Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

[/COLOR]

BLUE
Kama shida yangu ni jinsi ya kutamka naomba nisamehewe...Lakini the fact remains!...Wengine tulikulia machungani! ha ha haaa!

RED
mKUU,
kAMA SHIDA NI KISUKARI, huu ugonjwa unatibika na Ndodi kama mchezo..
Tofauti ya ngonjwa na mgonjwa itakuja kutokana na tiba alizojaribisha kuzitumia awali...kama hakujaribu dawa zozote then ndani ya wiki 15 kisukari ni hadithi!..SIMPLE!

GREEN:
Nikisema kuwa 3M itolewe sina maana mimi nina uwezo nayo tit-for-tat!...ieleweke hivyo...Wanaonijua wanafahamu margin yangu ya income.
Tusilete hisia kwenye ukweli...Ukichagua kwenda kwa ndodi(maana ni option) maana yake ni kwamba unachagua kutekeleza masharti!...malalamishi baada ya hapo hayatakiwi, utakuwa unajikwaza bila kupenda!

Suala la ku'bagain bei jamani lipo...Ndodi huwa anapita mara nyingi mahala nilipo mimi, na huwa anaweka sawa hilo jambo mara nyingi..bei ni maelewano, sio fixed!...Sasa ishu ya kumwomba apunguze pale anapokuwa na foleni, just go into his shoes...ni ngumu kidogo kupata muafaka!
Naombea ningeeleweka!
Nakuunga mkono all the way PJ.
Huduma ikiwa mbovu unasepa na siyo kuja kulialia hapa.Kwani tabibu ni Dr Ndodi Tu?..Si muende huko mtakakotetemekewa na kupunguziwa bei? Binafsi kama nina huduma yangu na ninaona watu ni wengi kuliko ninavyoweza kuhudumu basi nitaweka njia za kuwaondoa baadhi. Njia moja wapo ni kama hivi afanyavyo Dr Ndodi - pandisha bei kinoma! Wasio nazo wasogee kwingineko..kwa njia hii wahudumu tutagawana wateja. Customer care na Customer service inategemea unavyoweza kulipia. Kama kwa Ndodi kubaya nendeni kuzuri.
 
Nitamtafuta anipe ufafanuzi, haiwezekani dawa ya kisukari iuzwe mil.3 nooooooooooooooooooooooooo!!!!!
 
Pdidy haueleweki! Kwanza unamlalamikia Dr Ndodi, Pili unaendelea kupeleka watu kwake; we ni mtu wa aina gani?

Hao unaowapeleka wanapona au ...? Kama yeye amekaa kibiashara hilo ndio jambo la muhimu. tatizo waTZ hatujali muda wa mtu. Inawezekana jamaa yako alikuwa amepewa maelekezo yote lakini akawa mgumu wa kuelewa na akawa anapoteza muda kutaka jambo hilo hilo lirudiwe rudiwe na Dr akaona anampotezea muda wa kulamba 20K.

Tujali muda, kila mtu ana 24hrs per day na usipotumia vizuri uta-lost

Kuna baadhi ya madaktari ambao fee yao iko juu zaidi Tshs 40,000 & 60,000, lakini ukiingia ndani, wakati mwingine hata maongezi yao ni tiba tosha. Na ukitoka, wala hauhisi mapungufu kwa kutengana na pesa yako. Kwa hiyo mara nyingi imani iinaongeza tiba, kwa hiyo lazima daktari ajenge uwezo wa mgonjwa wake kumuamini, kwa hiyo ninaamini ni lazima ampe muda mgonjwa wake. Lakini kama issue ni kutiki kuwa ishirini ngapi zimeingia na ngapi unakosa nje kwenye foleni, sijui kama kuna 'ethics' hapa. (anyways, looks like ethics siyo issue kwa hapa). Angalizo, kazi ya daktari na konda zinatofauti kubwa sana ya kukimbizana na 'vichwa'!

Niliwahi kwenda hospitali kumpeleka mtoto, wakati najitahidi kuelezea matatizo ya mtoto, daktari alikuwa anakaribia kupindua karatasi kwa kuandika. Kwa kweli sijarudi tena!
 
Nakuunga mkono all the way PJ.
Huduma ikiwa mbovu unasepa na siyo kuja kulialia hapa.Kwani tabibu ni Dr Ndodi Tu?..Si muende huko mtakakotetemekewa na kupunguziwa bei? Binafsi kama nina huduma yangu na ninaona watu ni wengi kuliko ninavyoweza kuhudumu basi nitaweka njia za kuwaondoa baadhi. Njia moja wapo ni kama hivi afanyavyo Dr Ndodi - pandisha bei kinoma! Wasio nazo wasogee kwingineko..kwa njia hii wahudumu tutagawana wateja. Customer care na Customer service inategemea unavyoweza kulipia. Kama kwa Ndodi kubaya nendeni kuzuri.

Hivi hawa wa aina ya Ndodi hawako kwenye ule utaratibu wa "UDAKTARI NI WITO"?
 
nakuunga mkono all the way pj.
Huduma ikiwa mbovu unasepa na siyo kuja kulialia hapa.kwani tabibu ni dr ndodi tu?..si muende huko mtakakotetemekewa na kupunguziwa bei? Binafsi kama nina huduma yangu na ninaona watu ni wengi kuliko ninavyoweza kuhudumu basi nitaweka njia za kuwaondoa baadhi. Njia moja wapo ni kama hivi afanyavyo dr ndodi - pandisha bei kinoma! Wasio nazo wasogee kwingineko..kwa njia hii wahudumu tutagawana wateja. Customer care na customer service inategemea unavyoweza kulipia. Kama kwa ndodi kubaya nendeni kuzuri.

crap
 
Mmesahau NGETWA?jamaa alipata pesa balaa anaendesha range rover na hotel pale ubungo external inaitwa lunch time
 
Nakuunga mkono all the way PJ.
Huduma ikiwa mbovu unasepa na siyo kuja kulialia hapa.Kwani tabibu ni Dr Ndodi Tu?..Si muende huko mtakakotetemekewa na kupunguziwa bei? Binafsi kama nina huduma yangu na ninaona watu ni wengi kuliko ninavyoweza kuhudumu basi nitaweka njia za kuwaondoa baadhi. Njia moja wapo ni kama hivi afanyavyo Dr Ndodi - pandisha bei kinoma! Wasio nazo wasogee kwingineko..kwa njia hii wahudumu tutagawana wateja. Customer care na Customer service inategemea unavyoweza kulipia. Kama kwa Ndodi kubaya nendeni kuzuri.

Daaah! I ril cant biliv this!!!!!
 
.............. Jisachiii !!!

............. Jamaaa mwizi jumla ! ......anachanganya Dini kidogo, usanii sana, vitisho na mwisho anakula kiingilio !

........... unakukatisha tamaa ili ale kiingilio !

.......... yule sio tabibu ni mwizi jumla !!

............. wewe shtukaa ! yule mwizi ! TIBA MBADALA VITABU na MAJARIDA yako chungu nzima ! wala humuitaji ndodi !

.............. anachanganya Dini kukupumbaza !

............ huyu msukule nini ??!!

.............. wewe alikutibu nini ? Yaaaani Ndodi ni kuliko DOWANS !!!! Khhaaaa !!

......... muweke kwenye kilengeo!!!!!!!!!!!!!!!!:shock:

Iko gonjwa ndani ya kichwa yako?

AU akili yako iko shake well before!!
 
Mimi naamini kuwa kuna matibabu ya ugonjwa wa kisukari. watu wametoa michango mbalimabali kutoka na uelewa na imani ya kila mtu.
Kwa kifupi hapa Tanzania kama mtu huna pesa unaweza kufa hata kama kama ugonjwa wako ungeweza kutibika SABABU..huna uwezo wa kulipia gharama za matibabu.

Ungonjwa wa kisukari imekuwa ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu. hii inatokana na mienendo ya maisha yetu kwa sasa. Ukijuuliza ni kwanini miaka ya hivi karibuni ugonjwa huu umekuwa tishio kubwa la maisha ya watu, jibu rahisi ni kuwa maisha yetu siku hizi yamebadilika mno. Ni watu wachache sana wanapata muda wa mazoezi. Watoto wetu/wadogo zetu siku hawana muda wa kucheza ‘ready’, kombolela, kidali po, na michezo mingine mingi ambayo ilikuwa ikisaidia afya za watoto. Vivyo na kwa watu wazima nao muda mwingi wanatumia wamekaa ofisini au kwenye magari no time for exercise. Kweli mengine hayaepukiki.

Ni kweli kwamba hata kama utapata tiba ya ugonjwa wa kisukari basi baada ya hapo lifestyle yako inabidi ibadilike. Kwa wewe ambaye una tatizo hilo kuna haja ya kufuata ushauri wa daktari, na kuhudhuria kliniki. kujifunza zaidi kuhusu njia za kupambana na ugonjwa huu.

Kwa wale wanaosumbuliwa na wanaotaka kujifunza mnaweza kuandika kwa: lifestyleconsultant@yahoo.com , hakuna gharama yoyote inayolipwa kwa ushauri.NI BURE- Its free
 
Nitamtafuta anipe ufafanuzi, haiwezekani dawa ya kisukari iuzwe mil.3 nooooooooooooooooooooooooo!!!!!
Unfortunately dawa yaweza kuwa mkojo wako tu. sorry kama utadhani natania .
 
Kwa mujibu wa wachangiaji humu seems ikiwa huna pesa anza kukusanya michango ya jeneza
 
Samahani wajomba, hiyo m3 ni nyingi saaaaaaaaaaaaaaaaaaaana, mimi ninaedoctor wangu anaye tibu kwa tiba mbadala hata m2 hazitafika na kupona is must, na yeye akiona huponi anabandika na mikono analiitia Jina la Yesu! Unawajua Forever living products? hawa wa aloevera nomaaaaaaaaaaaaaaaaa zaidi ya ndodi! pole
 
Dawa ya kisukari ni nkutoipata na kama ukiipata basi timiza masharti ya matibabu.
Watanzania wenye ujuzi tuwe na uzalendo wa kuwahurumia fukara wenzetu wala tusitake faida kubwa kwenye masuala yanayohusu uhai wa mtu. Kama kwa Mungu tungelikuwa tunalipia uhai wetu walah hakuna ambaye angeishi....
 
Ndg waungwana huu ni mtazamo wangu binafsi kuhusu Ndodi "Dr"

Kwanza kabisa huyu mtu ni mjasiriamali mzuri sana hapa nchini ambaye ameweza kuteka watu wengi sana kwa maneno yake na tiba zake asilia ambazo kwangu mimi nina imani ni nzuri kuliko za hospitali kwani nyingi hazina kemikali na pia hutoa ushauri wa tiba mbadala kama kula right foods, mazoezi sehemu muafaka na vingine vingi.

Huyu mtu ni mjasiriamali na naweza kusema ni genious kwani ameweza kuangalia tatizo liko wapi na akalitumia kutengeneza hela (creativity phenomena) tena kwa kutumia tiba mbadala ambazo ukisikiliza maelezao yake nyingi ni za kweli

Pia mtu huyu ingawa sina uhakika kuhusu taaluma yake ila inaonyesha anajisomea sana hivyo ana ufahamu wa mambo mengi sana yanayohusu kitu anachofanya

Matatizo ya Ndodi

1. Hayuko organised, kama unafualtilia vipindi vyake utaona anachanganya sana mada na mwisho wa siku anashindwa kutoa kwa ufasaha alichodhamiria kukitoa (poor presentation skill)

2. Ana namba nyingi sana za simu (zaidi ya kumi) kitu ambacho kwa mtu ambaye yuko makini na mwenye kujipanga hawezi kuwa hivyo

3. Yuko kibiashara zaidi kuliko kitabibu kwani kama ukifuatilia vipindi vyake utaona anavutia zaidi kuonana nae kuliko kutoa suluhisho kwa ushauri

4. Kitu kingine kinachonishangaza ni kwamba pamoja na umaarufu alionao anakaa hotelini kama sehemu ya kazi, wakati nadhani ingekuwa vizuri kama angeanzisha kituo cha kueleweka maana pale hotelini kama kikinuka anaweza kukimbia kirahisi, mtu makini na mwenye nia ya kazi yake anatakiwa kuwa na kituo maalum (kwa mtizamo wangu)

5. Katika kuongea kwake ana masikhara mengi sana hivyo kipindi chake kimegeuka kuwa kama komedi hivi, wakati anatakiwa kuwa serious kwani suala la utabibu linagusa maisha ya watu

Kwa hayo matano naona ndio matatizo makuu sijui kuhusu customer care kwenye kituo chake maana sijawahi kufika ila kwa jinsi anavyoongea tu kwenye kipindi naona kama hayuko organised yeye binafsi
Maelezo yako nayaunga mkono 100% binafsi ni mpenzi sana wa vipindi vyake na kila kunapokuwa na vipindi vyake huwa najitahidi kuandika yaliyo ya muhimu na kupitia vipindi vyake nami nimeweza kuwasaidia wengine kukawa na matokeo mazuri.

Kwa upande wa matatizo kama ulivyoeleza ni kweli hayuko organised hasa pale anaporuhusu watu kupiga simu live ndipo muingiliano wa mada unapotokea kwa sababu ni kweli unaweza ukawa unaifuatilia mada aliyoanzisha asiimalize kama alivyotarajia hivyo ukawa umeachwa njiani na kipindi kingine akawa na mada nyingine.

Binafsi namwamini na ukisikiliza maelezo yake ukayafata utajiepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuepukika. ila walamikaji wengi niliowaona humu kwa kuwa wamezoea vya rahisi (kama vya wachina) bila kujua hasara zake basi wataendelea kulalamika milele.

Dawa zake zote zinatokana na matunda na matunda mengi inabidi ayaagize nje. kuna matunda yanaitwa kiwi, au hata haya olive au almond ni matunda ambayo hata Tanzania hayapo na kuyapata unakuta kilo moja mengine si chini ya Tshs 50,000 sasa unakuta dawa inahitaji mchanganyiko zaidi ya matunda aina tano kwa mfano. atumie kiasi gani kupata dawa origino isiyo feki kama za mchina za kuongeza makalio? na ya watanzania wangapi wanaohitaji huduma hiyo? bado kuna rasirimali watu na vitendea kazi mbali ya muda anaotumia, hivyo gharama lazima ziwepo ingawa ni kweli kwa mtu maskini kama mimi kuzimudu kamwe sitaweza. ninachojitahidi ni kufuata ushauri ili niepuke kuugua then nikashindwa kujitibu kwa kuwa gharama ni kubwa kwa kweli.

Ushauri kwa walamikaji wengi ambao nimewaona humu pengine kabla ya kulalamika tuwe tunachnguza. maana wengine hata afya bora kuifata shida mfano kunywa maji tu glass nane kwa siku shida ambayo ni kitu cha bure. sasa ukiugua gharama huziwezi unaanza kulalamika ufanyweje. Hatukatai magonjwa yapo ya kila aina duniani mengine hayasemeki ukiyaona mwezio kaugua huwezi kuamini dunia hii na hosipitali zipo maana kuna watu waoaamini hospitali ndio mwisho wa matatizo lakini madawa mengi ndio hujaza sumu mwilini mwisho siku ulikuwa unatibu moyo na figo zinaanza kuleta shida maana zimeshinda kuhimili sumu ya muda mrefu. mtu akikwambia tiba mbadala mansema mjasilia mali basi fata hata ushauri ili uepukane na huo ujasilia mali wake. Kupanga ni kuchagua. siku zote nasema ukiwa mzima shukuru Mungu. Kuna watu wanateseka. Tungekuwa na imani ya kuuchangiana kwa wagonjwa kama tunavyochangia harusi pengine tungepunguza malalamiko. Lakini mtu akiumwa mpaka aje achangiwe ugonjwa umekuwa sugu na kupona ni kudra za Muumba.

Kuna mtu kasema majarida ya tiba mbadala yapo kibao je ni wote wanayasoma? Mimi binafsi nina vitabu kama vitatu aina tofauti hivyo vya tiba mbadala kwa kutumia matunda na vyakula lakini nilichokinunua kwa bei ya chini ni Tshs 50,000 sasa wangapi wana-afford hiyo bei na ikiwa waTZ tuna sifa ya kutopenda kujisomea. Wengi wetu wapendacho ni rahisi, mtelemko, kutafuniwa halafu tumeze ndo maana tunaitwa shamba la bibi kwa ajili ya ufahamu wetu mdogo.

Mifano ni mingi ya ujinga tulio nao kama watu kusubiri usiku wakamwage uchafu barabarani mitaro ikiziba, mafuriko uchafu kila kona mwishoe kipindupindu, kuhara n.k ukienda hospitali dawa kanunue hela huna lawama kibao kwa serikali na yeyote atakekutibu kama Ndodi uwezo bado huna lakini chanzo umesahau kama ni wewe uchafu wako uliomwaga kwenye vyanzo vya maji tena usiku watu wasikuone.

Mimi naona tukielimika na ufahamu wetu wa mambo ukawa mkubwa hata akina Dowan wajao tutawaepuka. bila hivyo tutabaki kulalamika ndani ya blanketi hatuchukui hatua.
 
well said thanks
 
jaman wadau habar zenu kwanza. ni hivi huwa na nachanganyikiwa sana na utaaam wa dr. isaac ndonde kuhusu maswala ya kupangilia vyakula ili kuepusha unene.utata wangu ni hivi miaka michache iliyo pita wakati dr huyu alipo kuwa anaendesha kipind chake startv alikuwa mwembamba sana.sasa hivi amenawili(amenenepa) na kuna kila dalili kuwa atazid kunawil zaid ya alipo sasa.kipind kile kila mwisho wa kipind alikuwa anaomba watu wamchangie pesa za kulipia vipindi vyake ili viendelee kulushwa.nina mashaka kwamba hata yeye hafat anacho kifundisha kuhusu swala zima la kupangilia misos.otherwise asinge nenepa vile.au na yeye tumuite mganga njaa tuu kama yule sheikh wa magomeni na bla bla zake za kitabir!!?
 
Isaac Ndodi....Isaac Ndodiii!....same guy kila siku.../whyyyy?
Hakuna ishuzingine?
Akinenepa mnaulizana,...
Akikonda mnamshangaa..
Give him a break...kweeek!
 
Nae sasa kazidi porojo. Ni kweli alikuwa ana afya nzuri tu hapo kabla ila sasa mishavu kama nini. Hafanyi mazoezi huyo na inaonyesha anakula sana. sasa hivi anatetea unene wake eti hata mtu akinenepa anenepe wmili wote na sio sehemu fulani tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom