KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
Samahani kwa hilo Kaka,
Kwanza sikujua kwamba nina uwezo huo; Pili sikujua kumbe mbali ya kutoa hoja, pia wewe ni moderator na unaona mjadala naupeleka kusipo takiwa; Basi nimekuelewa naacha kuchangia kwenye uzi huu, na naomba wale wote ambao nimewaudhi kwa njia moja ya nyingine mnisamehe; Niwie radhi kaka, ila kumbuka - huu ni mgongano tu wa mawazo, na msukumo wangu sio kitu kingine zaidi ya uchungu juu ya jinsi gani chama chetu kinazidi kupotea, huku sisi vijana tukipigia debe malengo ya wazee ambayo ni ya muda mfupi sana, kwani in 10-15 yrs watakuwa hawapo tena katika siasa za nchi hii na watatuachia chama mfu au chenye migogoro mikubwa zaidi ya hii;
Hoja zangu humu hata kama zitakuwa zimekuudhi, naomba uelewe tu kwamba zililenga kujadili jinsi gani tunaweza kukirudishia chama chetu cha CCM hadhi yake ya zamani kwa kuangalia uhalisia wa mambo (sio ignorance and arrogance just because tumekamata dola), and in the process, mgongano wa mawazo ni jambo la kawaida; Nakuachia mjadala wako kwa moyo safi kabisa;
Na kuhusu wewe kuwa kiongozi wa taifa, mimi sijashindwa bali nimekataa kuwa mtumwa; kaulize;
Kila la Kheri;
Alamsiki;
wewe ni kada wa chama gani labda,maana hata mimi sasa umeanza kunichanganya,mwanzoni nilikua nakuona kama unafanya kazi nzuri ya kukikosoa chama chako wewe mwenyewe kwa nia ya kukijenga kwa kujkifanya kijirekebishe badala ya kuwaachia kazi hiyo wapinzani,lakini sasa unakwenda mbali zaidi na kunifanya nianze kukutazama kwa jicho la tahadhari,pengine unatumika kwa malengo maalum,otherwise vua joho la ccm nenda upinzani tuelewe moja kuliko kuuma uma maneno,ccm sio mamako ulikutana nayo barabarani na unaweza kuachana nayo huko huko kuliko kuendelea kuteseka nayo wakati unaamini haiwezi kusimama tena,nenda kajiunge na timu ya ushindi,tena mungu amekujalia una uwezo mkubwa sana wa kuandika,kupanga maneno na kushawishi,upinzani una safu nyembamba ya uongozi nenda kaongeze nguvu kule ili utupe changamoto sisi wafuasi wa chama mfu lakini kinachpendelea kukubalika na watz