Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

WanaJF,

Kwa wale wanaofuatilia mambo ya sayansi ya tiba mbadala/lishe, jina la Ndodi si geni masikioni mwao. Kuna wakati alikuwa anafundisha namna ya kula vizuri na jinsi ya kutumia mimea(mboga-mboga na matunda) kama dawa ya kuponya maradhi mbalimbali yanayowasumbua watu.

Dokta Ndodi pia alikuwa anatoa tiba za dawa zake ambazo kwa jinsi alivyokuwa anaeleza ni magonjwa ambayo mengi kati ya hayo yameshindikana hospitalini. Inasemekana gharama za dawa zake ni ghali sana kulinganisha na tiba ya hospitali au matabibu wengine wanaotibu kwa mimea asilia kama yeye hii nayo ni kutokana na magonjwa hayo kushindikana kutibika hospitalini.

Ni muda mrefu sasa sijamsikia akitoa huduma zake jambo ambalo linanifanya niamini kwamba atakuwa anatoa huduma/tiba zake nje ya nchi au ni umaskini wa watanzania kumudu gharama za matibabu ya dokta Ndodi.

Ni nini kilimfanya asitize huduma zake kupitia vyombo vya habari?

Nilisikia huyu dokta anatibu maradhi/magonjwa sugu ambayo hospitalini yameshindikana, kama ni kweli kwanini asiwezeshwe ili kuepuka kutumia gharama kubwa za matibabu nje ya nchi kwa baadhi ya watanzania ambao wengi wao hawamudu gharama za kwenda india kupata matibabu?

Wale wenye waliowahi kupata huduma za matibabu ya dokta Ndodi mnaweza kutuambia kitu.
 
Stiff competition has kicked him out of race. Zikaja herbal works cjui pale segerea, dr. Rahab pale ubungo plaza, cjui nani sanitarium clinic kule mbezi beach nawengine kibao, so ikaonekana huduma zake ni outdated compered to new merging markets with low prices..
 
Ndodi tapeli kama matapeli wengine wa mjini, kama kuna mtu mwenye ushuhuda wa kweli kuhusu Ndodi atueleze......
 
Ndodi tapeli kama matapeli wengine wa mjini, kama kuna mtu mwenye ushuhuda wa kweli kuhusu Ndodi atueleze......

Aliwahi kukutapeli nini mkuu? Weka kila kitu aazi wengine tumjue, kusena ntu ni tapeli bila kuobesha huo utapeli hakuna tofauti na uzushi/propaganda za wanasiasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom