Nimekuwa mwanachama wa JF kwa miaka sita sasa na kabla ya hapo nilikuwa mwanachama wa Jamboforums; Na kote huku kuwili, wakati wa kujiunga, sikuwahi kukutana na kipengele kinachouliza MISSION YAKO KAMA MWANACHAMA NI NINI; Vinginevyo kwa uelewa wangu, huu ni uwanja wa kubadilishana mawazo na kupimana kwa hoja, kwa kujenga na kwa maslahi ya taifa letu, na ni hivyo ndivyo nimekuwa nafanya kwa miaka sita;
Kwa kauli hii, basi kumbe mission yako ni kuja kupambana na hoja za Chadema; Sasa nimekusoma; Naomba ujue kwamba mimi sio mwenzako katika hilo, badala yake nipo humu kubadilishana mawazo na wana chadema, wana ccm, wana CUF, NCCR n.k kwa manufaa ya taifa, na ikitokea tunapishana, mgongano wa mawazo ni suala la kawaida towards that end;
Kwa hili naishiwa hata nguvu ya kukujibu kwani hata mwenyekiti taifa amelizungumzia hili i.e. makundi; kama hauoni factions ndani ya CCM ya sasa na haukubaliani na mimi katika hili, basi mimi na wewe tunaishi dunia mbili tofauti kabisa; Vinginevyo unaweza kuwa sahihi na mtazamo wako, lakini nitaendelea kupingana na mtazamo huo;
Yani hiki ndio kipimo chako rasmi on whether CCM imemeguka au haijameguka? No wonder tunapishana mtazamo;
Ingekuwa sio ya CCM isingeisaidia CCM;
Tuwe tuna chambua na matokeo, itatusaidia sana; Tumeshinda kata nyingi, pengine four times ya idadi ya kata walizoshinda Chadema lakini jumla ya idadi ya kura picha ni tofauti kabisa; hii inatuambia nini? Kura zetu CCM nyingi ni vijijini, Chadema ni Mijini; Na mwelekeo wa dunia ni urbanization ambapo ifikapo 2025, over 50% ya wakazi wa Africa, Tanzania ikiwemo watakuwa in urban areas; Are we investing for the future? Kwanini tunapoteza mvuto mijini? hazina yetu vijijini ni suala la muda tu;
Ninachozungumzia mimi ni FACTIONS within the party ambazo mara kwa mara kumekuwa na jitihada za kuzikutanisha kama njia ya kuokoa chama kisipasuke; Factions sio jambo jema kwa uhai wa chama, whether kuna chama kimoja au vyama mia moja ndani ya demokrasia husika;
One British Conservative - Enoch Powell (1912) alipata nena kwamba: A Party... is not a faction or club of individuals who associate for mutual assistance in acquiring and retaining office; It is a body of persons who hold, advocate and desire to bring into effect certain political principles and policies".
Huyo Mao, na pia mifano yako juu ya Democrats na Republicans wanaongelea on the later, sio the former; Sisi tupo kwenye the former na ndio hoja yangu ya msingi katika hili;
Sijafanya any scientific research zaidi ya kuwa observant wa maendeleo mbalimbali hasa huku site; wewe je, kuna research umefanya?
Ni vizuri kwamba umeweka a conditionality on this one i.e. kama itaweza..., na hii ni tofauti na hoja yako ya msingi kwenye bandiko namba moja; vinginevyo ushindi wetu sio straight forward tena kama zamani, na ndio maana Mwenyekiti ameona kuna utofauti kati ya Mukama na Kinana au Makamba na Kinana;
Hii kauli kidogo inatoka so authoritative, kana kwamba ushindi wa CCM sio lazima upitie sanduku la kura;
Chadema ina kansa na sio CCM? Tukiendelea kulikataa hili, tutakuja aibika vibaya sana siku ya siku; Chadema is experiencing growth and increase in popularity kwa sababu ya madhaifu yetu CCM, na hata mwenyekiti kalisemea hilo; Wewe unaita hiyo ni Kansa?
Kipimo cha Uimara ni nini? Sisi mgombea wetu ni yupi imara wa kuweza kukabiliana na nguvu ya Chadema ambayo sio ya dola bali ya UMMA? Tunamjua mgombea huyo? Tunamuandaa au tutampiga majungu hata kama ndiye angekuwa chaguo sahihi? I hope tutaachia nguvu za soko zitupatie mgombea imara kutoka CCM;
Mwenyewe unaanza kukubaliana na mimi kuhusu makundi ndani ya CCM ambayo hayana tija ingawa hapo awali ulileta hoja za Mao na Vyama vya marekani kwamba hivi ni vitu vya kawaida;
Hizi ndio kauli zenu CCM hata ngazi za juu, na mnajisahau kwamba milioni tano ilianza na moja; mtaendelea kupoteza watu wengi kwa kutokuwa tayari kusoma alama za nyakati; Vinginevyo hauna mamlaka ya kuniambia niende wapi kutumia haki yangu ya kikatiba katika masuala ya siasa; Lakini kama una mkono huko sijui wapi wa kuniondoa uanachama, na iwe hivyo; Mpaka muda huo ufike, rudi kwenye mwongozo wetu wa CCM (1982) ambao unasema hivi:
Ibara ya ( 5) Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi
58. Kuna mambo mawili tuliyojifunza ambayo ni muhimu pia kuyazingatia. La kwanza linahusu suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana kama njia ya kukijenga na kukiimarisha Chama na wanachama. Ni kweli kuwa katika TUJISAHIHISHE Mwalimu anasisitiza jambo hili na kwamba Katiba ya CCM inatamka waziwazi juu ya umuhimu wake. Lakini ni kweli pia kuwa hatujaijenga tabia hii ipasavyo. Mara nyingi tumependelea kuteteana, kufichiana makosa na hata kutafuta visingizio visivyo na msingi. Neno kuleana, kwetu sisi (ingawa kuna malezi mema na mabaya) limechukua nafasi ya kukosoana. Wanachama wenye upungufu husaidiwa kama wanakosolewa ili wajirekebishe...
59. Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana lina sura kadhaa. Kwanza linataka wanachama na viongozi kuwa tayari kusema kweli katika vitendo vyao na kukubali kuambizana ukweli. Pili, linataka wanachama na hasa viongozi wawe tayari kukosolewa bila kuhamaki na inapobidi kukubali kujirekebisha. Tatu ni kuwa Chama chenyewe katika vikao vyake vya ngazi mbalimbali kuwa na utaratibu wa kujikosoa.
Matumaini yangu ni TUTADUMU unconditionally i.e. hata tukiwa chama cha upinzani bila ya kuwa na dola mikononi; in fact, kwa mtazamo wangu, tukianguka 2015 ndio tutajua ukweli kina nani wanakipenda chama kwa dhati na nani walikuwa wanatafuta tu maisha ya mkato mkato; Kaka, Je, ikitokea tumeanguka 2015 utaendelea kuwa mwanachama wa CCM? I hope jibu lako halitajirudia tena kwamba 'infact ninasema hivi Wapinzani hawatashinda 2015';