Samahani kwa hilo Kaka,
Kwanza sikujua kwamba nina uwezo huo; Pili sikujua kumbe mbali ya kutoa hoja, pia wewe ni moderator na unaona mjadala naupeleka kusipo takiwa; Basi nimekuelewa naacha kuchangia kwenye uzi huu, na naomba wale wote ambao nimewaudhi kwa njia moja ya nyingine mnisamehe; Niwie radhi kaka, ila kumbuka - huu ni mgongano tu wa mawazo, na msukumo wangu sio kitu kingine zaidi ya uchungu juu ya jinsi gani chama chetu kinazidi kupotea, huku sisi vijana tukipigia debe malengo ya wazee ambayo ni ya muda mfupi sana, kwani in 10-15 yrs watakuwa hawapo tena katika siasa za nchi hii na watatuachia chama mfu au chenye migogoro mikubwa zaidi ya hii;
Hoja zangu humu hata kama zitakuwa zimekuudhi, naomba uelewe tu kwamba zililenga kujadili jinsi gani tunaweza kukirudishia chama chetu cha CCM hadhi yake ya zamani, and in the process, mgongano wa mawazo ni jambo la kawaida; Nakuachia mjadala wako kwa moyo safi kabisa;
Alamsiki;