From Ukonga Prison: Ikulu ilituma ujumbe mwingine kumtaka mwamba akubali "msamaha" wa Mama. Tundu Lissu akataa, amwambia afute kesi kwa kuwa ni uongo

From Ukonga Prison: Ikulu ilituma ujumbe mwingine kumtaka mwamba akubali "msamaha" wa Mama. Tundu Lissu akataa, amwambia afute kesi kwa kuwa ni uongo

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
3,611
Reaction score
9,269
Inasemakana Ikulu ya Samia ilituma wasaidizi wake tena Gereza la Ukonga kuonana na Tundu Lissu

Wakamwambia Mhe. Lissu kwamba mama yao yupo tayari kumsamehe Mhe. Lissu ila sharti lake ni moja akubali kuipeleka CHADEMA kwenye maridhiano.

Mhe. Lissu aliwauliza: "....Anisamehe kwa kosa gani wakati yeye ndo aliyenibambika hii kesi ya uwongo? Sihitaji na hakuna msahama kwa kosa au makosa yasiyokuwepo tena ukiambatana na masharti kwamba ukitoka ufanye hivi au vile. Mwambieni nataka afute hii kesi kwa sababu ni ya uwongo kwa kuwa yeye anajua hivyo na Mbingu na nchi yote inajua kwamba mimi sio Muhalifu...."
-------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------
Huu 👆🏻msimamo wa Tundu unanikumbusha msimamo wa wale vijana watatu Shadrack, Meshack na Abednego katika Biblia kitabu cha Daniel sura ya 3 yote walivyokataa kusujudu sanamu miungu ya mfalme (Rais) Nebukadneza wa Babeli. Hebu soma majibizano ya vijana hawa na mfalme👇🏻

Picha inaanza kwa njama za chawa wa mfalme kumshauri mfalme atengeneze sanamu ya miungu ya Babel itakayoabudiwa na wananchi wote wa nchi hiyo. Lengo la Chawa hawa haikuwa kumfurahisha mfalme bali kutumia mgongo wa mfalme kuwanasa vijana hawa watatu wacha Mungu Yehova ili wawe waovu kama wao na hivyo wawaue.

Mfalme Nebukaneza akaingia mkenge, akakabuliana na chawa hao, sanamu ikatengenezwa, ikasimikwa nchini kote na ikatungiwa sheria. Na yeyote atakayekiuka sheria hiyo kwa kukataa kuinama na kuibudu sanamu ya miungu ya mfalme, adhabu yake ni kupikwa kwenye tanuru la mto mkali sana wa gesi.

Shadrack, Meshack na Abednego walikataa katakata kumkufuru Mungu wao kwa kuabudu sanamu na miungu ya mfalme Nebukadneza. Na kwa sbb hii wakashitakiwa na kisha kuhukumiwa hukumu ya kifo...!

Na hivi ndivyo waendesha mashitaka wa serikali ya mfalme (Public Prosecutors) wa Babeli walivyo draft hati yao ya mashitaka;

Danieli 3:9-12 BHN
“....Uishi, ee mfalme!...Wewe, ee mfalme, ulitoa amri kuwa kila mtu anaposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na kila aina ya muziki, ainame chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu. Na kwamba mtu yeyote asiyeinama chini na kuiabudu sanamu hiyo, atupwe ndani ya tanuri ya moto mkali. Sasa, kuna Wayahudi fulani uliowateua kushughulikia mambo ya utawala wa mkoa wa Babuloni, yaani Shadraki, Meshaki na Abednego; watu hawa, ee mfalme, hawakuitii amri yako. Wanakataa kuitumikia miungu yako na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha....”


Baada ya kusikia haya, wakaitwa mbele ya mfalme ili kujibu mashitaka dhidi yao. Na mfalme akaanza kwa kuwalizs hivi;

Danieli 3:14-15 BHN
“......Je, ni kweli kwamba wewe Shadraki, wewe Meshaki na wewe Abednego, hamuitumikii miungu yangu wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi, mtakaposikia tena sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, je, mko tayari kuinama chini na kuiabudu sanamu niliyotengeneza? Kama mkikataa, mtatupwa mara moja katika tanuri ya moto mkali. Je, ni mungu gani anayeweza kuwaokoa mikononi mwangu...?”

Huyu mfalme alikuwa jeuri na kiburi sana kuliko Idd Amini Mama a.k.a Bi Msumi a.k.a Samia Suluhu Hassan. Lakini vijana hawa walikuwa watu wa haki ya Mungu na walimjibu mfalme Nebukadneza kwa ujasiri sana kuipinga amri yake batili hadharani kusema;

Danieli 3:16-18 BHN
“.....Ee Nebukadneza, sisi hatuhitaji kukujibu kuhusu jambo hilo. Ikiwa ndivyo, Mungu wetu ambaye tunamtumikia aweza kutuokoa katika tanuri ya moto mkali; tena atatuokoa mikononi mwako, ee mfalme. Lakini, hata kama haitafanyika hivyo, ujue wazi, ee mfalme, kwamba sisi hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyosimamisha.....”

Jibu hili lilimghadhabisha sana mfalme. Na hii ndiyo ikawa hukumu yake kwa vijana hawa;

Danieli 3:19-23 BHN
"....Hapo, mfalme Nebukadneza akawaka hasira, sura yake ikabadilika kwa chuki dhidi ya Shadraki, Meshaki na Abednego. Akaamuru mwako wa moto wa tanuri uongezwe mara saba kuliko kawaida yake. Akaamuru watu fulani wenye nguvu kabisa katika jeshi lake wawafunge Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika ile tanuri ya moto mkali. Basi, vijana hao wakafungwa hali wamevaa makoti yao, kanzu zao, kofia na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuri ya moto mkali. Kwa vile amri ya mfalme ilikuwa kali, ule moto ulikuwa umewashwa ukawa mkali sana, hata ndimi za moto zikawateketeza wale watu waliowapeleka Shadraki, Meshaki na Abednego. Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego, wakiwa wamefungwa, wakatumbukia katika ile tanuri ya moto mkali..."
Kwa kuwa vijana hawa walikuwa upande wa HAKI, Mungu aliugeuza moto ule wa gesi kuwa kivuli, haukuunguza hata uzi mdogo wa kanzu na mashati yao wala unywele wao. Kilichofuata baada ya tukio lile kukafanyika REFORMS za kisheria Babeli yote na taifa zima likazaliwa upya na kustawi sana huku vijana hao wote watatu wakishika nyadhifa kubwa ktk serikali ya Babeli kwa sbb ya uaminifu wao. Na ndio maana ya mithali hii 👉🏻 HAKI HUINUA TAIFA...
-------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------
Scenario hiyo👆🏻, it's exactly kama ilivyo ya ktk kesi ya Tundu Lissu. Samia Suluhu Hassan anataka kumlazimisha TL aabudu uchafu na uovu wake (miungu yake). TL anakataa na sasa anatishiwa kuuwawa kikatili. Sijui wataanzia wapi masikini hawa kuiua haki. HAKI huwa haiuwawi na badala huuchapa uovu na kuusigina kabisa...

Ndio kusema kuwa Samia Suluhu Hassan anatumia kesi ya mchongo ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu ili kumkomoa ndo maana ameagiza shauri likapakiwe mahakama ya rufani na mpaka leo Mahakama hiyo ya Rufani haijapanga tarehe ya kuanza kusikiliza Rufaa ambayo imekatwa na Mawakili wa Serikali kwa maelekezo ya Samia mwenyewe

Samia Suluhu bila hamjui vizuri Tundu Lissu. Anadhani kwa kufanya hivi itafika muda Mhe. Lissu atampigia magoti na kukubali kuiuza nafsi na utu wake na kisha kuipeleka CHADEMA kwenye maridhiano ya kimaigizo kama haya wanayoyapigia chapuo..

Hata hawakumbuki kuwa, Mh Tundu Lissu alishasema categorically kuwa kama wanataka kumnyonga kwa hii kesi ya uwongo yupo tayari ila hatotokea kumpigia magoti binadamu yeyote ili kunipa fadhila zake kama vile yeye ni Mungu muumba wa vyote...

Huku nje upande wa pili napo ni vilevile. Kuna kesi nyingine ya mchongo ya madai ya Mgawanyo wa mali za CHAMA na mazuio ya CHAMA kufanya shughuli zake za kisiasa. Ni silaha ya shinikizo la aina hiyo. Ni muendelezo huo huo wa kuwa blackmail Viongozi kwamba mkikubali kuingia kwenye maridhiano basi hizi kesi zote zitafutwa.

Nakumbuka wakati wa Uchaguzi Nduli Idd Amin mama na vibaraka wake walikuwa wanasema kwamba “CHADEMA wanajiona wao ni special sana wakati Tanzania Vyama vya upinzani viko vingi”

Sasa kama Vyama vya upinzani nchini viko vingi sana kwanini yupo Desperate, anahangaika na kutumia nguvu kubwa kiasi hiki kutaka CHADEMA ikubali kuingia kwenye maridhiano si akaridhiane na hivyo Vyama walivosema ni vingi???😂😂😂😂

Labda tumkumbushe tu Nduli Idd Amin Mama kwamba CHADEMA ni CHAMA CHA WANANCHI WA TANZANIA, IKO MIOYONI MWA WATU.

CHADEMA IMEBEBA MATUMAINI YA WATANZANIA WENGI.

CHADEMA NDO CHAMA PEKEE CHENYE LEGITIMACY KWENYE NCHI HII SO TUTAILINDA LEGITIMACY YETU KWA WIVU MKUBWA.
==============================================
Screenshot_20260317-144537.png
 
Ninaunga mkono hoja lakini kwa nyongeza chache,
1. Hakuna chana kinakosa "Legitimacy" kama ulivyoita ila watu ndio tunakosa Legitimacy.
2. Ninawaunga mkono CHADEMA (hasa T. A. LISSU) kwakuwa wanasumamia mahitaji ya wengi ya watanzania.
3. Hata huko CHADEMA wapo wengi wanakosa Legitimacy, wapo ambao kama wangekuwa Lissu pale alipo basi leo hii tungeongea lugha nyengine kabisa.
4. Hakuna chama kina mfumo na muundo mzuri kuzid CCM ila kutokana na kasumba za waafrika(Ubinafsi) ndio maana kimetufikisha hapa.
 
Samia amsamehe Lissu kwa kosa gani alilofanya Lissu?

Anayepaswa kuomba radhi hapa ni Samia. Aombe radhi kwa kuwaua Watanzania. Halafu baada ya hapo awajibike au awajibishwe.
Kukinukisha na kikanuka kweli
 
Back
Top Bottom