Kongamano la UVCCM Kuelekea Miaka 3 ya Uongozi wa Rais Samia na Miaka 47 ya Kuzaliwa kwa CCM

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

KONGAMANO LA UVCCM KUELEKEA MIAKA 3 YA UONGOZI WA RAIS DOKTA SAMIA NA MIAKA 47 YA KUZALIWA KWA CCM

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wamefanya Kongamano kubwa kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.

Katika Kongamano hilo Makamu wa Rais ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango ndiye alikua mgeni rasmi.

Aidha Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Ali Kawaida alimkabidhi Mhe. Dkt. Philip Mpango Fedha iliyotolewa na UVCCM kwaajili ya kumwezesha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025.

WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.24.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.17.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.16.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.12(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.11.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.25.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 22.06.25(1).jpeg
 
Uvccm wanachowaza ni wizi Tu ukoo wa panya.

Hapo inatafutwa sababu ya kupiga pesa Kwa mgongo wa Samia, eti kokangamano, upuuzi mtupu, sukari bei juu maisha yamekuwa magumu maradufu.
 
Hawa hata hawana vibrant social media, halafu ni vijana, dunia ya sasa iko mitandaoni.

Hata JF taarifa imefika ikiwa imeshakufa
 
Umeme, Maji, Bidhaa Zote Bei Juu Na Hakuna Kiongozi Anayesema Ufumbuzi Ni Upi Wao Wanasema Vita Zaidi Wanawahadaa Wananchi Kwa Khanga, Posho, Na Music Ya Hovyo Hovyo Tu
 
Back
Top Bottom