Alichokileta mtoa mada ni ukweli kwa 100%
Mfano hapo kwenye education, Kuna degree program inaitwa Bed psychology, inatolewa UDSM na UDOM. Kuna tofauti kwa jinsi inavyofundishwa mpaka mtu anapata gamba lake. Ukisoma UDOM ni lazima u-opt masomo mawili ya kufundishia Kama vile kiswahili, math, geog, history, biology n.k. Kama ilivyo kwa BAED na hii inakusaidia kuajirika ktk shule za msingi na sekondari kama walimu wengine.
Ila ukiisoma hii kozi UDSM, Hutakiwi ku-opt masomo ya kufundishia jambo ambalo linapelekea mhitimu kukosa fursa ya kufundishia shule za msingi na sekondari kwa masomo niliyotaja hapo juu.
Mtu huyu wa UDSM hawezi fanya application za ualimu zinazotangazwa mara kwa mara kupitia tamisemi.
Mbaya zaidi ili uajiriwe vyuo vya kati (cheti na diploma) wanaangalia zaidi uzoefu hivyo wanaajiriwa zaidi wale walimu ambao wapo makazini kwa muda fulani. (Sasa huna masomo ya kufundishia utakuje shuleni)
Wengi wa waliomaliza BED PSYCHOLOGY UDSM hawajui hata pakwenda kuomba kazi ingawa wamesoma education.
kwaiyo sio kila kozi ya UDSM ni nzuri au mbaya, zipo nzuri na zipo mbaya. Muhimu mtu kafanya utafiti kwa kila anachotaka kusoma.