Nashukuru kwa kunirekebisha juu ya generalization ya viongozi; ni kweli, sio viongozi wote wana matatizo, lakini matumizi yangu yalilenga zaidi katika kujenga hoja juu ya uwoga wa kufanya maamuzi magumu ya kukiokoa chama, nje ya kuhimiza kila mtu arudi kundini; Pia sikubaliani na mwenyekiti aliposema kwamba nje ya makundi ya Urais, CCM ni chama imara na hakina matatizo yoyote makubwa; Ukweli ni kwamba CCM has lost its political hegemony, hence legitimacy kwa miaka zaidi ya 20 sasa na hata Kolimba alizungumzia hili tena wakati ambao hapakuwa na makundi yoyote;
Kuhusu kuisambaratisha CCM mapema kuliko kusubiria isambaratishwe na upinzani - maana yangu ya msingi ni kwamba leo hii CCM bado ni moja sio kwa sababu ya wanachama na viongozi kushiba imani, bali ni kutokana na woga unaowatawala - aidha wengi sio safi na wanaogopa kuumbuliwa watakapoamua kufanya maamuzi magumu, wengi wapo kimaslahi zaidi, na pia wengi hawaoni agenda ya kufanya maamuzi magumu itakuwa ni ipi nje ya ufisadi wakati ukweli ni kwamba agenda zipo nyingi sana na nilizijadili katika uzi wangu mwingine 'Mangula, Kinana na hatima ya Taifa Letu';
Wapo wachache wenye uelewa kwamba CCM haiwezi kujisahihisha bila ya kuvunjika lakini tunarudi pale pale - uwoga ambao unatawaliwa na siasa za ANZA WEWE;
Naomba nikusumbue kwa kusoma kidogo maneno ya Mwalimu kisha tusaidiane kujadili iwapo CCM inaweza kujisahihisha bila ya kumeguka:
Miaka karibia 50 iliyopita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitoa kitabu chake cha "TUJISAHIHISHE" (May 1962).
Mwalimu Nyerere, Tujisahihishe, kurasa 1- 4, May 1962.