Dewji: Biashara yangu ya kwanza nilikuwa nauza Mafuta ya Taa, Baba yetu alikufa masikini

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mfanyabiashara mkubwa nchini Azim Dewji, ameweka wazi kuwa biashara yake ya kwanza kuifanya ilikuwa ni kuuza mafuta ya Taa.

Akifanya mahojiano na CloudsTv Dewji amesema,

"Biashara yangu ya kwanza nilinunua gari kwa mkopo, nikawa na gari lakini tulikuwa tunanunua mafuta ya taa kwenye madebe tunapeleka vijijini kwenda kuuza, wale wanapata huduma sisi tunapata kipato, ndio biashara ya kwanza kufanya."-Azim Dewji

Kwa upande mwengine Dewji ameelezea maisha ya dhiki waliyokuwa wanaishi,

"Maisha yetu hayakuwa mazuri sana, baba alikuwa sio tajiri. Alikuwa mtu wa kipato cha kati lakini alifariki akiwa maskini kwa sababu alikuwa hapendi kukaa na mali. Alipokuwa anakuja mtu mwenye shida basi yeye alikuwa anampatia"-Azim Dewji

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Azim dewji anamiliki biashara gani kwa sasa?
Azim dewji ni ndugu yake Gulamabbas dewji. Huyo Gulamabbas ndio Baba yake Mo Dewji. Huyo Gulam ndio muanzilishi wa hiyo kampuni ya familia ya akina Mo. Hao ndio waanzilishi wenye mzigo wenyewe, huyo Mo kaikutia kampuni katikati. Wengine wanasema Mo ni msimamizi wa mali, wengine wanasema Mo ni muuza duka tu.


Hata siku moja, hakuna Tajiri wa Kitanzania ambaye atakwambia ukweli jinsi alivyopata hela. Utajiri wa matajiri wengi wa Kitanzania una konakona na vichochoro vingi.
 
Back
Top Bottom