Fred Vunja Bei ateuliwa kuwa Mwenyekiti kamati ya Uchumi na fedha UVCCM Taifa

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Mfanyabishara Wa Nguo na Kijana Wa Kikinga Fredy Ngajiro Maarufu Kama Vunjabei ameteuliwa Kuwa M/kiti Wa Kamati Ya Fedha Ya Uvccm... Vijana Tafuteni Njuruku Hakuna Namna

----
Vunja bei.png

Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei jana tarehe 23 May 2021 amepitishwa na Baraza kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio huku katibu wake akifahamika kwa jina la Rose Manumba, Baraza lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na visiwani.
 
Back
Top Bottom