Ni kweli aweke cv's zake hadharani na awaeleze wananchi kama yeye ni Dr amespecialize kwenye nini? maana naona hakuna anachoshindwa
Hakuna kitu kibaya sana kama ukosefu wa ufahamu na kunyimwa fikira japo kiduchu, ukazungumza la maana.
Nikuulize ukishawekewa CV yake itakuwa imekusaidia nini?
Hospitalini kote unakoenda kutibiwa unawekewa CV za hao wanaokutibu au ukikuta tu mtu kavaa overcoat jeupe basi ushaamini huyu ndo daktari ili mraidi anafanya kazi muhimbili, au kwingineko. Nafikiri ungeacha ukiritimba wa mawazo.
Pamoja na hayo hulazimwishwi kumwangalia Dk. Ndodi kama anayoongea ni ya uongo na hayana hata faida kwako. Mbona channel ni nyingi tu tena zenye vipindi vya kukuburudisha bila kujifunza la maana ni wewe tu na muda wako. angalia futuhi, super sport, original comed, la maana labda taarifa ya habari kisha kula ugali wako fanya mambo yako mengine.
Tuache siye tunaopenda tusivikose vipindi vyake hata kama anaosoma vitabu vya turejee eden kama mdau hapo juu alivyosema. maanda hata Dk bingwa wa muhimbili ukiingia ofisini kwake hukosi vitabu juu ya meza kukujulisha kuwa soma vitabu upate maarifa. Hoja zingine huwa za kipuuzi.
Weka CV yako tuone kuwa angalau kwa kupitia CV yako watanzania wanaweza wakapata ufahamu na kuacha kuwa wajinga ndo waliwao au shamba la bibi. na pia kwa kupitia CV yako watajitahidi kuepukana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, kupunguza magonjwa ya moyo au kwa kupitia CV yako angalau namba ya wanaofeli kidato cha nne itapungua na uchumi wa nchi utaimarika aha au pengine dowan hawatalipwa **********n.k. CV, CV, CV, lol!
Jali yako unayoona yanakufaa maana siye wengine tulikuwa hatujui kuwa mkaa wa vifuu vya nazi unaondoa gesi na sumu mwilini mpaka niliposikia kwa dk ndodi. nikajaribu siku moja kutumia nilipokuwa na shida ya gesi nikapata ahueni baada ya muda mfupi, pia sikuwa najua dawa ya meno mpaka siku niliposikia ndulele na jinsi ya kutengeneza nikatengeneza mwenyewe na kutumia mpaka leo meno yangu yako vizuri maana nilikuwa nimeshaamua kwenda kung'oa. So sisi wajinga anatufaa kwa upande mwingine ndo maana tunapenda kumsikiliza maana tunaweza pata tusiyojua tukaepuka kwenda kulipia hizo M3 pale tutakapokuwa wagonjwa. wewe baki na kutaka CV yake hatahivyo nafikiri unawajua wenye CV wafate ukiwa na shida. mwacheni baba wa watu. hamwibii mtu watu wanakwenda wenyewe kwake kwa kuwa wana shida. Sidhani kama mtu hana shida atamfuata ndodi kwanza ukafanye nini. Nafikiri tungeilalamikia serikali yetu ijitahidi kupunguza mlipuko wa bei unaofanya gharama za maisha kuwa juu kila uchao.