
Huyu ameonesha ni jinsi gani alivyo kilaza.
Tatizo kubwa hapa ni kuwa zanzibar tayari ni nchi kitu kinachoipa nguvu ya kujipambanua kwan inafahamu fika kua hakuna serikali ya tanganyika.
Umefika wakati sasa wa kuwa na serikali ya tanganyika ila kuondoa upuuzi wote huu unaoendelea.
 
HOJA ILIYO HOT NI ILE INAYOHUSIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR ..NA SERIKALI YA MUUNGANO...Mbunge wa ZNZ analinganisha Muungano na ndoa..anasema "ukioa mke unaangalia ana sifa..na siyo huyu ana makalio makubwa au madogo."... hivyo udogo wa ZNZ si ishu....iheshimiwe.

Mh Tundu Lissu analengwa.....anaambiwa haelewi nini maana ya Urais wa kifalme! iTS REALLY HOT!

Sasa wenzangu wala urojo a.k.a 'mdebwedo' naomba nijuzwe miye! hapo 'Nke' ni nani na mme nani? kwi kwi kwi..!
 
Wa Zenji wala hawajamtukana zaidi ya kumpa ukweli ulivyo. Ila inaonenaka Chadema wanaogopa vivuli vyao wenyewe.<br />
<br />
Yetu macho.
<br />
<br />

Hehehehehhhhhh ukweli unauma somo, msitumie mishipa, moshi na kuvimbisha mashavu pahali pa kutulia na kuwa waungwana mueleweke...maneno wabunge hao waliochangia hayakupaswa kutamkwa na watu wazima ndani ya chombo cha kutunga sheria unless nao wanafikiri kwa 'masaburi'
 
wanzibari wamesema watashiriki kwa kila jambo linalohusu Tanzania liwe la Muungano au lisiwe la Muungano.hakuna serikali ya Tanganyika kokote. tusiwaonee kwa udogo wao wa idadi ya watu. Akaja mwingine akasema Waislam wa Tz Bara wamekosa haki kwenye mambo mengi tuu yanayowahusu mfano mahakama ya KADHI, haki ya kuoa au kuolewa mara tu unapovunja UNGO au KUBALEHE haki hii wameikosa Wanataka Katiba Iwarudishie. nilishindwa kuvumilia kusikiliza hoja za aina hii za kutetea kutaka kuoa au kuolewa kwenye umri wa Kitoto.

Hapo kwenye red ndio kumestua karibu kupata ugonjwa wa kiharusi. Siku hizi watoto wengi wa kike wanavunja ugo wakiwa na umri wa miaka 11 au 12! Na kwa maoni ya huyu mbunge ni kwamba mtoto huyo wa miaka 11 au 12 amefikia umri wa kuolewa! Kam hii sio child marriage basi sijui ni kitu gani? Hivi inakuwaje mbunge mzima anasimama bungeni kusema anatetea ndoa wa watoto? Kuna haraka gani? Watasoma lini na huku sio kuendeleza umaskini? Watu wa haki za binadamu wanatakiwa waingilie hili maana viongozi wenye mawazo kama huyu mbunge ni hatari kwa mtakabali wa watoto wa nchi hii.

Majaji huko Yemen wamekuwa na kesi kibao za watoto wa miaka 10 (miaka10) wanaoomba DIVORCE! Mtoto wa miaka 10 anaolewa na libaba la miaka 35-42! Hata wataalam wa afya watakumbia madhara ya watoto wa kike kufanya mapenzi wakiwa na umri mdogo. yapo. Na hii haraka ni ya nini na kama huyu mbunge sio muumini wa UBAKAJI WA WATOTO! (Sorry kutumia hilo neno) lakini kama mzazi sioni ni vipi mzazi anaweza kurusu mtoto wa miaka 11 aolewe. Sielewe. Naomba wanaJF bila kujali dini zetu tulaani hili. Ni ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto.

Mwisho, vitabu vyote vya dini, iwe biblia, Koran au hata Totra (kwa wayahudi) viliandikwa miaka zaidi ya 1,000 iliyopita. Hakuna mtu yeyote anayeweza kutoa ushahidi kuwa kila lililoandikwa kwenye hivi vitabu limetoka kwa mungu. Hakuna. Ila waumini wa madhehebu haya WANAAMINI kuwa yaliyoandikwa yametoka kwa mungu. Narudia, WANAAMINI. Na kuamini ni tofauti kabisa na EVIDENCE. Kwa maoni yangu ni vizuri basi wakati tunasoma hivi vitabu tusome with time-reference. Kwamba viliandikwa katika miaka hiyo kwa mazingira (context) fulani. Hivyo tutumie utashi wetu kutafsiri yaliyoandikwa ili kuboresha maisha ya mwanadamu. Kwa maana hiyo idea ya kuruhu watoto wa miaka 11 au 12 waolewe si sahihi hata kidogo, na inaonesha ni jinsi gani watu wanashindwa kutafsiri maandiko ya vitabu vya dini ili kuboresha maisha ya wanadamu.

Huyu mbunge kanichefua sana tena sana. Naomba mungu amzindue kwenye mawazo hayo potofu. atatuharibia watoto.
 
Unajua Secina Kombani alikotokea? Alikuwa secretary wa SUA kwa miaka mingi akajiendeleza kidogo na kuingia kwenye siasa. Pamoja na kujiendeleza kwake na kupewa wizara nzito ya masuala ya sheria wakati hata taaluma ya sheria japo certificate hana unategemea nini? kashindwa tu hata kuchanganya na za kwake ili hekima imtawale anazungumzia ushabiki wa chama! kwa mtaji huu hatuwezi kufika popote.

Mchakato wa Katiba wapelekewe wananchi waamue wanataka muungano wa namna gani? Maana Wazanzibar wanataka haki yao kama nchi sasa muungano wa nini tena? Wana Rais wao, bendere yao, mwimbo wao wa taifa na Katiba yao ambayo bara hatukushirikishwa. Hivi huu muungano kwa maslahi ya nani? kwanini wa bara tunatukanwa na kudhalilishwa kiasi hiki as if sisi ndio tunaung'ang'ania? Mwl. Nyerere alikuwa na nia nzuri sana kwa wakati huo, naamini angekuwepo hii leo kwa upepo unavyoenda hata yeye angetaka mabadiliko makubwa yafanyike kama si kuuvunja. They need us more than we need them! Wengi wetu tumeuchoka sana huu muungano, vinginevyo tuwe na serikali ya Zbr, ya Tanganyika na hiyo ya Muungano, vinginevyo tunacheza makidamakida na huu muungano fake!
Lakini hata kama alianzia usecretary kwa kukaa sasa kwenye uwaziri karibu kipindi ch pili angekuwa anapima mambo wakati anamtuhumu na Kumsuta Lissu kwamba ana act kama sio mwanasheria kwa maana hana lugha ya staha lakini alikuwa akimzodoa Waziri Kivuli kama vile mtoto na hakustahili kuwa na mawazo mbadala kwenye hotuba ya upinzani,amemdhalirisha Lissu kwenye mambo ya msingi kabisa kwa kutuma platform yakujibu hoja ametumia dakika 28 Kumnanga Lissu 7 kwa kuwaunga mkono wale masharabaro wabunge wenye matusi wa Zanzibar

hawa waachwe waendeshe nchi yao ni headache ya bila sababu,its our tax which makes them misbehave,wameshaanza wanachoma biashara za waabara kwao wakati wao wako kila mahala ya pembe ya nchi,lugha zao Bungeni CCM na CUF kuhusu Tanganyika ni za dharau sana mara wanatuita machogo sijui nini siwapendi wala siwataki kabisa kuwa kwenye muungano labda kama waafrika wenzangu lakini si vinginevyo,katiba na ije turudishe Tanganyika yetu
 
Sasa wenzangu wala urojo a.k.a 'mdebwedo' naomba nijuzwe miye! hapo 'Nke' ni nani na mme nani? kwi kwi kwi..!

Last time I checked all countries are reffered to as SHE, kwa hiyo hii ni ndoa ya WASAGAJI.
 
Hivi kusema Zanzibar kwenye katiba isihusike kwenye mambo yatakayohusu Tanganyika (bali wahusike kwenye mambo ya muungano tu) kama ambavyo Tanganyika haikuhusika kwenye katiba ya Zanzibar ni tusi?

Hivi kwani kuna Serikali ya Tanganyika au Serikali ya Mmungano.

Waznz watashiriki kwenye mambo yote ya Serikali ya Muungano. Lakin asilan hawatashiriki kwenye mambo ya Serikali ya Tanganyika.

naomba mlifahamu hilo. Kwani kwenye muungano wanaingia kwa mujibu wa katiba na sio ihsani.
 
Jamani hili Bunge linafanya marudio usiku ili na siye tulio maofiisini tupate kuona na kusikia mipasho ya bungeni, kwenye huo mjumba siku hizi kuna mambo.
 
Lakini hata kama alianzia usecretary kwa kukaa sasa kwenye uwaziri karibu kipindi ch pili angekuwa anapima mambo wakati anamtuhumu na Kumsuta Lissu kwamba ana act kama sio mwanasheria kwa maana hana lugha ya staha lakini alikuwa akimzodoa Waziri Kivuli kama vile mtoto na hakustahili kuwa na mawazo mbadala kwenye hotuba ya upinzani,amemdhalirisha Lissu kwenye mambo ya msingi kabisa kwa kutuma platform yakujibu hoja ametumia dakika 28 Kumnanga Lissu 7 kwa kuwaunga mkono wale masharabaro wabunge wenye matusi wa Zanzibar

hawa waachwe waendeshe nchi yao ni headache ya bila sababu,its our tax which makes them misbehave,wameshaanza wanachoma biashara za waabara kwao wakati wao wako kila mahala ya pembe ya nchi,lugha zao Bungeni CCM na CUF kuhusu Tanganyika ni za dharau sana mara wanatuita machogo sijui nini siwapendi wala siwataki kabisa kuwa kwenye muungano labda kama waafrika wenzangu lakini si vinginevyo,katiba na ije turudishe Tanganyika yetu

Celine Kombani ameboa sana sana!! ni ule ule unafiki akitetea kitumbua chake lkn moyoni sivyo anavyoamini! hata hao wabunge wa Zbr wanajua wanavyonufaika na huu muungano lakini wanaleta za kuleta! Ukitaka kujua wanavyofaidika huku mwangalie makamu wa rais wa poli wa Zbr, kwa cheo na nafasi yake ni mtu mkubwa sana kwenye hako kanchi kao lkn kutwa anasinzia kwenye viti vya Bunge la Muungano ili ap[ate posho utadhani hana majukumu ya kufanya huko Zbr kama makamu wa pili wa Rais - shame!

Wabunge wa kutoka Zbr wapo zaidi ya 70 ktk Bunge letu eti wanawakilisha population ya watu wasiozidi hata nusu ya wakazi wa Dar...! wabunge wa dar nadhani wapo kama 7 au 8 hivi na wanawakilisha watu zaidi ya milioni 5. Hawa wanatutania hawa, tumewachoka pia na hatuwataki kwenye hii ndoa fake! Kila mtu ashike time yake!
 
Jamani hili Bunge linafanya marudio usiku ili na siye tulio maofiisini tupate kuona na kusikia mipasho ya bungeni, kwenye huo mjumba siku hizi kuna mambo.

Mkuu Star TV huwa wanafanya marudio usiku. wanaendelea hadi alfajili
 
maneno ya Masaburi yana mantiki.
how comes mbunge unatumia mamilioni ya wavuja jasho kwa kumtukana mbunge mwanzako.
Lissu usife moyo. kaza buti wanakukubali moyoni, ila machoni wanazuga
 
maneno ya Masaburi yana mantiki.
how comes mbunge unatumia mamilioni ya wavuja jasho kwa kumtukana mbunge mwanzako.
Lissu usife moyo. kaza buti wanakukubali moyoni, ila machoni wanazuga
Yaani ukweli wenyewe wamemtukana matusi ya nguoni kwa kuringia kwamba wao ni nchi na ni wazanzibari ambao wako kwenye Bunge la Tanganyika tutawafanya nini hebu angalia nukuu hii ya Waziri Kivuli wa sheria kuna tusi hapo au ni facts hayo yaliyopo chini ndio ukweli wenyewe ,Selina Kombani naye kwa rating za mawaziri wenye majibu ya zero basi yeye anaongoza

Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Rasimu ya Muswada hayakubaliki kwa sababu yanaweka mchakato wa Katiba Mpya kwenye huruma na/au fadhila ya Rais wa Zanzibar na siasa za Zanzibar kwa ujumla. Kwa mapendekezo haya, Rais wa Zanzibar asipokubaliana na jambo lolote linalohitaji ridhaa yake basi mchakato mzima utasimama au kusitishwa. Aidha, endapo katika kura ya maoni inayopendekezwa, theluthi mbili ya Wazanzibari hawatakubaliana na Katiba Mpya basi Katiba hiyo haitapitishwa hata kama inakubaliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania Bara.

Mustakbala wa taifa letu hauwezi kuwekwa tena rehani kwenye siasa za Zanzibar na kwenye matakwa ya Wazanzibari kwa kiasi hicho. Kuhusiana na jambo hili, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar ahusishwe tu katika masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Nje ya masuala hayo, Rais wa Zanzibar hana sababu yoyote ya kuhusishwa na mchakato wa kikatiba unaohusu mambo ya Tanzania Bara."

Aidha, wajumbe wa Tume ya Mapitio ya Katiba ambao watatoka Zanzibar wahusike tu katika mchakato wa masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wananchi wa Zanzibar washiriki katika kura ya maoni inayohusu mfumo mpya wa Muungano tu. Hii ndio kusema kwamba, kama vile ambavyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Tanzania Bara hawajashirikishwa katika mchakato wa kikatiba wa Zanzibar kwa sababu ulihusu mambo yasiyokuwa ya Muungano, vivyo hivyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Zanzibar wasishiriki katika mchakato wa kikatiba wa mambo yasiyokuwa ya kikatiba kwa upande wa Tanzania Bara.``
 
''Wasomi wengi hata wa vyuo vikuu hawaijui katiba kama wanaijua hawailewi na kama wanailelwa hawajui vifungu'' (Prof Issa Shivji TBC1 24/8/2011)
Sishangai wabunge wa Zanzibar kutoelewa nini hasa Mh Tundu Lissu alimaanisha katika hotuba yake, walisikiliza hawakuelewa na pale walipoelewa kidogo hawakufahamu undani wa hoja, wanatumia nguvu nyingi kusukuma ukuta na ukipima workdone ni zero!
am out
 
Haina majotroo pia....we unajua maana ya neno 'Nduka' kwetu uChagani? Muombe 'Paw' hasinipe ban nikuambie!

Uchagani kabila gani? wamarangu, wamachame, wakibosho, au? wewe funguka tu acha uoga wa kike.
 
Mwalimu Nyerere alifanya mambo mengi mazuri, lakini hili la kuleta muungano alikosea sana,sasa ona tabu aliyotuachia, siku muungano huu ukivunjika nitafurahi kupita maelezo.NAUCHUKIA SANA MUUNGANO.
 
Back
Top Bottom