Hivi Kaka William,
Unajua kwamba chama chetu kimesha meguka ndani kwa ndani siku nyingi na tuna vyama zaidi ya viwili kimtazamo na kimalengo ndani ya CCM? Kinacho kosekana ni usajili wa tendwa; Isitoshe, viongozi wengi ndani ya CCM hawafanya kazi tena kwa mapenzi ya CCM, na hii ni hatari kwani wanasukumwa zaidi na UWOGA, UBINAFSI na UNAFIKI, masuala ambayo mwalimu aliyajadili sana jinsi gani ni tishio kwa uhai wa Chama;
Mimi ni Mwana CCM lakini kwa akili zangu timamu, naelewa kwamba kwa sasa CCM bado ni moja kwa sababu ya System tu, hakuna lingine; Chama kinacholindwa na system ni chama dhaifu;
Ni muhimu tukai sambaratisha CCM sasahivi kama nia yetu ni kuijenga upya, kuliko kusubiri kuja kusambaratishwa na Upinzani, kwani siku hiyo haipo mbali;
Hoja yako ya kutetea Chama chenye kansa ya kiungo ni hoja mfu kwani unachofanya ni kutetea na kuwa mtiifu kwa chama kwa mujibu wa katiba, sio kwa mujibu wa uhalisia wa soko la Siasa; Kaka, Kansa imesha sambaa, tukate tu hicho kiungo na tuanze maisha mapya;
- Well, Brother nimekuwa ninakusoma kwa muda kidogo sasa, sina uhakika of what is your mission hapa JF maana wengine wote unaowaona humu wana mission, wengi wao ni wapambe wa Chadema wanaotaka kutuvuruga CCM at any cost. For you to say kwamba CCM imemeguka ni absolutely over reaching! mimi nilikuwepo Dodoma majuzi kwenye Mkutano wetu mkuu nimegombea NEC viti 10 na kupata kura 800 na kushika nafasi ya 12, kama kweli CCM ingekuwa imemeguka no way ningeweza kupata kura zote hizo!! kati ya kura 2,000!
- Sijui ni System gani unayoisema ambayo sio ya CCM, kwamba CCM tunaweza kusambaratishwa na Upinzani sijui ni Upinzani upi huo, maana nonaujua majuzi tu wamepigwa chini kwenye Udiwani na CCM, makundi ndani ya chama cha siasa ni kawaida sana, Tanzania tulichelewa sana kuwa nayo kwa sababu ya kutawaliwa na chama kimoja kwa muda mrefu sana, brother kumbuka maneno ya Mwenyekiti Mao, aliposema "Ukiona watu wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kila wakati ujue kwamba mmoja wao ni mgonjwa au wote wawili ni wagonjwa" so it is ok kwa CCM kuwa na makundi kwa sababu hata Democrats kule US wanayo makundi so are Republicans!!
- Sina uhakika na maelezo yako umefanyia wapi huo utafiiti, lakini binasfi ninaamini sana CCM, infact kama itaweza ku-maintain hii hype ya sasa, Wapinzani watakuwa na wakati mgumu sana 2015, infact ninasema hivi Wapinzani hawatashinda 2015, matokeo ni kwamba Chama cha wasi wasi kama Chadema kwa kukosa Urais, kitakufa kifo cha panzi!! Kwamba CCM ina kansa? hapana kumbe hujajua kwamba kansa ipo Chadema, kati ya Mbowe, Slaa na Zitto!
- Halafu unapaswa kujua kwamba Chadema hawana mgomea imara wa Urais 2015, sasa watashindaje CCM iko vizuri sana wakorofi kina Mgeja umeona walivyoshugulikiwa na CC sasa hivi adabu mbele, waliotaka kupiga kura za maruhani ndio kabisaa yaani huzuni hata kusema, please brother naona na wewe unajaribu kuwa na mkono kwenye nyama na kwenye kunde CCM hatuhitaji wanachama kama wasio na msimamo kama wewe, kama umeona maji yamekushinda CCM nenda kwa usalama tu lakini wewe mtu mmoja huwaongelei wana CCM wote Millioni Tano!!
- KIDUMU CCM!!
Le Mutuz!!