Mkuu wewe huzungumzi uhalisia ila unazungumza kimahaba, yaani kama vijana wa teenager wakikutana na kutambiana, kila mmoja anajisifu kuwa demu wake mkali, turudi kwenye mada.
Kusema kwamba Barca kaifunga Madrid wakiwa ni wabovu utakuwa unakosea sana, Messi kuwafunga Madrid hakutegemei na ubovu wa Madrid, Madrid sio timu mbovu tangu msimu kuanza mpaka sasa, timu kuwa mbovu unazungumzia kama Arsenal, Man U n.k rejea mwaka ambao Barca anafungwa na Madrid Camp Nou, mwaka huohuo Barca alichukua treble, Madrid hakuambulia kitu, je kama alikuwa on form angetoka kapa? Angemfunga Barca Camp Nou kipindi ambacho MSN ikiwa ni moto zaidi? Hizi timu zikikutana uwanjani ni tofauti na Derby ya Man U v Man City. Hawa wanacheza mpira haswaaaaaaa, ni ufundi ndio unatoa matokeo, period.
Eti Buffon alifungwa na Messi akiwa ameshaanza kuchoka, unataka Messi adhihirishe ubora wake kumfunga nani? Manuel Neur kipindi ananyooshwa kwapa na Messi si ndo alikuwa Goal Keeper bora zaidi duniani? Almunia alikuwa mbaya? Iker Casillas je? Makipa wapo wengi tu ambao wamefungwa na Messi wakiwa ktk ubora wao.
Ila ntakuona mshamba wa mpira kama unaamini kwamba magoli aliyofungwa Buffon na Messi ni uzembe wa kipamba, utakuwa ni mjinga wa hali ya juu. Kuna nafasi ambazo mchezaji kama Neymar, Messi, Ronaldo au Suarez hawawezi kumuacha kipa yoyote yule duniani. Unatazama kipa tu ila hutazami viwango vya wachezaji ktk umakini wao wa kufunga sana sana Messi na Ronaldo.