PakaJimmy, kwanza asante kwa hii shuhuda ya Dr. Ndodi na hiyo asilimia 100% ya wanaopona. Naomba nami nikupe shuhuda yangu ya mgonjwa mmoja tuu ambaye sio tuu alifariki, bali pia aliingia umasikini hapo hapo kwa Ndodi.
Jamaa alikuwa na matatizo ya moyo na figo, akapimwa hospital, wakamwambia atafute milioni 14, akatibiwe nje ya nchi, ndipo wasamaria wakamtaja Ndodib jamaa akaanza kuhudhuria clinic yake. Kwanza aliuza gari, pili aliuza shamba na hatua ya tatu alikuwa mbioni kuuza nyumba ndipo kifo kikamkuta tena hapo hapo kwa Ndodi, cost aliyoingia was over and above M.14 zilizohitajika hospitalini. Inawezekana labda by the time anakwenda kwa Ndadi, it was allready too little too late, angemwambia na sio kumlia hela zake na kifo juu!.
Kwa vile huu ni uthibitisho wa kifo kimoja kati ya hiyo asilimia 100% uliyoisema wewe, then ili tuwe realistic, ishushe angalau isomeke wanapona kwa asimilia 99.9% ili wa uhakika wa asilimia 100% ambaki ni Mungu Peke yake.
Kwa upande wangu mimi binafsi, Dr. Ndodi namkubali sana vipindi vyake kwenye TV, ila pia sio tuu ni mtu kama wa masikhara masikhara, pia ukim observe kwa makini, utakubaliana na mimi, kutibu anatibu lakini pia ana uchizi fulani, not consistance at all. Siibezi tiba yake, lakini nabeza ustaarabu wake, upokee 20k ya mtu, kuingia tuu unamwambia katafute 3 M!, sifa kubwa ya tabibu ni kusikiliza. Dr. Ndodi ana papara na hatatulia, ukifuatilia vipindi vyake hilo utalibaini wazi.
Nilibahatika kukutana naye mahali, nami kama binadamu, nikamweleza tatizo langu la kiafya, alinikaribisha na kunihakikishia, litakwishwa mara moja. Pamoja na shida yangu, dhamira bado haijanituma, ila ikinituma, nitamtembelea na nitawaletea ushuhuda wa first hand news na sio habari za kuambiwa.