FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Samahanini Sana Jamaniii nilikuwa safari ndio naingia mjini Sasa hivi, nasikia Kuna msiba mzito Sana umetokea humu oohh poleni sana,

Nani anapokea rambirambi pls??

PNC 1 au mwekundu au jackline??

Maziko lini jamani ?? Wekeni namba za Mpesa, tigopesa n.k

Mkuu Iceman 3D umeshatoa rambirambi??

Qwiqwiqwiqwiqwiqwi ngoja nikacheekee chooni!
Hakuna mtu aliefiwa humu, zaidi nasikia kabakwa tu!
 
swala la suarez nina imani hata gardiola hasingeweza kumvumilia amekuwa flop kwa sasa anafunga kiunjanja ujanja maana amekuwa kama namba tisa ya kizamani anasubiri kupewa afunge.....huyu mwalimu nae wa timu ndogo toka mwanzo unaona kabisa upande wa semedo na roberto unapwaya lenyewe linataka timu ikae nyuma tu.....matokeo yake tunapata aibu
 
1523395990727.jpg
 
Roma imefanya maajabu baada ya kuwabamiza Barcelona 3-0 na hivyo kutinga nusu fainali za mabingwa Ulaya kwa faida ya goli la ugenini.
Barca walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na kuingia uwanjani wakiwa na akiba ya magoli, ambapo kutokana na mechi ya kwanza waliyoipiga Roma bao 4-1, Roma ilikuwa inalazimika kuifunga Barcelona 3-0.
Goli la Edin Dzeko dakika za awali za mchezo (6'), na Penalty ya Daniele de Rossi katika kipindi cha pili dakika ya 58 yamekamilishwa na Goli la Mlinzi Kostas Manolas alilofunga zikiwa zimesalia dakika nane tu mechi kufikia mwisho zimewafanya Barcelona pamoja nakuwa na Lionell Messi ambaye hakufurukuta, kuondokakichwa chini katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Umati uliokuwepo Stadio Olimpico ulilipuka mara baada ya kipyenga cha mwisho pale wachezaji wa akiba wa Roma na benchi lao la ufundi walipoingia katikati ya uwanja kushangilia na wachezaji wao.
Kulikuwa na machozi katika nyuso za mashabiki wasiamini kile walichokishuhudia katika mtanange huo ambao haukutegemewa kuisha ulivyoisha.
Roma imekuwa timu ya tatu katika Champions League kuweza kuyapindua matokeo ya namna hiyo ya goli tatu au zaidi. Timu pekee mbili ambazo awali ziliwahi kufanya hivyo ni Deportivo La Coruna dhidi ya AC Milan mwaka 2004 na Barcelona dhidi ya Paris St-Germain msimu uliopita.
 
Mashabiki wa barca wanashangaza kweli,kitendo cha messi kuwa genius wa mpira na timu kucheza vyema basi wanadhani wao ndio wanajua kuuchambua mpira kuliko mashabiki wa timu nyingine.
Poleni wakuu,hata mie nimeumia kwa ajili ya LM10.
 
hivi ndivyo huwa ukiamua kucheza game ya kujilinda. Napenda huyu kocha awe sacked. Huwezi wachezesha game ya kujilinda watu waliozoea kuattack miaka na miaka.
Ndio tulokua tunamsifu kua nibora kuliko makocha kama pep kwasababu kaweza kutuliza eneo la ulinzi, kumbe tulikua hatujakutana na watu wenye njaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom