Mdada maarufu, mwana mitandao na mtangazaji Diva the Bawse, aomba waja wamchangie pesa ili aweze kulipa kodi ya nyumba anayoishi, baada ya mmiliki wa nyumba hiyo kuja kumfanyia tukio la udhalilishaji kwa kuchelewa malipo.
Huyu bidada si alisema ana bwana ake mzungu? Wala hana shida ndogo ndogo hata WCB wasipo mlipa hela yake, yeye maisha yataenda km kawaida? Mara akaja na mibwato na mineno kuntu yeye pesa zipo na zinaingia kila siku kupitia products zake za urembo kutoka Diva Beauty, sasa imekuaje tena leo ashindwe kulipa kodi ya nyumba?
Afu sasa kodi inayotakiwa ni 10M, na hapo kachangiwa imefika 2M? kwanini anaishi maisha nje ya uwezo wake? Ndio shida ya kufake life, mwisho unaumbuka km hivi, Lol.
Haya Waja, Namba ndio hiyo, km una chochote kitu usisite kutupia hapo ili Diva wetu amalize deni la kodi yake.
Nacheka waja wanavyomchamba huko FB, woiiiih. 😂😂😂