Eminem alimchana sana Mama yake kwenye hii ngoma ya 'Cleanin Out My Closet' akionesha Dunia chuki ya wazi kwa Bi Mkubwa ambaye alikuwa mzinguaji enzi

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Wakati Dr. Dre anapelekewa Eminem ili amsaini, alimshangaa, hakuwa akiamini kama Mzungu huyo angeweza kuchana kama watu weusi lakini alipomsikiliza, sasa akawa na uhakika alimpata mwamba, mtu aliyekuja kuwa na ukubwa usio wa kawaida.

Huyu Eminem hakuwa na mahusiano mazuri na mama yake kama wanamziki wengi tunaowafahamu ambao uwa na uhusiano mzuri na mama zao kiasi cha kutowaambia lolote mbele ya mam zao, kwa huyu wamba Eminem ilikuwa tofauti sana, alimchukia kwa kuwa alimtesa sana utotoni mwake, anaweza kukwambia miongoni mwa watu waliotakiwa kufa kipindi hicho alikuwa mama yake.

Huyu maza alimtesa sana, tena sana, alimfanya mpaka kuwa na hasira sana. Sema kuna kipindi alijirudi ila baadaye maza alipozingua tena, akamwambia usinijuejue kabisa.

Okay! Tuje kwenye ngoma yake ya Cleanin‘ Out My Closet. Kwanza hilo jina lenyewe, huo ni msemo kama misemo yetu ya Kiswahili, una maana ya kutoa maneno yako ya ndani. Yaani mtu alikukera, sasa unaamua kutoa nyongo yako.

Kwenye korasi yake anamuomba msamaha mama yake, anamwambia sina lengo la kukuumiza ila leo, acha niteme nyongo tu ili niwe na furaha.

Anaanza kwa kutuuliza maswali, jamani hivi mshawahi kuteswa ama kunyanyaswa kama yeye? Anaanza kufunguka kwa yale yaliyotokea baina yake na mama yake.

Verse hiyo ya kwanza hakuanza kumchana, kwanza anazungumza na sisi, anatuweka sawa kwamba kwa kile atakachokwenda kukiongea, tumuelewe tu kwani ndiyo maisha aliyopitia.

Alipokuja verse ya pili, sasa akaanza kuzungumzia maisha yake hayo. Kwanza akatupa msemo kuhusu yeye kwamba yupo ndani ya kabati la nguo halafu humo ndani kuna mifupa ya binadamu, yaani alikuwa akiishi hivyo ila hakuna anayejua, sasa leo kabla ya kutupwa ndani ya jeneza na kulifunga, hebu tukae na kumsikiliza kilichotokea.

Akaturudisha mwaka 73. Anasema kipindi hicho mama na baba yake walikuwa wapumbavu tu, hawakumpa maisha ambayo wazazi walitakiwa kumpa. Walimuweka kwenye hali iliyompa mawazo kila wakati.

Yaani kwa kifupi alijua kabisa wazazi wangu wananichukia sana. Kwa chuki alizokuwa akizipitia, alitamani hata kuwaona wakifa, yaani waondoke tu duniani halafu maisha yake yatakuwaje? Atajua mbele ya safari.

Anaendelea kufunguka kwenye verse hiyo ya pili kwamba hawezi kuruhusu mtoto wake, Hailie aishi kama maisha aliyoishi, anasema hata alipokuwa na mkewe, Kim, alikuwa anamletea ujinga mwingi ila aliuma meno kwa ajili ya binti yake.

Yaani alivumilia yote hayo kwa ajili ya binti yake ili aje kuwa na maisha mazuri, asione wazazi wake wakiwa wanagombana na kumchukia kama ilivyotokea kwake.

Anakiri kwamba inawezekana alifanya makosa kama binadamu, lakini leo hii angeweza kusimama na kusema makosa yake, labda ndiyo yaliyopelekea kuchukiwa na wazazi wake mpaka mkewe.

Anasema alichokifanya kilikuwa ni ujinga, labda unaweza kuwa ni ukichaa lakini kitu cha maana alichokifanya wakati huo ni kutoa risasi ndani ya bunduki kwani vinginevyo angewafyatulia wote wawili. Yaani Kim na mwanaume aliyekuwa akiishi naye.

Why?

Mara ya kwanza Hailie alikuwa akiishi na mama yake, Kim ila maisha aliyokuwa akiishi, Eminem hakuwa akiyapenda, ila alikuwa hana cha kufanya kwa kuwa hakuwa na kitu.

So mchizi alianza kupambana kwa ajili ya maisha yake na ya mtoto wake. Alikuwa na hamu ya kumtoa kwa mama yake, asipate manyanyaso kama aliyoyapata, ila hana kitu, angefanyaje?

Ndiyo maana alipopata nafasi kwa Dre, akaona ni muda wa kumchukua mtoto wake na kuishi naye. Kuna kipindi alikosa mpaka kushiriki usiku wa kupokea tuzo za Grammy, na alishinda, ila alitoa udhuru kwamba asingeweza kwenda kwa kuwa anataka kubaki na mwanaye (What a dad).

Anaingia verese ya tatu.

Anasema asingetoa ngoma ya kumdiss mama yake mzazi ila anatuambia hebu isikilizeni vizuri hii ngoma, ni kweli nimemdiss mama ama nimezungumza ukweli? Halafu anatuambia hebu wewe chukua nafasi yangu, yaani vaa viatu vyangu ungefanyaje?

Anasema mama yake alikuwa akitumia madawa, halafu alikuwa akiyafanya hayo mbele yake. Na kila alipokuwa akienda kuangalia kitu kwenye mkoba wake, hamukuwa na kitu.

Yaani mama yake alihusudu sana madawa kumliko kumwangalia yeye. Wao walikuwa watu wa kupanga tu, anasema kuna kipindi mpaka akahisi yeye Eminem alikuwa na ugonjwa wa akili kwa yale aliyokuwa akipitia.

Anamwambia alikuwa hivyo mpaka alipokua, na sasa anahisi mama yake atakuwa na maumivu makubwa ya tumbo kila anapomuona amekuwa msanii mkubwa.

Anasema mama yake alitengeneza cd aliyokuwa akimfanyia mambo mazuri tu, alitaka kumuaminisha kwamba alikuwa mama bora, asiyekuwa na tatizo na wakati wakati anayafanya yote hayo, Eminem alikuwa na akili zake.

Anamwambia sasa hivi unazeeka na najua unajisikia sana baridi, na una upweke wa hali ya juu. Hayo hakuwa akiyapitia peke yake bali hata ndugu yake aliyeitwa Nathan.

Huyu Nathan wamechangia mama ila baba tofauti. Anamwambia mama yake cheki now Nathan anavyokua na kupiga michongo yake huku akijua mama ni mnafiki, yaani anajifanya kutupenda na wakati alituchukia.

Huyu Nathan kwa sasa yupo kwenye industry ya muziki anafanya kazi kama DJ na music producer. Na pia ni muigizaji.

Anamwambia hata mtoto wake, Hailie anakua mkubwa sasa, ila hutoweza kukutana naye maisha yake yote, na hatoweza kuwa kwenye mazishi yako utakapokufa.

Anaendelea kumwambia kwamba kinachomkera kwake ni kwamba hakukubali yote mabaya aliyoyafanya, yaani hakuadmit kwamba alikosea.

Anamwambia B*tch nenda katengeneze na wewe ngoma yako uwaambie watu kwamba ulikuwa mama bora kwetu. Anasema yaani nakuombea wewe mwanamke uende jehanamu na kuunguzwa na moto milele.

Anamkumbusha, unakumbuka Ronnie alipofariki? Huyu alikuwa mjomba ake na Eminem. Anasema alipofariki mjomba Ronnie ukasema ulitamani kuona mimi ndiye nimekufa. Sasa nakwambia hiviiiii....Nimekufa kama ambavyo wewe tayari umekufa kwangu.

Huyu jamaa wa kuitwa Eminem kuna kipindi alikuwa anafanya kazi nne kwa siku ili tu awe anamlipia mama yake bills ndani ya nyumba. Akawa anaishi humo home ila baadaye akafukuzwa, akaona poa, akachukua kila kitu akasepa, akataka alipwe gharama zake zote alizotumia, akalipwa nusu. Akaanza kujitafuta mitaani. Akakutana na Kim, akampa mimba😀

Oyaa! Mwamba alipambana sana.

So alikuwa na kinyongo na mama yake kitambo.
Ila back then, mama yake nusu afe wakati anajifungua Eminem.
Yaani alikaa leba kwa masaa 79, dakika za mwisho madaktari wakaokoa maisha yake. Madawa yalimuendesha.

Eminem alianza kuwaambia waandishi kuhusu mama yake. Ila baadaye akasema hizi pesa ninazozipata acha nimwandike mama yangu manake wanawake hawaaminiki. Alitaka afanye kama Hakimi.

Wakati akiwa anakamilisha taratibu, mama yake akampeleka mahakamani na kumtaka amlipe dola milioni 10.
Yaani aliyetaka ampe umiliki wa pesa zake kaenda mahakamani kutaka alipwe hela kisa katukanwa sana😀
Eminem akaona haiwezekani.

Akachana makaratasi. Bifu likakolea. Mama yake alifariki kwa cancer ya mapafu.
Si unajua ukivuta sigara, bangi na pombe ugonjwa gani utakuua? ndivyo ilivyotokea.
Alifariki akiwa na miaka 69.

Hii ngoma nimeisikiliza leo kila mstari...daaah! Halafu wapwa wakampa tuzo kwa kutoa ngoma kali.

View: https://youtu.be/RQ9_TKayu9s?si=ZMXfh42KmSM5hz5M
 
Wakati Dr. Dre anapelekewa Eminem ili amsaini, alimshangaa, hakuwa akiamini kama Mzungu huyo angeweza kuchana kama watu weusi lakini alipomsikiliza, sasa akawa na uhakika alimpata mwamba, mtu aliyekuja kuwa na ukubwa usio wa kawaida.

Huyu Eminem hakuwa na mahusiano mazuri na mama yake kama wanamziki wengi tunaowafahamu ambao uwa na uhusiano mzuri na mama zao kiasi cha kutowaambia lolote mbele ya mam zao, kwa huyu wamba Eminem ilikuwa tofauti sana, alimchukia kwa kuwa alimtesa sana utotoni mwake, anaweza kukwambia miongoni mwa watu waliotakiwa kufa kipindi hicho alikuwa mama yake.

Huyu maza alimtesa sana, tena sana, alimfanya mpaka kuwa na hasira sana. Sema kuna kipindi alijirudi ila baadaye maza alipozingua tena, akamwambia usinijuejue kabisa.

Okay! Tuje kwenye ngoma yake ya Cleanin‘ Out My Closet. Kwanza hilo jina lenyewe, huo ni msemo kama misemo yetu ya Kiswahili, una maana ya kutoa maneno yako ya ndani. Yaani mtu alikukera, sasa unaamua kutoa nyongo yako.

Kwenye korasi yake anamuomba msamaha mama yake, anamwambia sina lengo la kukuumiza ila leo, acha niteme nyongo tu ili niwe na furaha.

Anaanza kwa kutuuliza maswali, jamani hivi mshawahi kuteswa ama kunyanyaswa kama yeye? Anaanza kufunguka kwa yale yaliyotokea baina yake na mama yake.

Verse hiyo ya kwanza hakuanza kumchana, kwanza anazungumza na sisi, anatuweka sawa kwamba kwa kile atakachokwenda kukiongea, tumuelewe tu kwani ndiyo maisha aliyopitia.

Alipokuja verse ya pili, sasa akaanza kuzungumzia maisha yake hayo. Kwanza akatupa msemo kuhusu yeye kwamba yupo ndani ya kabati la nguo halafu humo ndani kuna mifupa ya binadamu, yaani alikuwa akiishi hivyo ila hakuna anayejua, sasa leo kabla ya kutupwa ndani ya jeneza na kulifunga, hebu tukae na kumsikiliza kilichotokea.

Akaturudisha mwaka 73. Anasema kipindi hicho mama na baba yake walikuwa wapumbavu tu, hawakumpa maisha ambayo wazazi walitakiwa kumpa. Walimuweka kwenye hali iliyompa mawazo kila wakati.

Yaani kwa kifupi alijua kabisa wazazi wangu wananichukia sana. Kwa chuki alizokuwa akizipitia, alitamani hata kuwaona wakifa, yaani waondoke tu duniani halafu maisha yake yatakuwaje? Atajua mbele ya safari.

Anaendelea kufunguka kwenye verse hiyo ya pili kwamba hawezi kuruhusu mtoto wake, Hailie aishi kama maisha aliyoishi, anasema hata alipokuwa na mkewe, Kim, alikuwa anamletea ujinga mwingi ila aliuma meno kwa ajili ya binti yake.

Yaani alivumilia yote hayo kwa ajili ya binti yake ili aje kuwa na maisha mazuri, asione wazazi wake wakiwa wanagombana na kumchukia kama ilivyotokea kwake.

Anakiri kwamba inawezekana alifanya makosa kama binadamu, lakini leo hii angeweza kusimama na kusema makosa yake, labda ndiyo yaliyopelekea kuchukiwa na wazazi wake mpaka mkewe.

Anasema alichokifanya kilikuwa ni ujinga, labda unaweza kuwa ni ukichaa lakini kitu cha maana alichokifanya wakati huo ni kutoa risasi ndani ya bunduki kwani vinginevyo angewafyatulia wote wawili. Yaani Kim na mwanaume aliyekuwa akiishi naye.

Why?

Mara ya kwanza Hailie alikuwa akiishi na mama yake, Kim ila maisha aliyokuwa akiishi, Eminem hakuwa akiyapenda, ila alikuwa hana cha kufanya kwa kuwa hakuwa na kitu.

So mchizi alianza kupambana kwa ajili ya maisha yake na ya mtoto wake. Alikuwa na hamu ya kumtoa kwa mama yake, asipate manyanyaso kama aliyoyapata, ila hana kitu, angefanyaje?

Ndiyo maana alipopata nafasi kwa Dre, akaona ni muda wa kumchukua mtoto wake na kuishi naye. Kuna kipindi alikosa mpaka kushiriki usiku wa kupokea tuzo za Grammy, na alishinda, ila alitoa udhuru kwamba asingeweza kwenda kwa kuwa anataka kubaki na mwanaye (What a dad).

Anaingia verese ya tatu.

Anasema asingetoa ngoma ya kumdiss mama yake mzazi ila anatuambia hebu isikilizeni vizuri hii ngoma, ni kweli nimemdiss mama ama nimezungumza ukweli? Halafu anatuambia hebu wewe chukua nafasi yangu, yaani vaa viatu vyangu ungefanyaje?

Anasema mama yake alikuwa akitumia madawa, halafu alikuwa akiyafanya hayo mbele yake. Na kila alipokuwa akienda kuangalia kitu kwenye mkoba wake, hamukuwa na kitu.

Yaani mama yake alihusudu sana madawa kumliko kumwangalia yeye. Wao walikuwa watu wa kupanga tu, anasema kuna kipindi mpaka akahisi yeye Eminem alikuwa na ugonjwa wa akili kwa yale aliyokuwa akipitia.

Anamwambia alikuwa hivyo mpaka alipokua, na sasa anahisi mama yake atakuwa na maumivu makubwa ya tumbo kila anapomuona amekuwa msanii mkubwa.

Anasema mama yake alitengeneza cd aliyokuwa akimfanyia mambo mazuri tu, alitaka kumuaminisha kwamba alikuwa mama bora, asiyekuwa na tatizo na wakati wakati anayafanya yote hayo, Eminem alikuwa na akili zake.

Anamwambia sasa hivi unazeeka na najua unajisikia sana baridi, na una upweke wa hali ya juu. Hayo hakuwa akiyapitia peke yake bali hata ndugu yake aliyeitwa Nathan.

Huyu Nathan wamechangia mama ila baba tofauti. Anamwambia mama yake cheki now Nathan anavyokua na kupiga michongo yake huku akijua mama ni mnafiki, yaani anajifanya kutupenda na wakati alituchukia.

Huyu Nathan kwa sasa yupo kwenye industry ya muziki anafanya kazi kama DJ na music producer. Na pia ni muigizaji.

Anamwambia hata mtoto wake, Hailie anakua mkubwa sasa, ila hutoweza kukutana naye maisha yake yote, na hatoweza kuwa kwenye mazishi yako utakapokufa.

Anaendelea kumwambia kwamba kinachomkera kwake ni kwamba hakukubali yote mabaya aliyoyafanya, yaani hakuadmit kwamba alikosea.

Anamwambia B*tch nenda katengeneze na wewe ngoma yako uwaambie watu kwamba ulikuwa mama bora kwetu. Anasema yaani nakuombea wewe mwanamke uende jehanamu na kuunguzwa na moto milele.

Anamkumbusha, unakumbuka Ronnie alipofariki? Huyu alikuwa mjomba ake na Eminem. Anasema alipofariki mjomba Ronnie ukasema ulitamani kuona mimi ndiye nimekufa. Sasa nakwambia hiviiiii....Nimekufa kama ambavyo wewe tayari umekufa kwangu.

Hii ngoma nimeisikiliza leo kila mstari...daaah! Halafu wapwa wakampa tuzo kwa kutoa ngoma

View: https://youtu.be/RQ9_TKayu9s?si=ZMXfh42KmSM5hz5M
 
Hajui thamani ya mama huyo
Sasa kwa namna ambavyo amemuelezea mama yake ukisikiliza vizuri alikuwa hampendi Eminem mpaka kuna muda anasema alitamani Eminem afe... uenda ilikuwa ni ujana wa huyo mama kichwa kikawa na vitu vingi mpaka kusahau watoto wake... lakini kwenye makuzi Eminem anakwambia hakupitia furaha mbele ya mama yake japo ndiye aliyemzaa na kumlea
 
Em ni mwandishi mzuri sana ila angle aliyoichagua kueleza maisha yake ni ngumu kdg, kwa mtu aliyekubeba miezi tisa na akakulea ukiwa hujui lolote hata akikosea inabidi ukaushe tu. Naomba mnipigie Stan- ya Eminem
 
Kuna mambo kabla mtu hujayapitia huwezi yaelewa hata uelezewe vp, likiwemo hili la mama wapuuzi na watoto wao.
 
Ngoma ninayoikubali ni hii,lose yourself, mockingbird,not afraid na sing for the moment.
Wahenga wenzangu apa tuko pamoja.
 
Em ni mwandishi mzuri sana ila angle aliyoichagua kueleza maisha yake ni ngumu kdg, kwa mtu aliyekubeba miezi tisa na akakulea ukiwa hujui lolote hata akikosea inabidi ukaushe tu. Naomba mnipigie Stan- ya Eminem
Af hii point ya kubeba miezi 9 huwa ni ya kijinga sana.

Kwan niliomba unibebe? Yaan mnachukulia kama mwanamke kuzaa ni kumpa favor mtoto, kama ni hivo je kifo cha mtoto ni nini sasa kama kuzaliwa ni favor?

Wanawake wanazaa kwa sabb nyingi sana lakini victim anakuja kuwa mtoto,

-kuna wanawake wanazaa ili wapate haki ya kumiliki mali za mwanaume,

- kuna wanawake wanazaa ili waolewe na wanaume waliowazalisha,

- kuna wanawake wanazaa ili tu wawaridhishe wanaume zao kwa kuwapatia watoto

- kuna wanawake wanazaa ili tu kuokoa ndoa zao wasiachike

- kuna wanawake wanazaa ili jamii tu imuone amezaa,

- Wengine wanazaa sabb mimba ilikataa kutoka walipojaribu kuitoa.

sasa kama sabb za kuzaa asilimia 90 ni za kibinafsi kwa nn uje uongee utopolo wa 'Kukubeba miezi 9' as if it was a favor? Na kama kuzaliwa ni favor je kufa kwa mateso ni nini?
 
Sasa kwa namna ambavyo amemuelezea mama yake ukisikiliza vizuri alikuwa hampendi Eminem mpaka kuna muda anasema alitamani Eminem afe... uenda ilikuwa ni ujana wa huyo mama kichwa kikawa na vitu vingi mpaka kusahau watoto wake... lakini kwenye makuzi Eminem anakwambia hakupitia furaha mbele ya mama yake japo ndiye aliyemzaa na kumlea
Wazungu tusiwaige sio binadamu asilia wa hii dunia
 
Af hii point ya kubeba miezi 9 huwa ni ya kijinga sana.

Kwan niliomba unibebe? Yaan mnachukulia kama mwanamke kuzaa ni kumpa favor mtoto, kama ni hivo je kifo cha mtoto ni nini sasa kama kuzaliwa ni favor?

Wanawake wanazaa kwa sabb nyingi sana lakini victim anakuja kuwa mtoto, kuna wanawake wanazaa ili wapate haki ya kumiliki mali za mwanaume, kuna wanawake wanazaa ili waolewe na wanaume waliowazalisha, kuna wanawake wanazaa ili jamii tu imuone amezaa, sasa kama sabb za kuzaa asilimia 90 ni za kibinafsi kwa nn uje uongee utopolo wa 'Kukubeba miezi 9' as if it was a favor?
Heshimu nguvu usioiweza, kila biniadamu aliyeletwa kwenye hii dunia ameletwa kwa sababu, pamoja na inbalances zote za duniani kuna sehemu unahusika kwa ajili ya kufanya iwe balanced. Hayo mengine ni hadithi, muuombe Mwenyezi Mungu akupe mwisho bora.
 
Unaongea mambo nje ya topic. Kuzaa ni jukumu la mwanamke na wala sio favor kwa mtoto anaeenda kuzaliwa. Hio ndo ilikua point yangu.

Shida ni pale wewe unapolazimisha huko kuzaa kuonekane ni favor kwa mtoto uliposema "...Kukubeba miezi 9...' that ain't a favor mzee, ni responsibility yake, na sometimes ni outcome ya uzinzi ambao ni dhambi. Ofcoz you gotta be responsible for your sins.

Na ndio maana kwenye 'Civilized societies' kila mtu lazima awe responsible, na ndio maana kwa wenzetu waliostaarabika mtoto ana haki nzr tu ya kumshitaki mzazi wake kama mzazi hamlei na kumtunza ipasavyo au kumpa haki zake. Sababu hayo ni majukumu ya mzazi na wala sio favor kwa mtoto. Lakini societies ambazo bado ni uncivilized na underdeveloped ndizo zinaendekeza huo ujinga.
 
Back
Top Bottom