Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Taifa, iliyokutana katika kikao chake maalum, leo tarehe 1 Oktoba, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Katika kikao hicho, Kamati Kuu imemteua Ndugu Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa UWT, kabla ya uteuzi huo Ndugu Mwegelo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

** Taarifa Kwa Umma ***

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyokutana
katika kikao chake maalum, leo tarehe 1 Oktoba, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Katika kikao hicho, Kamati Kuu kimemteua Ndugu Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa UWT, kabla ya uteuzi huo Ndugu Mwegelo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

Pia, Kamati Kuu imemteua Ndugu Fakii Raphael Lulandala kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, kabla ya uteuzi huo Ndugu Lulandala alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.

Katika hatua nyingine, Kamati Kuu imemteua Ndugu Hamad Khamis Hamad, kuwa mgombea wa CCM wa nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Matembwe.

Aidha, Kamati Kuu imewashukuru na kuwapongeza wanachama wote wa CCM na wananchi kwa ujumla katika Jimbo la Mbarali kwa kumchagua mgombea wa CCM Ndugu Bahati Kenneth Ndingo, kuwa Mbunge wao katika
uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba 20, 2023.

Pia, Kamati Kuu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na ziara aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambayo ilikuwa ya mafanikio makubwa sana . Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine, Rais alikagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za wananchi.

Pia, Kamati Kuu kimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa namna anavyoiongoza serikali katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Sophia Edward Mjema
Katibu Wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

1 Oktoba, 2023

images.jpeg


IMG-20231001-WA0028.jpg
 
Nilishaandika humu jukwaani miezi michache iliyopita juu ya mh jokate mwegelo kuwa ni kiongozi mwenye uwezo,bidii ya kazi,uchapa kazi na maarifa ya uongozi. Na nilipendekeza kuwa uchaguzi ujao achukue Fomu ya ubunge. Kwa hakika namtakia kila la heri mh jokate katika majukumu yake mapya ndani ya chama. Ni kiongozi mchapa kazi sana na kijana mbunifu na mwenye uwezo mkubwa sana kiuongozi
 
Cheo kikubwa sana kwa umri wake

Nazani ndio bosi wa UWT mwenye umri mdogo kuliko wote waliopita.

Ukitaka kujua ukubwa wa hicho cheo

Tazama majina ya ma X katibu wakuu wa UWT yana watu gani ?


Bosi wa UWT hagombei ubunge wa Viti maalum, anapitishwa moja kwa moja na jina lake linapelekwa tume ya uchaguzi (la kwanza). Hivyo jokate anakuwa kiti maalumu wa kwanza wa ccm bungeni 2025.

Pili ni mjumbe wa Kamati kuu (CC) ambayo hufanya maamuzi mazito ya chama. Na faida nyinginezo kadhaa ikiwemo ushawaishi kwa mgombea Urais ajaye............Nafasi hii ni muhimu sana kwa Jokate na Mama Samia kuelekea uchaguzi wa 2025
 
Back
Top Bottom