Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Raia Fulani, Jul 31, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nadhani wadau wengi humu mtakuwa mmeshamsikia au kumwona huyu bwana machachari ambaye ni dokta, mchungaji, mshauri, mwalimu, n.k. binafsi napenda kumsikiliza kila wakati anapotoa mada hasa ukichangia na ile spidi yake ya kuongea bila kukosea. tatizo lake ni mtu ghali sana linapokuja suala la matibabu. zaidi ya kumwona kwenye kioo, kuna ya ziada juu yake? tumzungumzie kwa wema tu kwani ni mtume yule
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  I can discern the guy is not famous enough to be known. Or the guys are ignorant enough to know him. Skip it
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huyu Dokta/Mchungaji tena kijana ni mfano wa kuigwa.Napenda vipindi vyake vya redio na TV kwa maana anazungumzia mambo ya maisha ya kawaida kabisa.Kipindi chake cha juzi Jumatano kuhusu namna ya kuchagua mchumba kwa vijana wa kike na kiume kilinivutia sana.Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  umeongea pwent. Huyu Dr. ni public speaker mzuri sana. Kwa wenzetu huko nje angekuwa mtu muhim sana. Na usemavyo kuhusu kujiunga humu lingekuwa jambo la busara. Labda yupo ila ni kwa vile hatujuani
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.

  weeeeeeeeeeeeeeee bili yake atalia nani?????????
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwani cha ajabu yeye kuja na kuchangia ni nini? Kwani unadhani wanaochangia humu hawana bei? Si ni kujitolea tu na hata yeye mbona anaalikwa sehemu mbalimbali kama makanisani kuzungumza na halipwi?
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ila kwa anavyosema wachumba watazamane na kuongea tu bila kujiexpres kwa karne hizi ni ngumu
   
 8. l

  libidozy Member

  #8
  Aug 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ujinga kwa kila mganga wa kienyeji kujiingiza katika mambo ya kiuchungaji ili watu wawakubali!Alianza Yahaya Hussein,akaja Ndodi sasa Joseph Kalokola Buberwa wa JKB international nae eti anatoa neno la mungu!Acheni kukufuru mungu kwa kutaka ufalme wa hapa duniani.Kalokola mke kamshinda na wametengana kwa kupigana magumi pale ubungo plaza mimi pamoja na wafanyakazi wake akina Vick,Mrutu na Ndutu ndio tulioamulia hizo ngumi leo nae anafundisha watu jinsi ya kuishi katika ndoa!Aibu.Hawa ni wafanyabiashara tuu wala hawatendi mambo ya mungu,achaneni nao.
   
 9. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawa watu wana akili sana.Wanajua kuwa kwa hali iliyopo sasa watu wanahitaji msaada kutokana na shida zao mbali mbali.Sasa situation inapokuwa hivyo wanawamanipulate wenye shida zao kutokana na mvuto wao wa kulonga.End of the day wanaliwa hela zao na hakuna lolote la maana.
   
 10. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unajua Dr Ndodi ni wa gharama kwa sababu vipindi vyake vinavyo rushwa kwenye runinga na radio anavilipia mwenyewe.Na kila week nilazima apande ndege kwenda mwanza kufanya kipindi.Unategemea hizo pesa anatoa wapi kama sio kucharge wateja wake kiasi kikubwa cha pesa ili aweze kuendelea kutuelimisha kupitia vyombo vya habari?
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mkuu umenena. Hata mi nashangaa ni lini buberwa kawa mchungaji. Hii inamaanisha dini ina influence sana ktk kutimiza mambo flani. Ndodi nae asiwe kwenye mkumbo huo. Tofauti zao ni bei za dawa zao. Ndodi ni ghali mno. Sijajua kama zinatibu kiukweli
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hizo trip ni za kujitangaza zaidi. Wanaomwalika wangemchangia kidogo ili gharama zipungue. Kuhusu kumanipulate mawazo ya watu ni kweli kabisa. Wabongo tuna matatizo mengi ambapo ni fursa kwa wajanja kama hao.
   
 13. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  inakuwaje mtu anakuwa ni Mchungaji na pia Mganga wa kienjeji? tiba zake nyingi si za kweli, mfn ndimu kutibu malaria!, wengi wamejaribu na kuishia na malaria kali wakaponea kwinini hospitalini, halafu bei zake ni aghali kuliko kwenda kutibiwa Apollo Hosp. INDIA, ila namkubali kuwa he is a good orator, which fits well with preaching the word of god.
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  unadhani hakuna tofauti kati ya tiba mbadala na uganga wa kienyeji? nadhani kabobea zaidi katika hizo tiba na ushauri zaidi ya uchungaji. huo uchungaji ni katika kujijengea imani kwa wateja. anasema ana tiba ya macho ili usivae miwani tena, ila inataka moyo! ni unga wa ndimu, unautia machoni. just imejin
   
 15. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  acha majungu na umbea, halafu umetoka nje ya mada.
   
 16. ludoking

  ludoking Senior Member

  #16
  Aug 3, 2009
  Joined: Oct 5, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Binafsi nimekuwa mfuatiliaje wa Vipindi vya Dr Isaack Ndondi kuanzia vile Channel 10 mpaka StarTv. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mambo ya msingi katika jamii ambayo uwepo wake kwenye screen kumewasaidia wengi. Vipindi vyote hivyo anavifanya kwa gharama zake mwenyewe, kwa hiyo hata gharama zake kimatibabu lazima ziwe juu. Laiti kama watanzania wasingeendelea kuifanya mioyo kuwa migumu na kumsaidia huyu bwana kama basi angekuwa msaada mkubwa jamii

  Binafsi huwa napata burudani saaaaafi napokuwa naangalia kipindi chake. Ni zaidi ya comedy . Pamoja na kujaliwa kipaji cha kuongea haraka haraka, pia huwa anajaribu kutumia lugha ambayo inaweza kueleweke kwa kila mtu.
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
   
 18. J

  Jafar JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mfanyabiashara - sishangai mbinu anazotumia
   
 19. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Wakuu naomba muone angalizo hapa chini.

  Inatakiwa tumzungumzie kwa wema!!!!!

  Utaona moja kwa moja sina nafasi ya kuchangi wema juu ya mtu huyu. Naomba upanue wigo ya mada hii ili tuweze toa mabaya pia.
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mkuu uwanja ni wenu kwani tunataka kufundishana hapa. yawezekana kuna kundi flani linavaa ngozi ya kondoo nasi tukaamini katika ukondoo wao
   
Loading...