Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Ndugu wapendwa najua mbaya kuuliza lakini sikuapenda kabisa kabisa jinsi ya huyu bwana anavyotreat watu na huu ugonjwa,...nimeulizwa na watu sana kuhusu kisukari nikawaelekeza kwa huyu mh naishia kutukanwa na kulaumiwa pasipo na haki

Ndugu mpendwa kumwona huyu bwna ni sh 20,000 NILIMPELEKA mtu jana lakiini wakati anatoka wakaanza kulalamika waliomtangulia alipokuja yeye alisema yaani nimeshoka nimechoka kabisa
akasema ameonana na dk alipomwona akaanza kumwambia shida zake wakati akiwa anaendelea
kumeweleza jamaa akamweleza shida yako inaitaji sh million 3 ,...kwa kweli baada yaa hapo akabonyeza kidude akaitwa mwingine wakati akiwa ndani ...,akamwamba aunt muda umeisha ...kwa kweli hii si uungwana nhisi mtu akija kwko dk anataka umweleze na pia umsikilize ......,na si kuangalia wako wangapi nje wanakusubiri

Nakutakia kazi njema bosi


Mkuu, kabla hata sijamaliza kusoma ulichoandika,,mi pia ni mhanga wa huyu bwana.
Mwaka juzi nilienda kwake kwa lengo la kununua dawa ya allergy, akaniambia akanitajia kiwango,,actually sikuwa na uwezo huo. Nikawa namwomba anipunguzie,,akanijibu kama huna hela niondoke kwani kuna lundo la watu wanamsubiri.

Nilisikitika sana,,na tangu siku hiyo nilisusia hata kuangalia vipindi vyake vya tv.
 
ndodi ana vipindi vingi sana kwenyetv stations...star tv na eatv...unadhani asipochaji hizo 3m atapata wapi hela ya kuendelea kuuza sura pale kwenye tv? huo sio uungwana kabisa kwa watz ambao wengi tuko masikini.

Inamaana hizo 3m analipwa?
Hakika Tz noma!!
 



Huwa anakandia wanawake wanene na wenye vitambi, wakati nyumba ndogo yake iko pale Mwanza imejaziana kila sehemu ya mwili including kitambi.


JF ni moto wa hoja.Kila kitu kipo wazi na uhakika.
Nyumba yake k ipo wapi?
 
Mwaka jana kwenye kipindi asubuhi cha tbc1,,katibu mkuu wa wizara ya afya au wa TBDF kama sijakosea, alikua anahojiwa na alisema kwamba tayari amekwisha pigwa marufuku kujitangaza kwenye vyombo vya habari, kwani ni kinyume na sheria.
Na kweli kwa kipindi kirefu hakuonekana,,ghafla nakaanza kumwana tena kwenye tv.

Inawezaekana kabisa kuna mlungula ulipitishwa.
 
Labda tuwekane sawa kwa haya kwanza:
1: Ukiingia gharama kwa dawa za Ndodi (na kufuata Masharti vyema)UNAPONA!..guaranteed!
2:Yule jamaa ana watu wengi mno, kiasi ukianza kubembeleza bei pale ndani hutakuwa entertained...utamchukia!. Ukitaka saundi ya bei za dawa umtafute akiwa nyumbani au nje ya pale ofisini...naongea kwa uzoefu!
3:Ndodi ana uzoefu na kazi ile sana, anachukulia kwamba akikwambia kitu mara moja utaelewa, vinginevyo kama unauliza sana tafuta muda private, si wakati akiwa na foleni ya watu nje!(Najua hii ni unprofessional kidogo, lakini na tukumbuke kuwa anahitaji kuzingatia muda ili aweze kufidia gharama za kupata dawa na kulipia kodi zote zinazomwangukia).
4:Hiyo 20K ni consultation fee kama ilivyo kwa hospitali zingine unapotaka kumwona specialist mazee!...Tuangalie zaidi Gravity ya ugonjwa!
5.Sina uhusiano wa kinasaba na Ndodi, ila nimetokea kumwelewa, na nina shuhuda za 100% za walioenda kwake kupona magonjwa ambayo hayatibiki hospitali..
Aksante.

PJ we ni envoy wa Ndodi?
Binafsi nilienda kwa ndodi almost 2wks ago hapa mwanza tai5hotel bahati mbaya sikumkuta ila sasa huduma niliyoikuta inauelekeo wa kuvuta pesa zaidi kuliko tiba.
Nilikutana na dada flani whom she claimed as a representatv wa Dk yaani kabla sijaelezea kilichonisibu binti alidakia sitakusikiliza b4 paying consultation fee!,
nilichomwambia sh20 sio issue nisikilize kwanza,
then tuendelee na maongezi,
aaaagh bint alikuwa relactant sana nikaona wizi mtupu bora nitambae zangu,
inshort jamaa wapo kipesa zaidi kuliko huduma coz gharama waingiazo si kweli kwamba it is a realistic cost per day,
eg kuna wagonjwa zaidi ya 100 wanataka kumwona kwa siku times 20000 is diz fear kwa uharisia?
Jamaa ni mwizi na hana upendo kwa watanzania na si mtu wa dini akumbuke sisi waTZ wengi wetu ni masikini so he has to review the whole process of attending customers.
 
Kama unafuatilia vipindi vyake ambavyo vimekaa ki'comercial zaidi, the way anavyo'present utagundua tu kuwa yupo kifedha zaidi.
Watu kama Ndodi ambao wengi wao ni kweli wana uwezo wa kutibu lakini hutumia advantage ya ugonjwa wa mtu kujizolea fedha na ndio maana sometimes hujisahau na kutanguliza zaidi fedha.
 
Mimi nilishawahi kwenda kuwaona wasaidizi wake wa Mwanza kwa tatizo la mzio (allergy). Kumuona daktari niliambia elfu kumi na matibabu niliambiwa laki tano! Hiyo fee ya kumuona ndiyo hasa yeye huilenga, linalofuatia ni kukukatisha tamaa kwa kukutajia bei kubwa.....sasa ushindwe usishindwe bei utajiju, yeye keshalamba fee. Inatakiwa ufikirie kwa undani sana ndo utagundua unaibiwa, sababu lengo kuu ni kupata ile fee na kwa asilimia ndogo ndiyo kukutibu!
 
Mkuu, kabla hata sijamaliza kusoma ulichoandika,,mi pia ni mhanga wa huyu bwana.
Mwaka juzi nilienda kwake kwa lengo la kununua dawa ya allergy, akaniambia akanitajia kiwango,,actually sikuwa na uwezo huo. Nikawa namwomba anipunguzie,,akanijibu kama huna hela niondoke kwani kuna lundo la watu wanamsubiri.

Nilisikitika sana,,na tangu siku hiyo nilisusia hata kuangalia vipindi vyake vya tv.

.............. Jisachiii !!!

Kama unafuatilia vipindi vyake ambavyo vimekaa ki'comercial zaidi, the way anavyo'present utagundua tu kuwa yupo kifedha zaidi.
Watu kama Ndodi ambao wengi wao ni kweli wana uwezo wa kutibu lakini hutumia advantage ya ugonjwa wa mtu kujizolea fedha na ndio maana sometimes hujisahau na kutanguliza zaidi fedha.

............. Jamaaa mwizi jumla ! ......anachanganya Dini kidogo, usanii sana, vitisho na mwisho anakula kiingilio !

Inamaana hizo 3m analipwa?
Hakika Tz noma!!

........... unakukatisha tamaa ili ale kiingilio !

PJ we ni envoy wa Ndodi?
Binafsi nilienda kwa ndodi almost 2wks ago hapa mwanza tai5hotel bahati mbaya sikumkuta ila sasa huduma niliyoikuta inauelekeo wa kuvuta pesa zaidi kuliko tiba.
Nilikutana na dada flani whom she claimed as a representatv wa Dk yaani kabla sijaelezea kilichonisibu binti alidakia sitakusikiliza b4 paying consultation fee!,
nilichomwambia sh20 sio issue nisikilize kwanza,
then tuendelee na maongezi,
aaaagh bint alikuwa relactant sana nikaona wizi mtupu bora nitambae zangu,
inshort jamaa wapo kipesa zaidi kuliko huduma coz gharama waingiazo si kweli kwamba it is a realistic cost per day,
eg kuna wagonjwa zaidi ya 100 wanataka kumwona kwa siku times 20000 is diz fear kwa uharisia?
Jamaa ni mwizi na hana upendo kwa watanzania na si mtu wa dini akumbuke sisi waTZ wengi wetu ni masikini so he has to review the whole process of attending customers.

.......... yule sio tabibu ni mwizi jumla !!


Ndg waungwana huu ni mtazamo wangu binafsi kuhusu Ndodi "Dr"

Kwanza kabisa huyu mtu ni mjasiriamali mzuri sana hapa nchini ambaye ameweza kuteka watu wengi sana kwa maneno yake na tiba zake asilia ambazo kwangu mimi nina imani ni nzuri kuliko za hospitali kwani nyingi hazina kemikali na pia hutoa ushauri wa tiba mbadala kama kula right foods, mazoezi sehemu muafaka na vingine vingi.

Huyu mtu ni mjasiriamali na naweza kusema ni genious kwani ameweza kuangalia tatizo liko wapi na akalitumia kutengeneza hela (creativity phenomena) tena kwa kutumia tiba mbadala ambazo ukisikiliza maelezao yake nyingi ni za kweli

Pia mtu huyu ingawa sina uhakika kuhusu taaluma yake ila inaonyesha anajisomea sana hivyo ana ufahamu wa mambo mengi sana yanayohusu kitu anachofanya

Matatizo ya Ndodi

1. Hayuko organised, kama unafualtilia vipindi vyake utaona anachanganya sana mada na mwisho wa siku anashindwa kutoa kwa ufasaha alichodhamiria kukitoa (poor presentation skill)

2. Ana namba nyingi sana za simu (zaidi ya kumi) kitu ambacho kwa mtu ambaye yuko makini na mwenye kujipanga hawezi kuwa hivyo

3. Yuko kibiashara zaidi kuliko kitabibu kwani kama ukifuatilia vipindi vyake utaona anavutia zaidi kuonana nae kuliko kutoa suluhisho kwa ushauri

4. Kitu kingine kinachonishangaza ni kwamba pamoja na umaarufu alionao anakaa hotelini kama sehemu ya kazi, wakati nadhani ingekuwa vizuri kama angeanzisha kituo cha kueleweka maana pale hotelini kama kikinuka anaweza kukimbia kirahisi, mtu makini na mwenye nia ya kazi yake anatakiwa kuwa na kituo maalum (kwa mtizamo wangu)

5. Katika kuongea kwake ana masikhara mengi sana hivyo kipindi chake kimegeuka kuwa kama komedi hivi, wakati anatakiwa kuwa serious kwani suala la utabibu linagusa maisha ya watu

Kwa hayo matano naona ndio matatizo makuu sijui kuhusu customer care kwenye kituo chake maana sijawahi kufika ila kwa jinsi anavyoongea tu kwenye kipindi naona kama hayuko organised yeye binafsi

............. wewe shtukaa ! yule mwizi ! TIBA MBADALA VITABU na MAJARIDA yako chungu nzima ! wala humuitaji ndodi !

Hivi ni mchungaji?

.............. anachanganya Dini kukupumbaza !

Pamoja na yote mazuri na mabaya yanayosemwa na watu kumhusu huyu Dr. Ndodi, mimi nina angalizo;

1. Je nani anyeweza kutujulisha kilichotokea hadi akamwambia huo mgonjwa wa pdiddy alete mil.3? hapo lazima tukubali kwamba kulikuwa na mazungumzo, katika hali ya kawaida kama mgonjwa hakuridhika lazima atafute namna ya kumsema vibaya dk wake na hawezi kusema ya upande wake, kwahiyo sidhani kama ni jambo la busara kuanza kumshambulia mtu wa watu kwa maelezo ya upande mmoja. kama kungekuwa na maelezo ya upande wa pili hapo tungeweza kuwa fair katika mashambulizi tunayoelekeza kwa dr. ndodi.

2.Suala la uhai wa mtu ama kifo chake linabaki kwenye mamlaka ya MUNGU mwenyezi, tusijaribu kumrundikia ndodi tuhuma ambazo hastahili. Hata rais wa zamani wa Yugoslavia,bw.Tito alifariki dunia akiwa amezungukwa na madaktari bingwa wa kila aina lakini kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kutoa na kuchukua uhai alikuwa ameamua tito alifariki dunia akiwa amezungukwa na madaktari bingwa.
Kama kuna mtu katibiwa kwa ndodi na hakupona hilo sio jambo la ajabu kwakuwa yeye ni mwanadamu tu, siye MUNGU, hata huko mahospitalini watu wanakufa tena wakiwa wametumia gharama kubwa. Mwl. Nyerere alipelekwa uingereza kutibiwa lakini alifariki ni sawa na wengine waliokwenda sehemu mbalimbali kutibiwa na hawakupona. Na kuna wengine wengi wanatibiwa kwenye hospitali kubwa hapa nchini ama nje ya nchi, kwa waganga wa kienyeji na kwingineko na hupona ama vinginevyo, jamani tusimnyoshee kidole huyu muungwana kwa suala la kifo, maana tunasahau msururu wa watu waliopona kwa tiba yake na walikuwa wamekata tamaa huko mahospitalini.

3. Kwakuwa anakuwa na vipindi vya television na anatoa namba zake watu wanatuma sms na hata kupiga simu, mbona sijawahi kusikia mtu akituma sms ama kupiga simu kulalamika zaidi ya kusikia watu wakiulizia matatizo yao mbalimbali ili wasaidiwe? Mi nadhani kama kuna tatizo kwenye huduma zake watu wasingekuwa wanamiminika kila siku kwenda kwake, au kama ana customer care mbovu na bado watu wanamiminika kwenda kwake basi tatizo haliko kwake pekee.

............ huyu msukule nini ??!!

Jamani, labda mimi nina coincidence mbaya/ au niite NZURI na huyu mganga...Nina maelezo POSITIVE tu kuhusu huyu mtu...
Shida za watu ni kwamba mnadharau tiba za asili/Mbadala na kuthamini dawa za Hospitali..Mentality mbaya hii!...
Turudi Bustanini Edeni...tiba zote zinapatikana kwenye vyakula vya asili!


.............. wewe alikutibu nini ? Yaaaani Ndodi ni kuliko DOWANS !!!! Khhaaaa !!


Ndodi ni mjasiriamali....

......... muweke kwenye kilengeo!!!!!!!!!!!!!!!!:shock:
 
Ndugu pole sana kama kumdhihak mtu kwako busara nimeanza kukuogopa inshort alieenda yuko vyema sana kifedha one of CEO ktk shirika la umma na kwake kilichomsumbuani uhakika wa kupona kwa hiyo mil 3 ...na hapo ndipo alipopagawa na majibu ya dk ndodi ni dk mzuri sikatai ila nikwambie kama hizi 20 za kumwona nimewapeleka watu wengi sana kwake wengi..na mwisho kuishia maalalamiko mara gali sana ni ngumu kwa mtu wa MUNGU kuwa kibiashara zaidi badala ya kuangalia utasaidiaje kuwaponya kupitia kipaji MUNUG alichokupa...nahisi anaitaj kumuuliza MUNGU tena je hii huduma ametumwa na Mungu Ama lah....bado dk naitaji kuona ukienda mbali kwa huduma hii lakini nisingependa kuona ofisi zake zikihudhuriwa na MATAJIRI WENYE PESA ZO KAMA WAKINA
PAKAJIMMY NA SUMBALAWINO....KILA LA KHERI JAMANI MUNGU NDIE MWEZA YOTE
hana lolote huyo tapeli,anataka pesa kwanguvu we unazan mchezo asubuh awe mwanza mchana dar na jion amalizie arusha unazani hizopesa zakupanda ndege atatoa wapi kama sio kufanya usanii asanye hizo 20 kwa kila kichwa?
 
Akili ni nywele kila mtu ana zake . nisha sanuka huu ni ufisadi wa mwingine
 
EEEEEH Ndodi analipa kodi kutoka kwenye haka kampunga anachopopoa kwa "WAGONJWA"?
 
Sasa huyo ndugu yako anataka kupona au abaki na 3M?
NINACHOJUA NI KWAMBA AKITOA HIYOFEDHA atapona BILA YA SHAKA...
Labda alijisikia duni kwa vile hana hiyo hela...
Mara ingine hata umasikini unasababisha ulalamiishi usiokuwa na sababu!

Mkulu
Heshima mbele, huyu jamaa ni TAPELI. Ana-capitalize on ignorance ya watanzania katika suala la AFYA KINGA na TIBA.
 
Hivi mteule dr ndodi haya yalioelezwa humu atayasoma?
Au kuna wasaidizi wake watamwambia?
Maana mengi yameelezwa ...yanagusa hisia na uhalisia wa wahanga.
Lakin amevuna dr... Alionesha funguo ya gari yake kama sijasahau nliambiwa ni Hummer au V..!
Wenye taarifa waliweke wazi.
 
EEEEEH Ndodi analipa kodi kutoka kwenye haka kampunga anachopopoa kwa "WAGONJWA"?
huduma za afya na elimu, hazikatwi kodi!, ndio maana viji dispensary kila kona na shule kibao za kulipia, ni za kukusanyia tuu!.
 
Hakuna guarantee ya dawa kwa mgonjwa elewa huo u-guarantee unaanza pale mgonjwa anapohudumiwa vizuri akajenga saikolojia ya kumwamini dr. Ikiwa kinyume na hapo dawa zinaweza zisifanye kazi. Akaja kuponywa na majani ya mpera wa nyumbani kwa jirani yake ambao hauna thamani ya mil 3 na akaambiwa dawa na muungwana kwa mdomo bila kuhitaji malipo.

Nawachukia wanaofanya matatizo ya ugonjwa wa wenzao kuwa miradi!

Brilliant Mohammed,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom