Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Nani unaona anafaa kuwa Rais kati ya Wawili hawa?

  • Edward Lowassa

    Votes: 103 13.0%
  • Dr. Willibrod Slaa

    Votes: 640 80.6%
  • Wote hawafai/sijaamua

    Votes: 51 6.4%

  • Total voters
    794
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Mh onyesha busara ktk hili ndo maana nasema huwezi kuishi bila siasa,Lowassa anaweza kabisa kusimama akutoa hoja na majibu pamoja na maswali kwa Dr Slaa. Hawa ni kati ya watu ninaowakubali sana, Tz isingekuwa inapelekeshwa na kiinchi kama Rwanda mbele ya Slaa au Lowassa.

MWAKYEMBE, MAGHUFULI, ZITTO, lakini kwa sababu ya uhuni tu, tena uhuni uliopitiliza unaniletea SLAA na LOWASSA, basi nitampa LOWASSA.
 
Maadui wa Lowassa ni hao wanaouota urais huku sifa zao kama za babu yangu {kusimulia hadithi tu}
 
Hakika umenigusa moyo wangu, Kwa wale tunaoipenda Tanzania hakika hawa ndo maraisi wetu watarajiwa. Mimi kama ningekuwa CDM hakika Slaa anatosha na kama ningekuwa CCM hakuna kama Lowasa lakini kwa ulegelege wa upinzani wana JF raisi ajaye ni Lowasa, CCM haibebeki bila Lowasa, Lowasa ndiye rada ya CCM kwa sasa. Sikio la kufa halisikii dawa hujuma yoyote kwa Lowasa njia nyeupe kwa Slaa. Kitu kingine ni hiki watu wa kaskazini ndo maana nawaita Wakikuyu kwa ushirikiano na wanavyojithamini {hapa hata mniite mkabila} tangu enzi na enzi inajulikana hivyo. Wakati hawa watu wakipita kwenye kura za maoni ni sherehe Kaskazini huku kanda ya ziwa {usukumani} ndoho tabhu. Na kama uchaguzi huru ukiwepo baina ya hawa watu,serikali ya mseto haikwepeki. Mnisamehe

Rais anatakiwa mmoja , hata hivyo kwa jinsi hali ilivyo na ukizingatia kuwa kuna watu walidiriki hata ksema Kaskazini wajitenge, na kwa sababu SLAA chama chake kinaongoza njama za chini chini za kuvunja muungano, hakika Tanzania ya sasa haihitaji rais kutoka kaskazini.
 
Tatizo lake ni kuamini kwamba akiwateka viongozi wa dini basi amemaliza kila kitu!
Yupi bora aliyeamua kutoa au aliyezificha Uswisi? Mimi hata mning'oe jinsia yangu Lowassa alijiuzuru kulinda CCM tu lakini walegwa wapo wamepakata nanihii zao tu kwenye majengo ya umma,ndio maana kawa mkimya asije kufanya nchi isitawalike.
 
Wadau Nani hasa anafaa kuwa Rais wetu kwa maslahi ya taifa letu kati ya Dr.Slaa na Lowassa...kimisimamo na maamuzi naona kama wana fanana vile labda kwa vile wote wanatoka ukanda mmoja na makabila yao yana uhusiano flani hivi,ila nina uhakika kwenye karama ya uongozi na vision za kimaendeleo wana utofauti mkubwa sanaa.we unaonaje?
Kaka/dada unaona mbali sana au u mdogo wangu nanihii?
 
Dr Slaa ni mwamba wa Tanzania!! Ni muwazi pia ni jasiri na yupo tayari kusema ukweli mahali popote inapobidi kufanya hivyo,Lowasa aliwahi kusema ukweli lini,zaidi ya kuzidi kuandamwa na Richmond,kama sio yeye aseme hadharani ili ukweli ujulikane!! Dr.Slaa ni level nyingine sio akina Lowasa,Lowasa level zake ni m/kiti wa kitongoji yeyote wa Chadema sio Dr.
 
mkristo vs mkristo hahahahaa. "kama kuna wagombea wengi na katika hao kuna waislamu wawili basi ukiona muislamu mmoja anaelekea kushinda mchague huyo huyo"

Mkuu bado msimamo wako ni huu huu au umebadili?.
 
Kwanza tuweke udini na ukabila pembeni. Umri ni huko chini (ujana) juu ni uwezo wako wa kufikiri. Hatujui ni nani atakayepitishwa na chama. lakini kwa mawazo yangu hasa baada ya kufuatilia safari ya Slaa ughaibuni huyu mzee uwezo wake wa kuiongoza hii nchi anao. hata kama wabunge wa chama chake hawatakuwa wengi kama rais atawasafisha mafisadi wote ktk anga la TZ a.k.a Moringe Sokoine.
 
Kwanza tuweke udini na ukabila pembeni. Umri ni huko chini (ujana) juu ni uwezo wako wa kufikiri. Hatujui ni nani atakayepitishwa na chama. lakini kwa mawazo yangu hasa baada ya kufuatilia safari ya Slaa ughaibuni huyu mzee uwezo wake wa kuiongoza hii nchi anao. hata kama wabunge wa chama chake hawatakuwa wengi kama rais atawasafisha mafisadi wote ktk anga la TZ a.k.a Moringe Sokoine.

Pembe uko sahihi kabisa. na nimi naamini kabisa kuwa slaa kuwa rais ni suluhisho la matatizo ya watanzania yaliyosababishwa na ccm akiwemo lowasa. Pia lowasa kuwa rais ni sababu tosha ya kuzidi kwa matatizo hapa nchini.
 
Wakati gazeti la Nipashe likianzisha kura ya maoni miongoni mwa wana-CCM wanaotajwa kuwania kuteuliwa na CCM kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao kwa lengo la kugombea nafasi ya uraisi kupitia chama hicho na huku bwana Lowassa akiongoza kwa kura,nafikiri ni busara na sisi kupitia mtando huu wa JF kumpambanisha bwana Lowassa na Dr. Slaa katika kinyang'aricho hicho cha uraisi kwa mwaka 2015.

Tupige kura kwa kuandika jina tu la mgombea unaedhani atafaa kuwa raisi endapo itatokea hao wawili wanateuliwa kuviwakilisha vyama vyao katika uchaguzi mkuu ujao.

NB😛iga kura bila kuendesha campaign yoyote.

Wakuu,ukienda hata kwenye ukurasa wa facebook kuhusu hii poll,utagundua tofauti baina ya hawa watu wawili ni sawa na mbingu na ardhi!

Hii poll hapa JF ni kioo tosha cha kuongoza vyama hivi wakati wa uteuzi utakapofika.

------------------------------------------------------------------

*Kwa maoni zaidi ya washiriki wa JamiiForums kupitia ukurasa wa Facebook - Dr. Wilbrod Slaa Vs Edward Lowassa (JamiiForums facebook page)
attachment.php

 

Attachments

  • facebook.png
    facebook.png
    32.9 KB · Views: 22,902
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom