Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Isaac Ndodi....Isaac Ndodiii!....same guy kila siku.../whyyyy?
Hakuna ishuzingine?
Akinenepa mnaulizana,...
Akikonda mnamshangaa..
Give him a break...kweeek!

Oooh Sorry Dr. Ndodi!!!!
 
Huyu Dokta/Mchungaji tena kijana ni mfano wa kuigwa.Napenda vipindi vyake vya redio na TV kwa maana anazungumzia mambo ya maisha ya kawaida kabisa.Kipindi chake cha juzi Jumatano kuhusu namna ya kuchagua mchumba kwa vijana wa kike na kiume kilinivutia sana.Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.

Watu wengi wanampondea siku hizi, mimi naomba kutoa ushuhuda, amenisaidia sana, tena bure kwa kuangalia kwenye tv tu. Kuna siku aliweka mada ya kufanya mazoezi, kunywa maji kwa wingi, matunda na mboga mboga, nimefuata kanuni zake na zimenisaidia, awali nilikuwa nikiona mtu mwembamba nilikuwa natamani kweli wembamba, tatizo lilikuwa kwenye hivi vitu vinaitwa bear na nyama choma, lakini tangu nilipoangalia kile kipindi kwa kweli imenisaidia sana. Siku hizi bear nakunywa week end tu.

Huwa nakwazika anapojiita Mtume, wakati anauza dawa mpaka 400,000. Kuna aunt yangu aliwahi kwenda kwake kwa matibabu alikuwa hapati mtoto, hakumuuliza mambo mengi, ile kusema hapati mtoto tu 400,000/= hapo ndo alinichosha ni Mtume gani ambaye huwa anasaidia watu kwa kuwalipisha mijihela mingi hivyo? Kuna mwingine yuko huku Loliondo anatibu sana magonjwa ya aina zote ambayo hayatibiki kwa shs.500.00 tu, cancer, ukimwi, kisukari na mengine kibao ambayo unayajua wewe mwana jf.
 
Huyu Dokta/Mchungaji tena kijana ni mfano wa kuigwa.Napenda vipindi vyake vya redio na TV kwa maana anazungumzia mambo ya maisha ya kawaida kabisa.Kipindi chake cha juzi Jumatano kuhusu namna ya kuchagua mchumba kwa vijana wa kike na kiume kilinivutia sana.Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.

Sio medical doctor..labda tuambie udokta mwingine wa mtaani
 
inabidi serikali impatie support ya kutosha ili dawa zake kila mtanzania awe na uwezo wa kuzipata kama vile babu wa loliondo! lkn dawa

ya maleria tu kwa ndodi ni tsh 400,000/=, je mtanzania wa kawaida atawezaje kumudu??

otherwise!! tunamuombea maisha mema na marefu!!!!!!
 
sasa hivi ni loliondo tu bei karibu na bure na tiba ya uhakika.
 
Sasa hivi ndodi 'kaiva ile mbaya! Kasakafia kupita maelezo. Si ndodi yule wa miaka minne iliyopita. Tusubiri na Babu naye anze kunawiri
 
me naona ni tapeli tu, kwa sababu hizo dawa zake anauza bei ghali sana halafu ukiacha kutumia ugonjwa unarudi kama kawaida hata kama dozi ni ya wiki mbili, hizo wiki mbili zikipita ukiacha kutumia ugonjwa unarudi kama vile hujawai kutumia dawa yoyote.
 
Ni ujinga kwa kila mganga wa kienyeji kujiingiza katika mambo ya kiuchungaji ili watu wawakubali!Alianza Yahaya Hussein,akaja Ndodi sasa Joseph Kalokola Buberwa wa JKB international nae eti anatoa neno la mungu!Acheni kukufuru mungu kwa kutaka ufalme wa hapa duniani.Kalokola mke kamshinda na wametengana kwa kupigana magumi pale ubungo plaza mimi pamoja na wafanyakazi wake akina Vick,Mrutu na Ndutu ndio tulioamulia hizo ngumi leo nae anafundisha watu jinsi ya kuishi katika ndoa!Aibu.Hawa ni wafanyabiashara tuu wala hawatendi mambo ya mungu,achaneni nao.

uko sawa mkuu!.
 
Huyu ni mfanyabiashara - sishangai mbinu anazotumia

Mkuu umenena katika mstari mmoja. Huyu jamaa anayeitwa Dindo naweza kumwelezea kama ni acabra dabra kama sio tapeli. Jamaa yangu alilipa hela hadi laki saba lakini hakuna kupona wala nini. mpwa wangu pia ingawaje kwa kipato chake laki 3 alizolipa ni sawa na milioni tatu - hakuna cha kupona wala mtoto wake. Kibaya anatumia Biblia kunyaka watu. Jamani tumwogope Muumba. Wanaomshabikia ni wale wanaopenda porojo zake. Waugue waende au wapeleke ndugu zao ndipo watakapozijua true colours za huyu jamaa.
 
Pwent? au pont, Any way sio kitu, mtoa mada amesema huyu bwana ni ghali sana, ukitaka kumuona ni Tsh 50,000/= hapo matibabu bado,

Ni vyema tukamuomba akaangalia kipato cha watanzania akapunguza kidogo.

Pont au point? any way wote mmeeleweka.
 
Ndodi ni mshenzi na tapeli mkubwa. Mwanaume gani anaongea kama malaya mitaani. Dawa zake ni bei kubwa sana na sidhani kama kuna tiba ya ghali kiasi hicho hapa nchini. Wanaomfagilia ndodi ni wale wanaopenda porojo. Wakitaka wamfahamu vizuri basi waende zahanati yake wakaulizie bei za dawa zake. Watashikwa na butwaa. Mshenzi sana huyo.
 
isack ndodi. Huyu jamaa ni kiboko. Sijajua yupo kundi gani. Dawa bure lakini kiingilio ni ghali kuliko dawa
 
To me he is boaring kwa kuwa hakuna mada asiyejua yeye na kuna muda anapotosha mambo asiyoyajua
 
Ndodi ni mshenzi na tapeli mkubwa. Mwanaume gani anaongea kama malaya mitaani. Dawa zake ni bei kubwa sana na sidhani kama kuna tiba ya ghali kiasi hicho hapa nchini. Wanaomfagilia ndodi ni wale wanaopenda porojo. Wakitaka wamfahamu vizuri basi waende zahanati yake wakaulizie bei za dawa zake. Watashikwa na butwaa. Mshenzi sana huyo.
Naunga mkono mada asilimia 100,hawezi kuwa mtume na ni mfanyabiashara,na kwa sasa wanakosa soko cos babu anatoa kikombe mia tano tu.
 
Acha kabisa LIBIDOZY kwani tofauti kati ya Buberwa na Dr. Ndondi ni sawa na tofauti kati ya Farao na Musa.

Buberwa ni member wa group ya anti-Christ na nina sema hivi kutokana na hotuba zake ambazo hazina hadhi ya kuitwa mahubiri bali KEJELI zinazosababishwa na UPOFU WA KIROHO.

Dr. Ndondi anakusaidia si lazima ukanunue dawa lakini vipindi vyake ni dawa tosha. ni kweli ni mtu muhimu mno katika jamii ya watanzania ingawaje hawa madaktari wetu wa kuchonga wamemkataza kujitangaza kwa kigezo eti SI RUKSA KIMAADILI YA UTABIBU DAKTARI KUJINADI KWA WAGONJWA. Huyu dokta hata kma hana doctorate ya Darasani lakini ni zaidi sana kuliko hawa wanaozeeka au kufa na utaalam wao bila kmnufaisha mtu zaidi ya familia zao.

Wadanganyika kuweni makini sana ...Convicing power anayo na si kila mwenye convicing power anaongea ukweli..kwa tulio somea taaluma huwa tunaona anavyoibia watu kwa kuchanganya changanya maneno...He is a good at marketing tho what he markets is totally a lie...amkeni wadanganyika si kila unachoambiwa ni kweli....ni kama ilivyo internate si kila habari unayoiona kwenye net ni kweli kazi kwako kuchuja,,,,watoto wa mjini wanasema akili kumkichwe.
Ndondi ni kweli ni public speaker mzuri mwenye mvuto na asiyechosha anapokalia kipindi chake sawasawa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom