Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,615
- 40,165
Wizara ya Elimu nchini Ethiopia imetoa Mwongozo mpya unaopiga marufuku Viongozi wa Serikali na viongozi wa Kisiasa nchini humo kutunukiwa Shahada za Heshima (Honorary Doctorate).
Agizo hilo ambalo limetiwa saini na Waziri wa Elimu Nchini Ethiopia Profesa Berhanu Nega kuwasilishwa kwa Vyuo vikuu na taasisi za Elimu nchini humo limezitaka taasisi hizo hususa ni Vyuo ambavyo Wanafunzi wake hawajahitimu angalau awamu nne na havitoi Shahada ya Uzamilivu havitoruhusia kutokoa shahada ya Heshima.
Mwongozo pia unaeleza kuwa Shahada za Heshima zinaweza kutolewa kwa raia wa Ethiopia au Wageni waliotoa mchango wa kipekee katika taaluma au nyanja zao za kazi. Tuzo hiyo inaweza kutolewa kwa mtu mmoja au kikundi kilicho hai au kilichofariki, mradi kimekidhi vigezo vilivyowekwa.
Aidha kuna masharti ya vizuizi Kifungu cha 2 Ibara ya 10 kimeeleza kuwa wafanyakazi wa kudumu wa vyuo vikuu, wajumbe wa Seneti au miundo ya uongozi hawawezi kupokea shahada ya heshima wakati bado wako kazini, isipokuwa pale ambapo uhusiano wao rasmi na chuo hicho umeisha na pia viongozi wa serikali walioko madarakani hawataruhusiwa kuteuliwa kabisa.
Sambamba na hilo kwa mujibu wa masharti ya mwongozo huo chuo kikuu kitakachotoa shahada ya heshima kinapaswa kuwa kimehitimisha angalau wanafunzi wa awamu nane, kinatoa kozi ya PhD, kinakubalika kwa viwango vya kitaifa na kimataifa na kutokana na masharti haya, vyuo vipya kama vile Selale, Dembi Dolo, Mekdela Amba, Raya, na Debarak havitaruhusiwa kwa sasa kutoa shahada za heshima.
Source Millard Ayo