Rais Samia kuongoza maelfu ya Watanzania kumpumzisha Edward Lowassa katika nyumba yake ya milele

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nyota ya matumaini,nuru ya wanyonge na mama wa upendo atawaongoza maelfu ya watanzania katika kumpumzisha Hayati Edward Lowassa waziri Mkuu mstaafu katika nyumba yake ya milele kule Monduli mkoani Arusha.

Kwa sasa Mheshimiwa Rais yupo ulaya ambako anaendelea na ziara za kikazi na kiserikali kwa mialiko maaulum, kutokana na ushirikiano mzuri na mahusiano mazuri ambayo amefanikiwa kuyajenga tangia alipoingia madarakani mwaka 2021,ambapo kwa sasa amekuwa akipata mialiko mingi
sana kutokaa maeneo mbalimbali na pia kutembelewa na wageni mbalimbali wakubwa kutoka mataifa mbalimbali kutoka kila pembe ya Dunia.

Ambapo ni katika ziara hiyo aliweza kukutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa kanisa la katoliki Duniani papa Fransis na baadaye kuelekea nchini Norway ambako nako alipokelewa kwa mapokezi mazito sana na ya heshima kubwa sana yaliyoteka vyombo vyote vya habari vya kimataifa hapa ulimwenguni.

Rais Samia anarejea na kushiriki katika mazishi hayo kwa kutambua mchango mkubwa wa Hayati Edward Lowassa katika Taifa letu na alama alizoziacha zinazoendelea kukumbukwa na watanzania.lakini pia ni Rais Samia Mwenyewe aliyefanya kazi kubwa sana ya kumuuguza Mheshimiwa Lowassa wakati anaumwa. Hata alipokuwa Afrika ya kusini alimuagiza waziri mkuu mheshimiwa kasimu majaliwa kwenda kumfikisha salamu zake na kuwapo pole familia na kuwaahidi kuwa Rais wao na serikali yao ipo pamoja nao.

Ndio maana familia imetoa shukurani za dhati sana na kipekee sana kwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kwa namna alivyopigania maisha na uhai wa hayati Edward lowassa. lakini kwa bahati mbaya ni kuwa kila kitu na wakati wake na wakati wa Mungu ukifika kuitwa basi mwanadamu hawezi kuzuia .wakati wa kuitwa kwa hayati Edward Lowassa kulikuwa kumewadia na kufika na hatimaye ametangulia mbele za haki huku akiacha majonzi na simanzi kwa Taifa zima,huku akililiwa na kuombolezwa na watu wa vyama vyote ,dini zote na rika zote.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
IMG-20240210-WA0047.jpg
IMG-20240210-WA0043.jpg
IMG-20240213-WA0004.jpg
IMG-20240210-WA0044.jpg
IMG-20240213-WA0003.jpg
IMG-20240212-WA0005.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nyota ya matumaini,nuru ya wanyonge na mama wa upendo atawaongoza maelfu ya watanzania katika kumpumzisha Hayati Edward Lowassa waziri Mkuu mstaafu katika nyumba yake ya milele kule Monduli mkoani Arusha.

Kwa sasa Mheshimiwa Rais yupo ulaya ambako anaendelea na ziara za kikazi na kiserikali kwa mualiko maaulum, kutokana na ushirikiano mzuri na mahusiano mazuri ambayo amefanikiwa kuyajenga tangia alipoingia madarakani mwaka 2021,ambapo amekuwa akipata mualiko mingi sana na pia kutembelewa na wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali kutoka kila pembe ya Dunia.

Ambapo ni katika ziara hiyo aliweza kukutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa kanisa la katoliki Duniani papa Fransis na baadaye kuelekea nchini Norway ambako nako alipokelewa kwa mapokezi mazito sana na ya heshima kubwa sana yaliyoteka vyombo vyote vya habari vya kimataifa hapa ulimwenguni.

Rais Samia anarejea na kushiriki katika mazishi hayo kwa kutambua mchango mkubwa wa Hayati Edward Lowassa katika Taifa letu .lakini pia ni Rais Samia Mwenyewe aliyefanya kazi kubwa sana ya kumuuguza Mheshimiwa Lowassa wakati anaumwa. Hata alipokuwa Afrika ya kusini alimuagiza waziri mkuu mheshimiwa kasimu majaliwa kwenda kumfikisha salamu zake na kuwapo pole familia na kuwaahidi kuwa Rais wao na serikali yao ipo pamoja nao.

Ndio maana familia imetoa shukurani za dhati sana na kipekee sana kwa Mheshimiwa Rais kwa namna alivyopigania maisha ya hayati lowassa. lakini kwa bahati mbaya ni kuwa kila kitu na wakati wake na wakati wa Mungu ukifika kuitwa basi mwanadamu hawezi kuzuia .wakati wa kuitwa kwa hayati Edward Lowassa kulikuwa kumewadia na kufika na hatimaye ametangulia mbele za haki huku akiacha majonzi na simanzi kwa Taifa zima,huku akililiwa na kuombolezwa na watu wa vyama vyote ,dini zote na rika zote.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.View attachment 2903941View attachment 2903942View attachment 2903944View attachment 2903945View attachment 2903947View attachment 2903950
Tunachokifahamu sisi wenye akili ni kwamba, CCM ikikusifia sana kwenye msiba wako fahamu kwamba walikuwa chawa wa Ziraili kipindi unaagana na dunia...

Lowassa aliuchukia umaskini sana. Tuliimbishwa sana mabaya yake for the sake of Kikwete asije akaanguka madarakani. Ndo maana uchaguzi wa awamu ya pili ya utawala wake aliamua kuhamishia udhibiti wa kampeni zote kwa familia kwa kigezo kwamba urais ni jambo la kifamilia.... Nakumbuka sana hizi kauli za kipuuzi ambazo zilizalisha zama za aina mmpya ya wizi wa kura...

Lowassa ametangulia lakini ameacha legacy yake inayoishi.
 
CCM Ndio iliyomlea na kumkuza Mh Lowassa na kumpatia kila nafasi iliyotambulisha mbele ya macho ya watanzania katika kuonyesha uwezo wake wa kiuongozi.

CHADEMA chama chako ndio chama kilichokuwa muda wote kinamtupia matusi na kila aina ya kejeli .kwa hakika CHADEMA inapaswa kukaa kimya na siyo kulia lia eti wanataka kuongea msibani.
 
Baada ya kukatwa jina lake. Alienda kujiunga na CUF kugomea urais ambao mkampora ushindi....

Tuishi kwa uongo sasa
 
Edward Ngoyai Lowasa ameondoka. Yuko mahali salama pasipo na mgao wa umeme wala usanii wa treni za umeme. Amepumzika baada ya kazi ngumu. Anapokufa mtu mzito kama Lowassa, kuna makundi matatu hujitokeza;
1. Wanaolia
2. Wanaofurahia
3. Wasiojua kama walie au wafurahie.

Makundi yote matatu tunayo katika kifo cha Edward Lowasa. Mimi sijui nipo kundi gani lakini niseme mambo manne ninayokumbuka:

1. Dola yetu ina mihimili mitatu: Bunge, serikali na mahakama. Lakini Lowassa alisababisha kuzaliwa kwa mihimili mitatu ndani ya mhimili wa bunge:

  • Wa kwanza ni Spika Samwel Sitta
  • Wa pili ni Wabunge mitume wakiongozwa na Mwakyembe
  • Mhimili wa 3 ulikua Edward Lowasa mwenyewe.

Hakika Bunge la 9 halitasahaulika kwa WEMA na UBAYA wake.

2. Alikuwa mtetezi asiye na mtetezi. Alikitetea chama chake, kikamtelekeza. Alimtetea Rais wake akamsaliti. Aliitetea nchi lakini nchi ikawatetea watesi wake.

3. Aliwapenda Wamasai, lakini Watesi wake wakamchonganisha na Wamasai. Wakahoji umasai wake na kudai Lowassa ni Mmeru. Lakini upendo wake kwa Wamasai ukawa na nguvu kuliko fitina za watesi wake. Akiwa hai na akiwa maiti Edward amebaki kuwa Mmasai.

4. Alisalitiwa na wengi aliowasaidia. Baada ya kumtumia kwa maslahi yao na kumtelekeza alibaki na Regina. Tujifunze kujali familia zetu. Mwisho wa yote, mzigo unabebwa na familia. Mambo ya “Pengo halitazibika” ni ulaghai mtupu. Kufa uone watakavyoziba pengo hata kabla ya mazishi.

LOWASSA KATIKA UBINADAMU WAKE:
A. Aliwaamini watu kuliko walivyomuamini.

B. Aliuchukia umaskini kwa vitendo. Watesi wake wakatumia hoja hii kumchonganisha na wananchi maskini. Wakasahau kuwa hata maskini wanauchukia umaskini wao na wanatamani kutoka.

C. Aliamini uzalendo si umaskini. Unaweza kuwa tajiri na ukawa mzalendo.

D. Alitumikia vyama 2 vikubwa. Vikamchafua na kumsafisha. Vikambeza na kumtukuza. Ameondoka akiwa mshindi kwa vyama vyote viwili.

E. Ameishi duniani miaka 70. Lakini Historia yake ni ndefu kuliko miaka yake. Ni mfupi wa umri lakini mrefu wa historia. Nenda Edward. Pole kwa Mama Regina, Watoto na wajukuu.!
 
Back
Top Bottom