Dunia nzima vyuo vizuri vya udaktari wa tiba viko attached na hospitali. Kwa sababu udaktari wa tiba ni fani unayosoma nadharia, halafu unaenda kuangalia na kufanya vitu practical. Utasoma kuhusu miili ya watu halafu utatakiwa kuiangalia. Utasoma kuhusu wagonjwa wa magonjwa fulani halafu utatakiwa kuwaangalia.
Sasa UDSM kuna hospitali gani pale?
Labda nimeondoka Tanzania siku nyingi, siku hizi wamejenga hospitali ya viwango vya kufundishia udaktari pale?
Mtu anayeelewa udaktari atajua kwamba, ceteris paribus, Muhimbili au hata Bugando patafundisha udaktari vizuri zaidi ya UDSM. For the simple reason that UDSM doesn't have a hospital, to my knowledge.
Hakuna chuo bora. Kuna chuo bora kwa kitu fulani.
Kuna watu wa technology wanapata nafasi kwenda Harvard wanakataa. Kwa sababu katika technology Harvard si chuo mahiri. Katika technology unaongea MIT, Stanford na vyuo kama hivyo ambavyo havipo hata kwenye Ivy League.
Harvard kiko stronger kwenye business, governance na law.
Sasa kama Harvard kinaonekana kwenye mambo mengine kimepwaya, kuna vyuo havina status ya Ivy League vinakishinda, utasemaje UDSM ni chuo bora zaidi bila hata kuangalia bira katika nyanya gani na kwa nini?
Mimi kama naajiri MD, graduate wa Muhimbili ana advantage over wa UDSM right out the gate.