Mrejesho wa miaka 10 ya msoto baada ya kuhitimu chuo kikuu

Trinity

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
1,713
3,226
Kichwa cha uzi cha husika, Kwanza nawasalimu wote katika jina la mwokozi ambaye ni Mungu wa kweli muumba mbingu na nchi.

Niende direct, miongoni mwa watu walio hustle kitaa baada ya kuhitimu chuo nahisi ni mm pekee though nafahamu na wengine wapo.

Si kwamba nilitulia tu bila kufanya shughur yoyote hapana, nilifanya dili nyingi sana changamoto ilikua mtaji mdogo na kipato kuwa kidogo kuliko mahitaji.
Mambo niliyo yafanya na changamoto zake ni kama ifuatavyo;

1. Kilimo, nililima sana kule Morogoro Kasanga karibu na bwawa la mindu.
Nilinunua mashine na mpira mita 200 ya kumwagilia ili nitoe maji kwenye mto mpaka shambani.
Nilifanya kazi usiku na mchana, ninaposema usiku namaanisha usiku kucha unapambana kutumia maji maana yanatumika na wengi hivyo option pekee ni kutumia wakati wengine wamelala.
Nililima mahindi ya gobo, nilifanikiwa kuyafikisha asilimia 60 na asilimia 40 hayakufika Kwa sababu mto uliwahi kukauka, ikabidi niwauzie masai wachungie ng'ombe.

2. Nilianzisha biashara ya kuuza mahindi makavu Iringa kihesa, biashara ilikua vzr changamoto mtaji wangu ulikua gunia 3 yaani debe 20. Nilikua nauza siku mbili zikienda sana siku 3 zinaisha maana wamama wanaopika pombe na wale wanaopenda kuandaa dona walikua wateja wangu.
Ilifika mahali watu wanakuja wanahitaji gunia 10 lakin uwezo sikua nao.
Biashara ilikua vzr na nilianza kuona mwanga wa kutoboa kimaisha maana niliweka mbinu madhubuti kuongeza mtaji.
Baada ya muda kidogo ile fremu pamoja na fremu jirani zilikua na mgogoro wa mirathi hivyo mahakama iliamuru zisitumike.

3. Biashara ya boda boda, hii ilikua mkombozi wangu daima japo nilikua napata pesa ya kula na kulipa kodi, mara chache nikawa namtumia mwanangu niliyempeleka kwa bibi yake baada ya mambo kuwa magumu.

4. Kununua na kuuza mkaa pori, hii biashara niliifanya wakati nafanya boda boda nikaona ngoja nijiongeze niwe naenda vijijini huko Kalenge, isman n.k
Biashara hii niliipenda baada ya jamaa yangu namuitaga mchungaji kuifanya na kunionesha ina faida.
Kweli siku ya kwanza nilienda nikapakia gunia 3, mchungaji akawa ananishangaa maana yeye huwa anabeba gunia 2 na wachache hubeba 3.
Biashara ilikua ina faida sana maana gunia moja unachukua porini kwa 12,000/= wewe unakuja kuuza 30,000/= Ukitoa gharama za mafuta na kula uhakika ilikua unabakiwa na 20000/= Kwa siku.
Changamoto ya hii biashara mpaka nikaacha ilikua ni kuwindana na maafisa wa maliasili, ilikua wakikukamata unaenda kuitoa pkpk kwa laki 3 mpaka laki 5.

5. Kufanya kazi private hasa za ualimu, nimefundisha mpaka ualimu ulianza kuniingia damuni.
Changamoto hivi sasa shule za binafsi hasa sekondari zina watoto wachache nafikiri kutokana na ujio wa shule za serikali nyingi (kata), ufinyu wa ajira elimu imekua haina mvuto kwani siku hizi hakuna wanao resit au mambo ya kusafisha vyeti sio ki vile.

6. Kazi ya udalali, hii ni kazi nzuri ila niliona napigwa mno.! Yaani unatumiwa gari unalinadi Instagram weee, mwisho wa siku unamuunganisha mnunuzi na muuzaji, wanashushana na kukubaliana bei na wanauziana halafu baada ya siku kadhaa unastuka biashara ilifanyika ukidai ubahil na kuzungushana kunaanza.
Lakinie pia ukimuonesha mtu nyumba inayouzwa, kesho yake anamtafuta mmiliki wanauziana pasipo uwepo wako.
Nikaona ujinga nikaachana nayo lkn nafikiri ilipaswa niongeze ubunifu na kuzuia mianya ya upigwaji sema niliachana nayo mapema mno nikawa najipanga kuirudia.

Kwa nini nasema mrejesho, niliwahi pitia kipindi kigumu nikatamani kuuza vyeti maana Kila nikiviangalia napata hasira, nilileta ule uzi humu, wengi walikejeli wengine walinitia moyo.!
Mbarikiwe sana wote maana nilikua nazingatia sana maneno hasa ya matumaini kuliko ulivyo fikiri,
Mungu ni mwema, vile vyeti vimenisaidia kama miongoni mwa comment Kwamba nivitunze ipo siku vitanisaidia, hivi sasa ni mtumishi wa serikali, natambua si kwamba ndo nimetoboa kwa mshahara, hapana I have to make more effort.

Mambo niliyo jifunza katika uhangaikaji,
1. Uaminifu ni jambo la msingi, inafungua milango ya watu na Mungu kukusaisia.

2. Usimtegemee mtu/ndugu yeyote hata kama atakuahidi kukusaisia. Mwisho wa siku atakukimbia tu, yupo tayari hata atoe line hewani.dah!

3. Ukifanya kazi ya hadhi ya chini, lazima kuna mazingira utadharauliwa tu, kubari dharau!

4. No permanent situation.

5. Mungu yupo na anasikia maombi Kwa lolote unalopitia iwe maradhi, uchumi, addiction, ukimuomba Kwa dhati anakusikia na kukusaisia.

6. **** huna pesa, upendo ni mdogo kwa ndugu na marafiki.

7. Usitende wema ukategemea utakumbukwa siku ya shida yako.

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Kichwa cha uzi cha husika, Kwanza nawasalimu wote katika jina la mwakozi ambaye ni Mungu wa kweli muumba mbingu na nchi.

Niende direct, miongoni mwa watu walio hustle kitaa baada ya kuhitimu chuo nahisi ni mm pekee though nafahamu na wengine wapo.

Si kwamba nilitulia tu bila kufanya shughur yoyote hapana, nilifanya dili nyingi sana changamoto ilikua mtaji mdogo na kipato kuwa kidogo kuliko mahitaji.
Mambo niliyo yafanya na changamoto zake ni kama ifuatavyo;

1. Kilimo, nililima sana kule Morogoro Kasanga karibu na bwawa la mindu.
Nilinunua mashine na mpira mita 200 ya kumwagilia ili nitoe maji kwenye mto mpaka shambani.
Nilifanya kazi usiku na mchana, ninaposema usiku namaanisha usiku kucha unapambana kutumia maji maana yanatumika na wengi hivyo option pekee ni kutumia wakati wengine wamelala.
Nililima mahindi ya gobo, nilifanikiwa kuyafikisha asilimia 60 na asilimia 40 hayakufika Kwa sababu mto uliwahi kukauka, ikabidi niwauzie masai wachungie ng'ombe.

2. Nilianzisha biashara ya kuuza mahindi makavu Iringa kihesa, biashara ilikua vzr changamoto mtaji wangu ulikua gunia 3 yaani debe 20. Nilikua nauza siku mbili zikienda sana siku 3 zinaisha maana wamama wanaopika pombe na wale wanaopenda kuandaa dona walikua wateja wangu.
Ilifika mahali watu wanakuja wanahitaji gunia 10 lakin uwezo sikua nao.
Biashara ilikua vzr na nilianza kuona mwanga wa kutoboa kimaisha maana niliweka mbinu madhubuti kuongeza mtaji.
Baada ya muda kidogo ile fremu pamoja na fremu jirani zilikua na mgogoro hivyo mahakama iliamuru zisitumike.

3. Biashara ya boda boda, hii ilikua mkombozi wangu daima japo nilikua napata pesa ya kula na kulipa kodi, mara chache nikawa namtumia mwanangu niliyempeleka kwa bibi yake baada ya mambo kuwa magumu.

4. Kununua na kuuza mkaa pori, hii biashara niliifanya wakati nafanya boda boda nikaona ngoja nijiongeze niwe naenda vijijini huko Kalenge, isman n.k
Biashara hii niliipenda baada ya jamaa yangu namuitaga mchungaji kuifanya na kunionesha ina faida.
Kweli siku ya kwanza nilienda nikapakia gunia 3, mchungaji akawa ananishangaa maana yeye huwa anabeba gunia 2 na wachache hubeba 3.
Biashara ilikua ina faida sana maana gunia moja unachukua porini kwa 12,000/= wewe unakuja kuuza 30,000/= Ukitoa gharama za mafuta na kula uhakika ilikua unabakiwa na 20000/= Kwa siku.
Changamoto ya hii biashara mpaka nikaacha ilikua ni kuwindana na maafisa wa maliasili, ilikua wakikukamata unaenda kuitoa pkpk kwa laki 3 mpaka laki 5.

5. Kufanya kazi private hasa za ualimu, nimefundisha mpaka ualimu ulianza kuniingia damuni.
Changamoto hivi sasa shule za binafsi hasa sekondari zina watoto wachache nafikiri kutokana na ujio wa shule za serikali nyingi (kata), ufinyu wa ajira elimu imekua haina mvuto kwani siku hizi hakuna wanao resit au mambo ya kusafisha vyeti sio ki vile.

6. Kazi ya udalali, hii ni kazi nzuri ila niliona napigwa mno.! Yaani unatumiwa gari unalinadi Instagram weee, mwisho wa siku unamuunganisha mnunuzi na muuzaji, wanashishana na kukubaliana bei na wanauziana halafu baada ya siku kadhaa unastuka biashara ilifanyika ukidai ubahil na kuzungushana kunaanza.
Lakinie pia ukimuonesha mtu nyumba inayouzwa, kesho yake anamtafuta mmiliki wanauziana pasipo uwepo wako.
Nikaona ujinga nikaachana nayo lkn nafikiri ilipaswa niongeze ubunifu na kuzuia mianya ya upigwaji sema niliachana nayo mapema mno nikawa najipanga kuirudia.

Kwa nini nasema mrejesho, niliwahi pitia kipindi kigumu nikatamani kuuza vyeti, nilileta ule uzi humu, wengi walikejeli wengine walinitia moyo.!
Mbarikiwe sana wote maana nilikua nazingatia sana maneno hasa ya matumaini kuliko ulivyo fikiri,
Mungu ni mwema, vile vyeti vimenisaidia kama miongoni mwa comment Kwamba nivitunze ipo siku vitanisaidia, hivi sasa ni mtumishi wa serikali, natambua si kwamba ndo nimetoboa kwa mshahara, hapana I have to make more effort.

Mambo niliyo jifunza katika uhangaikaji,
1. Uaminifu ni jambo la msingi, inafungua milango ya watu na Mungu kukusaisia.

2. Usimtegemee mtu/ndugu yeyote hata kama atakuahidi kukusaisia. Mwisho wa siku atakukimbia tu, yupo tayari hata atoe line hewani.dah!

3. Ukifanya kazi ya hadhi ya chini, lazima kuna mazingira utadharauliwa tu, kubari dharau!

4. No permanent situation.

5. Mungu yupo na anasikia maombi Kwa lolote unalopitia iwe maradhi, uchumi, addiction, ukimuomba Kwa dhati anakusikia na kukusaisia.

6. **** huna pesa, upendo ni mdogo kwa ndugu na marafiki.

7. Usitende wema ukategemea utakumbukwa siku ya shida yako.

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
Endelea kupambana kiongozi, lakini swali langu moja tu kwanini nchi hii mtu akipata ajira serikalini anapumua na kuona amemaliza? kwa mishahara ipi? au watu wanaiba sana huko.
 
Inaonekana anakuwa na uhakika wa kila mwezi kupata pesa japo ni kidogo lakini uhakika upo.

Posho za hapa na pale.

Tukija huku kwenye utafutaji maself made basi lazima upate mbinu ya kuongeza pato kila mwezi na biashara yako isife.

Mana hakuna kustaafu kwamba utapewa pesa zako baada ya hapo.
 
Kichwa cha uzi cha husika, Kwanza nawasalimu wote katika jina la mwakozi ambaye ni Mungu wa kweli muumba mbingu na nchi.

Niende direct, miongoni mwa watu walio hustle kitaa baada ya kuhitimu chuo nahisi ni mm pekee though nafahamu na wengine wapo.

Si kwamba nilitulia tu bila kufanya shughur yoyote hapana, nilifanya dili nyingi sana changamoto ilikua mtaji mdogo na kipato kuwa kidogo kuliko mahitaji.
Mambo niliyo yafanya na changamoto zake ni kama ifuatavyo;
1. Kilimo, nililima sana kule Morogoro Kasanga karibu na bwawa la mindu.
Nilinunua mashine na mpira mita 200 ya kumwagilia ili nitoe maji kwenye mto mpaka shambani.
Nilifanya kazi usiku na mchana, ninaposema usiku namaanisha usiku kucha unapambana kutumia maji maana yanatumika na wengi hivyo option pekee ni kutumia wakati wengine wamelala.
Nililima mahindi ya gobo, nilifanikiwa kuyafikisha asilimia 60 na asilimia 40 hayakufika Kwa sababu mto uliwahi kukauka, ikabidi niwauzie masai wachungie ng'ombe.

2. Nilianzisha biashara ya kuuza mahindi makavu Iringa kihesa, biashara ilikua vzr changamoto mtaji wangu ulikua gunia 3 yaani debe 20. Nilikua nauza siku mbili zikienda sana siku 3 zinaisha maana wamama wanaopika pombe na wale wanaopenda kuandaa dona walikua wateja wangu.
Ilifika mahali watu wanakuja wanahitaji gunia 10 lakin uwezo sikua nao.
Biashara ilikua vzr na nilianza kuona mwanga wa kutoboa kimaisha maana niliweka mbinu madhubuti kuongeza mtaji.
Baada ya muda kidogo ile fremu pamoja na fremu jirani zilikua na mgogoro hivyo mahakama iliamuru zisitumike.

3. Biashara ya boda boda, hii ilikua mkombozi wangu daima japo nilikua napata pesa ya kula na kulipa kodi, mara chache nikawa namtumia mwanangu niliyempeleka kwa bibi yake baada ya mambo kuwa magumu.

4. Kununua na kuuza mkaa pori, hii biashara niliifanya wakati nafanya boda boda nikaona ngoja nijiongeze niwe naenda vijijini huko Kalenge, isman n.k
Biashara hii niliipenda baada ya jamaa yangu namuitaga mchungaji kuifanya na kunionesha ina faida.
Kweli siku ya kwanza nilienda nikapakia gunia 3, mchungaji akawa ananishangaa maana yeye huwa anabeba gunia 2 na wachache hubeba 3.
Biashara ilikua ina faida sana maana gunia moja unachukua porini kwa 12,000/= wewe unakuja kuuza 30,000/= Ukitoa gharama za mafuta na kula uhakika ilikua unabakiwa na 20000/= Kwa siku.
Changamoto ya hii biashara mpaka nikaacha ilikua ni kuwindana na maafisa wa maliasili, ilikua wakikukamata unaenda kuitoa pkpk kwa laki 3 mpaka laki 5.

5. Kufanya kazi private hasa za ualimu, nimefundisha mpaka ualimu ulianza kuniingia damuni.
Changamoto hivi sasa shule za binafsi hasa sekondari zina watoto wachache nafikiri kutokana na ujio wa shule za serikali nyingi (kata), ufinyu wa ajira elimu imekua haina mvuto kwani siku hizi hakuna wanao resit au mambo ya kusafisha vyeti sio ki vile.

Kwa nini nasema mrejesho, niliwahi pitia kipindi kigumu nikatamani kuuza vyeti, nilileta ule uzi humu, wengi walikejeli wengine walinitia moyo.!
Mbarikiwe sana wote maana nilikua nazingatia sana maneno hasa ya matumaini kuliko ulivyo fikiri,
Mungu ni mwema, vile vyeti vimenisaidia kama miongoni mwa comment Kwamba nivitunze ipo siku vitanisaidia, hivi sasa ni mtumishi wa serikali, natambua si kwamba ndo nimetoboa kwa mshahara, hapana I have to make more effort.

Mambo niliyo jifunza katika uhangaikaji,
1. Uaminifu ni jambo la msingi, inafungua milango ya watu na Mungu kukusaisia.

2. Usimtegemee mtu/ndugu yeyote hata kama atakuahidi kukusaisia. Mwisho wa siku atakukimbia tu, yupo tayari hata atoe line hewani.dah!

3. Ukifanya kazi ya hadhi ya chini, lazima kuna mazingira utadharauliwa tu, kubari dharau!

4. No permanent situation.

5. Mungu yupo na anasikia maombi Kwa lolote unalopitia iwe maradhi, uchumi, addiction, ukimuomba Kwa dhati anakusikia na kukusaisia.

6. **** huna pesa, upendo ni mdogo kwa ndugu na marafiki.

7. Usitende wema ukategemea utakumbukwa siku za shida yako.

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
sahihi chief, wengine wajifunze pia ili wajue inawezekana
 
Back
Top Bottom