Dr. Ulimboka is smart and good Now..

Ndugu yangu nafikiri wakati wa mgomo wewe hukuwa na mgonjwa hospitali. Nafikiri wengi wetu tuliokuwa na wagonjwa hatukukubaliana nao.

Kama ulikuwa na mgonjwa kweli ungekubali atibiwe na daktari ambaye moyo wake haumtumi kutibu wakati huo?
 
Tunahitaji madaktari walio kuwa kwenye harakati pamoja nae wathibitishe Kama uli ni msaliti Au mwanaharakati
 
Mungu atakulaani wewe, kizazi chako na wengine wote walio na wanaopotosha ukweli. Ukweli ni kuwa mishahara haikuwa ajenda namba moja bali huduma bora za afya. Watanzania wengi walikufa na wanaendelea kufa kwa sababu zile ambazo zilipiganiwa na madaktari. Unafiki wenu wa kubadili madhumuni ya migomo ya watumishi utawahukumu siku ya mwisho.

Acha jazba 'doctor', mpotoshaji ni wewe! Kila mtu anajua kuwa kilichokuwa kinapiganiwa ni maslahi hii habari ya 'huduma bora za afya' kama ni kweli wangeanza kuacha kuomba rushwa kwa wagonjwa, acheni siasa.
 
Hamjui msemalo.Mimi binafsi nimekutana na Dr Ulimboka na kuongea nae kidogo.
Shortly sisi Watanzania ndio tuliomsaliti na mwisho kujikuta amesimama peke yake.Kelele zetu za kwenye keyboard hazina maana.Lakini yeye mwenyewe aliniambia ipo siku haki itapatikana hata kama si sasa.
Swala la kuongwa ni uongo na hata yeye linamsikitisha sana.

suppose angekuwa amehongwa angekwambia ndio nimehongwa na ninafuraha sana???!!
 
Mungu atakulaani wewe, kizazi chako na wengine wote walio na wanaopotosha ukweli. Ukweli ni kuwa mishahara haikuwa ajenda namba moja bali huduma bora za afya. Watanzania wengi walikufa na wanaendelea kufa kwa sababu zile ambazo zilipiganiwa na madaktari. Unafiki wenu wa kubadili madhumuni ya migomo ya watumishi utawahukumu siku ya mwisho.

hii ndio list ya madai yao:

1.Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2.Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3.Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4.Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5.Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6.Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7.Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8.Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9.Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
10.Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
11.Huduma za afya ziboreshwe nchini.
12.Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.

kati ya madai 12 ni matatu tu ndio sio maslahi yao binafsi.....yaliyobaki yote ni MASLAHI YAO BINAFSI
 
Umeshapewa ufafanuzi bado huelewi bora kukuacha tuu. Ukiona uwezo wako wa kuelewa ni mdogo usijadili mambo ya msingi utayapotosha. Kwa taarifa yako baada ya kumgomo ule kutofanikiwa vifo vya ndugu zetu watanzania vimeongezeka sio kwa kukosa huduma za madaktari bali ukosefu wa vifaa na madawa kama walivyokuwa wanapigania madaktari.

mwache huyo,amevurugwa
 
Nasikia walimharibu kila kitu, wakamngoa meno pamoja na kucha, mwenye taarifa jamani atujuze. watu wengi walikufa kwa sababu yake, Mungu amsamehe
 
raia masikini wengi walikufa sababu ya huo mgomo wa madaktari wakiongozwa na uyo ulimboka,viongozi wa utibiwa nje waliokufa ni masikini.
Uyo Ulimboka alivuna alichopanda na siku zote malipo ni hapa hapa duniani.

migomo yenyewe haikusaidia waliambiwa kama utaki kazi uache,mishahara waliyotaka ni sawa na bajeti nzima hivo tungesimamisha shughuli zote tungekuwa tunalipa mishahara tu.

uyo ni muuaji mkubwa

Thats rubish! u realy talk rubish
 
Few months ago, kuna member mmoja hapa aliulizia juu ya dr. Ulimboka.
Nimeutafuta ule uzi sijauona!!

So kwa kupitia thread hii, naomba nimjulishe kuwa dr ulimboka yuko poa, nimekutana nae jioni hii hapa boma - hai.
Nimeongea nae!
Yuko poa and ok.

Mungu walinde wote wanaoteswa kwa ajili ya kutetea haki.
Amen!!

Muambie kuwa hatakufa kabla ya kuwaona watesi wake hoi.mwambie wameshaanza kuathirika.
 
Tunahitaji madaktari walio kuwa kwenye harakati pamoja nae wathibitishe Kama uli ni msaliti Au mwanaharakati

Uli ni mwana harakati aliyemwaga damu yake kwa ajili ya wengine mateso ya ajabu kwa ajili ya wengine ulimboka for life
 
Hivi walioanzisha jf walikuwa wamekusudia kuwa na michango isiyo na utafiti au great thinkers maana yake ni uhuru wa kuongea hata kama unachoongea ukijui? ! Ifike mahala hasa katika mwaka ujao, iwe ni marufuku mtu kuchangia post ambayo huna uelewa nayo. Mods piga ban hoja zote za ubabaishaji zinazotupotezea mwelekeo. Inapendeza sana kusoma maoni ya wanazuoni wa mada husika na tukaelimika bila kuvuruga jamani!
 
Acha jazba 'doctor', mpotoshaji ni wewe! Kila mtu anajua kuwa kilichokuwa kinapiganiwa ni maslahi hii habari ya 'huduma bora za afya' kama ni kweli wangeanza kuacha kuomba rushwa kwa wagonjwa, acheni siasa.

Nanukuu kauli mojawapo ya madaktari kipindi cha mgomo "hatuwezi kuendelea kushuhudia ndugu zetu wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya mfano scaner machine ni mbovu tunahitaji matengenezo serikali inadai haina pesa huku wao wanamiriki benzi za mil90..." hilo kombojr unalionaje?
 
shujaa aliyehongwa na serikal akasahau kuwa ilijuea llllkuwa afe yeye, chezea hela, sasa shavu hilooo, mwana garajat wa njaa huyo, akina mandela hawatatokea tena
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza, mtaongea mengi ila ipo siku mtafunga midomo yenu. Ukweli ni kwamba Dr. Uli ni shujaa wa wengi, alichokipigania ni mazingira bora ya kazi na huduma bora za afya kwa watanzania wote.
 
Few months ago, kuna member mmoja hapa aliulizia juu ya dr. Ulimboka.
Nimeutafuta ule uzi sijauona!!

So kwa kupitia thread hii, naomba nimjulishe kuwa dr ulimboka yuko poa, nimekutana nae jioni hii hapa boma - hai.
Nimeongea nae!
Yuko poa and ok.

Mungu walinde wote wanaoteswa kwa ajili ya kutetea haki.
Amen!!

Haki ndio lakini je haki ya kudai pesa ndio inalinganishwa na uhai wa mtu?
 
Back
Top Bottom