Dr. Ulimboka is smart and good Now..

Dr. Ulimboka is smart and good Now..

Few months ago, kuna member mmoja hapa aliulizia juu ya dr. Ulimboka.
Nimeutafuta ule uzi sijauona!!

So kwa kupitia thread hii, naomba nimjulishe kuwa dr ulimboka yuko poa, nimekutana nae jioni hii hapa boma - hai.
Nimeongea nae!
Yuko poa and ok.

Mungu walinde wote wanaoteswa kwa ajili ya kutetea haki.
Amen!!
kiwatengu
===>Tunamtakia afya njema,ila kwa aliyofanyiwa hakupaswa kukaa kimya hata siku moja!
 
Last edited by a moderator:
Katika issue hii ya Dr. Ulimboka, kuna mijitu na watu. Bado nampongeza Dr. Ulimboka kwa uthubutu wao. Kwa ujinga na uoga wetu watanzania tukashindwa kuwaunga mkono madaktari katika jambo la msingi kama lile.

Wanyama wanapanda ndege, madini yanakwapuliwa, gasi ndiyo hiyo inaondoka, mabilioni yanahifadhiwa Uswisi na Visiwa vya Jesery, hospital hakuna dawa na watu wanazidi kuangamia katika muda usio wao ili hali wao wanatibiwa nje, mashule hayana sifa za shule na watoto wao wanasoma nje, n.k. Mitanzania tumebweteka tuuuu hata inapotokea watu wachache kuonyesha njia ya kupinga wizi na dhuruma inayofanyika kwa nchi hii! Mfano akina Dr. Slaa wameonyesha wizi mkubwa tu unaofanyika nchini, Zitto na mabilioni yaliyofichwa nje, wanamtwara wamegoma gesi, n.k. Watz tumewaungaje mkono watu hawa?

Tukiwa huku JF tunajifanya kujua na kuwalaani watu waliojaribu japo kuthubutu! Kama si uji.nga ni nini? Kama tumeshindwa japo hata kuwaunga mkono wapambanaji ni bora tukae kimya kuliko kuwanenea upuuzi tunao wanenea watu wa watu.
 
atakulaani wewe mwenyewe,ule mgomo wa madaktari ulisababisha vifo vya masikini wala siyo kukomoa viongozi.Pamoja na kugoma nini kimebadilika? zaidi waliambiwa waache kazi na wao wenyewe wakajirudisha kazini.
Kuna njia nyingi za kufikisha malalamiko siyo kwa mgomo,madaktari wakigoma ni mahafa makubwa sana kwa raia masikini.Ndugu yako angekufa kwa sababu ya mgomo huo ndio ungeelewa nini nasema.

Najua Tanzania na nchi nyingi za Africa tuna matatizo kwenye sekta za Afya tofauti na nchi zilizoendelea lakini lazima ujue maendeleo hayaji kwa siku moja,ulaya wameanza kuendelea toka karne ya 15,kamwe usijifananishe nao.

Cha muhimu serikali iboreshe sekta za afya lakini madaktari wanaogoma wanakomoa wananchi masikini,wenye uwezo wanaenda hospitali binafsi ,wengine ata nje ya nchi.

usilete siasa hapa angalia wanaotaabika ni hakina nani,uyo ulimboka kitendo alichofanyiwa siyo kizuri ila siwezi kumuonea huruma sababu kuna watu walikufa kwa sababu ya kuongoza huo mgomo uliokuja kushindwa.

Na ata hao madaktari walimsaliti ,kwenye shida hawakuwa naye,mgomo wa madaktari usiufananishe na migomo ya bodaboda au wasukuma mikokoteni.

Madaktari wakigoma ni majanga wala usiunge mkono,huyo ulimboka ni smart kwako tu,mi kwangu ni muhuaji tena aliyetelekezwa na madaktari wenzake

Umeshapewa ufafanuzi bado huelewi bora kukuacha tuu. Ukiona uwezo wako wa kuelewa ni mdogo usijadili mambo ya msingi utayapotosha. Kwa taarifa yako baada ya kumgomo ule kutofanikiwa vifo vya ndugu zetu watanzania vimeongezeka sio kwa kukosa huduma za madaktari bali ukosefu wa vifaa na madawa kama walivyokuwa wanapigania madaktari.
 
Hapa ndo utaelewa kiasi cha uelewa mdogo wa watanzania, I can't believe I'm reading this.

Na Watawala wanafurahia sana hali hii maana ndiyo inawaweka hapo walipo na kufanya watakacho. Baba V utakuta hawa wasemayo haya ndio wanaitwa wamesoma na ndio wajanja wa mjini. Aibu tupu nchi hii!
 
Last edited by a moderator:
Hamjui msemalo.Mimi binafsi nimekutana na Dr Ulimboka na kuongea nae kidogo.
Shortly sisi Watanzania ndio tuliomsaliti na mwisho kujikuta amesimama peke yake.Kelele zetu za kwenye keyboard hazina maana.Lakini yeye mwenyewe aliniambia ipo siku haki itapatikana hata kama si sasa.
Swala la kuongwa ni uongo na hata yeye linamsikitisha sana.
 
atakulaani wewe mwenyewe,ule mgomo wa madaktari ulisababisha vifo vya masikini wala siyo kukomoa viongozi.Pamoja na kugoma nini kimebadilika? zaidi waliambiwa waache kazi na wao wenyewe wakajirudisha kazini.
Kuna njia nyingi za kufikisha malalamiko siyo kwa mgomo,madaktari wakigoma ni mahafa makubwa sana kwa raia masikini.Ndugu yako angekufa kwa sababu ya mgomo huo ndio ungeelewa nini nasema.

Najua Tanzania na nchi nyingi za Africa tuna matatizo kwenye sekta za Afya tofauti na nchi zilizoendelea lakini lazima ujue maendeleo hayaji kwa siku moja,ulaya wameanza kuendelea toka karne ya 15,kamwe usijifananishe nao.

Cha muhimu serikali iboreshe sekta za afya lakini madaktari wanaogoma wanakomoa wananchi masikini,wenye uwezo wanaenda hospitali binafsi ,wengine ata nje ya nchi.

usilete siasa hapa angalia wanaotaabika ni hakina nani,uyo ulimboka kitendo alichofanyiwa siyo kizuri ila siwezi kumuonea huruma sababu kuna watu walikufa kwa sababu ya kuongoza huo mgomo uliokuja kushindwa.

Na ata hao madaktari walimsaliti ,kwenye shida hawakuwa naye,mgomo wa madaktari usiufananishe na migomo ya bodaboda au wasukuma mikokoteni.

Madaktari wakigoma ni majanga wala usiunge mkono,huyo ulimboka ni smart kwako tu,mi kwangu ni muhuaji tena aliyetelekezwa na madaktari wenzake

Na wewe ndiye mwakilishi wa mazombiez yaliyoiazana Afrika, madakatari walikuwa wanagoma ili serikali iweke vifaa tiba Hospitalini ili kupunguza vifo visivyo na sababu, ninyi ndiyo mlikuwa bize ku sabotage mgomo na kuifanya serikali isitimize wajibu wa kulinda uhai wa wananchi wake. Madakatari wamefundishwa kuchunguza magonjwa kwa kutumia vifaa maalumu, wameletwa hospitali vifaa vya kuchunguzia magonjwa havipo,wanagoma vifaa viwekwe zombie wewe unakasirika,kabla ya mgomo na baada ya mgomo kusitishwa ndugu zako maskini wameacha KUFA HOSPITALINI ?
 
Atakuwa kapata somo hawezi fanya utoto tena kama funzo lilikuwa kubwa sana.

Mafunzo ndio yanatolewa hivyo kwa kung'oa kucha meno bila ganzi.?

Huo ni zaidi ya ugaidi.!!
 
Nakushauri uende kanisani au msikitini ukaombe dua kwa nguvu.

Wewe unaamini kuwa wasingegoma basi watu wasingekufa, jambo ambalo siyo sahihi kabisa. Ni afadhali waligoma halafu tukajua hatuna waganga kuliko wangekuja kututibu bila kugoma ila wakatudunga sindano za sumu wagonjwa wote.

Majuzi tu umeamabiwa kuwa wanasiasa wetu wanalipwa kuliko wanasiasa wa nchi zinazotupatia misaada, je kwa nini usilalamikie hilo kama kweli unajua kuwa hatuna hela ya kulipa mishahara mikubwa?

Ndugu yangu nafikiri wakati wa mgomo wewe hukuwa na mgonjwa hospitali. Nafikiri wengi wetu tuliokuwa na wagonjwa hatukukubaliana nao.
 
Haya yapo kila nchi sio tz tu labda uwe hujatembea duniani. Na kama unaamini kifo ni ahadi basi usilalamike hata hao wanaotibiwa kwa uhakika watakufa tuu hata kama CT SCAN zitakuwepo kila wilaya bado kifo kitabaki palepale

hatujaskia mandela kupelekwa KENYA KWA MATIBABU,,,USISEME YAPO KILA NCHI,,,,,
tuboreshe huduma zetu za afya mdau,wale kinamama ukienda pale wodi ya wazazi wanavyolala chini ni fair???kuna mke au hawara wa waziri analala chini??mgomo umetokea mara 1 au 2,ila watanzania wangapi wanakufa kwa sababu ya ukosefu wa vifaa tiba??au kwa sababu haviripotiwi,,,,tuwe objective sana,me huwa natembelea muhimbili,pale mwaisela watu wanalala sakafuni,hadi mlangoni,,,,
 
kufa si ahadi japo najua ni lazima . wakati mwingine matibabu mabovu.huduma mbaya na migomo ya madaktari upelekea vifo vya wagonjwa

migomo haitokei mwaka mzima,,,,tatizo kubwa ni lilelile,,,juzi ripot ya kamat ya huduma za jamii imeeleza wazi kuwa hospital hazina dawa,na MSD inaidai serikali bilions of money,hivo serikal kuu itakapoilipa msd,dawa ndo zitapatikana,sasa hapa watu wanakufa kwa kukosa dawa,madaktar wanahusikaje???
 
uyo mkuu wa kaya alijichagua mwenyewe? kama ni kiongozi wa mbaya wakupewa lawama ni nyie mnaopiga kura.

mnaokubali kupewa kofia na kanga za bure

eeeh umehamia huku tena???,umehama kwenye hoja,umekuja kwenye kashfa,,,,
sidhan kama huu ndo mjadala wetu,any way nikuache na ujinga wako,maana sikujui hunijui
 
Swali langu je gegedo linafanya kazi? Maana nasikia vijana wa msangi/ighondu/zocka waliharibu kila kitu kwa babu!

Kabakia jina tu, wazee walisaga zile goroli zikawa ujiuji sasa anaitwa aka mauji
 
Wadau, kila mtu anasema analoamini yeye, kitu ambacho ni sawa na ndio maana ya kujadili, kutofautiana ni jambo la kawaida, ila kutukana ni ustaarab gani?
Kurudi kwenye mada, tatizo lipo, tatizo sio ulimboka, tatizo ni la kimfumo, ambalo kimsingi ni tatizo la kiuongozi, sio wa wizara ya afya tu bali serikali yote. Kila upande unamakosa, hakuna aliye sahihi ndio maana tatizo bado lipo.
Huduma mbovu za afya na ukosefu wa vitendea kazi na malipo mazuri pia kwa wahudumu wa afya ni tatizo kubwa na la msingi. Lakini sababu ni nini? Uongozi mbovu, siasa chafu na kukosa uzalendo. Siamini kuwa serikali haina uwezo wa kuboresha huduma za msingi kama afya. Ila ni matumizi mabaya ya fedha za umma na mipango mibovu ya vipaumbele. Huwezi kusolve kila tatizo, lakini mkakati wa vipaumbele ni upi? Hayo ma-V8 tu gharama za kuyanunua na kuyatumia ni uwendawazimu mkubwa kutumia magari ya kifahari na engine kubwa hivyo tena 4WD kutembelea kwenye barabara za lami tena zaidi mijini.
Pesa wanazolipana wanasiasa na viongozi yote haya ni ishara kuwa tatizo sio pesa, tatizo ni plan na vipaumbele lakini kubwa zaidi ni sera ambayo kwa ujumla wake inakuwa ni tatizo la serikali. Siioni sababu ya kuitetea serikali hapa ikiwa wao wanatibiwa nje ya nchi kwa fedha zetu nyingi wakati zahanati vijijini hata OPV hazina.
Mgomo huwa ni namna ya kulazimisha mabadiliko hasa pale majadiliano yanaposhindwa, ila mgomo wa kumtibu mgonjwa kuwa acha wafe hilo sikubaliani nalo. Aliyepoteza ndugu yake katika mgomo ule anaelewa ninachosema. Mgomo wa huduma ambazo madhara yake yana mbadala ni sawa, mfano daladala wakigoma hata kwa mguu watu watatembea, lakini ukigomea uwepo wa uhai wa binadam, akitoweka utampata wapi? Ulimboka alipata mateso ambayo nafeel sorry, lakini gharama ya mgomo ule ni kubwa sana, maisha yamepotea, rambirambi ni kutu gani? Na mbaya zaidi, no changes.
Malipo waliyodai madaktari ni dalili za ubinafsi na uchoyo. Siamini kama daktari ndio mtumishi wa thamani kuliko wengine. Mwanajeshi je? Polisi je? Wote wanahusika na kulinda maisha ya watu kwa mazingira tofauti tu.
Naamini sehemu ya kutatua haya ni kuchagua viongozi wazuri wenye kumjali mtu mnyonge na masikini.
 
Mgomo utarudi tena na tena. Mpaka pale kitapoeleweka huu sio.mwisho ni mwanzo tu.
 
Umeshapewa ufafanuzi bado huelewi bora kukuacha tuu. Ukiona uwezo wako wa kuelewa ni mdogo usijadili mambo ya msingi utayapotosha. Kwa taarifa yako baada ya kumgomo ule kutofanikiwa vifo vya ndugu zetu watanzania vimeongezeka sio kwa kukosa huduma za madaktari bali ukosefu wa vifaa na madawa kama walivyokuwa wanapigania madaktari.

achana nae huyo,,,,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom